You are on page 1of 1

Swahili Bible Anonymous

Abrahamu!` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa
10
Abrahamu. Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda
11
mazuri, utakatwa na kutupwa motoni. Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba
mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata kubeba
12
viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Yeye anashika mkononi
chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome
13
kwa moto usiozimika." ic Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani,
14
akamwendea Yohane ili abatizwe naye. Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, "Je, wewe
15
unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe." Lakini Yesu akamjibu, "Acha
tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka."
16
Hapo Yohane akakubali. Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu
17
zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake. Sauti kutoka
mbinguni ikasema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye."

Chapter 4

1 2
Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku
3
arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. Basi, mshawishi akamjia, akamwambia,
4
"Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate." Yesu akamjibu, "Imeandikwa
katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."`
5
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
6
akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: `Mungu
atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye
7 8
jiwe."` Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: `Usimjaribu Bwana, Mungu wako."` Kisha Ibilisi
akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9 10
akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu." Hapo, Yesu
akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia
11 12
yeye peke yake."` Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia. Yesu
13
aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya. Aliondoka Nazareti, akaenda

You might also like