You are on page 1of 9

Somo la 5 kwa ajili ya Julai 31, 2021

Mathayo 11:28-30 ni ujumbe maalumu


kuhusu pumziko katika Kristo.
Ni bora tukafahamu kina cha pumziko ambalo
Yesu ametupatia kwa kujifunza ujumbe wake.
Kulingana na muktadha wa haraka wa aya hii (Mt. 11:27),
tunaweza kusema kwamba Yesu anaweza kutupatia
pumziko kwa kuwa Yeye ni Mungu, na ni mmoja na Baba.
Yesu hatupatii pumziko la moja kwa moja na lisilokuwa na
masharti. Kuna sharti rahisi tu: “Njoni.”

Tunapaswa kufanya mambo mawili ili


kuja kwa Yesu. La kwanza kabisa ni
rahisi sana: kusumbuka na kulemewa,
na kuhisi hitaji la pumziko.
La pili ni kukataa kuitawala mizigo yetu
wenyewe, na kuileta kwa Yesu ili
aichukue.
Nira ilikuwa ikiwekwa shingoni mwa wanyama ili kurahisisha
kazi yao (k.m . kulima).
Hata hivyo, nira ilikuwa ni mpaka pia. Mnyama hakuwa huru
isipokuwa kufanya kile mwangalizi wake anachokitaka.

Yesu anaweka nira YAKE juu yetu, ili mizigo


yetu iwe rahisi kuibeba. Kwa upande
mwingine, tunajikabidhi kwenye mapenzi
Yake kwa kuipokea nira Yake, na ndipo
tunajifunza kufanya kwa namna anayotaka
tufanye.
Tunakuwa washirika na Kristo kwa kujitia
nira Yake. Tuna kazi ya kufanya Naye na
kwa ajili Yake.
“Uko salama ikiwa tu, utajitoa kwa
ukamilifu na utii, ujiunganisha mwenyewe
na Kristo. Nira ni nyepesi, kwa kuwa Kristo
anabeba mzigo. Unapoubeba mzigo wa
msalaba, utakuwa mwepesi; na msalaba
huo kwako ni ahadi ya uzima wa milele. Ni
fadhila kwa kila mmoja kwa furaha
kumfuata Kristo.”
E. G. W. (Sons and Daughters of God, March 15)
Paulo aliandika kwamba Yesu ni mpole (2Kor. 10:1), kama
Musa (Hes. 12:3). Upole ni tunda la Roho Mtakatifu
(Gal. 5:22-23). Kila muumini anapaswa kutenda kwa upole
(Kol. 3:12; 1Tim. 6:11; Tit. 3:2).
Upole na unyenyekevu wa Yesu haukumanisha kwamba
hawezi kujibu kwa uwazi mbele ya wapinzani Wake.
Alitenda kwa upole na hakulazimisha matakwa Yake kwa
nguvu.

Unyenyekevu Wake ulikuwa wazi pale alipijitoa ili asulubiwe


(Filp. 2:8). Akawa Mwokozi wetu. Alikuwa Yeye pekee awezaye kutuweka
huru na mzigo wa dhambi, kupunguza maumivu yetu, na kutupatia
pumziko la nafsi zetu.
Nira zimekuwa zikitumika kama ishara ya utumwa na
utumikishwaji.
Katika muktadha huu, tunaweza kuona nira ambazo
ni nzito na ziletazo utumwa. Kwa mfano, tohara
(Matendo 15:10) au wokovu kwa matendo (Gal. 5:1).

Tofauti na nira hizo, nira ya Yesu ni nyepesi kubeba. Nira Yake ni ishara ya
“sheria ya uhuru” (Yakobo 2:12). Tutakapofahamu kuwa la amri za Mungu,
siyo “nzito.” (1Yn. 5:3).

Yesu hutushikilia pale tunapokuwa


tumefunikwa kwa haki Yake na kutembea
pamoja Naye. Hutuinua tunapoanguka na
kutuongoza katika haki.
Nira daima zilivaliwa na wanyama wawili, kwahiyo ilipunguza
kazi ya mmoja mmoja. Ikiwa mmoja wa wanyama hao alikuwa
dhaifu, mwingine angemsaidia kwa nguvu zake.
Yesu ndiye mwenye nguvu, na tunaweza kumwamini.
Anafanya mzigo uwe mwepesi kwetu.
Yesu ni kielelezo chetu. Yethro alimfundisha Musa kugawana mzigo
na wengine (Kut. 18:13-22), inatupasa pia kuwasaidia wengine:
“Mchukuliane mizigo na kuitimiza sheria ya Kristo.” (Gal. 6:2)
Kuwabebea wengine mizigo inamanisha
kuwarejesha wale wanaoanguka,
kusaidiana sisi kwa sisi katika nyakati
ngumu, kusaidiana na wengine...
Kubebeana mizigo ni jamba ambalo
Mungu ametuamuru sisi kama Kanisa.
Inahitaji upole na inaleta huruma.
E. G. W. (SDA Bible Commentary, book 5, on Matthew 12:29, p. 1092)

“Kujitia nira pamoja na Kristo, humanisha kufanya


kazi katika njia Zake, kuwa mshirika Naye katika
mateso na maumivu kwa wanadamu waliopotea.
Inamanisha kuwa mwalimu mwema wa roho. Kristo
atatufanya vile tutakavyo katika hizi saa nzuri za
majaribia. Tutakuwa vyombo viteule ikiwa tutakubali
kufanywa hivyo. Inatupasa kuungana na Mungu katika
kazi ya ya kutengeneza, bia zetu zikiwa zimewasilishwa
katika mapenzi ya kiungu.”

You might also like