You are on page 1of 5

“ Siku moja nilipokuwa kwenye gari langu nikiendesha kutoka Morogoro kupelekea Daresalaam.

Nikiwa maeneo ya Msamvu Morogoro, gafla polisi mmoja alinisimamisha nami nikapaki gari
yangu pembeni. Yule polisi alionekana akiwa na mtu mmoja hivi,alikuwa akionekana wakiongea
na bila shaka walikuwa wakifahamiana. Nami nilikuwa peke yangu ndani ya gari.

Kabla sijashuka na kumfuata polisi pale alipokuwepo na yule mtu,wao wakawa wameshafika na
tukasalimiana. Kisha yule polisi akaniambia “basi bhana maana nilitaka nikuombe lifti kwa ajili
ya ndugu yangu huyu maana anakwenda pia Dar-es-salaam, lakini hata hivyo naona mmejaa
sana humo na yeye hawezi kukaa maana hakuna nafasi…sawa asante”.

Sasa mimi nilishangaa vile asemavyo polisi kwamba tumekaa kwenye gari wakati mimi nilikuwa
peke yangu. Lakini nami nikamuitikia “sawa boss wangu,haya kazi njema” nami ikaendelea na
safari yangu. Kumbe nilizungukwa na ulinzi wa Bwana, malaika walinizunguka na kufanya
kituo. Labda ningempokea yule mtu,tungelipata na majanga huko mbele ya safari yangu lakini
Mungu akanilinda kwa njia ya utiisho wa malaika. ” Mtumishi mmoja alikuwa akisimulia
hayo.

Kumbe kuna umuhimu mkubwa sana wa kujifunza kuhusu malaika na huduma zao kwetu sisi
wapendwa wa Bwana. Ikiwa biblia imewataja malaika mara nyingi,basi lazima kutakuwa na
mambo mengi ya kujifunza kuhusu malaika maana haiwezekani wakatajwa tu alafu ikawa basi,
kuna jambo la kujifunza hapo. Na inawezekana kabisa ukawa na maswali mengi kuhusu malaika
maana somo la huduma za malaika ni adimu sana, sishangai ukiwa na maswali kama vile;
Advertisements
REPORT THIS AD

Hivi malaika ni akina nani? Au malaika wapo kweli hata siku za leo? Wanafanya kazi gani? Je
malaika wanaonekanaje? Hivi wanaongea,kama ndio wanaongea lugha gani? Inanisaidia nini
kujua mambo ya malaika? Je tunapaswa kuwasujudia malaika? Hivi,…na hivi… Eti malaika
akija mimi nitaijuaje sasa? Je mambo ya malaika si ya Mungu mwenyewe, kuna mahusiano gani
na mimi? N.K

Hivyo nikili wazi kwamba sina uwezo wa kukufundisha mambo ya ndani hasa yahusuyo malaika
bali ninajaribu kufundisha sehemu tu, maana hata mimi mwenyewe sijui mambo haya magumu.
Lakini kwa mujibu wa neno la Mungu katika biblia najaribu kuelezea kama ilivyoandikwa.
Usomapo ujumbe huu muombe Roho mtakatifu akusaidie upatekuelewa zaidi ya haya yote.

Lakini usiwe na haraka sana, taratibu utaelewa huduma za malaika kwa watakatifu. Kusema
ukweli hili ni mojawapo ya somo ambalo limebeba vitu vingi sana,nami mpaka ninaogopa
kukuandikia. Nami nimejisikia nikujuze machache tu. Lengo kubwa la somo hili ni;

1. Uweze kuelewa huduma za malaika


2. Uongeze ufahamu wako wa kiimani.

Ijapokuwa tutajifunza kwa ufupi,basi hatuna budi kujifunza mambo muhimu yafuatayo;

1. Malaika ni akina nani?


2. Je kuna aina ngapi za malaika?
3. Je malaika waliumbwa?
4. Je tunapaswa kuwaabudu au kuwasujudia?
5. Malaika wapo wangapi?
6. Je wanatumia lugha katika kuwasiliana wao kwa wao?
7. Mifano iliyo hai ya malaika akiwatokea watu.
8. Mazingira yanayowavutia malaika hata kuhudumu. N.K

01. MALAIKA NI NANI?

Neno hili lina asili ya lugha ya Kiyahudi “ malaak” na Kiyunani “Aggees” kiingereza tunasema
“angel” maneno hayo yana maana moja tu. Neno la kiasili kutoka katika lugha ya Kiyahudi na
Kiyunani inaeleza neno malaika kuni ni “ mjumbe”. Mjumbe huyu ni mjumbe wa Mungu. Na
wakati mwingine biblia inaeleza kuwa malaika ni mjumbe wa kawaida ( ordinary messenger) wa
kibinadamu. Kwamba yeyote aliyetumwa na Mungu ni mjumbe mfano Yohana mbatizaji
alikuwa “mjumbe” aliyetumwa na Mungu kuitengeneza njia ya Bwana kwa ajili ya utangulizi wa
Yesu Kristo ( Mathayo 11:10)

Hivyo,wale wote waliotumwa na Bwana ni wajumbe wa Mungu,na ndio maana tukiona, Ufunuo
wa Yohana ukiwataka ni malaika ( tazama malaika wa yale makanisa saba Ufunuo sura 2 na sura
ya tatu) tazama;

“Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika;…” Ufunuo 2:1a

Malaika anayetajwa hapo ni mtu aliyepewa dhamana na Mungu kusimamia kanisa la Bwana mtu
huyo ameitwa ni mjumbe wa Mungu (malaika). Hata wewe uliyekuwa kusimamia kazi ya Bwana
ni mjumbe wa Mungu ni malaika.Yesu Kristo anajulikana pia kuwa ni mjumbe wa agano jipya
(He is the great angel of the new covenant) ( Malaki 3:1).

“Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,


Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,
Mkiisikiliza sauti ya neno lake.” Zaburi 103:20

Tazama kwa makini andiko hilo hapo juu na utagundua kwamba Mungu anasema na watu ambao
ni watumishi wa Mungu akiwataka wote kwa pamoja mimi na wewe tumsifu Bwana. Neno
malaika hapo linaelezea nafsi ya mtu. Wewe pia ni malaika wa Bwana na ndio maana katika
tenzi namba 7 (Ni tabibu wa karibu) katika kiitikio chake huwa tunaimba hivi;

“ Imbeni , malaika,

Sifa za Yesu Bwana

Pweke(pekee)limetumika;

Jina lake Yesu.”


 Maana ya pili ya neno “malaika” yenye taswira hope ile ya neno “mjumbe” Tuanze na
andiko hili;

“Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,


Uketi mkono wangu wa kuume
Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”
Waebrania 1:13-14

Andiko hili linaeleza katika wepesi wa kuelewa kwamba malaika ni roho watumikao wakitumwa
na Mungu kuwadumia wale watakao urithi wokovu/umilele. Kwa kuwa ni roho basi hawana
jinsia ya kike wala kiume kwa maana wao si binadamu ( Mathayo 22:30)

Biblia inawataja malaika katika majina tofauti tofauti kama ifuatavyo;

1. Jeshi/majeshi yaliyo mengi.( Soma Mathayo 26:53,Luka2:13,Waebrania 12:22-23,


Daniel 7:10)
2. Roho zenye nguvu zaidi ( 2 Petro 2:11, Ufunuo 5:2,18:21,19:17)
3. Roho zinazoweza kufanya kazi kwa haraka zaidi (Waamuzi 13:20, Daniel 9:21, Mathayo
13:49 n.k)
4. Wajumbe wa roho watumwao na Mungu ( Zaburi 91:11, Waebrania 1:14)

02. AINA ZA MALAIKA.

Lengo kubwa si kutaja majina ya malaika bali kujua kwamba malaika wamegawanyika namna
gani kwa mujibu wa kweli ya neno la Mungu. Biblia imejibu swali hili vyema kabisa. Hivyo
tunazijua aina zao ni kama ifuatavyo;

1. Malaika wa nuru/ wa Mungu( Zaburi 91:11-12, Mwanzo 2:1 n.k)


2. Malaika walioasi/malaika wa giza/maana shetani naye alikuwa mmoja wa
malaika,akaasi. (2Petro 2:4, Mathayo 25:41, Ufunuo 12:19 n.k)

Jambo moja ambalo unapaswa kulijua ni kwamba, malaika hajapewa nafasi ya kutubu kama
ulivyopewa wewe na mimi leo, bali wao wakiasi hutupwa na kumtumikia shetani. Hivyo basi
itumie vizuri nafasi iliyopewa na Mungu ukiomba toba.

Malaika wapo wengi sana kiidadi, lakini mimi nitawazungumzia wachache kama si wawili
ambao tunawasoma mara nyingi katika habari njema ( injili) na biblia nzima. Nao ni kama
ifuatavyo;

01. Malaika wa habari njema.

Jina la malaika Gabriel ndie malaika mkuu wa shirika la utangazaji wa habari lenye makao yake
huko mbinguni.gā´bri -el Kiyahudi ni ( ‫ גּבריאל‬, gabhrı̄ ’ēl ,) neno Gabri maana yake ni “mtu au
mjumbe” na neno “ elimu” maana yake ni “Mungu” hivyo ni “mtu/mjumbe wa Mungu” Tunaona
Gabriel akiwatokea wachungaji na kuwapasha habari njema za kuzaliwa kwa mwokozi wa
ulimwengu (Luka 2:8-10). Habari zake pia zimeandikwa ( Daniel 8:16-2, Luka 1:19,26,
Matendo 27:23-26, Daniel 9:20-23 N.K)

02. Malaika wa kusifu na kuabudu.

Actually,kazi kuu ya malaika wote ni kazi ya kusifu na kuabudu na ndio kazi yetu sote mimi na
wewe. Kundi hili la malaika wa kusifu na kuabudu ukuu wa Mungu linafanya kazi huko
mbinguni lakini pia hapa duniani pamoja nasi wakati tunapozama kusifu na kuabudu. “wingi wa
jeshi la mbinguni,wakimsifu Mungu...” Luka 2 :13.

Wakati wa ibada zetu za sifa na kuabudu ndio wakati ambapo Mungu pamoja na malaika zake
hushuka ( Zaburi 22:3) kwa kuwa Mungu huketi kwenye sifa za watu wake. Hivyo, kilele cha
ibada hakipo kwenye neno bali kipo kwenye sifa na kuabudu. Na ili ibada iwe kamilifu ni lazima
ipambwe na sifa na kuabudu kutoka rohoni maana hapo ndipo Mungu uwatafuta watu kama hao
wamuabuduo katika roho na kweli ( Yohana 4:23) soma; ufunuo 5:1-14,Isaya 6:yote,Zab.80:1
N.k

03. Malaika wa ulinzi.

Wakiongozwa na kamanda amiri jeshi mkuu Mikaeli “ lakini Mikaeli, malaika mkuu,…”
Yuda1:9. Yeye Mikaeli ndiye jemedari Mkuu wa usalama na ulinzi. Maana malaika wa Bwana
hufanya kituo na kutuzungukia watakatifu ( Zaburi 34:7). Wakati Daniel akiomba malaika wa
habari Gabriel alikuja kumpasha habari juu ya kuomba kwake. Lakini tunaona akazuiliwa huyo
malaika na mkuu wa uajemi,ndipo malaika mkuu wa ulinzi, Mikaeli akapambana hata Gabriel
akamfikishia majibu Daniel kwa kuomba kwake,soma Daniel 10:11-21,11:1).Ni Mikaeli na
malaika zake waliopambana na ibilisi yule joka wa zamani hata wakamshinda na ibilisi
akatupwa hata nchi ( Ufunuo 12:7-11). Soma pia Yoshua 5:13-14

03. JE MALAIKA WALIUMBWA?

Kwa mujibu wa neno inaonesha wazi kabisa kwamba malaika waliumbwa maana biblia
inasema;``Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.” Mwanzo 2:1 kumbuka, malaika
wanaitwa pia ni jeshi kubwa la mbinguni. Lakini neno hili “jeshi” kama lilivyo tumika katika
Mwanzo 2:1 halimaanishi kwamba ni malaika pekee ndio waitwao jeshi bali vitu vyote
vilivyoumbwa ni jeshi la BWANA Yeye Mungu akiwa ndiye mume Bwana Mungu wa majeshi.
Lakini pia tena tunasoma ;

“Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka;
vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.” Wakolosai 1:16

Biblia inasema kwamba hakuna kitu kisichokuwa na Mungu isipokuwa Yeye Mungu tu
hakuumbwa. Hata shetani aliyekuwa rusifa aliumbwa kama malaika wa sifa.

04.JE TUNAPASWA KUWAABUDU AU KUWASUJUDIA?


Yule tunayepaswa kumuabudu ni BWANA MUNGU tu. “ …kwa maana imeandikwa, Msujudie
Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Mathayo 4:10 & Kumb.6:13 wala hatutakiwi
kuomba kwa majina yao bali kila mmoja na aombe katika kina Bwana Yesu Kristo tu (Yohana
14:13-14,2:5)

Hivyo haitakiwi kuomba kwa majina yao, biblia inaeleza tena “ Nami nikaanguka mbele ya
miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu
zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho
ya unabii.” Ufunuo 19:10 soma tena ufunuo 22:8-9.

Maandiko hayo yanatuambia kwamba tusidhanie kwamba kila mmoja wetu anamalaika mlinzi
katika maisha yetu. Ulinzi wetu upo katika damu ya Yesu Bali malaika wanatuhudumia kila siku
kwenye mambo mengi ( Mathayo 18:10, Luka 16:22)….

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.

Kwa msaada zaidi, ushauri na maombezi + 255 683 877 900

You might also like