You are on page 1of 52

1

PONA KWA NENO LA MUNGU KWA


NENO LA MUNGU

Sehemu ya Kwanza

HOMA
IKAMWACHA

FRANCIS M. LANGULA

2
Haki zote zimehifadhiwa
Hairuhusiwi kwa namna yoyote ile kunakili au kudurufu sehemu ya
kitabu hiki, kuuza au kusambaza kitabu hiki bila idhini ya mwandishi,
kwani kufanya hivyo ni ukiukwaji wa haki za mwandishi.

Chapa ya kwanza 2022


© Hakimiliki, Francis M. Langula
+255754711247 au +255717123348
francis.langula@gmail.com
facebook: @mwl.francislangula
Android App; http://langula.xyz/francis
Telegram: https://t.me/neno_na_pst_francis

Kimesanifiwa na Kuchapishwa na;


TANZANICE COMPANY
Dar es Salaam, Tanzania
Mob: +255 653 409 946
Email:kaswidecom@gmail.com

3
4
YALIYOMO

UTANGULIZI ................................................................................... 7
Kuhusu Pona kwa Neno la Mungu .................................... 7
Kuhusu Homa Ikamuacha .................................................... 7
Sehemu Ya Kwanza ...................................................................... 9
HOMA IKAMWACHA, AKAPONA ................................ 9
Homa, dalili ya ugonjwa ...................................................... 11
Homa, kitu halisi kabisa, ndio chanzo cha mateso .. 13
Ameshikwa na homa kali .................................................... 13
Sehemu Ya Pili ............................................................................. 16
SIRI AMBAZO ZA KUPONYA NA KUHUDUMU
UPONYAJI .................................................................................. 16
Siri ya 1: Jitofautishe na ugonjwa.................................... 19
Siri ya 2: Ugonjwa (Magonjwa) ni kitu hai na halisi
chenye uwezo wa kusikia na kuelewa .......................... 24
Siri ya 3: Homa (ugonjwa) ni mgeni asiye na uhalali
kukaa katika mwili wako ..................................................... 34
Siri ya 4: Ugonjwa haubembelezwi kuondoka ........... 39

5
Sehemu Ya Tatu........................................................................... 42
UMEPEWA MAMLAKA ..................................................... 42
Nini maana ya kukemea? ................................................... 42
Tumepewa mamlaka ............................................................ 43
Tamka ukiwa na NIA MOJA TU ......................................... 45
Chukua hatua sasa................................................................. 47
HITIMISHO .................................................................................... 50

6
UTANGULIZI

KUHUSU PONA KWA NENO LA MUNGU

Kitabu hiki kinachoenda kwa jina la HOMA


IKAMUACHA, ni kitabu cha kwanza katika
mfululizo wa mafundisho ya PONA KWA NENO
LA MUNGU.

Lengo hasa la mafundisho katika mfululizo huu


wa vitabu vya PONA KWA NENO LA MUNGU, ni
mtu wa Mungu kujifunza uponyaji wa Kiungu
kutoka kwenye Neno la Mungu kwa kiwango
ambacho imani ya mtu huyu kuhusu uponyaji
itainuliwa na kuimarika hata kufika mahali pa yeye
mwenyewe, kama ni mgonjwa aweze kuamini
kuhusu uzima na uponyaji kwa kiwango ambacho
anapokea uponyaji wake, au ikiwa si mgonjwa,
aweze kumuamini Mungu anayeweza kumtunza
katika afya kamilifu bila kushambuliwa na
magonjwa, lakini pia aweze kuwafundisha na
kuwahudumia watu wengine uponyaji.

KUHUSU HOMA IKAMUACHA


Katika kitabu hiki cha HOMA IKAMUACHA,
tutajifunza siri ambazo zinaweza kutusaidia
kupona kama tunaumwa au kuhudumu uponyaji
kwa wagonjwa.
7
Neno ‘homa’ kwenye kitabu hiki linasimama
badala ya ugonjwa wowote. Nimetumia homa
ikamuacha kwa sababu ya andiko letu la msingi
ambalo ndio tunapatia ufunuo wa fundisho hili.
Kama wewe ni mgonjwa au unatamani
kuhudumia watu uponyaji, soma kitabu hiki kwa
umakini mkubwa, lakini pia kama una mtu ni
mgonjwa hakikisha anapata mafundisho ya kitabu
hiki na ninaamini yatamfaa sana.

Unaposoma na kujifunza kitabu hiki, ninakushauri


kama inawezekana usome tena na tena, wakati
unafanya hivyo ni rahisi kupata kile ambacho
kimekusudiwa kwa ukamilifu wake na imani yako
itainuka au kuimarika na utapokea kila
kilichokusudiwa na Roho Mtakatifu katika kuuleta
ufunuo huu muhimu kuhusu afya na uponyaji.
Karibu tujifunze na kufurahia uponyaji na afya
kwa Neno la Mungu.

8
Sehemu Ya Kwanza

Homa Ikamwacha, Akapona

Nitanukuu maandiko matatu ambayo yote


kimsingi yanaongelea jambo moja lakini
yameandikwa na waandishi tofauti. Tutasoma
maandiko ambayo ameandika Mathayo, Marko
na Luka ambayo yote yanaeleza uponyaji wa
mama mkwe wa Petro, lakini kuna namna tofauti
wameandika ambayo inaweza kutusaidia kupata
ufunuo tofauti.

Mathayo 8:14-17
[14] Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro,
akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe,
amelala kitandani hawezi homa. [15]Akamgusa
mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka,
akawatumikia. [16]Hata kulipokuwa jioni,
wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo
kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa
hawawezi, [17]ili litimie lile neno lililonenwa na
nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu
wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

9
Yesu anafika nyumbani kwa Petro, anamkuta
mama mkwe wa Petro, yaani mama wa mke wa
Petro akiwa ni mgonjwa, ana homa. Yesu
akamuwekea mikono Yule mama, HOMA
IKAMUACHA, mama mkwe wa Petro akaondoka
akawatumikia au kuwahudumia.

Marko 1:31 “Akamkaribia, akamwinua kwa


kumshika mkono, homa ikamwacha,
akawatumikia.”

Kwenye hili andiko pia unaona neno “HOMA


IKAMUACHA, akawatumikia” linarudia tena.

Luka 4:38-39
[38] Akatoka katika sinagogi, akaingia katika
nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni,
mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na
homakali, wakamwomba kwa ajili yake.
[39] Akasimama karibu naye, akaikemea ile
homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka,
akawatumikia.

Luka, ambaye alikuwa ni Tabibu (Daktari), naye


anaelezea habari ile ile. Ukifuatilia masuala ya
uponyaji na magonjwa kwenye vitabu vya injili,
utagundua Luka alikuwa anaelezea uponyaji na
magonjwa tofauti na waandishi wengine kwa
sababu ya taaluma yake ya utabibu.

10
Tafsiri ya kingereza ya andiko hilo la Luka
inasema “The fever left her, and she was healed”
yaani “homa ikamuacha, akapona”.

Kwa maandiko hayo tuliyosoma, ni wazi kabisa,


‘homa’ ilikuwa ni kitu halisi na ndio ilikuwa chanzo
cha mateso ya huyu mama mkwe wa Petro.

Homa, dalili ya ugonjwa

Kwa ambao tunafahamu kidogo masuala ya


magonjwa na utabibu, kimsingi homa sio ugonjwa
wenyewe bali homa ni dalili ya nje ambayo
inaashiria kwamba kuna ugonjwa ndani ya mwili.
Ninachoamini ni kwamba, kwenye kesi hii, kwa
sababu hakukuwa na vipimo vyovyote
vimefanyika, kilichokuwa kinaonekana nje na
kuhisiwa kwa huyu mama ilikuwa ni homa kali, na
anaposema homa ikamuacha, maana yake
kilichomuacha sio tu homa (ambayo ni dalili ya
nje), bali kile kilichosababisha homa pia
kiliondoka na ndipo huyu mtu akawa mzima.
Kwa hiyo, tunaposema homa kwenye kitabu hiki,
tunamaanisha dalili za nje (zinazoonekana) za
ugonjwa pamoja na chanzo halisi cha hizo dalili
au ugonjwa. Kwa zama hizi tulizopo, tunajua
kwamba, mtu akiwa na homa, huwa ni matokeo
au dalili ya nje ya ugonjwa fulani uliopo ndani,
homa yenyewe kimsingi sio ugonjwa au sio
11
chanzo cha ugonjwa bali ni muitikio wa mwili au ni
dalili ya nje. Mwili kuchemka (homa), ni muitikio
wa mwili kwa ugonjwa au tatizo lililopo ndani ya
mwili.

Maandiko yanasema wazi huyu mtu alishikwa na


homa kali, lakini hatujui hii homa ilisababishwa na
nini; inawezekana ndani yake kulikuwa na
ugonjwa mwingine mkubwa au mdogo
uliosababisha homa.
Kwa sababu, mtu mwenye maambukizi ya
bakteria (bacterial infection) kwenye mwili,
anaweza kupata homa, mtu mwenye shida ya
kwenye ubongo, anawaeza akapata homa, wakati
mwingine malaria, typhoid au ugojwa mwingine
wowote ndani ya mwili unaweza ukasababisha
homa. Ninachotaka uone hapa ni kwamba, homa
ni dalili au matokeo ya nje kwa ugonjwa au jambo
ambalo linaendelea ndani ya mwili.

Kwa hiyo, huyu mama inawezekana alikuwa na


tatizo kubwa ndani yake, ambalo kwa nje
lilisababisha akawa na homa kali, kama ambavyo
Luka ameeleza kwamba huyu mama alishikwa na
homa kali akawa hawezi. Homa ilikuwa kali
kiwango ambacho alilala kitandani hawezi kabisa
kuinuka.

12
Kwa hiyo, kwa lugha ya sasa na kwa ambayo
nimeyasema, homa inaweza kusimama badala ya
ugonjwa wowote.

Homa, kitu halisi kabisa, ndio chanzo cha


mateso

Maandiko hayo tuliyosoma yanadhihirisha wazi


kabisa kwamba, homa ilikuwa ni kitu halisi kabisa
na ilikuwa chanzo cha mateso ya huyu mama.
Maandiko yanaonesha wazi kwamba, kuna tofauti
ya wazi kabisa (clear distinction) kati ya homa na
mtu, au kati ya ugonjwa na mtu kama ambavyo
tutajifunza mbele.
Lakini pia unaona, Homa au ugonjwa uliingia
ndani ya mtu na kumfanya huyu mtu kuwa
mgonjwa.

Ameshikwa na homa kali

Homa ni kitu kingine na mtu ni kitu kingine.


Kulikuwa na tofauti ya wazi kati ya ugonjwa na
mtu ndio maana maandiko yanasema katika Luka
4:38 "...alikuwa ameshikwa na homa kali..."

Kwa hiyo, kulikuwa na kitu halisi kinaitwa homa,


ambacho kilikuwa kimemshika. Ni kama vile
useme, mtoto ameshikwa na mama yake, maana
13
yake kuna watu wawili, kuna mama na kuna
mtoto. Ndivyo Neno linasema, huyu mama mkwe
wa Petro, alikuwa ameshikwa na homa, kulikuwa
na kitu halisi kinaitwa homa kimemshika, hii
inadhihirisha wazi kwamba kuna utofauti wa wazi
kabisa kati ya homa na mtu au kati ya ugonjwa na
mtu.

Na hapa ndio tunazipata siri nyingi za uponyaji


ambazo zinaweza kumsaidia mtu yoyote mwenye
ugonjwa aina yoyote kupona, na anayetaka
kuhudumu uponyaji kuweza kuhudumu.

Lengo la mafundisho haya ni kwa watu ambao ni


wagonjwa wapone, lakini pia kwa wale
wanaotamani kuwahudumia watu wengine
uponyaji waweze kuwahudumia uponyaji. Zama
hizi tulizo nazo ni zama za uponyaji, ni zama
ambazo Mungu anajidhihirisha kwa kiwango
kikubwa cha kuponya ili kuuthibitishia ulimwengu
kwamba, yuko Mungu aliye hai anayeweza
kuponya hata yale ambayo yamewashinda
madaktari, ili kugeuza mioyo ya watu wajue
kwamba, kuna Mungu ambaye yuko juu ya
teknolojia. Pamoja na kwamba kuna teknolojia
nyingi za masuala ya utabibu, lakini bado kuna
magonjwa ambayo hayatawezekana kwa
teknolojia, na unahitajika mkono na nguvu za
Mungu za kuponya.

14
Unapoendelea kujifunza, pokea uzima ikiwa
wewe ni mgonjwa, lakini pokea upako na neema
ya kuponya wagonjwa na kumdhihirisha Kristo
aponyaye.

15
Sehemu Ya Pili

SIRI AMBAZO ZA KUPONYA NA


KUHUDUMU UPONYAJI

Kila andiko lina siri nyuma yake

Neno la Mungu ni fumbo, kila andiko unalolisoma,


lina fumbo ambalo linahitaji Roho Mtakatifu
atusaidie kulifumbua (ufunuo) ili tuweze kufaidika
na Neno hilo. Hili neno ambalo unaweza ukaliona
ni kama dogo kabisa linalosema “homa
ikamuacha”, lina fumbo kubwa ndani yake
ambalo Neno la Mungu linasema “Roho Mtakatifu
huyafumbua mafumbo ya Mungu”. 1 Wakorintho
2:10-13.

Kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu ni kutufumbulia


mafumbo, na fumbo ambalo halijafumbuliwa
haliwezi kutusaidia; namaanisha andiko ambalo
halijafunuliwa au ambalo haujaupata ufunuo ulio
ndani yake haliwezi kukusaidia sana. Andiko
ambalo umepata ufunuo uliojificha ndani yake
ndilo linaweza kukusaidia. Ndio maana Daudi
anaomba anasema katika Zaburi 119:18
16
“Unifumbue macho yango niyatazame maajabu
yatokayo katika sheria yako [Neno lako]”,
ikionyesha wazi, kwenye Neno la Mungu kuna
maajabu (miujiza) ambayo kama hatutafumbuliwa
macho hatuwezi kuyaona.

Ndivyo ilivyo, hili neno ambalo linaonekana ni


rahisi sana linasema “homa ikamuacha”, lina
fumbo kubwa ndani yake ambalo tukilifumbua
kwa hakika tutaona limebeba uponyaji na uzima
ndani yake.

Kila habari ya uponyaji aliofanya Yesu


iliyoandikwa naweza kusema ni fumbo; maana
yake kuna siri nyingi ndani yake ambazo
zinaweza kutufundisha mambo makubwa sana
kuhusu uponyaji na kuhudumu uponyaji.
Ninaamini hata andiko hili, lengo halikuwa tu
kuweka kumbukumbu (record) ya mtu kupona
homa, kwa sababu kama ndivyo, homa ni kama
vile kitu kidogo tu, na Yesu amefanya miujiza
mingi sana mikubwa; kwa hiyo ukiona muujiza
umeandikwa (umerekodiwa), ujue kuna fumbo au
siri kubwa za kujifunza.

Maandiko yanasema kuna mambo mengi sana


ambayo Yesu alifanya na hayakuandikwa, kwa
sababu yangeandikwa kusingekuwa na nafasi ya
kutosha (Yohana 21:25), maana yake ni kwamba
yale yaliyoandikwa yana ujumbe zaidi ya ule
17
ulioandikwa, yana siri nyingi nyuma yake zaidi ya
kile tu kilichoandikwa.

Kwenye sehemu hii, nataka tuziangalie hizi siri


ambazo Roho Mtakatifu amezifunua kwetu
zinazohusiana na uponyaji ambazo zinaweza
kutusaidia kupona na kuhudumu uponyaji. Wewe
ambaye ni mgonjwa, bila kujali unaumwa
ugonjwa gani, iwe ni kansa, au ukimwi, au
kisukari, vidonda vya tumbo, pressure au
ugonjwa wowote unaopona au usiopona, au
wewe ambaye unataka kuhudumu uponyaji kwa
wagonjwa, zingatia hizi siri za muhimu sana ili
uanze kuona matokeo ya uzima na afya
unaotokana na Neno la Mungu.

18
Siri ya 1:

Jitofautishe na ugonjwa

Wewe ambaye ni mgonjwa, lazima kwanza


ujitofautishe na ugonjwa, lakini pia ikiwa
unamuhudumia mtu uponyaji, mtofautishe mtu
unayemuhudumia na ugonjwa; anza kumuona
mtu na ugonjwa ni vitu viwili tofauti,
usivichanganye. Weka msitari kati yako na
ugonjwa.

Luka 4:38-39
[38] Akatoka katika sinagogi, akaingia katika
nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni,
mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na homa
kali, wakamwomba kwa ajili yake.
[39] Akasimama karibu naye, akaikemea ile
homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka,
akawatumikia.

Siri ya kwanza ya uzima ni kujitofautisha na


ugonjwa, hata kama unaumwa, anza
kujitofautisha wewe na ugonjwa. Wewe sio
ugonjwa; unajua kuna mtu ameumwa mpaka
amejiunganisha na ugonjwa, yaani anajihisi kama
yeye ni ugonjwa na ugonjwa ni yeye kwa sababu
amekaa kwenye hali ya ugonjwa kwa muda mrefu

19
sana. Habari njema ninayokuletea leo ni kwamba,
wewe sio ugonjwa wala wewe sio mgonjwa.
Ninasisitiza kwamba, Wewe sio ugonjwa, wala
wewe sio mgonjwa, isipokuwa kuna kitu halisi
kinaitwa Homa (Ugonjwa) kimekushika ndio
kinakufanya ujisikie hivyo unavyojisikia, na hicho
kitu kinaweza kukuacha ukabaki wewe uliye na
afya yako.

Kama una ugonjwa wowote na umeelewa vizuri


ulichojifunza mpaka hapa, unaweza ukajiambia
kwa ujasiri kwamba:

“Mimi sio ugonjwa na wala mimi sio


mgonjwa, isipokuwa kuna kitu halisi
kinaitwa ugonjwa ambacho kimenishika na
hicho ndio kinanifanya nijisikie hivi
ninavyojisikia, na hicho kitu kinaweza
kabisa kuniachia nikabaki mimi niliye na
afya yangu nzuri, na kwa jina la Yesu leo
hicho kitu kinaniachia”

Angalia hayo maandiko yanavyosema kwamba


huyu mama mkwe wa Petro alikuwa “Ameshikwa
na homa kali…” halafu Yesu “…akaikemea ile
homa, ikamuacha”, kwa hiyo kulikuwa na mama
mkwe wa Petro upande mmoja na Homa
(ugonjwa) upande mwingine, kwa hiyo huyu
mama hakuwa ugonjwa wala hakuwa mgonjwa,
isipokuwa kulikuwa na kitu halisi kinaitwa ‘homa’
20
kikatoka upande wake, kikaenda na kumshika au
kumuingia, kilipomuingia na kushikamana na
yeye ndipo huyu mama akaanza kujisikia homa
na kujihisi mgonjwa na akawa na hali hiyo
iliyoelezwa kwenye maandiko.

Ndivyo ilivyo hata kwako, wewe si ugonjwa wala


wewe sio mgonjwa isipokuwa kuna kitu halisi,
kinaitwa ugonjwa, kilikuwa mbali nawe, kikaja
kikashikamana na wewe ambaye ulikuwa ni
mzima kabisa, kiliposhikama na wewe
kikakufanya uwe na hali hiyo ya ugonjwa.

Wewe unaweza, ugonjwa ndio hauwezi

Ukweli ni kwamba wewe unaweza kutembea


vizuri, isipokuwa kuna kitu kingine kinaitwa
ugonjwa, na hicho kitu moja ya sifa zake hakina
uwezo wa kutembea vizuri, kilikuja kikashikamana
na wewe (mwili wako) halafu hicho ndio
kikakufanya ushindwe kutembea lakini wewe
halisi unaweza kutembea.
Wewe hauna maumivu, isipokuwa kuna kitu
kingine kilikuingia ndio kikakufanya uhisi hayo
maumivu; wewe hauna uvimbe, isipokuwa kuna
kitu kingine, chenye huo uvimbe kiliingia ndani
yako na kuweka huo uvimbe ndani yako.

Hii ndio siri ya kwanza muhumu sana ya kupokea


uzima ambayo lazima uidake, kwamba “wewe sio
21
mgonjwa, isipokuwa kuna kitu kingine ndio
kimesababisha ujisikie hivyo unavyojisikia”; ni
lazima ujitofautishe wewe na ugonjwa.

Hata kama unasikia maumivu kiasi gani,


hakikisha unajitofautisha wewe na maumivu au
ugonjwa.

Kilichomzuia huyu mama kuwatumikia ni kitu


kinaitwa homa, kilichomlaza kitandani huyu mama
ni kitu halisi kinaitwa homa. Huyu mama alikuwa
anaweza kabisa kumtumikia Yesu, huyu mama
alikuwa hatakiwi kabisa kulala kitandani lakini
kuna kitu kingine kinachoitwa homa ndicho
kilimlaza kitandani na ndicho kilimzuia kumtumika
Yesu.

Neno la Mungu linasema kwenye kitabu cha


Marko 1:42 “Na mara ukoma wake ukamtoka,
akatakasika.”

Maana yake ni kwamba, kulikuwa na kitu halisi


kinaitwa ukoma, ambacho kilimuingia huyu mtu,
ndicho kikamfanya huyu mtu akawa na ukoma,
kile kitu kinachoitwa ukoma kilipotoka, huyu mtu
akatakasika, kwa hiyo, huyu mtu hakuwa mkoma,
mpaka pale kitu halisi kiitwacho ukoma
kilipomuingia, na kilipotoka akatakasika.

22
Tukianza kuyaona magonjwa kwa mtazamo huu,
tutashughulika nayo vizuri zaidi.
Acha kujichanganya wewe halisi na huo ugonjwa,
kwa sababu wewe ni kitu kingine na ugonjwa ni
kitu kingine, Mimi sio ugonjwa wala mimi sio
mgonjwa.

Kama umeelewa na ufahamu huu umeingia ndani


yako piga kelele kwa ujasiri ujiambie

“Mimi sio mgonjwa wala mimi sio ugonjwa”

Kwa hiyo, tangu sasa, hata unapohisi maumivu,


unapoyafikiria maumivu, yaone hayo maumivu ni
kitu kingine tofauti kabisa na wewe.

23
Siri ya 2:

Ugonjwa (Magonjwa) ni kitu hai na halisi


chenye uwezo wa kusikia na kuelewa

Ukishajitofautisha wewe na ugonjwa kama


nilivyoeleza, baada ya kuweka alama ya wazi na
ukajiona wewe tofauti kabisa na ule ugonjwa;
nenda hatua hii ya pili, anza kuuona ule ugonjwa
kwamba ni kitu hai na halisi kabisa. Kwa sababu
ukweli nikwamba ndivyo ilivyo kwamba ugonjwa
ni kitu hai na halisi kabisa.

Kwa lugha nyingine tunaweza kusoma ugonjwa ni


‘mtu’ kwa maana ya ‘person’. Naweza kusema,
ugonjwa una ‘personality’, yaani ni kitu halisi na
hai kabisa chenye ufahamu na uelewa.

Turudi tena kwenye andiko letu la msingi la Luka


4:39 “[Yesu] Akasimama karibu naye, akaikemea
ile homa, [Homa] ikamwacha; mara hiyo [Mama
mkwe wa Petro] akaondoka, akawatumikia.”

Ugonjwa una ufahamu

Unajua kukemea maana yake ni kuzungumza na


kitu, kwa hiyo Yesu alizungumza na homa,
aliikemea homa. Chochote ambacho unaweza
kuzungumza nacho maana yake kina ufahamu
24
(personality), kwa hiyo kina uwezo wa kusikia,
kutembea nk, yaani kinasikia na kuelewa na
kuweza kuitikia.

Anza kuuona ugonjwa ni halisi na uko hai


unaweza kusikia na kuitikia; kwa hiyo, kansa sio
likitu tu lisilo na uhai, kansa sio tu kile
unachoambiwa hospitali, achana na hiyo taarifa
kwanza, twende kwenye sayansi ya kiroho ya
uponyaji.

Hizo vimbe au uvimbe (fibroid) sio tu madamu


damu na manyamanyama yamejikusanya
tumboni, weka hizo taarifa pembeni, sayansi hii
ya kiroho ya afya inatuonesha wazi kwamba,
kansa ni kitu halisi, uvimbe (fibroid) ni kitu halisi
kabisa, maumivu ya kichwa ni kitu halisi kabisa,
kupooza (paralysis) ni kitu halisi kabisa, na kila
aina ya ugonjwa unaoweza kuutaja nihalisi kabisa
chenye masikio, macho, miguu; kinaweza kusikia
na kuelewa, kinaweza kutembea, kinaelewa
kikielekezwa, kina uwezo wa kutii. Anza kuona ni
halisi, acha kuuona huo ugonjwa kwa macho na
akili za kibinadamu kwamba ni upele tu, au ni
uvimbe tu, au ni chakula tu kimesababisha nk.
Achana na hizo taarifa zitakufanya uendelee
kuwa chini ya kifungo cha magonjwa, hizo taarifa
zitakufelisha, huu sio wakati wake, huu ni wakati
wa kuuona ugonjwa ni halisi ili uweze
kuushughulikia ipasavyo.
25
Kansa ni halisi, vidonda vya tumbo ni halisi,
shinikizo la damu (pressure) ni halisi; kwa hiyo
hatua ya kwanza jitofautishe na kujitenganisha
nao, na pili anza kuuona ni kitu halisi kabisa ndio
maana Neno la Mungu linasema “Yesu
akaikemea homa”. Hauwezi kukemea kitu
ambacho hakielewi, ni kama unapomkemea
mbwa na kumwambia “toka”, maana yake
anakusikia na kukuelewa. Hauwezi kuikemea
meza au kiti au jiwe na kuviambia “toka hapa” na
vikaitikia, kwa sababu hivyo vitu havina uhai
(personality); lakini unaweza kumkemea mtu kwa
kumwambia “toka hapa” na akaitikia kwa sababu
yeye ni hai na halisi.

Maandiko haya yanaonesha wazi Yesu hakuwa


anazungumza na mama mkwe wake Petro bali
alikuwa anazungumza na homa; manaa yake
homa inasikia, homa inaelewa na inaweza
kuitikia, ndio maana Neno linasema “Yesu
akaikemea ile homa” kisha unaona tena “Homa
ikamuacha”.
Maandiko hayasemi Yesu akaichukua homa na
kuitoa bali aliikemea homa na kisha “homa
yenyewe ndio ikamuacha”, maana yake homa
yenyewe kwa sababu ina ufahamu, ikaelewa lile
kemeo la Yesu, halafu homa yenyewe ikaanza
kutoka kwa huyu mama na kumuacha.

26
‘Watu’ wawili, Homa na Mama mkwe wa Petro

Luka 4:39 “[Yesu] Akasimama karibu naye,


akaikemea ile homa, [Homa] ikamwacha; mara
hiyo [Mama mkwe wa Petro] akaondoka,
akawatumikia.”

Kwenye hili andiko letu la msingi tunaona


personalities mbili, au watu hai wawili, mmoja
tunamuona ‘Homa’ na wa pili tunamuona ‘mama
mkwe wa Petro”, na tunaona wazi kwamba hawa
wote wawili waliitikia kemeo. Homa iliitikia kemeo
la Yesu na kuchukua hatua ya kuondoka
kumuacha huyu mama, na mara baada ya ile
homa kuchukua hatua ya kumuacha Yule mama,
Yule mama na yeye pia akachukua hatua
(kitendo) ya kuinuka kwenye kitanda na kuanza
kuwatumikia.

Baada ya kuwa umejitenga na ugonjwa, hakikisha


unaanza kuuona huo ugonjwa ni kitu halisi,
chenye uhai, chenye masikio, kinaweza kuelewa.
Kwa sababu homa ilikuwa na ufahamu, ilikuwa
inaelewa, ilikuwa ina miguu ambayo hiyo miguu
iliitumia kumuingia huyu mama na ilitumia miguu
hiyo hiyo kuondoka kwa huyu mama.

Ninaposema homa au ugonjwa una masikio na


miguu nk, ninachofanya ninajaribu kuleta
fundisho hili kwenye lugha yetu ambayo
27
tunaielewa kirahisi; inaweze isiwe miguu kama
tuliyonayo sisi lakini maana yangu ni kwamba,
inaweza ku-move (yaani kuchukua hatua/kuhama
toka sehemu moja kwenda nyingine) kama vile
sisi tunavyoweza kutoka sehamu moja kwenda
nyingine (to move) kwa miguu yetu. Na kama
iliitikia Yesu alichoongea maana yake ilikuwa ina
masikio ambayo ilitumia kusikia, na kama ilisikia
na kutii, maana yake ilikuwa ina uelewa wa
kuelewa kile kinachosemwa. Homa ilikuwa ni
halisi ndio maana Yesu alizungumza nayo.

Wewe ni kitu kingine na ugonjwa ni kitu


kingine chenye uelewa.

Magonjwa yanasikia, magonjwa yanaelewa,


magonjwa yana ufahamu, magonjwa yana miguu
ya kuingilia kwa mtu, yana miguu ya kuondokea
kwa mtu pia; magonjwa ni halisi, ukiyasemesha
yanasikia na kuelewa.

Maandiko yanasema Isaya 35:10 “…huzuni na


kuugua zitakimbia”; hivi viwili vinashirikiana,
huzuni na kuugua, ugonjwa ukiingia huzuni pia
inaingia, na neno linasema huzuni na kuugua
vitakimbia, na kama vitakimbia maana yake vina
miguu au uwezo wa kukimbia. Tukianza kuyaona
magonjwa kwa mtazamo huu, tutashughulika
nayo vizuri zaidi kuliko mwanzo.

28
Unaposoma kitabu hiki, kama unaumwa, anza
kujitofautisha wewe na ugonjwa, uone huo
ugonjwa sio wewe na wewe sio huo ugonjwa,
lakini pia anza kuuona kama kitu halisi, unaweza
ukausemesha huo ugonjwa nao ukakuelewa kwa
sababu una masikio na miguu ya kuondokea. Ni
kweli kuna magonjwa mengine yanakuwa
matukutu yanajifanya hayasikii wala kuelewa,
lakini ukweli ni kwamba yanasikia na kuelewa,
ukiendelea kuyang’ang’ania yakuachie lazima
yataondoka; kila unapoutamkia ugonjwa, unasikia
na kukuelewa.

Marko 11:23
[23] Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia
mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala
asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba
hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

Maandiko haya yanathibitisha kwamba, sio tu


ugonjwa lakini hata vitu vina uwezo wa kiroho wa
kusikia. Ndio maana Neno linasema “yeyote
atakayeuambia mlima huu”; maana yake sio tu
magonjwa pekee yanayosikia bali kila kitu chenye
jina kina masikio na kinaweza kusikia na kutii.

Kila ugonjwa una jina ili usikie na kutii

Moja ya kusudi la kuwa na jina ni ili kutambulika,


ili ukiitwa usikie na kuitikia, na pia ili kujua
29
maagizo yanaelekezwa kwa nani. Kwa hiyo,
kama magonjwa yana majina, ni ili yasikie na
kutambulika, na ili yapokee maelekezo. Hata
kama jina la ugonjwa halijagundulika, bado
ugojwa unalo jina ambalo ni‘ugonjwa’. Ukweli ni
kwamba, kila ugonjwa una jina katika ulimwengu
wa roho hata kama kwenye mwili huo ugonjwa
haujapewa jina.

Na hii ndio sababu Mungu alimkirimia Yesu Jina;


kama kungekuwa na zawadi nyingine kubwa zaidi
ya jina ya kumpa Yesu, Mungu angempatia hiyo,
lakini hakukuwa na zawadi nyingine kubwa zaidi
ya JINA.

Unaweza ukajiuliza kwanini Mungu alimpa jina?


Alimpa jina kwa sababu kila kitu huku duniani,
mbinguni na kuzimu kina jina, kwa hiyo kwa
kumpa jina lililo kuu kuliko majina yote, maana
yake amemuweka juu ya vyote vyenye majina.
Utajiri ni jina, umasikini ni jina, jina la Yesu liko juu
ya utajiri, liko juu ya umasikini.

Neno la Mungu linaposema Jina la Yesu liko “juu


ya majina yote” maana yake ni mamlaka iliyo juu
ya majina yote, yaani kwa jina hili la Yesu
unaweza ukaamuru kila chenye jina kwa sababu
kiko chini ya jina la Yesu lililo juu ya majina yote.

30
Kwa hiyo, unaposema kwa kumaamisha “kwa jina
la Yesu”, kila kitu kinasikiliza ni nini kinafuata, ni
agizo lipi linafuatia.

Kila ugonjwa una jina, na kama una jina, maana


yake jina la Yesu liko juu ya huo ugonjwa, kwa
hiyo likitajwa jina la Yesu, ugonjwa unasikiliza ni
maelekezo gani yanafuata, kwa hiyo ukiuambia
ugonjwa ondoka, unaelewa na kwa kutumia
miguu yake utaondoka na kukuacha.

Kama wewe ni mgonjwa, anza kuufikiri na kuuona


huo ugonjwa sio wewe, hauhitaji masaa mengi
kuanza kujiona hivyo, amua tu sasa hivi, kisha
anza kuona huo ugonjwa una ufahamu
(personality), ni kitu halisi, na ukiusemesha
utaelewa na kuondoka. Anza kuuona una miguu
ya kutokea, anza kuuona una masikio ya
kusikilizia, anza kuona kwamba, kwa sababu
ugonjwa huo una jina, basi hauwezi kubisha
mbele ya Jina la Yesu lipitalo majina yote; anza
kuona huo ugonjwa hauwezi kubisha mbele ya
mamlaka tuliyonayo katika Kristo Yesu.

Jina la Yesu, jina juu ya kila chenye jina

Wafilipi 2:9-11
[9] Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

31
[10] ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu
vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya
nchi;
[11] na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI
BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Angalia haya maandiko yanavyosema, “ili kwa


jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu…” maana
yake sio tu watu pekee bali ni magoti ya watu
pamoja na ya vitu mbalimbali. Kila kitu kina
uwezo wa kusikia na kutii, Yesu alipewa jina juu
ya majina yote kwa sababu vitu vyote vina majina.
Jina juu ya majina yote maana yake ni nafasi
iliyojuu ya nafasi zote. Kila chenye jina kinasikia,
na kina nafasi, kwa hiyo nafasi ya Yesu ni juu ya
nafasi zote. Kila kitu ambacho kinaamriwa kwa
jina la Yesu kinaweza kuelewa na kutii.

Maandiko yanasema “ili kwa jina la Yesu kila goti


lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na
vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU
KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu
Baba.”

Vitu vyote vya mbinguni, duniani, na chini ya nchi


vina majina na nafasi, na kwa jina kuu la Yesu
vinaweza kuitikia maelekezo linapotamkwa jina la
Yesu. Kukiri Yesu ni Bwana maana yake ni
kukubali kutiishwa chini ya U-Bwana wa Yesu,
yaani kusema “Yesu ni Bwana na mimi ni
32
mtumwa nitatii kila atakachonielekeza kwa
utukufu wa Mungu Baba”.

Mathayo 8:15-17 “Akamgusa mkono, homa


ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye
pepo; akawatoa pepo kwa neno lake,
akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie
lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na
kuyachukua magonjwa yetu.”

Udhaifu au ugonjwa ni kitu halisi kabisa ndio


maana Yesu aliutwaa udhaifu wetu na
kuyachukua magonjwa yetu.

33
Siri ya 3

Homa (ugonjwa) ni mgeni asiye na


uhalali kukaa katika mwili wako

Siri ya tatu ya kupokea uponyaji na kutembea


katika afya na kuhudumu uponyaji, ni kuanza
kuuona ugonjwa kama mgeni asiye na uhalali
katika mwili.

Kama wewe una ugonjwa wowote, ukweli ni


kwamba, wewe halisi sio mgonjwa, isipokuwa
kuna mgeni amekuvamia anaitwa ugonjwa
(malaria, kansa, ukimwi, vidonda vya tumbo,
uvimbe, figo zimefeli, maumivu ya kichwa nk),
huyu mgeni asiye halali kwenye mwili wako
akikuachia, akiondoka, utainuka na kuwa mzima
kabisa kwa sababu wewe halisi ni mzima.

Huyu mgeni sio mgeni halali katika mwili wako,


huo ugonjwa sio mgeni halali ndani ya mwili
wako, kwa hiyo, unayo mamlaka kumuondoa.

Mwili wako ni nyumba halali ya Roho


Mtakatifu

Neno la Mungu linasema Mwili wangu ni hekalu la


Roho Mtakatifu, 1 Wakorintho 6:19-20 “[19] Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho
34
Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na
Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;[20]
maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu”

Siku zote mwenye nyumba ndio mwenye uhalali


wa kukaa katika nyumba, yaani kama nyumba ni
yangu, mwenye uhalali wa kukaa kwenye
nyumba yangu ni mimi na Yule ambaye
nitampatia mimi uhalali kukaa.

Mwili wako na wangu ni nyumba au ni makao ya


Roho Mtakatifu, kwa hiyo mwenye uhalali wa
kukaa ndani ya mwili wangu sio homa bali ni
Roho Mtakatifu; homa au ugonjwa havina uhalali
kisheria kukaa ndani ya mwili wangu na wako.
Chochote ambacho kitajaribu kuingia kukaa
katika mwili wangu bila ruhusa ya Roho Mtakatifu,
hicho sio halali kukaa katika mwili.

Ninachotaka uone ni hiki, wewe sio mgonjwa,


isipokuwa kuna mpangaji asiye halali ndani ya
mwili wako na huyo mpangaji ndio anasababisha
mwili wako kuwa na ugonjwa; na kwa sababu sio
halali maana yake huyo mpangaji anatakiwa
kuondoka, na kama atakataa kuondoka kwa hiari,
anatakiwa kuondoka kwa kulazimishwa.

35
Mpangaji anaondolewa kwa nguvu
Kwa mfano una nyumba yako, umeweka
wapangaji halafu wale wapangaji muda wao wa
kukaa humo umeisha, utakachofanya utawapa
taarifa ya kuwalazimu waondoke (notice),
wakikataa kuitikia ile taarifa na kuondoka,
hauwezi kusema kwa sababu wamekataa
kuondoka basi nitawaacha waendelee kuishi
humu bila uhalali.

Kimsingi wakikataa kuondoka, utaenda hatua


inayofuata ya kisheria, na sheria ikipitisha
kwamba wanatakiwa kuondoka, na wakakataa
kuondoka kwa taarifa ya kawaida, kuna vyombo
maalumu vya nguvu kwa ajili ya kuondoa
wapangaji wa aina hiyo. Hivyo vyombo kazi yao ni
kuwaondoa kwa nguvu wale wapangaji ambao
wameshindwa kutii sheria bila shuruti, kazi yao ni
kwenda kwenye nyumba na kutoa kila mtu na kila
kitu kwa nguvu na kuikabidhi nyumba kwa mmiliki
halali wa nyumba.

Ndivyo ilivyo, ugonjwa hauruhusiwi kukaa kwenye


mwili wako, kama unakubali utaondoka kwa
upole, utaratibu na bila shari (polite notice) na
kama hautaki kuitikia taarifa kuondoka bila shari,
basi unaondolewa kwa lazima (nguvu) kwa
sababu sio mgeni halali, amepanga bila uhalali,
kwa hiyo hakuna haja ya kujadiliana nao. Hakuna
36
haja ya kuendelea kukaa na kuridhika (kuwa
comfortable) na ugonjwa, usikubali kuridhika na
ugonjwa hata kama huo ugonjwa umechelewa
kuondoka kwa sababu huyo ni mpangaji asiye
halali, hana uhalali wala haki ya kuendelea kukaa
kwenye mwili wako.
Ugonjwa kukaa muda mrefu hakuupatii huo
ugonjwa uhalali wa kuendelea kukaa kwenye
mwili wako, usikubali ugonjwa uendelee kukaa
kwako.

Wewe sio mgonjwa


Kwa ufahamu huu maana yake ni kwamba kama
wewe una changamoto ya afya unaweza
ukasema hivi;

“Mimi si mgonjwa isipokuwa huyo mpangaji


asiye halali ndani ya mwili ndio husababisha
mwili kuwa mgonjwa...”

“Mimi sina masharti ya vyakula, ninaweza kula


vyakula vyote, lakini mpangaji anayekaa ndani
ya mwili wangu ndio mwenye hayo masharti,
yeye ndio hawezi kula baadhi ya vyakula, akila
anaumwa...”

“Mimi sina dalili zozote ninazozihisi, mimi


siumwi kichwa, ila kuna mpangaji yuko ndani
yangu ndio ana hayo maumivu...akiondoka
huyo mpangaji ataondoka na maumivu yake”
37
“Mimi naweza kuinama na kuinuka vizuri, mimi
ninaweza kukimbia bila shida, mimi ninaweza
kufanya kila kitu, isipokuwa mpangaji
(ugonjwa) ndio unanifanya nisiweze,
akiondoka huyo mpangaji nitaweza kufanya
vyote, na anaondoka sasa kwa Jina la Yesu”

Mama mkwe wa Petro alikuwa anaweza kuinuka


vizuri, alikuwa anaweza kuwatumikia wageni,
lakini Yule mpangaji aitwaye homa alipoingia
ndani yake, ambaye ndiye alikuwa anamfanya
alale kitandani ashindwe kuinuka, kutembea, nk,
Yule mpangaji alipoondoka, Yule mama akainuka
na kuanza kuwatumikia kwa sababu yeye ndivyo
alivyokuwa, ilikuwa ni kawaida yake kuwatumikia
wageni.

Ninataka kukufikisha mahali pa kuona kwamba,


wewe sio mgonjwa, wewe halisi ni mzima kabisa,
wewe unaweza kufanya kila unachotaka kufanya,
isipokuwa kinachokuzuia ni kitu kingine
(mpangaji) halisi ambacho kinasikia na kuelewa
na kikiamriwa kuondoka kinaondoka na kukuacha
wewe ambaye ni mzima kabisa.

38
Siri ya 4

Ugonjwa haubembelezwi kuondoka

Siri ya nne ni kwamba, huyu mpangaji asiye


halali, habembelezwi kuondoka, analazimishwa
kuondoka. Ukimbembeleza anaweza asikubali
kukuachia, kwa hiyo mlazimishe.

Ugonjwa haubembelezwi kuondoka bali


unalazimishwa kuondoka, kwa sababu lugha
pekee ambayo shetani na mawakala wake
wanaielewa ni lugha ya nguvu/ amri (command
and authority language). Siku zote
unaposhughulika na shetani, usiwe na ustaarabu,
shetani haitaji ustaarabu anahitaji lugha ya amri,
lugha ya lazima, yaani kumlazimisha kwa
mamlaka.

Ninaposema lugha ya nguvu au mamlaka,


haimaanishi kutoa sauti kubwa au makelele, lakini
inamaanisha lugha yenye mamlaka na
kumaamisha kama ambavyo nitaelezea mbele
kwenye kitabu hiki.

Ugonjwa ni sawa na nyoka katika nyumba

Ukitaka kuushughulikia ugonjwa wowote vizuri,


uone huo ugonjwa kama vile nyoka ameingia
39
kwenye nyumba yako. Nyoka akiingia ndani ya
nyumba yako, hakuna namna utastarehe
(utakuwa comfortable) naye ndani ya nyumba,
hata kama ukijaribu kumuua ukashindwa bado
utaona ni nyoka na anapaswa kuondoka.
Hauwezi kuwa huru na nyoka ndani ya nyumba,
ukishindwa kumuua, bado utasema lazima
nipambane naye mpaka nimuue au aondoke, kwa
sababu kwa namna yoyote na kwa gharama
yoyote hatakiwi kukaa na wewe ndani ya
nyumba. Ndivyo ilivyo, ugonjwa hautakiwi kukaa
ndani ya mwili wako, hata kama umejaribu njia
kadhaa bado haujafanikiwa, endelea kulishika
hilo kwamba ugonjwa hautakiwi kukaa ndani ya
mwili wangu, na ling’ang’anie hilo.

Wakati mwingine magonjwa hayaondoki kwa


sababu tumekubali kuishi nayo, tumeamua
kujenga urafiki nayo, tumeamua kuridhika nayo.
Unatakiwa kuukataa ugonjwa na kuuambia,
“hautakaa humu ndani ya nyumba yangu, ndani
ya mwili wangu, aidha unataka au hautaki”, kwa
sababu ugonjwa haubembelezwi.

Huyu mpangaji asiye halali, analazimishwa


kuondoka kwa sababu lugha pekee ambayo
Shetani na mawakala wake yakiwemo magonjwa
wanaielewa vizuri ni lugha ya lazima (command).

40
Luka ameeleza hivi, Luka 4:39 “[Yesu]
Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa,
ikamwacha; mara hiyo akaondoka,
akawatumikia.”

Unajua, kama nilivyosema, hauwezi kukikemea


au kuzungumza na kitu wakati hakisikii, andiko
hilo linathibitisha kwamba, ugonjwa ni kitu halisi
kabisa. Maandiko hayo yanasema Yesu
aliikemea ile homa, hakuomba kwa Mungu bali
alizungumza na homa, na hakuzungumza nayo
kwa kuibembeleza bali aliikemea.

41
Sehemu Ya Tatu

UMEPEWA MAMLAKA

Neno la Mungu linasema, tumepewa mamlaka,


kwa mamlaka hii na sisi tunaweza kuikemea
homa. Sio kuibembeleza bali kuikemea na
kuiamuru kwa Jina la Yesu.

Nini maana ya kukemea?

Luka ameeleza hivi, Luka 4:39 “[Yesu]


Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa,
ikamwacha; mara hiyo akaondoka,
akawatumikia.”

Neno “kukemea” lililotumika hapo lina maana,


“kutoa amri ambayo, unayemwambia au kumpa
amri hiyo, hana machaguo
(options) isipokuwa kutii tu.”
Kwa hiyo, Yesu aliuambia ugonjwa amri moja
isiyo na machaguo, ugonjwa ulikuwa ni halisi na
unasikia na kuelewa, alipoukemea alikuwa
anatoa amri moja isiyo na machaguo; hakuwa
42
anauambia unaweza ukatoka au usitoke, bali
ilikuwa ni amri moja tu ya kutoka. Kwa hiyo
haikuwa tu kukemea bali ilikuwa ni kutoa tamko
lililomaanisha kwamba hii homa lazima iondoke
na si vinginevyo.

Magonjwa huwa yanaelewa matamko ya aina


hiyo, ukitamka tamko la aina hii, magonjwa
yanaelewa maana yake, yaani tamko moja lisilo
na machaguo, tamko moja lisilo na nia mbili,
tamko moja lenye maana moja tu.

Tumepewa mamlaka

Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya


kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule
adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

Kama vile Yesu alivyoikemea homa kwa


mamlaka, hata na sisi tunayo mamlaka hiyo hiyo,
tumepewa hiyo mamlaka ya kukemea magonjwa
nayo yakatii. Unaweza kabisa ukauambia
ugonjwa tamko moja lenye maana moja tu na
ugonjwa ukakuelewa.

Usitoe amri au tamko huku ukiwa na machaguo,


saa ya kuukemea ugonjwa sio saa ya kuwa na
machaguo, kwamba usipoondoka ugonjwa
nitafanya kitu fulani au nitaenda sehemu fulani
43
kupata msaada, huo sio wakati sahihi wa kuwaza
hayo, hayo sio mawazo sahihi wakati wa
kumshughulikia adui.

Ninamaanisha kwamba, wakati ambapo


umeamua kuukemea ugonjwa kwa kuuamuru
uondoke kwa jina la Yesu, sio wakati wa kufikiria
kitu kingine chochote kama vile dawa au msaada
mwingine wa kimatibabu. Sasa, simaanishi hivyo
vingine ni vibaya, inawezekana unatumia dawa
na hakuna shida kabisa, lakini wakati ule wa
kuuamuru ugonjwa (the moment of prayer or
commanding), sio wakati wa kufikiri dawa wala
mbadala mwingine wowote.

Neno la Mungu linasema, kila jambo lina wakati


wake (Muhubiri 3:1), halafu mahali pengine
anasema kila kitu Mungu amekifanya kizuri kwa
wakati wake (Muhubiri 3:11).
Ni muhimu sana kuujua wakati wa kutoa amri kwa
magonjwa, usipojua kuhusianisha wakati na vitu
unavyofanya, hautaona matokeo.

Kwa mfano, kucheka ni jambo zuri, lakini


ukicheka wakati usio sahihi maana yake
umefanya jambo zuri nje ya wakati, na kwa
sababu ni nje ya wakati, basi wakati unaweza
ukalifanya jambo hilo zuri kuwa baya. Kulia ni
kuzuri kwa wakati wake, vile vile kucheka ni
kuzuri kwa wakati wake.
44
Ninachomaanisha ni kwamba, wakati wa
kuushughulikia ugonjwa kwa imani kwa njia ya
mamlaka Mungu aliyotupatia, huo sio wakati wa
kufikiria dawa, sio wakati wa kufikiria wataalamu
wa tiba au kufikiria hospitali, sio wakati wa
kufikiria tiba mbadala, sio wakati wa kufikiria kitu
kingine chochote, bali ni wakati wa kufikiri
uponyaji kwa mamlaka, ni wakati wa kutamka
tamko moja ambalo umelimaanisha lisilokuwa na
machaguo. Usitoe amri ukiwa na machaguo,
kwamba ugonjwa huu usipoondoka nitatumia (au
ninayemuombea atatumia) kitu fulani kama
mbadala, huo sio wakati wake hata kama hilo
jambo sio baya. Huu ni wakati wa ugonjwa
kuondoka kwa tamko lenye mamlaka na nguvu za
Mungu.

Tamka tamko linalomaanisha na lisilo na


machaguo kwamba shetani, hauna machaguo, hii
ni saa yako ya kuondoka na hakuna chaguo
lingine zaidi ya kuondoka na ni kuondoka sasa.

Tamka ukiwa na NIA MOJA TU

Maandiko yanasema katika Yakobo 1:6-8 “Ila na


aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana
mwenye shaka ni kama wimbi la bahari
lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku
na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa
45
atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili
husita-sita katika njia zake zote.”

Wakati wa kuukemea ugonjwa sio wakati wa


kuona mashaka, tamka tamko moja ukiwa na nia
moja.

Kabla ya kutoa amri, kutamka au kuomba,


hakikisha umedhamiria ndani yako, ya kwamba
ninaenda kutoa amri moja kwa huu ugonjwa na
nikiwa ninamaanisha kitu kimoja tu, nikiwa na nia
moja tu, ya kwamba ugonjwa lazima uniachie au
umuachie unayemuombea, ni lazima uondoke na
si vinginevyo. Usianze kuomba au kumuombea
mtu kama bado haujadhamiria ndani yako na
kuwa na nia moja kama nilivyoeleza.

Tamka kitu kimoja ulichomaanisha na umaanishe


kitu kimoja unachokitamka, kwa imani na kwa
hakika ugonjwa (homa) utasikia, utaelewa na
utaondoka na kukuacha au kumuacha huru
unayemuombea.

Maanandiko yanasema katika Marko 1:42 “Na


mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.”

Ukoma ukitoka mtu anatakasika, homa ikiondoka


mtu anakuwa mzima, ugonjwa ukiondoka mtu
anakuwa mzima.

46
Chukua hatua sasa

Ninaamini umejifunza na kuelewa na sasa uko


tayari kutoa tamko moja lenye maana moja kwa
huo ugonjwa.

Tamko hilo ni sawa kabisa na kumpa swali


shetani ambalo ni la kuchagua, ni lazima alijibu
hilo swali, na kwenye uchaguzi unampa jibu moja
ambalo ni lazima alichague.
Tunaupa huo ugonjwa jibu la kuchagua, kwamba
jibu lake ni kuondoka kwenye huo mwili wako, na
ni lazima ugonjwa uchague jibu hilo.

Mimi na wewe unayesoma kitabu hiki tukubaliane


kwamba tunauambia ugonjwa tamko moja lenye
maana moja. Mimi ninaamini ya kwamba
tunausemesha ugonjwa tamko moja lenye maana
moja.

Kama wewe ni mgonjwa, huu ndio wakati wako


sahihi wa kupokea uponyaji na uzima. Weka
mkono mahali ambapo unaumwa na ninaandika
hapa maombi ambayo yanamaanisha jambo moja
tu, kwamba huo ugonjwa lazima ukuachie, homa
lazima ikuachie.

47
MAOMBI YA UPONYAJI

“Baba katika Jina la Yesu, niko mbele zako kwa


ajili ya mwanao ambaye ameshika kitabu hiki na
ana ugonjwa kwenye mwili wake, sawa na Neno
lako ambalo tumejifunza ya kwamba Yesu
aliikemea ile homa na homa ikamuacha, nami
kwa mamlaka niliyopewa ninaenda kinyume na
huo ugonjwa.

Ninatamka ya kwamba, mtu huyu sio mgonjwa


wala yeye si ugonjwa, isipokuwa kuna mgeni
ambaye hana uhalali kukaa ndani yake, na huyu
mgeni anasikia, anaelewa ana miguu ya kuingilia
na kutokea na anaweza kutii mamlaka.
Ninatamka tamko lenye maana moja kwako
ugonjwa, kwa jina linalopita majina yote, jina la
Yesu Kristo, ninakuamuru na kukuapisha, WEWE
UGONJWA ACHIA HUO MWILI NA KILA
SEHEMU YA MWILI ULIYOISHIKA KATIKA JINA
LA YESU.

KWA JINA LA YESU ACHIA TUMBO, ACHIA


MAPAFU, ACHIA FIGO, ACHIA MOYO, ACHIA
DAMU, ACHIA KIUNGO, ACHIA MGONGO,
ACHIA UTI WA MGONGO, ACHIA UBONGO,
ACHIA MASIKIO, ACHIA MFUMO WA HEWA,
ACHIA MIGUU, ACHIA MIKONO ACHIA KILA
ENEO LA MWILI HUO SASA.
48
WEWE NI MPANGAJI USIYE NA UHALALI,
NINAKUAMURU ACHIA HIYO NYUMBA YA
ROHO MTAKATIFU; HAUTAKAA TENA NDANI
YA HUO MWILI KATIKA JINA LA YESU KRISTO
ALIYE HAI.
NINAACHILIA UZIMA WA MUNGU UPITE
KWENYE MWILI WAKO, KILA MAHALI
PALIPOKUWA NA UGONJWA PAKAWE NA
UZIMA WA MUNGU KWA JINA LA YESU.

ASANTE MUNGU MKUU KWA SABABU


UMEMGUSA MTOTO WAKO HUYU NA
UMEMPONYA, ASANTE KWA SABABU VIMBE
ZOTE ZIMEYEYUSHWA KWA JINA LA YESU.
ASANTE KWA SABABU MATESO YOTE
YAMEKOMESHWA KWA UTUKUFU WAKO.

KWA JINA KUU LA YESU TUMEOMBA NA


KUPOKEA, AMINA.”

49
HITIMISHO

Mungu akubariki sana kwa kutenga muda


kusoma na kujifunza kupitia maandishi ya kitabu
hiki. Ninaamini umehudumiwa na Mungu na
umeponjwa, lakini pia umepokea ujasiri wa
kuhudumu uponyaji kwa watu.
Kumbuka kwamba, kitabu hiki ni sehemu ya
kwanza katika mfululizo wa vitabu vya PONA
KWA NENO LA MUNGU, ninakushauri
uhakikishe unapata nakala inayofuata ili uendelee
kujifunza kuhusu uponyaji.
Ikiwa Mungu amekuponya na unapenda
kuwasiliana na mimi unaweza ukanitafuta kwa
mawasiliano niliyoweka kwenye kitabu hiki.

Kama Haujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma,


Ninakushauri leo ukate shauri toka moyoni
mwako na kuamua kwa dhati kuokoka na
kumrudia Mungu ili uweze kumfurahia Mungu
katika mponyaji kama ambayo tumejifunza. Kama
uko tayari kuokoka au kumrudia Mungu, basi
tafuta mahali pa utulivu, kisha upige magoti na
kisha ufuatishe SALA YA WOKOVU hapo chini.

Kama hauna nafasi nzuri ya kupiga magoti basi,


popote ulipo, unaweza kusali SALA YA WOKOVU
kwa kumaanisha kutoka moyoni mwako, na
baada ya hapo utakuwa umeokoka.
50
SALA YA WOKOVU:
“Bwana Yesu, niko mbele zako, nimetambua ya
kwamba mimi ni mwenye dhambi na ninastahili
hukumu, lakini pia ninatambua ya kwamba Wewe
Yesu ulisulibiwa msalabani na ukafa ili kulipa
hukumu yangu, na siku ya tatu ukafufuka
kukamilisha wokovu kwa kila anayekuamini. Na
mimi leo, ninaamini ndani ya Moyo wangu na
ninakiri kwa kinywa changu, ya kwamba wewe
Yesu ndio njia ya kweli na uzima ya kwenda
mbinguni. Ninaomba unisamehe dhambi zangu
zote, na uniokoe leo. Ufute jina langu kwenye
kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu
cha uzima. Unijaze na Roho wako Mtakatifu
aniwezeshe kudumu katika wokovu.
Nimeomba haya na kuamini, KATIKA JINA LA
YESU, AMEN.”

Kama umefanya uamuzi wa kuokoka na


kufuatisha sala hii, unaweza ukawasiliana na
mimi kwa ushauri zaidi kupitia namba za simu
kwenye kitabu hiki, lakini pia unaweza kufuatilia
mafundisho yatakayokusaidia kukua kiroho kwa
kufuata link zilizowekwa hapo chini. Pia ni
muhimu sana utafute kanisa wanaoamini
WOKOVU na uanze kusali hapo.
Kupata mafundisho mengine, ya sauti na
kuandika(Audio & Text) bure, ya Mwl. Francis
M. Langula
51
 TELEGRAM
Mafundisho ya wote (Audio):
https://t.me/Neno_na_Pst_Francis
Mafundisho maalumu ya vijana (Audio):
https://t.me/RYG4Christ
 WhatsApp Groups :
o Nitumie ujumbe WhatsApp
+255754711247
 Youtube: Mwl. Francis M. Langula
 Facebook
https://www.facebook.com/mwl.francislangula
https://www.facebook.com/UponyajiWaKiMung
uKwaWote
 Instagram: @francis.langula
 Mafundisho kwenye simu yako - Android
Application
o Ingia Playstore
o Tafuta (Search) “Neno App” au
“Francis Langula”
o Download “Neno App” na
ufurahie mafundisho
o Au unaweza kufuata link hii
http://langula.xyz/francis

52

You might also like