You are on page 1of 3

NAMNA AMANI INAVYOWEZA KUAMUA

KWA AJILI YAKO.


Wafilipi 4:7 inasema ‘Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote , itawahifadhi mioyo yenu na nia
zenu katika Kristo Yesu’.

Wakolosai 3:15″ Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili
mmoja tena iweni watu wa shukrani “.

Yohana 14: 27 ‘Amani yangu nawaachieni; amani yangu nawapa;niwapavyo mimi si kama
ulimwengu utoavyo.Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga’

Ule mstari wa 6 wa kitabu cha Wafilipi sura ya nne unasema “Msijisumbue kwa neno lolote ;bali
katika kila neno kwa kusali na kuomba , pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu’’ Kimsingi mstari huu unazungumza suala la mahitaji/maombi ambayo watu wanakuwa
nayo siku zote na wanayapeleka mbele za Mungu. Katika haya mahitaji mhusika anakuwa
anahitaji kujua/kupata jibu kwa kuwa linamsaidia au litamsaidia katika kufanya maamuzi fulani.

Haya ni maombi ambayo mhusika anasubiri kwa hamu jibu ili afanye maamuzi. Mfano, Binti
anayeomba kujua je, kijana aliyemfuata kutaka kumuoa ni wa mpango wa Mungu au kijana
anayetaka kujua ni binti gani katika wengi waliopo ambaye hakika ni mapenzi ya Mungu
waoane, au pia mtu anayeomba kujua je ni mpango wa Mungu aache kazi na kuanza huduma n.k
au tuseme mwanafunzi ambaye anenada kuanza mwaka wa kwanza chouni na anataka kujua ni
kozi gani Mungu anataka asomee? Nk.

Sasa, Kibiblia amani imewekwa au unapewa amani ili ikusaidie kufanya hayo maamuzi. Maana
imeandikwa katika Wakolosai 3:15 “Na amani ya Kristo iamue mioyoni
mwenu…………’.Sasa hii ina maana ni lazima amani iamue kwanza na kisha wewe ufuate
uongozi wa amani yaani amani ya Kristo ikuongoze wewe kufanya mamuzi, ikuelekeze upi ni
uamuzi sahihi na mzuri.
Je, amani inaamuaje ?
Advertisements
REPORT THIS AD

Kwa kuuhifadhi moyo wako na nia yako katika Kristo Yesu.

Ezekieli 38:10 inasema Bwana Mungu asema hivi; itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia
moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; na pia Nehemia 6:8 kwenye kipengele cha
mwisho inasema ‘Lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni’, ukisoma pia ‘Mathayo
15:19 inasema ‘kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi,
uasherati,wivi,ushuhuda wa uongo na matukano’. Hivyo basi ukiiunganisha hiyo mistari mitatu
utajua kwamba kumbe mawazo huingia moyoni, mawazo hubuniwa moyoni na kisha
mawazo hutoka moyoni.
Moyo wa mtu ni uwanja wa mapambano ambao ndani yake kuna mawazo mengi sana ambayo
humwingia mtu na kubuniwa yakisubiri kutoka. Yapo mawazo ya kutoka kwa Mungu,shetani au
ya mtu binafsi. Na mara zote yale ya shetani ni ya kupinga kusudi la Mungu kwa huyo mtu na
pia mara nyingi ya kutoka kwa mtu pia huwa hayalingani na ya Mungu.

Sasa kwa kujua hilo Yesu alituachia amani, kinachotokea wakati unaomba ni hiki , amani
inaukamata moyo wako ili kuhakikisha kwamba mawazo mengine ya Shetani yanayoweza
ingia ndani yako yasiweze kuuondoa moyo wako kwenye nafasi ya wewe kukaa ndani ya
kusudi la Bwana ili kulinda nia ya Kristo ndani yako isiharibiwe.

Hii ina maana kazi ya amani ni ya ulinzi. Kwa hiyo tunaweza kusema licha ya amani kuwa
mwamuzi, amani pia ni mlinzi. Amani anafanya kazi ya kuulinda moyo wako na nia yako
isiharibiwe na mawazo ya kutoka kwa shetani kwa kuwa mawazo hayo yamebeba kusudi baya.
Kwa hiyo amani inapigana kuhakikisha moyo wako hauharibiwi na mawazo mengine yaliyoko
kinyume na mapenzi ya Mungu juu ya ombi au hitaji ulilonalo mbele za Mungu. Sasa
ikishaulinda moyo wako dhidi ya mawazo mengine kuhakikisha kwamba hayaharibu mpango wa
Mungu juu yako ndio inakuongoza katika uamuzi ambao ni sahihi.

Na ili kujua uamuzi huo ni sahihi amani itakupa raha nafsini mwako, utajisikia furaha na nafsi
yako kufunguka juu ya kufanya jambo fulani. Ukiona hayo mazingira ndani yako fuata amani
inakokuelekeza kumbuka amani ni mwamuzi na mlinzi. Sasa siku zote mlinzi huwa hampeleki
bwana wake kwenye hatari na hii ina maana amani itakuongoza kufanya uamuzi ambao ni bora
na ulio katika mpango wa Mungu.

Uzuri wa amani ya Kristo ni huu inakuonyesha uamuzi ambao ni wa hatari/mbaya kwako na


pia inakuonyesha na kukuongoza katika uamuzi ambao ni mzuri kwako. Inakuonyesha
kwamba huo uamuzi ni mbaya kwa kukosesha raha, furaha na uhuru juu ya uamuzi unaotaka
kuufanya. Na pia inakuonyesha kwamba huo ni uamuzi bora kwa kukupa raha na furaha na
uhuru juu ya huo uamuzi.Kwa kifupi niseme unapoomba maombi ya namna hii halafu ukakosa
amani ndani ya moyo wako jua kwamba huo uamuzi huenda ni wazo la shetani au huenda ni la
Mungu lakini, huo sio muda muafaka wa kutekeleza hilo wazo japo hili linategemeana na aina ya
hitaji ulilonalo.

Hivyo ukikosa amani usitekeleze hayo mawazo yanayokujia kama jibu, endelea kuomba na
kama hali hiyo ikiendelea basi usifanye huo uamuzi maana mlinzi hayuko na wewe. Sasa kama
ni la Mungu lakini muda wake bado, Mungu ni waminifu atakujulisha na kukufunilia hilo pia.

Lakini unapoomba ukiiona amani katika mawazo yanayokuja kama majibu jua kabisa hilo ni
wazo la Mungu na ndani yake limebeba mpango na njia za Mungu za jibu la ombi lako. Lakini
pia pima kwanza hayo mawazo kwa njia ya neno la Mungu uone kama viko sawa maana
Shetani hujigeuza ajifanye malaika wa Nuru. Hata siku moja shetani hawezi kukuletea wazo
ambalo linaendana na neon la Mungu.

Soma huu mstari utaelewa ninchosema zaidi Zaburi 34:14 ‘Uache mabaya ukatende mema,
utafute amani ukaifate’.Maana yake achana na maamuzi mabaya tulia sikiliza amani
iankuongoza wpi na kisha ifuate maana yeye ndiye mlinzi wa moyo wako.
Ni imani yangu kwamba ujumbe huu utakusaidia kujibu mawali mengi uliyokuwa nayo mbele za
Mungu.

Amani ya Kristo na iwe pamoja nawe.

You might also like