You are on page 1of 2

Page 1 of 2

1. Namkataa shetani na kazi zake zote, na mambo yake yote katika Jina la Yesu
2. Navunja maagano yote niliyowekewa na niliyoweka kwa kujua na kutokujua, mapatano yote na
kuzimu maagano yote na mauti katika Jina la Yesu
3. Ninajivua kila aina ya vazi la kipepo nililovalishwa, kila aina ya vyakula vya maagano nilivyolishwa,
iwe waziwazi au katika ndoto, najivua vyote katika Jina la Yesu
4. Natangaza kwamba mimi ni mali ya Mungu. Vitu vyote nilivyomezeshwa, uchawi wote niliolishwa,
makubaliano yote niliyoyaweka na shetani, majini, wanga, wachawi najivua katika Jina la Yesu
5. Najitenga na kila makubaliano, leo, nayakana yote. Nayavunja kwa agano jipya la “DAMU YA
YESU”. Naweka agano la kweli na Yesu Kristo wa Nazareti Mwana wa Mungu aliye hai kuwa
mimi sio tena mali ya shetani bali ya YESU. Nautoa wakfu moyo wangu, nafsi yangu, mwili wangu
na roho yangu itawaliwe na YESU peke yake.
6. Shetani nakukumbusha ya kuwa huna uhalali wa kukaa ndani yangu tena maana nina Bwana
mwingine, YESU KRISTO. Ni lazima usujudu mbele zake, lazima goti lako lipigwe mbele za
YESU kwa kuwa wewe ulishindwa hadharani na ulimwengu wa roho wote ni shahidi wa jinsi
ulivyoshindwa, ukanyang’anywa uwezo, ukaharibiwa kabisa kwa kupondwa kichwa pale Kalvari.
7. Kila uchafu wako wote ambao uliweka juu yangu, ndani yangu, iwe nyama za watu, damu, usaha
wa wafu, udongo, vinyesi, manyoya, na kila kitu kiovu ondoa kwangu kwa Jina la Yesu Kristo wa
Nazareti.
8. Uchafu wote ulioweka tumboni mwangu, katika mwili wangu, sehemu zote za mwili wangu, sirini
na ambazo sio za siri, navilaani kwa Jina la Yesu na watu wote waseme amina.
9. Najitenga na kazi zako zote shetani, Kwa Jina la Yesu. Ulozi, wanga, uaguzi, uuaji, kula nyama za
watu, kunywa damu za watu najitenga kabisa katika Jina la Yesu.
10. Najivua na kukana kila aina ya pete niliyopewa kuzimu, nafunga upya ndoa na Bwana mpya Yesu
Kristo. Shetani nimekukataa, nimekukataa, nimekukataa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti
toka maishani mwangu. Mimi sio mali yako tena. Mimi ni mali ya Mungu aliyeniumba. Mimi ni mali
ya Yesu Kristo. Mimi ni mali ya Roho Mtakatifu.
11. Nimefufuka pamoja na Yesu Kristo, na uhai wangu umefichwa katika Kristo ndani ya Mungu.
12. Nimeketishwa pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho mahali juu sana kuliko ufalme wote na
mamlaka na nguvu na usultani na kila jina litajwalo katika ulimwengu huu na ule ujao pia.
13. Nimeokolewa katika nguvu za giza, nimehamishwa na kuingizwa katika ufalme wa mwana wa
pendo la Mungu, hapa shetani huna lako.
14. Picha zote za kuzimu za kipepo, televisheni za kuzimu nazitia giza katika Jina la Yesu.
Mkinitafuta hamtaniona, mtamuona Yesu na mtajuta kwa Jina la Yesu Kristo wa nazareti
15. Majini, wanga, wachawi mnaonichungulia na kunifuatilia naamuru macho yenu yawe vipofu kwa
Jina la Yesu. Vidole vyote vinavyonyooshwa kuelekea kwangu vikauke kwa Jina la Yesu Kristo wa
Nazareti.
Page 2 of 2

16. Mitego yenu yote ya siri naitegua katika Jina la Yesu. Manuizo yote ya siri na lugha za mapepo
nazifuta kwa Jina la Yesu Kristo wa nazareti.
17. Navunja maagano yote ya damu, chale katika mwili wangu, hirizi za siri nilizovishwa, nguvu za
mapepo na majini yaliyounganishwa kwa siri na maisha yangu vyote naviharibu kwa Jina la YESU
Kristo wa Nazareti.
18. Naamuru kitovu changu kilichochukuliwa nikiwa mdogo, kilichofanyiwa agano lolote, nalivunja
agano hilo kwa Jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai. Nafuta kila patano lililowekwa na
mababu na mabibi wa ukoo kupitia kitovu changu na viungo vingine vya mwili wangu kuvunjika
katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai
19. Naunganisha uhai wangu, nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu na damu ya Yesu sasa na
ninajitenga na ibilisi kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai.

You might also like