You are on page 1of 1

NYUZI KUMI “KUKAMILISHA SIFA” – Zaburi 33:2, Zaburi 92:3, Zaburi 144:9

1) Uliigawa bahari ya shamu, wana wa Israeli wakapita.

2) Uliwalisha wana wa Israeli mana – chakula kutoka mbinguni

3) Kwa mikate mitano na samaki wawili, ulizidisha samaki na mikate hiyo, watu zaidi ya

elfu tano wakala na kusaza.

4) Kwa mkono wenye nguvu (Ishara na ajabu) – uliwatoa wana wa Israeli Misri

5) Ulikufa, ukazikwa na siku ya tatu ukafufuka - uliishinda nguvu ya mauti.

6) Ulifufua na unaendelea kufufua wafu, uliponya na unaendelea kuponya aina zote za

magonjwa, ulisamehe na unaendelea kusamehe wenye dhambi, unawaweka huru

waliofungwa.

7) Wewe ni Mungu uliyeziumba mbingu na nchi

8) Kwa neno lako uliyetenga maji ili pakavu paonekane.

9) Jina lako linapita majina yote, mbinguni, duniani na chini ya nchi.

10) Ummemuumba mwanadamu kwa sura na mfano wako, umempulizia puani pumzi ya

uhai, naye ni nafsi hai.

You might also like