You are on page 1of 6

MASWALI NA MAJIBU

ULIZA UJIBIWE

BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU


NENO - KUCHEZA?

BY RENATUS M. IZUMANGIJI

Pr. Renatus M. Izumangiji Page 1


ULIZA UJIBIWE
UTANGULIZI

Biblia ina majibu ya maswali wanayouliza wanadamu hapa duniani. Somo hili limekusudiwa
kutoa changamoto iliyopelekea wasomaji wa Biblia kushindwa kuyatafsiri Maandiko
Matakatifu kama yalivyokusudiwa na Mungu kwa kupitia waandishi wa awali waliotumiwa
na Roho Mtakatifu kuufikisha ujumbe katika vizazi vyote .

Utafiti huu umefanywa kwa kuvipitia vitabu au maandishi ya awali kuhusu NENO
KUCHEZA (DANCE, DANCING;,PLAYING,TWISTING, TURN, MOVE ROUND,
SKIPING, JUMPING ) kama linavyosomeka na maana zake kwa lugha inayotumika leo
ambayo imepelekea kuyachukua maneno hayo na kutafsiriwa tofauti na muktadha wa ujumbe
halisi. Hivyo kwa msomaji wa somo hili, usome kwa nia ya kujifunza ukimruhusu Roho
Mtakatifu kukusaidia kuyaondoa mawazo na mtazamo wako au uliokwisha upokea kwa
waalimu pasipo kufuata maana halisi.

Mtiririko wa somo hili ni kwa mfumo wa maswali na majibu ambayo yamekuwa ndizo hoja
za wengi wanaotaka kuhoji juu ya mjadala ambao umepelekea kuwachanganya wasikilizaji
au wanaotaka kujua uhalisia wa mada hii.

Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke akiwa na uhuru wa kuchagua, Adam na Hawa


walikosa si kwa sababu walikuwa hawajui bali walikuwa wameonywa na Mungu wasile
matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasije wakafa, kama inavyosomeka katika
(Mwanzo 2:17). Hivyo nakuomba uchague uzima kwa kuiamini Biblia.

KWA MAWASILIANO, MAONI, USHAURI, MASWALI,WASILIANA NA

PR. RENATUS M. IZUMANGIJI

SIMU NAMBA, ( 0756802242 AU 0785822225 ).

KARIBU TUJIFUNZE NA BWANA AKUBARIKI.

Pr. Renatus M. Izumangiji Page 2


SWALI; Ikiwa Biblia katika kitabu cha Zaburi 150:4, imeruhusu kucheza; kwa nini kanisa
la Waadventista Wasabato haliruhusu kucheza?

JIBU; Neno KUCHEZA lililotafsiliwa toka Biblia ya kiingereza DANCING limetokana na


neno la KIEBRANIA, Machol = ‫מָחֹול‬
֪
Neno hilo husomeka Machol unasoma kwenda kushoto kwa lugha ya Kiebrania, lenye
maana ya CHORUS yaani kuitikia kwa pamoja, kwa furaha, nalo hupatikana pia katika
Zaburi 149:3; Yeremia 31:4, 13; Maombolezo 5:15 na Zaburi 30:11. Halimaanishi
kuyumbisha viungo kwa kufuatisha mapigo ya muziki.

SWALI; Kama ndivyo hivyo, kwa nini katika kitabu cha 2Samwel,6:14,21 Daud anaonekana
kucheza mwenyewe na kukazia kuwa yeye atacheza mbele za Bwana daima?

JIBU; Neno KUCHEZA katika 2Samwel 6: 14,21 kwa KIEBRANIA linasomeka = ‫ּכ ַָרר‬
Karar – Neno hili lenye maana ya zunguka kwa shangwe,(MOVE ROUND) hasa kwa wale
wanaoashiria kwamba wameshinda katika vita au katika mashindano kwa hiyo ni shangwe
kama za arusi (Wajita huimba “Kandolela”. Na wasukuma huimba “Ng`walisolelichagijo,
chaa”. Ndiyo maana Mikali binti Saul mkewe mfalme Daud alipomdharau alipata laana ya
kutopata mtoto hata kufa kwake.( 2sam 6:23) maana walikuwa wameshinda na kulikomboa
Sanduku la Bwana.

SWALI; Kama shangwe hizo ambazo hakuna madhara kwa wale wanaoshangilia, ni kwa
nini binti Herodia analaumiwa na wachambuzi wengi wa maandiko kwa kusababisha kifo cha
Yohana Mbatizaji kwa kucheza mbele ya mfalme baba yake na mbele ya wageni pale
ukumbini?

JIBU ; Neno ALICHEZA/ AKACHEZA katika kitabu cha Mathayo 14:6 na Marko 6:22,
kwa lugha ya KIYUNANI soma kwenda kuli (GREEK) , Ni Orcheomai = ὀρχέομαι,
Neno hili humaanisha kurusha juu miguu ( LIFT UP THE FEET) kwa hiyo mchezo wa
kurusha miguu kwa binti aliye juu ya eneo la maonyesho (stage show) kwa watu wakiwa
chini kutazama tena wegi wao walikuwa wamekunywa pombe, walichanganyikiwa hata
mfalme akatoa ahadi iliyoleteleza Yohana Mbatizaji mtumishi wa Mungu kukatwa kichwa.
Neno hili ndilo Waingereza wametohoa na kupata neno “ORCHESTRA”. Yaani kikundi cha
wanamuziki wanaotumia aina mbalimbali za vyombo vya muziki na kucheza si kwa ibada.

SWALI ; Kama wanawake wakiwa kwenye (stage show) hawaruhusiwi kurusha miguu juu ,
mbona Miriam naye alicheza na wanawake wakimfuata nyuma?

JIBU; Neno lililotumika katika kitabu cha Kutoka 15:20 kwa lugha ya awali ya
KIEBRANIA ni (Mechowlah) = ‫מְחֹלָה‬
Neno hili pia kwa KIYUNANI huitwa khoros (choros) = χορός
Neno hili la Kiyunani ndilo ambalo Waingereza wamepata neno Chorus lenye maana ya
maneno yanayoimbwa kwa kurudiarudia katika tukio la furaha kama vile tukio la Mwana
mpotevu hawakuwa na muda wa kujifunza wimbo unaomhusu mwana mpotevu. Hivyo
Miriam aliimbisha Chorus wimbo wa kurudiarudia kulingana na tukio la kuangamizwa kwa
jeshi la Farao. Neno hili hupatikana pia katika Waam.11:34; 1samw.21:11; 29:5. Maneno
Pr. Renatus M. Izumangiji Page 3
yaliyo katika 1samwel 29:5 ni ya kurudiarudia kama yanavyojionyesha(“Sauli ameua elfu
zake, Na Daud makumi elfu zake”).

SWALI; Kulikuwa na shida gani kwa mabinti wa kule Shilo waliotoka na KUCHEZA, na
Biblia inasema watu walifanya walivyotaka katika kitabu cha Waamuzi 21:23, 25?

JIBU: Neno WALIOCHEZA kwenye (Waam 21:23) katika lugha ya awali ya


KIEBRANIA ni Chul = ‫חּול‬
Neno hili humaanisha KUJINYONGANYONGA Kwa kiingereza TWIST or TURN ni
mchezo wenye kuashilia tendo la NGONO hasa kujinyonga viuno ili watazamaji wavutiwe
na ndicho kilichopelekea wale vijana wajichagulie kulingana na walivyovutiwa na kukamata
binti wa kuoa bila kufuata utaratibu, kwa sababu walichochewa na tamaa, na Biblia inasema
kila mtu alifanya yaliyokuwa mema machoni pake mwenyewe maana hapakuwa na mfalme.
( Waam 21:25). Kwahiyo wanaofanya hivyo ni kwa matakwa yao maana hawana mfalme wa
kuwaongoza yaliyo mema. Wengi wameiga toka hapo na kuingiza kanisani mahali
pasipohusika na mchezo huo mbaya.

SWALI; Katika kitabu cha 1Samwel 30: 16 , Biblia ya Kiingereza (KJV) inasema “And
when he had brought him down, there they were, spread out over all the land, eating
and drinking and dancing, because of all the great spoil which they had taken from
the land of the Philistines and from the land of Judah”. (1Sa 30:16 NKJ). Kiswahili
inasema “Na hapo alipokuwa amewaongoza chini,tazama,hao walikuwa wametawanyika juu
ya nchi yote, wakila na kunywa na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara, kubwa
walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda”.

Je watu hawa walikuwa wakicheza mchezo gani baada ya kula na kunywa? Katika Biblia ya
Kiswahili utakuta neno Karamu na Kiingereza (NIV)- New International Version
Husomeka “He led David down, and there they were, scattered over the countryside,
eating, drinking and revelinga because of the great amount of plunderb they had
taken from the land of the Philistines and from Judah. (1Sa 30:16 NIV)

Kabla sijatoa jibu la kucheza niruhusu nikuonyeshe chagamoto ya maandiko katika aya hiyo
hapo juu. Mwandishi wa New International Version ametaja jina David yaani Daud --‫ּדָ ֔ ִוד‬

Biblia ya Kiebrania katika fungu hili haitaji jina Daud bali imetumia kiwakilishi bila kutaja
jina, jambo hilo haliwezi kukutia hofu maana mwandishi wa New International Version
amechukua mada toka fungu la 15 akarudia kuweka jina badala ya kiwakilishi. Na mwandishi
wa Kiswahili ametumia kiwakilishi cha wingi maana Daud alikuwa na watu wengine mia
sita, lakini ya kiingereza imechukua mlengwa mkuu wa kisa hiki ambaye ni mfalme Daud
kama unavyoweza kusema “Leo Raisi wa Tanzania ametembelea hospital na kujionea
wagonjwa”. Kiuhalisia hawezi kuwa peke yake tu.

JIBU; Neno lililotumika hapo Dancing au reveling ni Chagag, yaani - ‫חגַג‬ָ


Neno hili humaanisha Shangwe, Nderemo, Vifijo katika sherehe kwa lugha ya kiingereza ni

Pr. Renatus M. Izumangiji Page 4


enjoy party: to have an enjoyable time in the company of others, especially at party
Kwa hiyo neno hili halihusiani na mambo ya ibada kanisani.

SWALI; Kwa nini Amos nabii anamlaum Daud kwa kujifanyizia vinada vingi katika Amos
6:3-6. Je, vinanda haviruhusiwi kanisani?

JIBU; Maneno yaliyotumika vinanda kwa lugha ya awali ni mawili (1) nebel = ‫נֶבֶל‬
(2) Keliy = ‫ּכלִי‬
ְ
Maneno haya hutafsiliwa kama vyombo vya muziki (musical instruments, vessels), kwa
hiyo Daud aliajili vikundi vya muziki kwa ajili ya maburudisho pale ikulu vilivyo toa
huduma wanapotoka vitani kwa ushindi yaani ( ORCHESTRA) na Brass band, vikundi hivi
havikuhusika na huduma ya ibada. Amos anawalaum wale wanaotumia miziki ya aina hiyo
katika ibada. Vyombo hivyo vimeonyeshwa katika kitabu cha Mwanzo 31:27 ambavyo
vilitumika katika sherehe mbalimbali za kale. Kanisa linasisitiza kusiwe na midundo
mchanganyiko inayoleta mihemuko na kuufanya mwili uhitaji kutikisika kwa kufuata mapigo
hayo. Sherehe hizo nyingi zilikuwa za kifamilia kama zilivyo leo sherehe za (Send off na
Kitchen party ) zilizoshamili siku hizi.

SWALI; Kwa nini Sulemani katika kitabu cha Mhubiri 3:4, anasema “Wakati wa kulia na
wakati wa kucheza. Wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza”. Kosa lake ni lipi mbona
anakazia swala la kucheza?

JIBU; Neno lililotumika hapa ni raqad = ‫ָרקַ ד‬


Neno hili kwa lugha ya kiingereza humaanisha ( skip au jump) rukaruka kwa furaha na
shangwe kama ndama wa mazizini tena bila muziki. Na kama utatumia muziki ni kama
wanavyofanya wacheza mpira wanapokuwa wameishinda timu pinzani wanavyopuliza
pembe za wanyama, matarumbeta na kurukaruka wakiwafanyia mizaha washabiki wa timu
iliyoshindwa. Neno hili hupatikana pia katika kitabu cha 1Nyak 15:29 ambapo utakuta
maneno mawili ya Kiebrania = ‫ָׂשחַק ָרקַ ד‬
Maneno hayo hapo moja ni sachaq {saw-khak'} na la pili ni raqad moja lina maana Play na
lingine skip na mtu akikuambia kwa kiingereza kwamba ( play music ) hana maana ya
dance music, bali anamaanisha piga au kama ni kinanda maana yake bonyeza vile vitufe (
Button bar ). Soma 1Nyak 15:29 KJV (And it happened, as the ark of the covenant of the LORD
came to the City of David, that Michal, Saul's daughter, looked through a window and saw King David
whirling and playing music; and she despised him in her heart. (1Ch 15:29 NKJ)
Neno hili raqad hupatikana pia katika kitabu cha Ayub 21:11 (Huwatoa kama kundi watoto
wao, Na watoto wao hucheza. Kwa hiyo watoto wa ng`ombe hawachezi muziki ila
kurukaruka tu.

Kwa mafungu hayo na maelezo yake nakutakia kuendelea kujifunza zaidi ili kupata maarifa
na Bwana akubariki kwa kutumia muda huo wa kujifunza, na kama nilivyotangulia kusema
ya kwamba sehemu yoyote yenye utata usisite kuwasiliana ili tuendelee kujifunza zaidi kwani
masomo yanayotatiza ni mengi tutaendelea kuyatoa panapo patikana nafasi ya kuyachambua.

BWANA AKUBARIKI.

Pr. Renatus M. Izumangiji Page 5


Ndimi katika shamba la Bwana- Mch. Renatus M. Izumangiji.

( 0756802242 / 0785822225 ).

Pr. Renatus M. Izumangiji Page 6

You might also like