You are on page 1of 20

4.

Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

Ruhusa ya kutangaza maneno kwa mtu aliyedhulumiwa; Allah-Subhaanahu wa taala Anasema; 148. Allah Hapendi utangazwaji wa maneno mabaya ila kwa yule mwenye kudhulumiwa. Na Allah Yu Mwenye Kusikia, Mwenye kujua. Ali bin Abi Talha amesema kwamba Ibn Abbas ameeleza kuhusu Aya (Allah Hapendi utangazwaji wa maneno mabaya) kwamba Allah-Subhaanahu wa taala Hapendi mtu yeyote kumuomba Yeye mabya dhidi ya mtu mwingine isipokuwa ikiwa mtu kadhulumiwa. Katika hali hiyo Allah-Subhaanahu wa taala Anaruhusu aliyefanyiwa vibaya kumuomba Yeye dhidi ya huyo aliyemdhulumu. Na hii ndiyo maana Allah-Subhaanahu wa taala Anasema; (...ila kwa yule mwenye kudhulumiwa). Lakini ni bora sana mtu kuwa na subira. Al-Hasan Al-Basri ameeleza; Mtu asimuombee laana mtu yeyote aliyemdhulumu ila aombe, Eeh Allah, Uliye mtukufu Nisaidie mimi dhidi yake na Unichukulie mimi haki yangu kutoka kwake Na katika upokezi mwingine Al-Hasana amesema; Allah-Subhaanahu wa taala Ameruhusu mtu kuomba dhidi ya aliyemdhulumu bila ya kuchupa mpaka. Abdul-Karim bin Malik Al-Jazari anasema kuhusu Aya hii; Pale mtu anapokulaani wewe, wewe pia unaweza kumlaani yeye kwa kisasi. Lakini ikiwa mtu atasema uwongo dhidi yako, wewe huwezi kusema uwongo dhidi yake. Na kwa hakika yeyote atakayechukua kisasi baada ya yeye kudhulumiwa, basi, katu hapana njia ya kuwalaumu wao.(Q42:41) Imam Abu Daud amerikodi kwamba Abu Hurayrah amesema ya kuwa Mtume wa Allah-Subhaanahu wa taala amesema; Kwa maneno yoyote yale ambayo yatatumiwa na watu wanaolaaniana, basi, yule aliye anza ndiye atakayeubeba ule mzigo, isipokuwa ikiwa yule aliyedhulumiwa atachupa mpaka.

94

Wanafiki na wale waliyo wandani wa makafiri watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahanamu. Isipokuwa ikiwa wao watatubu kabla ya kifo chao; Allahu-Subhaanahu wa taala Anasema; 145. Kwa hakika waliyo wanafiki wao watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni... Siku ile baada ya hukumu kwa ile kufuru yao iliyo kubwa. Al-Walib (Ali bin Abi Talha) amesema kwamba Ibn Abbas amesema (katika tabaka la chini kabisa Motoni) maana yake chini kabisa ya Moto. Na wanazuoni wengine wanasema Moto una kina cha chini kabisa kama vile Pepo ilivyo na daraja za juu kabisa. Ibn Jarir amerikodi kwamba Abdullah bin Masud amesema, (kwa hakika waliyo wanafiki wao watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni) maana yake ndani ya masanduku ya Moto utakaowazingira wao, watakuwa wamefungiwa ndani yake Ibn Abi Hatami amerekodi kwamba pale Ibn Masoud alipoulizwa kuhusu hatima ya wanafiki, alisema; Wao watafungiwa katika masanduku ya Moto na watafungiwa humo katika tabaka ya chini kabisa Motoni. .....na katu wewe hutapata kwa ajili yao msaidizi yoyote. Ili kuwaokoa wao na adhabu iliyotiwa uchungu inayowakabili wao. Kisha Allah-Subhaanahu wa taala Anasema; Yeyote miongoni mwa hao wanafiki atakayetubu toba iliyo ya kweli na halafu akaifuatisha kwa matendo yaliyo mema huku akitumai rehema ya Mola wake. Na ndiyo maana Allah-Subhaanahu wa taala Anasema;

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

Ila wale ambao watatubu na wakajirekebisha na wakaishika kwa nguvu kamba ya Allah-Subhaanahu wa taala na kuihalisi Dini yao kwa ajili Yake... Wakibadilisha kule kujionyesha kwao (yaani ria katika mambo ya ibada) kwa unyenyekevu wa kweli ili kwamba matendo yao mema yapate kuwanufaisha wao, hata kama yakiwa machache. Basi, hapo watakuwa pamoja na wale waliyo waislamu (yaani siku ile ya kufufuliwa).

Na hivi karibuni Allah Atawapa wale waliyo waislamu tunzo iliyo kubwa kabisa. Kisha Allah-Subhaanahu wa taala Akaeleza ya kuwa Yeye ni mkwasi Asiyehitaji chochote na yeyote na kwamba Yeye Huadhibu waja kwa sababu ya madhambi yao! Na nini Allah Atakuwa Amefanya kwa kuwaadhibu nyinyi ikiwa nyinyi mtaikubali haki na kuipokea imani...! ..Na Allah Yu Mpole mno, Mwenye khabari zote. Allah-Subhaanahu wa taala Anawapenda watu waliyo na shukurani na Yeye Anawajua vyema wale wanaomuamini kwa dhati na Yeye Atawapa wao zawadi zilizo maridhawa.

93

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:145. Kwa hakika waliyo wanafiki wao watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni na katu wewe hutapata kwa ajili yao msaidizi yoyote. 4:146. Ila wale ambao watatubu na wakajirekebisha na wakaishika kwa nguvu kamba ya Allah na kuihalisi Dini yao kwa Allah, basi, hapo watakuwa pamoja na wale waliyo waislamu. Na hivi karibuni Allah Atawapa wale waliyo waislamu tunzo iliyo kubwa kabisa. 4:147. Na nini Allah Atakuwa Amefanya kwa kuwaadhibu nyinyi ikiwa nyinyi mtaikubali haki na kuipokea imani! Na Allah Yu Mpole mno, Mwenye khabari zote.
Marufuku ya kuwafanya wale ambao Si waislamu kuwa wandani (yaani watu wa kuwapa siri); Katika Aya ya 144 Allah-Subhaanahu wa taala Anasema;

Enyi, mliyoamini! Katu nyinyi msiwafanye makafiri kuwa marafiki (yaani wa kuwapa siri zenu) badala ya waislamu wenzenu.... Allah-Subhaanahu wa taala hapa Anawakataza waja Wake wanaomuamini Yeye kuwafanya wasiri wale waliyo makafiri, na hili ni pamoja na kufanya shirika nao, kutaka ushauri kwao na kutoa siri za waumini kwao. Katika Aya nyingine Allah-Subhaanahu wa taala Anasema;

Na Waislamu wasiwafanye makafiri kuwa marafiki (yaani wasiri) kinyume na Waislamu wenzao. Na yeyote anayefanya hivyo yeye hana uhusiano wowote na Allah ila ikiwa nyinyi mtakhofu shari kutoka kwao. Na AllahSubhaanahu wa taala Anakutahadharisheni nyinyi na ghadhabu Zake.... (Q3:28). Ikimaanishwa; Yeye Anakuonyeni nyinyi juu ya adhabu Yake ikiwa nyinyi mtayafanya yale Anayokukatazeni nyinyi. Na ndiyo maana Akaongeza hapo;

...Je, nyinyi mnataka kuweka ushahidi uliyo bayana dhidi yenu wenyewe mbele ya Allah (kuwa nyinyi ni wanafiki)? Ikimaanishwa; Ushahidi unaohalalisha nyinyi kupata adhabu. Ibn Abi Hatami anasimulia kwamba Ibn Abbas amesema; Neno Sultan ndani ya Qurani maana yake ni Ushahidi Kuna mlolongo mzuri wa upokezi wa maneno haya ambayo hata Mujahid, Ikrimah, Said bin Jubayr, Muhammad bin Kaab, Al-Quraiz, Adh-Dhahak, As-Suddi na An-Nadr bin Arabi wote wanayakubali.

92

4:136. Enyi mliyoamini! Muaminini Allah na Mtume Wake na Kitabu (yaani hii Qurani) ambacho Yeye Ameteremsha juu ya Mtume Wake na Vitabu ambavyo Yeye Aliteremsha hapo kabla. Na yeyote anayemkataa Allah na malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ile ya Mwisho, basi, kwa hakika yeye amekwishapotoka mbali kabisa na haki.

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:137. Kwa hakika wale waliyoikubali imani kisha wao wakakufuru halafu wao wakaamini halafu wakawa makafiri tena kisha wakazidisha kufuru; Allah Hatawasamehe wao wala Hatawaonyesha wao njia. 4:138. Watangazie wale waliyo wanafiki ya kuwa kwao wao iko adhabu yenye kutiwa uchungu. 4:139. Wale wanaowafanya makafiri kuwa rafiki badala ya Waislamu wenzao. Je, wao wanatafuta utukufu kwao? Basi, utukufu wote ni wa Allah. 4:140. Na kwa hakika Allah Amekwishateremsha kwenu nyinyi katika Kitabu kuwa pale nyinyi mnaposikia Aya za Allah zikipingwa na kuchezwa shere, basi, katu nyinyi msikae pamoja nao hadi wao waingie katika mazungumzo mengine! Vinginevyo na nyinyi mtakuwa mfano wao. Kwa hakika Allah Atawakusanya wale waliyo wanafiki na waliyo makafiri wote katika Moto Jahannamu. 4:141. Wale ambao walikuwa wanatazama nafasi zenu, pale nyinyi mnapopata ushindi toka kwa Allah wao husema; Je, sisi hatukuwa pamoja nanyi? Na ikiwa makafiri watapata fungu wao huwaambia wao; Hivi sisi hatukuwa na uwezo juu yenu na tukakulindeni nyinyi dhidi ya Waislamu? Basi, Allah Atahukumu kati yenu nyinyi wote Siku ile ya hukumu. Na katu Allah Hatawapa makafiri njia dhidi ya Waislamu. 4:142. Kwa hakika wale waliyo wanafiki wanafikiri ya kuwa wao wanamhadaa Allah na Yeye Atawashika wao kwa hadaa zao. Pale wao wanaposimama kwa kuswali wao husimama na mioyo iliyoshindwa ili kujionyesha tu kwa watu na wala hawajishughulishi katika kumkumbuka Allah (kwa nyiradi mbali mbali) ila kidogo tu. 4:143. Wakiyumbayumba kati ya hayo (ya Uislamu na Ukafiri) Si wa upande huu wala upande ule na yule ambaye Allah Amemwacha yeye kwenda kombo wewe hutaweza kumpatia yeye njia. 4:144. Enyi, mliyoamini! Katu nyinyi msiwafanye makafiri kuwa marafiki (yaani wa kuwapa siri zenu) badala ya waislamu wenzenu. Je, nyinyi mnataka kuweka ushahidi uliyo bayana dhidi yenu wenyewe mbele ya Allah (kuwa nyinyi ni wanafiki)? 91

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:128. Na ikiwa mwanamke yeyote ataogopa kukandamizwa au kupuuzwa na mume wake, basi, hapana dhambi juu yao kuwa wao watafute kati yao mapatano. Na mapatano ni bora zaidi (kuliko magomvi na kutengana katika ndoa). Na nyoyo zimezongomezwa na tamaa. Na ikiwa nyinyi mtafanya yaliyo mazuri na kumcha Allah, basi, kwa hakika Allah Yu Mwenye khabari ya matendo yenu yote. 4:129. Na katu nyinyi hamtaweza kwamba muwatendee wanawake katika hali iliyo sawa hata ikiwa nyinyi mtatamani kufanya hivyo, hivyo, basi hii isiwe ndio sababu ya nyinyi kuelemea kabisa upande mmoja na kumwacha yule mwingine kuwa kama aliyetungikwa kati. Na ikiwa nyinyi mtafanya yaliyo mazuri na kumcha Allah, basi, kwa hakika Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 4:130. Na ikiwa wao wawili watatengana, basi, Allah Atamfanya kila mmoja wao kuwa huru na mwingine kwa ukarimu Wake. Na Allah Yu Karimu mno, Mwenye hekima. 4:131. Na ni miliki ya Allah tu vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Na kwa hakika wale waliyopewa Kitabu kabla yenu nyinyi na nyinyi pia nyote mmekwishaamrishwa kumcha Allah. Lakini ikiwa nyinyi mtakufuru, kwa hakika ni miliki ya Allah tu vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Na Allah Yu Mkwasi juu ya mahitaji-yote, Mwenye Kutukuzwa. 4:132. Na ni miliki ya Allah tu vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Na Allah Yu Mwenye Kutosha kuachiwa mambo. 4:133. Enyi watu! Ikiwa Yeye Atataka Yeye Atakuondoeni nyinyi na Kuleta wengine. Na Allah Yu Mwenye uwezo wa kulifanya hilo. 4:134.Yeyote anayetamani tunzo za Duniya, basi, kwa Allah ndiko kwenye tunzo za Duniya na Akhera. Na Allah Yu Mwenye kusikia, Mwenye kuona. 4:135. Enyi mliyoamini! Nyinyi simameni imara kwa ajili ya haki mkitoa ushahidi kwa Allah hata ikiwa katikao mna khasara kwenu nyinyi au kwa wazazi wenu au kwa ndugu zenu. Dhidi ya yule ambaye nyinyi mtatoa ushahidi akiwa ni tajiri au masikini, vyovyote iwavyo Allah ni Mwenye uwezo mkubwa kuliko yeyote juu yao, basi, nyinyi msifuate matakwa yenu msije kuwa mbali kabisa na haki. Na ikiwa nyinyi mtapotosha (ushahidi) au kupuuza, basi, kwa hakika Allah Yu Mwenye khabari ya matendo yenu yote. 90

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:119. Ninaapa kwa hakika mimi nitawapotoa wao na kwa hakika mimi nitaamsha ndani yao tamaa na kwa hakika mimi nitawaamuru wao kuchana masikio ya mifugo (kuweka alama ya miliki) na kwa hakika mimi nitawaamuru wao kugeuza umbo Aliloumba Allah (kwa mikorogo na matumizi ya nywele na kucha za bandia). Na yeyote anayemfanya shetani kuwa rafiki mbali na Allah, basi, yeye amekwishapata khasara iliyo bayana. 4:120. Shetani huwaahidi wao na huchochea ndani yao tamaa. Na Shetani hawaahidi wao kitu ila hadaa tu. 4:121. Mwisho wao ni Moto Jahanamu na katu wao hawatapata mahali Pa kuukwepea. 4:122. Lakini wale waliyoamini na wakafanya matendo yaliyo mazuri hivi karibuni Sisi Tutawaingiza wao katika mabustani ambayo hupita mito kwa chini yake na humo wao wataishi milele. Ahadi ya Allah iliyo kweli. Na ni nani mbali ya Allah aliye mkweli katika ahadi? 4:123. Haitakuwa kwa mujibu wa matakwa yenu wala kwa matakwa ya watu wa Kitabu! Yeyote anayefanya maovu yeye atalipwa kwayo na yeye hatapata mbali na Allah Mlinzi wala Msaidizi yeyote. 4:124. Na yeyote anayefanya yaliyo mema iwe ni mwanaume au mwanamke na yeye ni Muislamu, basi, wao wataingia Peponi na katu wao hawatadhulumiwa hata chembe. 4:125. Na ni nani aliye bora katika Dini kuliko yule anayeitiisha dhati yake kwa Allah-Subhaanahu wa taala na ni mfanyaji wa matendo yaliyo mazuri na anafuata imani ya Ibrahimu aliyejitenga mbali na uzushi wote (wa kuabudu masanamu)? Na Allah Alimfanya Ibrahimu kuwa rafiki wa karibu. 4:126. Na ni miliki ya Allah tu vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Na Allah Yu Mwenye udhibiti juu ya kila kitu. 4:127. Na wao wanakuuliza wewe hukumu yako kuhusu wanawake. Wewe waambie; Allah Anakupeni nyinyi hukumu kuwahusu wao na yale yanayosomwa kwenu katika hii Qurani kuhusu yatima wasichana ambao nyinyi hamuwapi wao kile kilichoamrishwa kwa ajili yao na nyinyi mnapuuza kuwaoa wao na kuhusu watoto walio wanyonge na kuhusu hili kuwa nyinyi mdumishe uadilifu kwa yatima. Na lolote zuri ambalo nyinyi mnafanya, basi, Allah Yu Mwenye khabari zake. 89

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:109. Mnasikia! Nyinyi ndio mnaowatetea wao katika haya maisha ya Duniya, basi, ni nani atakayewatetea wao mbele ya Allah Siku ile ya hukumu au ni nani atakayekuwa mtetezi wao? 4:110. Na yeyote anayetenda baya au dhuluma dhidi ya nafsi yake mwenyewe, halafu yeye akatafuta msamaha wa Allah Atakuta Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 4:111. Na yeyote anayechuma dhambi, basi, chumo lake ni dhidi ya nafsi yake mwenyewe. Na Allah Yu Mwenye Kujua, Mwenye hekima. 4:112. Na yeyote anaechuma dhambi, kisha yeye akaitupa kwa asiye na hatia, kwa hakika yeye ameleta masingizio na dhambi iliyo bayana. 4:113. Na ewe mpendwa (Mtume Muhammad-Swallallahu alayhi wasallama)! Lau Si rehema na huruma ya Allah iliyo juu yako wewe, basi, baadhi ya watu miongoni mwao walitamani ya kuwa wakupotoe wewe na wao hawapotoi ila nafsi zao wenyewe. Na wao hawatakudhuru wewe kitu. Na Allah Ameteremsha juu yako wewe hiki Kitabu na hekima na Amekufundisha wewe yale ambayo hukuyajua hapo kabla. Na ni nyingi mno neema za Allah zilizo juu yako wewe. 4:114. Hapana jema katika mengi ya mashauriano yao, ila ya wale wanaoamrisha (utoaji wa) sadaka au matendo yaliyo mazuri au kutengeneza amani kati ya watu. Na yeyote anayefanya hayo kwa kutafuta radhi ya Allah, basi, hivi karibuni Sisi Tutampa yeye tunzo iliyo kubwa kabisa. 4:115. Na yeyote anayempinga Mtume baada ya njia ya haki kubainishwa kwake na yeye akafuata njia mbali na njia ya waliyo waumini (yaani Waislamu), Sisi Tutamwacha yeye katika yale ambayo amechagua na kisha Sisi Tutamtupa yeye Motoni. Na ni mahali pabaya palioje kwa mtu kurejea! 4:116. Allah Hasamehe Yeye Kufanyiwa washirika lakini Yeye Husemehe kilicho chini ya hapo kwa yule ambaye Yeye Anataka. Na yeyote anayemfanyia Allah washirika kwa hakika yeye amepotoka mbali kabisa na haki. 4:117. Washirikina hawaabudu kitu mbali na Allah ila masanamu yasiyo na uhai na wao hawaabudu ila shetani aliyeasi. 4:118. Yule ambaye Allah Amemlaani. Na alisema; Kwa hakika mimi nitachukua kundi kubwa la waja Wako. 88

4:102. Na ewe Mpendwa (Mtume MuhammadSwallalahu alayhi wasallam)! Pale wewe unapokuwa kati yao, basi, wewe waongoze wao katika swala na uache kundi lisimame pamoja nawe na wachukue silaha zao, basi, watakapomaliza kusujudu kwao waondoke na warudi nyuma; Na hapo kundi ambalo bado halijaswali wakati huo lije na kukufuata katika swala na wao pia uwaache wachukue njia za kujilinda kwao na silaha zao. Makafiri wanatamani lau nyinyi mgekuwa wazembe na silaha zenu na mizigo yenu ili wao wapate kukuvamieni nyinyi. Na hapana makosa juu yenu nyinyi ikiwa mtapata matatizo kwa mvua au nyinyi kuwa wagonjwa ya kuwa nyinyi mziache silaha zenu na mchukue hadhari yenu. Kwa hakika Allah Amewaandalia wale waliyo makafiri adhabu kali yenye kudhalilisha. 4:103. Na pale nyinyi mnapomaliza swala, basi, mumkumbuke Allah (kwa nyiradi mbalimbali) mkiwa wenye kusimama, wenye kukaa na wenye kulalia mbavu zenu. Na pale nyinyi mnapokuwa na amani, basi, imarisheni swala kama kawaida. Kwa hakika swala kwa Waislamu ni wajibu uliowekewa nyakati maalumu.

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:104. Na msiwe wazembe katika kuwatafuta makafiri; Ikiwa nyinyi mnasumbuka, basi, na wao pia wanasumbuka namna mnavyosumbuka nyinyi; Na nyinyi mnataraji toka kwa Allah vile ambavyo katu wao hawatarajii. Na Allah Yu Mwenye Kujua, Mwenye hekima. 4:105. (Ewe mpendwa Mtume)! Mimi Nimeteremsha kwako wewe hiki Kitabu na ukweli ili wewe upate kuhukumu kati ya watu vile unavyoongozwa na Allah. Na hivyo wewe usiwe mtetezi wa wale waliyo wasaliti (wa nafsi zao). 4:106. Na utafute msamaha wa Allah, kwa hakika Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 4:107. Na wewe usiwatetee wale wanaozihadaa nafsi zao. Kwa hakika Allah Hampendi kila aliye mdanganyifu mno, aliye mwingi wa dhambi. 4:108. Wao wanajificha kwa watu lakini hawajifichi kwa Allah na Allah Yu pamoja nao pale wao wanapopanga katika nyoyo zao yale mambo yanayomchukiza Yeye. Na Allah Yu Mwenye Kuyazingira yote yale wanayotenda. 87

4. Suuratun Nisaai

4:95. Wale waislamu wanaobaki nyuma (majumbani) bila ya kuwa na udhuru (unaokubalika kisharia) na wale wanaoshindana katika njia ya Allah kwa mali zao na nafsi zao hawako sawa. Allah Amewainua madaraja wale ambao walishindana kwa mali zao na nafsi zao juu ya wale waliobaki (wasiende vitani kwa dharura). Na Allah Amewaahidi wao wote kilicho kizuri (yaani Pepo). Na Allah Anawapenda zaidi wale wenye kushindana, kwa nguvu zao zote juu ya wale wenye kubaki, kwa tunzo kubwa. 4:96. Toka Kwake madaraja na msamaha na huruma. Na Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma.

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:97. Wale ambao roho zao hutolewa na Malaika na huku wao ni wenye kudhulumu nafsi zao. Malaika huwaambia wao; Nyinyi mlikuwa katika nini? Wao watasema; Sisi tulikuwa wanyonge katika nchi. Wao watawaambia; Ardhi ya Allah haikuwa na nafasi ya kutosha ya nyinyi kuhajiri ndani yake? Basi, makazi ya watu hao ni Moto Jahanamu. Na hapo ni mahali pabaya mno Pa mtu kufikia! 4:98. Ila wale wanaokandamizwa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto ambao katu wao hawawezi kubuni mpango au kupata njia yoyote (ya kujisaidia). 4:99. Basi, hao ndio ambao huenda Allah Akawasamehe wao makosa yao. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Aliye Msameheji mno. 4:100. Na yule ambaye atatoka na kuacha meko na nyumba yake katika njia ya Allah atakuta sehemu na nafasi tele katika ardhi. Na yeyote anayetoka nyumbani kwake akihajiri kwa Allah na Mtume Wake halafu kifo kikamkuta yeye, basi, tunzo yake I kwa Allah. Na Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 4:101. Na pale nyinyi mnaposafiri katika ardhi, basi, hapana dhambi juu yenu nyinyi ikiwa nyinyi mtaswali kwa kupunguza baadhi ya swala zenu kwa kukhofu makafiri kuwadhuru nyinyi. Kwa hakika waliyo makafiri ni maadui zenu waliyo bayana.

86

4. Suuratun Nisaai

4:90. Ila wale ambao wanauhusiano na wale watu ambao kati yao na nyinyi yapo makubaliano au wakujieni nyinyi kwa nyoyo zao kukosa nguvu za kupigana dhidi yenu au kupigana na watu wao wenyewe. Na lau Allah Angetaka kwa hakika Angewapa wao udhibiti juu yenu na hapo kwa hakika wangepigana nanyi. Basi, ikiwa wao watajitenga nanyi na hivyo kutopigana na wao wakakunyoosheeni nyinyi mkono wa amani, hapo katu Allah Hajafungua kwenu nyinyi njia yoyote dhidi yao. 4:91. Wewe utawakuta wengine wenye kutamani kuwa salama kutoka kwenu na kuwa salama kwa watu wao. Kila pale watu wao wanaporudishwa kwenye uharibifu, wao hufuata kichwa-kichwa. Basi, ikiwa wao hawatajitenga nanyi wala kukupeni nyinyi amani wala kuzuwiya mikono yao dhidi yenu, basi, nyinyi wakamateni wao na muwauwe popote pale mtakapowakuta. Na hawa ndiyo wale ambao dhidi yao Sisi Tunakupeni nyinyi amri iliyo bayana. 4:92. Na haifai kabisa kwa muislamu kumwaga damu ya Muislamu mwenzake ila kwa bahati mbaya na yeyote atakayemuuwa Muislamu mwenzake kwa bahati mbaya, basi, yeye amwache huru mtumwa muislamu na fidia ya damu ilipwe kwa ndugu wa marehemu aliyeuwawa ila ikiwa wao watasamehe kama sadaka. Lakini ikiwa yeye (huyo aliyeuwawa) ni kutoka kwa watu ambao ni maadui zenu na yeye ni muislamu, basi, ni kumwacha huru mtumwa Muislamu. Na ikiwa yeye ni toka kwa watu ambao kati yao na nyinyi yapo makubaliano, basi, yeye atalipa fidia kwa ndugu wa marehemu na kuacha huru mtumwa muislamu. Lakini kwa yule ambaye mikono yake haitaweza (kupata njia ya kumwacha huru mtumwa muislamu), basi, yeye atafunga miezi miwili yenye kufuatana, hii ndiyo toba yake kwa Allah. Na Allah Yu Mwenye Kujua, Mwenye hekima. 4:93. Na yeyote anayemuuwa muislamu kwa makusudi, malipo yake yeye ni Moto Jahanamu humo yeye ataishi milele na ghadhabu ya Allah I juu yake na Anamlaani yeye na Amemuandalia yeye adhabu kubwa kabisa. 4:94. Enyi mliyoamini! Pale nyinyi mnapotoka kwa ajili ya vita vya kidini fanyeni uchunguzi wa kina (kabla ya kumuuwa mtu vitani) na msimuambie yeyote anayekusalimuni nyinyi kuwa wewe Si muislamu, mkitafuta vizuri vya haya maisha ya Duniya, basi, kwa Allah zipo ngawira za kutosha. Hata nyinyi mlikuwa hivyo hapo kabla, kisha Allah Akakutunukieni nyinyi ridhaa Yake (na Akawafanya nyinyi kuwa waislamu); Kwa hivyo nyinyi mnawajibika kucghunguza. Kwa hakika Allah Yu Mwenye khabari ya yote mnayofanya.

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

85

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:82. Basi, hivi wao Si wenye kuitafakari hii Qurani? Na lau ingekuwa ni toka kwa asiyekuwa Allah, kwa hakika wao wangalikuta ndani yake makosa mengi. 4:83. Na pale linapowajia wao jambo lolote la kuridhisha au la kutia khofu wao hulitangaza; Na lau wao wangelirudisha kwa Mtume au kwa wale wenye mamlaka miongoni mwao, bila shaka wangalipata uhakika wake toka kwa wale wanaochunguza na kujua matokeo. Na lau Si huruma ya Allah na rehema Yake juu yenu nyinyi kwa hakika nyinyi mngalimfuata shetani ila wachache tu miongoni mwenu. 4:84. Basi, ewe Mpendwa! Pigana katika njia ya Allah, wewe hutakalifishwa ila nafsi yako na uwahimize Waislamu; Huenda Allah Akazuia mashambulizi ya waliyo makafiri. Na majeshi ya Allah ni yenye nguvu kubwa kabisa na adhabu Yake ni kali mno. 4:85. Yeyote anayetetea kwa ajili ya jambo jema lipo fungu kwa ajili yake. Na yeyote anayetetea kwa ajili ya jambo baya lipo fungu kwa ajili yake. Na Allah Yu Mwenye nguvu juu ya kila kitu. 4:86. Na pale nyinyi mnapotolewa salamu kwa maamkizi yaliyo mazuri, basi, nyinyi muitikie kwa maamkizi yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au rejesheni mfano wake. Kwa hakika Allah Yu Mwenye Kukijua kila kitu. 4:87. Allah ni Ambaye mbali Naye hapana Mola Anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Yeye tu. Na kwa hakika Yeye Atakukusanyeni nyinyi nyote Siku ile ya Kiyama ambayo katu haina shaka. Na ni nani Aliye mkweli katika maneno mbali na Allah! 4:88. Na mmepatwa na nini nyinyi hata mgawanyike makundi mawili kuhusu wale wanafiki? Na Allah Amewarudisha wao nyuma kwa sababu ya vile vitendo vyao vibaya. Nyinyi mnatamani kumuongoa yule ambaye Allah Amemwacha yeye kwenda kombo? Na yule ambaye Allah Amemwacha yeye kwenda kombo katu wewe hutapata njia kwa ajili yake. 4:89. Wao wanatamani ya kuwa lau na nyinyi mgekufuru namna wao walivyokufuru na hivyo nyinyi nyote kuwa sawa. Basi, katu nyinyi msimuone yeyote kati yao kuwa rafiki ila kama wao wataacha meko na nyumba zao katika njia ya Allah. Ikiwa wao watapuuza tena, basi, wakamateni na wauweni wao popote mnapowakuta na katu nyinyi msimfanye yeyote miongoni mwao kuwa rafiki au msaidizi. 84

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:75. Na mmepatwa na nini nyinyi hata hampigani katika njia ya Allah na kwa kuwahami watu wanyonge na wanawake na watoto ambao wanaomba; Ee, Mola Wetu! Ututowe sisi katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu na Utupe sisi mlinzi toka Kwako na Utupe msaada wowote toka Kwako. 4:76. Wale ambao wameamini hupigana katika njia ya Allah na makafiri hupigana katika njia ya shetani, basi, piganeni na marafiki wa shetani. Kwa hakika mkakati wa shetani (kila siku) ni dhaifu. 4:77. Hivi, wewe hujawaona wale ambao waliambiwa; Zuwiyeni mikono yenu na muimarishe swala na mlipe zaka. Basi, pale kupigana kulipowajibishwa kwao, tazama; Baadhi yao wakaanza kuwaogopa watu kama inavyostahiki kumuogopa Allah au hata zaidi ya hivyo. Na wao wakasema; Ee, Mola wetu! Kwa nini Umewajibisha kupigana juu yetu, Ungeturuhusu sisi kuishi kwa muda zaidi. Wewe sema; Anasa za hii Duniya ni kidogo na za Akhera ndio bora zaidi kwa wale waliyo wacha Mungu na nyinyi hamtadhulumiwa kitu hata kiwe kidogo mfano wa kipande cha uzi. 4:78. Popote utakapokuwa kifo kitakupata wewe hata uwe kwenye ngome zilizo madhubuti. Pale mazuri yanapowapata wao, hapo wao husema; Hili ni toka kwa Allah na ikiwa baya limewapata wao hapo husema; Hili ni kutoka kwako wewe. Wewe sema; Yote hutoka Kwake Allah! Basi, wamepatwa na nini wao, inaonekana wao ni wasiyojua lolote! 4:79. Ewe mtu! Zuri lolote linalokufikia wewe ni toka kwa Allah! Na baya lolote linalokusibu wewe ni toka kwako mwenyewe (ni athari ya madhambi unayofanya). Na ewe Mpendwa (Mtume Muhammad-Swallalahu alayhi wasallam)! Tumekutuma wewe Mtume kwa watu wote na Allah Yeye Anatosha kuwa shahidi. 4:80. Yeyote anayemtii Mtume kwa hakika yeye amemtii Allah. Na yeyote anayepuuza, basi! Sisi Hatukukutuma wewe kuwa mlinzi juu yao. 4:81. Na wao wanasema; Tumetii, lakini wanapoondoka katika hadhara yako, kundi miongini mwao hupanga njama nyakati za usiku dhidi ya yale waliyosema. Na Allah Huandika yale wanayopanga usiku kisha ewe Mpendwa! Wewe wapuuze wao na umtegemee Allah. Na Anatosha Allah kuwa Mwendeshaji wa mambo yote. 83

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:65. Basi! Kwa Jina la Mola wako wewe katu wao hawatakuwa waislamu ila kwanza wao wakufanye wewe (Mtume Muhammad-Swalallahu alayhi wasallama) kuwa hakimu katika mashauri yote miongoni mwao halafu wao wasione uzito wowote nyoyoni kuhusu kile ulichoamua na wakikubali toka kina cha nyoyo zao. 4:66. Na ingekuwa Sisi Tumewajibisha kwao kuwa; Ziuweni nafsi zenu au tokeni mkiacha meko na majumba yenu, basi, ni wachache tu miongoni mwao ndiyo wangetekeleza. Na lau wao wangefanya vile wanavyoambiwa! Hilo lingekuwa bora zaidi kwao na imara zaidi katika kule kuithibitisha imani yao. 4:67. Na lau ingekuwa hivyo! Kwa hakika Sisi Tungaliwapa wao tunzo iliyo kubwa kabisa toka Kwetu. 4:68. Na kwa hakika Sisi Tungaliwaelekeza wao njia iliyonyooka. 4:69. Na yeyote anayemtii Allah na Mtume Wake, basi, yeye atakuwa pamoja na wale wenye radhi ya Allah mfano wa wale Mitume, wasemaokweli na mashahidi na wale watu waliyo wema. Na ni wenza wazuri walioje! 4:70. Huo ni ukarimu wa Allah. Na Allah Yu Mwenye Kuwatosha, Aliye Mjuzi mno. 4:71. Enyi mliyoamini! Mchukue hadhari, halafu nyinyi muwaendee wale waliyo maadui platuni kwa platuni au muwaendee wao nyote kwa pamoja. 4:72. Na miongoni mwenu nyinyi yuko yule ambaye kwa hakika yeye atabaki nyuma, kisha ikiwa nyinyi mtapatwa na janga lolote yeye atasema; Ni mapenzi ya Allah kwangu mimi kwamba mimi sikuwa pamoja nao. 4:73. Na ikiwa nyinyi mtapata neema ya Allah, basi, kwa hakika yeye atasema, kana kwamba hapana urafiki wowote kati yenu nyinyi na yeye; Natamani ningekuwa pamoja nao maana hapo ningepata, kupata kwa kutosha. 4:74. Basi, waache wale wanaouza maisha ya hii Duniya kwa yale ya Akhera wapigane katika njia ya Allah. Na yeyote anayepigana katika njia ya Allah halafu yeye akauliwa au yeye akashinda, basi, hivi karibuni Sisi Tutampa yeye tunzo iliyo kubwa kabisa. 82

4:57. Na wale ambao wameamini na wakafanya matendo yaliyo mazuri; Hivi karibuni Sisi Tutawaingiza wao katika mabustani ambayo mito hupita chini yake, humo wao wataishi milele. Humo wao watakuwa na wake waliyo bikira na Sisi Tutawaingiza wao kwenye starehe za vivuli maridhawa. 4:58. Kwa hakika Allah Anakuamrisheni nyinyi kuzilipa amana kwa wenyewe na kuwa pale nyinyi mnapohukumu kati ya watu mhukumu kwa uadilifu. Kwa hakika Allah ni kuzuri kulikoje Anavyokuaseni nyinyi. Kwa hakika Allah Yu Mwenye Kusikia, Mwenye Kuona. 4:59. Enyi mliyoamini! Mumtii Allah na mumtii Mtume na wale wenye mamlaka ya kutoa amri miongoni mwenu. Halafu ikiwa kutatokea khitilafu yoyote miongoni mwenu, basi, nyinyi muirejeshe kwa Allah na Mtume Wake ikiwa kweli nyinyi ni mnaomuamini Allah na Siku ile ya Mwisho. Hilo ndiyo zuri zaidi na bora kabisa mwisho wake. 4:60. Je, wewe! Hujawaona wale ambao hudai ya kuwa wao wanayaamini yale ambayo yameteremshwa kwako na yale ambayo yaliteremshwa kabla yako? Halafu wao wanataka kumfanya shetani kuwa muamuzi, wakati wao wamekwishaamrishwa kuwa wamkatae kabisa. Na shetani anataka kuwapotosha wao mbali kabisa na iliyo haki.

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:61. Na pale wao wanapoambiwa; Njooni kwenye Kitabu kilichoteremshwa na Allah na kwa aliye Mtume, hapo wewe utawaona wale wanafiki wakitawanyika wakigeuza sura zao. 4:62. Basi, itakuwaje! Pale ile adhabu itakapowaangukia wao kwa sababu ya yale ambayo mikono yao imetanguliza? Halafu ewe Mpendwa! Wao wanakuja kwako wewe wakiapa kwa Allah ya kuwa; Kusudio letu ni wema na mapatano tu. 4:63. Allah Yu Mwenye Kuyajua yote, basi, wewe wapuuze na uwaase wao na uwaambie wao maneno yenye kuridhisha. 4:64. Na Sisi Hatukumtuma Mtume yeyote ila kwamba yeye atiiwe kwa kutaka Kwake Allah. Na kama pale wao wanapodhulumu nafsi zao wangekuja kwako ewe Mpendwa (Mtume Muhammad-Swallalahu alayhi wasallam)! Halafu wao wakaomba msamaha kwa Allah na Mtume akawaombea wao, basi, kwa hakika wao wangemkuta Allah kuwa Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 81

4. Suuratun Nisaai

4:47. Enyi watu wa Kitabu! Muyaamini yale ambayo Sisi Tumeteremsha yenye kukisadikisha Kitabu mlichonacho kabla Sisi Hatujafuta baadhi ya nyuso na kuzigeuza nyuma ya migongo yao au Sisi Tuwalaani wao namna Tulivyowalaani watu wa Sabt (yaani siku ya Jumamosi). Na Amri ya Allah I yenye kutekelezwa.

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:48. Kwa hakika Allah katu Yeye Hawasamehe wale wanaomfanyia Yeye washirika, lakini Yeye Atasamehe kile kisichokuwa hicho kwa yeyote ambaye Yeye Anataka. Na yeyote anayemfanyia Allah washirika kwa hakika yeye amezusha dhambi iliyo kubwa kabisa. 4:49. Je, wewe hujawaona wale ambao huzitakasa nafsi zao? Sivyo hivyo! Ni Allah tu Ndiye Humtakasa yule Anayemtaka. Na wao hawatadhulumiwa kitu hata kiwe mfano wa ki-uzi kilicho kwenye ufa wa kokwa la tende. 4:50. Tazama! Vipi wao wanazusha juu ya Allah uwongo. Na hilo peke yake ni dhambi tosha. 4:51. Hivi! Wewe hujapata kuwaona wale watu ambao walipewa sehemu ya Kitabu; Wao wanaamini masanamu na mashetani na wao huwaambia wale waliyo makafiri; Nyinyi ni wenye kuongoka njia kuliko waislamu! 4:52. Hawa ndio wale ambao Allah Amewalaani wao. Na yeyote ambaye Allah Amemlaani, basi, katu wewe hutopata kwa ajili yake yeye msaidizi yeyote. 4:53. Au wao wanafungu lolote katika ufalme? Na ikiwa hivyo, basi, wao hawataweza kuwapa watu hata ile chembe. 4:54. Au ndo tuseme wao wanawahusudu watu kwa vile ambavyo Allah Amewapa wao kwa ukarimu Wake? Basi, Sisi Tuliwapa Kitabu na hekima (yaani Unabii na Utume) watoto wa Ibrahimu na Tuliwapa wao ufalme mkubwa. 4:55. Halafu baadhi yao walimuamini Yeye na wengine walimpuuza; Unaowatosha wao ni Moto Jahanamu wenye kuwaka vikali mno. 4:56. Wale ambao wamezikataa Aya Zetu hivi karibuni Sisi Tutawafanya wao kuingia Motoni. Kila pale ngozi zao zinapobabuka Sisi Tutazibadilisha kwa ngozi zingine ili wao wapate kuionja adhabu. Kwa hakika Allah Yu Mwenye nguvu mno, Mwenye hekima. 80

4. Suuratun Nisaai

4:38. Na wale ambao hutoa mali zao kwa kujionyesha kwa watu na hali ya kuwa wao hawana imani na Allah wala Siku ile ya Mwisho na ambao shetani ni mshirika wao, basi, ni mshirika mbaya alioje! 4:39. Na yapo madhara gani ikiwa wao watamuamini Allah na Siku ile ya Mwisho na wakatoa katika vile ambavyo Allah Amewapa wao? Na Allah Yu Mwenye Kuwajua wao.

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:40. Allah katu Yeye Hadhulumu kitu hata kiwe ni cha uzani wa chembe. Na ikiwa patakuwa na kitendo kizuri Yeye Hukizidisha na Hutoa toka Kwake tunzo iliyo kubwa. 4:41. Basi, itakuwaje! Wakati Sisi Tutakapoleta toka kila umati shahidi na ewe Mpendwa Muhammad! Sisi Tukulete wewe kuwa shahidi na mdhamini dhidi ya wao wote? 4:42. Siku hiyo, wale ambao hawakuamini na wakamuasi Mtume watatamani kwamba ardhi ingesawazishwa juu yao baada ya wao kuzikwa humo na katu wao hawataweza kumficha Allah kitu chochote. 4:43. Enyi mliyoamini! Katu nyinyi msiiendee swala huku nyinyi mmelewa ila kwanza nyinyi myajue yale mnayosoma wala wakati nyinyi mna janaba ila kwanza muoge isipokuwa kama nyinyi mnasafiri. Na ikiwa nyinyi mnaumwa au mko safarini au kuwa mmoja wenu katoka chooni au nyinyi mmewagusa wanawake na hamkupata maji, basi, mchukue mchanga safi na mpanguse kwao nyuso zenu na mikono yenu (yaani Mtayammamu). Kwa hakika Allah Yu Mwenye kusamehe, Aliye Msameheji mno. 4:44. Je, wewe hujapata kuwaona wale watu waliyopewa sehemu ya Kitabu ? Wao wananunua upotofu na wao hutamani ya kuwa na nyinyi pia muipotee njia. 4:45. Na Allah Anawajua vyema maadui zenu. Na Allah Anatosha kuwa Mlinzi na Allah Anatosha kuwa Msaidizi. 4:46. Baadhi ya mayahudi hupotoa maneno kutoka nafasi yake na wao husema; Sisi tumesikia na hatutii na (husema) sikia usiwe mwenye kuelewa na husema raaina wakipindisha ndimi zao wakiikejeli Dini. Na lau wao wangesema; Tumesikia na tumetii na bwana utusikilize na bwana utuangalie ingalikuwa bora kwao na adilifu zaidi. Lakini Allah Amewalaani wao kwa ukafiri wao na hivyo wao hawaamini ila wachache tu. 79

4. Suuratun Nisaai

4:31. Ikiwa nyinyi mtajitenga na madhambi makubwa yale ambayo nyinyi mnakatazwa Sisi Tutakusameheni nyinyi madhambi yenu mengine na Tutawafanya nyinyi muingie sehemu yenye kutukuzwa (yaani Peponi).

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:32. Na nyinyi msitamani vile ambavyo Allah Amewafanya wengine kuwa bora kwavyo juu ya wengine. Kwa wanaume lipo fungu katika chumo lao na kwa wanawake pia lipo fungu katika chumo lao. Na mumuombe Allah katika neema Zake. Kwa hakika Allah Yu Mwenye Kukijua kila kitu. 4:33. Na kwa kila mmoja Sisi Tumefanya warithi wa mali ambazo huachwa na wazazi na ndugu na wale ambao nyinyi mmeapizana mkataba nao, basi, muwape wao fungu lao. Kwa hakika Allah kila kitu Ki mbele yake. 4:34. Wanaume ndiyo wenye mamlaka juu ya wanawake kwa sababu Allah Amemfanya mmoja wao kuwa juu ya mwingine na kwa sababu wanaume hutumia mali juu yao, kwa hivyo! Wanawake wazuri ni wale waliyo watii, pale mume hayupo wao hutunza vile ambavyo Allah Ameamuru vitunzwe. Na kwa wale wanawake ambao nyinyi mnakhofu uasi toka kwao, basi, muwaonye wao na mjitenge nao katika malazi na wapigeni (Si kwa kuwatoa damu) na ikiwa wao watakuja chini ya amri yako, basi, usitafute njia yoyote ya kuchupa mpaka dhidi yao. Kwa hakika Allah Yu Mwenye kutukuka wa Juu kabisa, Aliye Mkubwa. 4:35. Na ikiwa nyinyi mtakhofu ugomvi kati ya mume na mke, basi, teueni msuluhishi toka upande wa familia ya mwanaume na msuluhishi upande wa familia ya mwanamke, ikiwa wao wawili watataka mapatano, basi, Allah Atajaalia maungano kati yao. Kwa hakika Allah Yu Mjuzi mno, Mjua-yote. 4:36. Na mumuabudu Allah tu na nyinyi msishirikishe Naye yeyote na mfanye wema kwa wazazi na ndugu na yatima na wahitaji na majirani wa karibu na majirani wa mbali na aliye mshirika wa upande wako na msafiri aliyeharibikiwa na wale watumishi wenu wa kiume na kike. Kwa hakika Allah Hawapendi watu wenye kiburi, wenye majivuno. 4:37. Wale ambao wao hufanya ubakhili na huwashawishi wengine kufanya ubakhili na huficha vile ambavyo Allah Amewapa wao kwa ukarimu Wake. Na Sisi Tumewaandalia waliyo makafiri adhabu yenye kudhalilisha.

78

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya tano : Q4:24-Q4:147)

Walmuhsanaatu.

4:24. Na waliyoharamishwa kwenu nyinyi ni wanawake waliyo na waume ila wale wanawake wa makafiri ambao nyinyi mmewapata (mateka vitani). Haya ni maelekezo ya Allah kwenu nyinyi na wengine wasiokuwa hao ni halali kwenu nyinyi, ila kwamba muwatafute wao kwa mali zenu na kuwaowa na sio kutamani zinaa. Kwa hivyo, kwa wale wanawake ambao nyinyi mnataka kuwaoa, basi, wapeni wao mahari zao kama ilivyopangwa. Na hapana dhambi juu yenu nyinyi katika vile ambayo nyinyi mmeridhiana nao baada ya yale yaliyopangwa. Kwa hakika Allah Yu Mjuzi mno, Mwenye hekima. 4:25. Na yule kati yenu nyinyi ambaye yeye hawezi kuoa mwanamke huru aliye muumini kwa kutokuwa na uwezo wa kutosha, basi na aowe katika wale wajakazi waumini waliyo katika miliki ya mikono yenu. Na Allah Yu Mwenye kuijua imani yenu nyinyi vizuri sana; Baadhi yenu nyinyi ni kutoka kwa wengine, kwa hivyo muwaoe wao kwa idhini ya bwana zao na muwape wao mahari zao kama ilivyo desturi na kuwaowa wao na sio kutamani zinaa wala kuwaweka vimada. Na pale wao watakapoolewa na halafu wakafanya yale machafu (ya zinaa), basi, juu yao ni nusu ya ile adhabu iliyo juu ya wale wanawake waungwana. Haya ni kwa ajili ya yule kati yenu ambaye yeye anaogopa kule kuzini. Lakini ni bora zaidi kwenu nyinyi kuwa na subira. Na Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 4:26. Allah Anataka Kukufafanulieni nyinyi Amri Zake na Kukujulisheni nyinyi njia za wale wa kabla yenu na Kukuelekeeni nyinyi na huruma Yake. Na Allah Yu Mjuzi mno, Mwenye hekima. 4:27. Na Allah Anataka Kukuelekeeni nyinyi na huruma Yake na wale wanaofuata matamanio yao wanataka na nyinyi mpotoke mbali kabisa na njia iliyo sahihi. 4:28. Allah Anataka Kukufanyieni nyinyi wepesi. Kwani mtu Ameumbwa dhaifu. 4:29. Enyi mliyoamini! Katu nyinyi msiliane kwa dhuluma mali miongoni mwenu ila iwe ni biashara kwa makubaliano miongoni mwenu. Na katu nyinyi msijiue wenyewe. Kwa hakika Allah Yu Mwenye huruma mno kwenu. 4:30. Na yeyote atakayefanya hayo kwa kuchupa mpaka na dhuluma, basi, Sisi Tutamfanya yeye kuingia Motoni. Kwa Allah hilo Li jepesi mno. 77

QURANI TUKUFU
kanzul Iman
(Khazina ya Imani)

na Imam Ahmad Raza Qadri Rahmatullah Alayhi

Iliyotarjumiwa katika lugha ya Kiingereza na Prof. Sayyid Shah Faridul Haque

na kutarjumiwa katika lugha ya kiswahili na Maalim. Yusufu Rajabu Kanyama.

You might also like