You are on page 1of 89

ZAWADI KWA WANANDOA

(Zawadi Kwetu)

Mwandishi: Yuwsuf 'Aliy Badiwi


Mfasiri: Abuu AArwa
Zawadi Kwa Wanandoa

Vitabu

Zawadi Kwa Wanandoa

Mwandishi: Yuwsuf 'Aliy Badiwi


Mfasiri: Abuu Aarwa
B
YALIYOMO.

 01-Zawadi Kwa Wanandoa: Mkataba: Makubaliano Na Maridhiano

 02-Zawadi Kwa Wanandoa: Nguzo Za 'Aqd Na Sharti Zake


 03-Zawadi Kwa Wanandoa: Mahari
 04-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutanguliza Na Kuchelewesha Mahari
 05-Zawadi Kwa Wanandoa: Chombo
 06-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumuusia Mke:
 07-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake
 08-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake
 09-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia wa Mume kwa Mkewe
 10-Zawadi Kwa Wanandoa: Usia wa Mama kwa Bintiye
 11-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutangaza Ndoa
 12-Zawadi Kwa Wanandoa: Yachukizayo Kwenye Sherehe ya Harusi
 13-Zawadi Kwa Wanandoa: Karamu ya Harusi (Walima)
 14-Zawadi Kwa Wanandoa: Siku Ya Mwanzo Ya Ndoa
 15-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo
 16-Zawadi Kwa Wanandoa: Swalah Ya Sunnah Kwa Wanandoa
 17-Zawadi Kwa Wanandoa: Unapomwingilia Mkeo
 18-Zawadi Kwa Wanandoa: Malipo Ya Kuingiliana
 19-Zawadi Kwa Wanandoa: Adabu Za Kuingiliana
 20-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuoga Baina Ya Matendo Ya Ndoa
 21-Zawadi Kwa Wanandoa: Adabu Za Mtu Na Ndugu Za Mke Wake
 22-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu Ya
Nyuma
 23-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuoga Katika Chombo Kimoja
 24-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuondosha Bikira
 25-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumchezea Mke
 26-Zawadi Kwa Wanandoa: Tendo La Ndoa Ni Ibada
 27-Zawadi Kwa Wanandoa: Kubusu Kabla Ya Kuingiliana
 28-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuchezea Chezea Kinembe
 29-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutafuta Raha Bila Ya Jimai
 30-Zawadi Kwa Wanandoa: Uhuru Wa Kuangalia Uchi
 31-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuondosha Nguo Zote
 32-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuchezeana Kwa Kuangaliana!
 33-Zawadi Kwa Wanandoa: Athari Za Sauti Na Harakati Katika
Kuchezeana
 34-Zawadi Kwa Wanandoa: Kulidekeza Jina La Mke
 35-Zawadi Kwa Wanandoa: Adabu Za Maisha Ya Ndoa
 36-Zawadi Kwa Wanandoa: Tabia Njema
 37-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuishi Nae Kwa Wema Hata Ikiwa
Unamchukia
 38-Zawadi Kwa Wanandoa: Uwastani Katika Wivu
 39-Zawadi Kwa Wanandoa: Uwastani Wa Kutoa Katika Matumizi
 40-Zawadi Kwa Wanandoa: Kujipamba Kwa Ajili Ya Mkeo
 41-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumsaidia Mke Katika Kazi Za
Nyumbani
 42-Zawadi Kwa Wanandoa: Kukubali Kukosolewa Na Mke Kwa
Moyo Mkunjufu
 43-Zawadi Kwa Wanandoa: Kujua Fiqhi Ya Wanawake
 44-Zawadi Kwa Wanandoa: Asimgongee Mwanamme Kumgongea
Mke Wake Usiku

 45-Zawadi Kwa Wanandoa: Baina Ya Wakwe Na Mke Wa Mtoto


Wao
01-Zawadi Kwa Wanandoa:
Mkataba: Makubaliano Na
Maridhiano

Zawadi Kwa Wanandoa

01-Mkataba: Makubaliano Na Maridhiano

‫عقد الزواج‬

Mkataba wa Ndoa ni dalili tosha inayoonesha kuwepo kwa maelewano na


makubaliano baina ya pande mbili, na kuridhiana baina ya mke na mume
katika kusimamisha mahusiano ya kisheria baina yao. Huwakilishwa
maridhiano haya katika maneno yanayotamkwa na yenye kupita baina ya
hawa wenye kuwekeana mkataba huu, na huitwa kuwa ni Ijab na Qabuul
02-Zawadi Kwa Wanandoa:
Nguzo Za 'Aqd Na Sharti Zake

Zawadi Kwa Wanandoa

02- Nguzo Za 'Aqd Na Sharti Zake

‫أركان العقد وشروطه‬

'Aqd inakamilika kwa kukamilika kwa masharti yafuatayo:

a) Idhini ya Walii.

b) Kuridhika kwa bibi harusi mtarajiwa.

c) Kutimia kwa tamko la ndoa


yaani Ijaab na Qabuul (yaani iijab na qubuul iliyounganishwa kwa tamko
la ndoa au yenye kufidisha maana hiyo).

d) Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.

e) Kubalighi na kuwa na utambuzi baina ya wanandoa, hivyo haifai


kuwepo kwa ndoa ikiwa mmoja wapo ni mwendawazimu au mdogo
kwa umri na bado hajabaleghe.
'Aqd hii inalazimika kwa pande zote mbili husika, ila katika baadhi ya
hali kama vile mwanamke kudanganywa na kughuriwa na
mwanamme au mwanamme kuoa mwanamke asiyezaa kisha
akagundua kuwa hazai na hakujua hilo kabla, katika hali hii anayo haki
ya kuvunja 'Aqd.

Na kwa hali hiyo hiyo ni kujionesha mwanamme kuwa ni mchaji


Allaah na mtu mwenye msimamo kisha baada ya muda ukadhihirika
ukweli kuwa ni muovu na ni mtu mpotevu hana sifa hizo za mwanzo,
hapa vile vile itavunjika 'Aqd yao.

Na kwa mfano huo huo ni kuoa kwa mwanamme msichana akitegemea


kuwa ni bikra kisha ikadhihirika kuwa sio bikra, au akaona aibu
nyingine iliyokuwa ni dhahiri na ya wazi kabisa au maradhi yenye
kuchukiza.

Imepokewa kutoka kwa Ka’ab bin Zaid kuwa Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) alioa mwanamke wa kabila la Banii Ghafaar,
alipokwenda kwake na baada ya kuweka nguo zake na kukaa katika
kitanda na kuona baina ya kitovu na mbavu weupe ambao ulimuondoa
na kukaa mbali nae na kuondoka kitandani, kisha akamwambia:
“Chukua nguo zako.” na hakuchukua alichompa (katika mahari.)” (Ahmad)

Amesema 'Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allahu 'anhu) kwa yule


bwana aliyeoa mwanamke nae (mwanamme) hazai, ‘Mwambie kuwa
wewe huzai na mpe uhuru wa kuchagua.’
03-Zawadi Kwa Wanandoa:
Mahari

Zawadi Kwa Wanandoa

03- Mahari

‫املهر‬

Ulipaji wa Mahari huwa unategemea jamii waliyopo waoaji na huwa


haina kiwango maalum. Na huitwa hayo mahari ‫ صداقا‬kwa maana ya
kuwa ni dalili ya ukweli wa mtu kutaka kuoa, na huitwa wakati
mwingine kuwa ni ‫ حنلة‬kwa maana ya kipewacho mtu kisichokuwa na

mbadala, na huitwa wakati mwingine kuwa ni ‫ حباء‬kwa maana ya


anachopewa mtu katika mali ili kumkirimu sahibu yake, au huitwa
kuwa ni ‫ عالقة‬yaani chenye kuunganisha baina ya wanandoa wawili.

Ndoa katika Uislam haiwi ila kwa Mahari, kwa dalili ya neno Lake
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :

‫وآ توا النساء صدقاتهن نحلة‬


“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)
Na Akasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Surat Al-
Ahzaab:

‫يا أيها النيب إنا أحللنا لك أزواجك الاليت آتيت أجورهن‬


“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-
Ahzaab: 50)

Na Akasema vile vile katika Surat An-Nisaa:

‫فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة‬


“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao
yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Uislam haukupanga malipo maalum ya mahari, cha kuzingatia hapa


katika mahari ni maridhiano ya pande mbili husika, lakini
kinachopendeza ni kuwa iwe hafifu na kinachowezekana bila ya taklifa
kwa yule muoaji.

Imepokewa kutoka kwa Aamir bin Rabia kuwa mwanamke wa kabila


la Banii fazara aliolewa kwa Ndara mbili, akasema Mtume (Swalla
AAllaahu 'alayhi wa sallam):

‫ فأجازه‬, ‫ نعم‬: ‫أرضيت عن نفسك ومالك بنعلني؟ فقالت‬


“Je, kwa Nafsi yako na kwa mali yako umeridhika kwa ndara mbili?
yule mwanamke akajibu: ‘ndio’, akamkubalia.” (At-Tirmidhiy)
Kutoka kwa Sahl bin Saad kuwa Mtume (Swalla AAllaahu 'alayhi wa
sallam) alimjia mwanamke akamwambia:

“Ee, Mtume wa Allaah mimi nimeitoa Nafsi yangu kwako, baada ya


kusema hivyo ikawa taabu kubwa (kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) ), akasimama mtu akasema, ‘Ee, Mtume wa Allah niozeshe
mimi kama wewe huna haja nae’, akasema Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) , ‘Je, una chochote cha kutoa sadaka?’ akajibu mtu
yule: ‘Sina isipokuwa ni hili shuka langu ninalojifungia,’ akasema
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Ukimpa hii shuka yako
utakaa bila kuwa na shuka ya kutumia, tafuta kitu kingine,’ akasema
mtu yule, ‘Sina kitu kingine.’ Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) kumwambia mtu yule, ‘Tafuta walau pete ya chuma’, mtu
yule akatafuta na hakupata kitu, akasema Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) kumwambia mtu yule, ‘Je, umehifadhi chochote
katika Qur’an?’ Akasema mtu yule, ‘ndio, sura kadha na kadha, na
akataja sura hizo.’ Hapo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
akasema, ‘Nimekuozesha kwa hicho ulichokuwa nacho katika Qur-
aan.’”

(Al-Bukhaariy na Muslim)

Imepokewa kutoka kwa Anas, kuwa Aba Twalhah alimposa Umu


Sulaym, akasema Umu Sulaym kumwambia Aba Twalhah, Wa-Allaahi!
mfano wako harejeshwi, lakini wewe ni kafiri na mimi ni Muislamu, na
haiwi halali kwangu kuolewa nawe, ukisilimu hiyo ndio mahari yangu,
na sitotaka kingine zaidi ya hilo. Na hiyo ndio ikawa mahari yake
(baada ya kusilimu Aba Twalhah).

Hadithi zote hizi za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)


zilizotangulia zinakubali mahari hata ikiwa ni ndogo kiasi gani.
04-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kutanguliza Na Kuchelewesha
Mahari

Zawadi Kwa Wanandoa

04-Kutanguliza Na Kuchelewesha Mahari

‫املعّج ل واملؤّج ل‬

Inafaa na inajuzu kutanguliza na kuchelewesha mahari. Kulipa


mwanzo na nyingine kuchelewa kama ilivyo kuwa ni ada na desturi ya
mahala na uwezo wa mtu.

Lakini kinachofaa zaidi ni kutanguliza chochote kwa yaliyopokewa na


ibn Abbas kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alimkataza
Ali kumuingilia bibi Fatma mtoto wake hadi awe ametoa chochote
katika mahari. Ali (Radhiya Allaahu 'anhu) akasema kumwambia
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Sina chochote’. Akasema
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : ‘Liko wapi deraya lako la
kihutwamiyya?’ Akampa ikawa ndio mahari yake.” (Abu Daawuwd, An-
Nasaaiy na Ahmad)
Na akasema bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) : “Ameniamrisha
mimi Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) nimuingize mwanamke
kwa mumewe kabla hajampa chochote.” (Abu Daawuwd).
05-Zawadi Kwa Wanandoa:
Chombo

Zawadi Kwa Wanandoa

05-Chombo

‫اجلهاز‬

‫اجلهاز‬ ni kutayarisha anachokihitaji bibi harusi katika vyombo vya


nyumbani kama vile fanicha ili aweke nyumbani kwake. Kilichozoeleka
ni kuwa Bibi harusi na ndugu za bibi harusi ndio wenye kutayarisha
vyombo hivyo na kuvipanga na kuitengeza nyumba, na wengineo
huwa wana tabia ya kuvionyesha vyombo hivyo kwa sherehe na hafla
za wazi. Leo hii sherehe kama hizi zinaishia katika mitaa wanayoishi
watu wa hali ya chini, ‘Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) alimtayarishia vyombo bibi Faatwimah ndani yake pana nguo
zilizofumwa kwa manyoya ya mbuni, na kiriba cha kuwekea maji na
mto wa kulalia uliowekewa mmea wenye harufu nzuri.’ (An-Nasaaiy).
06-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kumuusia Mke:

Zawadi Kwa Wanandoa

06-Kumuusia Mke

‫استحباب وصية الزوجة‬

Anas amesema: walikuwa Masahaba wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi


wa sallam) anapoelekea mke kwa mumewe, wanamuhimiza katika
kumuhudumia mumewe na kuangalia na kuchunga haki zake.
07-Zawadi Kwa Wanandoa:
Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake

Zawadi Kwa Wanandoa

07- Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake

‫وصّية األب ابنته‬

'Abdullaah bin Ja'far bin Abi Twaalib amemuusia binti yake kwa
kumuambia, ‘Ole wako na wivu, nao ni ufunguo wa Talaka. Na ole wako na
malalamiko mengi, nayo hupelekea katika bughudha. Na jitie wanja kwani
huko ndiko kujipamba kuzuri zaidi. Na kizuri katika vizuri zaidi ni Maji.’
08-Zawadi Kwa Wanandoa:
Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake

Zawadi Kwa Wanandoa

08-Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake

‫وصّية العم لصهره‬

'Aliy bin Abi Tawalib (Radhiya Allaahu 'anhu) alipo posa kwa Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kumposa mtoto wake Fatma, alisema
Mtume juu yake sala na salamu:

"‫صحبته‬ ‫"هي لك على أن حتسن‬

“Huyo ni wako maadamu utaufanyia uzuri usuhuba wake.” (Imepokewa na


Abu Na'iym)

Na 'Uthmaan bin Anbasa bin Abi Sufyaan akaposa kwa 'Ami yake 'Utbah
kutaka kumuoa binti yake, akamkalisha ubavuni mwake na akaanza
kupangusa kichwa chake, kisha akamwambia, ‘Mtu wa karibu zaidi
(ndugu) amemposa ninayempenda zaidi, siwezi kumrudisha, na sina sababu
ya hilo. Nimekuozesha nawe ni azizi kwangu zaidi kuliko binti yangu, naye
moyo wake umegandana nami zaidi kuliko wako, hivyo mkirimu na ulimi
wangu utaona tamu kukutaja, wala usimshushie hadhi yake ikapungua hadhi
yako kwangu, na nimekuweka karibu pamoja na ukaribu wa udugu tulionao,
hivyo basi usiupeleke moyo wangu mbali na moyo wako.’
09-Zawadi Kwa Wanandoa:
Wasia wa Mume kwa Mkewe

Zawadi Kwa Wanandoa

09- Wasia wa Mume kwa Mkewe

‫وصية الّز وج إلى زوجته‬


Amesema Abu Dardaai kumuusia mkewe: ‘Ukiniona mimi nimekasirika
jaribu kuniridhisha, nami nikikuona umekasirika nitakuridhisha, vinginevyo
hatutoweza kukaa pamoja.’

Na akasema mmoja wa waume kumwambia mke wake:

Chukua msamaha wangu yatadumu mapenzi yangu (mawadda),

Wala usizungumze katika kilele cha ghadhabu

pindi ninapo ghadhibika.

Wala usinigonge kwa mgongo wako hata mara moja

Kwani wewe hujui ni wapi jua linapozamia

Na wala usizidishe malalamiko na nguvu kuondoka

Na moyo wangu ukakukataa, na mioyo hugeuka

Nami nimeona mapenzi katika moyo na maudhi vile vile

Zikikutana, basi mapenzi hayakai yataondoka.”


10-Zawadi Kwa Wanandoa: Usia
wa Mama kwa Bintiye

Zawadi Kwa Wanandoa

10- Usia wa Mama kwa Bintiye

‫وصّية األم ال بنت‬

Amru bin Hujri aliposa kwa Malik kan-da, kumposa Ummu Iyaas binti Auf
bin Muhalim Asshaybaniy, na ilipofika siku ya sherehe ya ndoa yake Mama
yake Umama bint al-Harith alichepuka nae pembeni na kumuusia,

"Ee, Binti yangu: hakika usia ukiachwa kwa fadhila ya adabu (yaani
isingekuwa na haja ya kuwausia wenye adabu nzuri) ningeliacha kwako,
lakini usia mwanangu ni ukumbusho kwa msahaulifu, na msaada kwa
mwenye akili. Na lau kwamba mwanamke asingemuhitajia mume basi
wazazi kadhalika wasingehitajika. Ni muhimu sana haja zao kuwa pamoja,
basi mimi ningekuwa ni mtu nisiyemhitajia baba yako, lakini mwanangu
wanawake kwa wanaume wameumbiwa, na wao wameumbwa kwa ajili ya
wanaume.

Ee, Binti yangu: Hakika wewe unaacha mazingira uliyoyazoea na unaacha


maisha uliyokulia, unakwenda usipopajua na mwenza usiyemzoea, na
atakuwa ndie mwangalizi wako, hivyo basi kuwa kwake kijakazi nae
atakuwa ni mtumwa wako asiyetamani kukukosa. Hifadhi kwake mambo
kumi, atakuwa kwako hazina:

1) Unyenyekee kwake kwa kukinai.

2) Umsikilize vizuri na kumtii.

3) Na uangalie maeneo ya macho yake na pua yake.

4) Hivyo basi, macho yake yasione au kuangalia yanayochukiza kwako na


wala yasinuse ila harufu nzuri kutoka kwako.

5) Angalia wakati wake wa kulala na chakula chake.

6) Kwani hakika mbabaiko wa njaa unaunguza na kukosa usingizi


kunaghadhibisha.

7) Chunga mali yake na ulinde heshima yake na watoto wake.

8) Na matumizi ya mali yawe mazuri na katika kuishi nae upange vizuri


maisha.

9) Usimuasi kwa jambo na usitoe siri zake.


10) Kwani wewe ukikengeuka na amri yake utapandisha chuki na hasira
katika kifua chake, na ukitoa siri zake hutosalimika kwa kumvunjia ahadi
yake, kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa hana raha, na kukasirika hali
ya kuwa amefurahi."

Msingeacha vijiji vyenu

Na kama si ngano nyeusi

Basi wasingenenepa binti zenu

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik amesema: “Alipita Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) mwanzoni mwa kuhamia kwake Madiynah
akiwa na harusi pamoja na wanawake, na mmoja wao alikuwa akisema:

Na akazawadiwa Kondoo akipiga ukelele mkubwa kabisa

Na mumeo yupo Shamba na unajua ya kesho.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema: “Usiseme hivyo bali


sema:

‫فّح يونا حنّييكم‬ ‫أتيناكم أتيناكم‬

Tumewajia tumewajia, Tusalimieni tuwasalimie


12-Zawadi Kwa Wanandoa:
Yachukizayo Kwenye Sherehe ya
Harusi

Zawadi Kwa Wanandoa

12- Yachukizayo Kwenye Sherehe ya Harusi

‫منكرات األفراح‬

Katika jumla ya mambo yenye kuchukiza katika sherehe ya ndoa ni

 Kuzidi kwa ala za muziki, na nyimbo mbaya chafu za matusi


zenye kuchochea hisia za chuki na ngono zenye kuimbwa na
watu waliobobea katika maasia. Kisha kibaya zaidi ni ule
mchanganyiko wa wanawake na wanaume ambalo ni jambo lisilo
la lazima kabisa katika sherehe na haswa zaidi za harusi.
Kadhalika kuingia kwa wapiga picha na wapiga ngoma na
wachezaji wake kwa Bwana na Bibi harusi na kuwaona
wanawake na fitna (mapambo yao) zao na kudhihirika uchi wao
mbele yao, hivyo basi kupelekea kudhihiri kwa makosa katika
mazingira yaliyotawaliwa na shetani.

 Na katika jumla ya machukizo ni upigaji wa honi za magari na


mazumari mabarabarani, jambo lenye kusababisha kuamsha na
kuwastua waliolala, wagonjwa na wanafunzi waliopo
madarasani.
 Na mengine yenye kuingia katika machukizo ni ile ada chafu na
mbaya ya kujifakharisha baina ya watu iliyopo katika baadhi za
sehemu, kwa mfano mmoja wao kusema: Shabbash kwa Fulani,
na anaanza kutaja mali alizotoa katika kuchangia harusi, na
anatokezea mwingine anayehamasika na anatoa zaidi ya yule wa
mwanzo kwa lengo la kujifakharisha na kujitukuza na kujiona
mbele za watu.

 Na katika yasiyopendeza ni kuingia kwa Bwana harusi ndani


kwa Bibi harusi na kukaa nae pembeni, katikati, ya wanawake
wasiojisitiri, wenye kujionesha, na haingii peke yake bali ataingia
na nduguze wengine.

 Na mengineyo katika hayo ni ulipuaji wa fataki na baruti eti


kudhihirisha furaha yao na kuonekana washiriki wazuri wa
harusi ile. Huu ni ujahili na upotefu, je, ni Mabwana harusi
wangapi na Mabibi harusi wangapi ambao harusi zao ziligeuka
kuwa ni khitma kwa hayo na Mabwana harusi wengine
kuingizwa jela na si kuingia kwa mkewe!!.

 Hali kadhalika mandhari ya sherehe yanapoonyesha ufakhari na


kujiona na israfu na kujikalifu kwa taklifa zisizokuwa za msingi
na ambazo anagharimika kwazo Bwana harusi kwa taabu ni
katika mambo yenye kuchukiza katika sherehe za harusi.

 Uvaaji wa kupita mipaka kwa wanawake kwenye sherehe za


harusi na utengenezaji wa nywele na kujifananiza na wasiokuwa
Waislamu, yote haya yanagharimu fedha nyingi sana mbali na
uchafu unaoenezwa na fitna za hali hizi.
13-Zawadi Kwa Wanandoa:
Karamu ya Harusi (Walima)

Zawadi Kwa Wanandoa

13- Karamu ya Harusi (Walima)

‫الوليمة‬

Walima ni Sunnah iliyokokotezwa kwa neno lake Mtume (Swalla Allaah


'alayhi wa sallam) kwa A'bdur-Rahmaan bin 'Awf:

‫أومل ولو بشاة‬


“Tufanyie Karamu walau kwa mbuzi mmoja.” (Ahmad)

Na Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) amesema vile vile:

‫إنه ال بّد للعرس من وليمة‬


“Hakika katika harusi hakuna budi kufanywa karamu.”(Ahmad)
“Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) aliwafanyia karamu baadhi ya
wake zake kwa vibaba (Mudain) viwili vya shairi.” (Al-Bukhaariy na
Ahmad)

Ama tofauti ya aina ya chakula kinachotumika katika karamu hutegemea


desturi za watu na ada zao na uwezo wao wa kifedha. Ni wajibu wa mwenye
kualikwa katika karamu kuitikia mwito huo ili kuingiza furaha kwa wale
waliomwalika. Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) amesema:

‫إذا دعي أحدكم إىل وليمة فليأهتا‬


“Anapoalikwa mmoja wenu katika karamu na ahudhurie.” (Al-Bukhaariy
na Muslim)

Na katika hadithi nyingine Mtume juu yake sala na salamu anasema:

‫من ترك الّد عوة فقد عصى اهلل ورسوله‬


“Atakayeacha kuitika mwito basi atakua amemuasi Allah na Mtume
wake.”(Al-Bukhaariy na Muslim)

Na Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) amesema vilevile:

“Lau ningealikwa kwenda kula kongoro basi ningelikwenda, na lau


ningalipewa zawadi ya mkono ningalipokea.” (Al-Bukhaariy)

Inapendeza wale ambao wataalikwa kwenye karamu wawe ni mafakiri na


pasiwepo katika karamu hiyo Munkaraat (ubadhirifu na Israfu), Mtume wa
Allaah juu yake Swalah na amani anasema:
‫شّر الّطعام طعام الوليمة يدعى هلا األغنياء ويرتك الفقراء‬
“Chakula kibaya zaidi ni karamu ambayo wanaalikwa matajiri na kuachwa
mafakiri.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Na mwaliko huo unapendeza zaidi uitikiwe na waja wema wa Allaah


(Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neno Lake Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa
sallam) :

‫ال تصاحب إّال مؤمتا وال يأكل طعامك إّال تقّي‬


“Usisuhubiane ila na muumini tu, na asile chakula chako ila Mchaji
Allaah.” (Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy)

Matajiri wanahamasihwa washiriki katika kutengeneza chakula cha


mafakiri, kwani amesema Anas (Radhiya Allaahu 'anhu) katika kisa cha
Ndoa ya Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) kwa bibi Swafiyah, hata
ilipofika njiani Bibi Sulaym alitayarisha chakula na akakipeleka usiku, na
ilipofika asubuhi yake Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) akasema:
“Atakayekua na kitu basi aje nacho.” Anas anasema: “Habari zikaenea vitu
vikawa vingi! Ikawa kila mmoja anakuja na kitu, wengine walileta samli
wengine tende wakatengeneza hays (aina ya chakula kama ugali wa tende
uliochanganywa na samli) ikawa wanakula kutokana na chakula kile na
wanakunywa katika zile hodhi waliokinga katika maji ya mvua, na hiyo
ndio iliyokuwa karamu ya Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) .” (Al-
Bukhaariy na Muslim)

Na du'aa inayosomwa kwa Bwana harusi wakati mtu anapohudhuria karamu


ni:

‫ ومجع بينكما يف خري‬,‫ وبارك عليك‬,‫بارك اهلل لك‬


“Allaah Akubariki na Akubarikie mke huyo na Awakusanye pamoja katika
kheri.” (Abu Daawuwd)

Mtume juu yake sala na amani amekataza kupeana pongezi za


kijahilia. Hasan bin 'Aqiyl bin Abi Twalib alioa kisha watu wakaingia
(kumpongeza) wakisema: upate utajiri na watoto, Hasan (Radhiya Allaahu
'anhu) akasema msiseme hivyo, kwani Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa
sallam) amekataza hilo. (Ibn Maajah, Ad-Daarimy na Ahmad)

Inapendeza kuwaombea dua wanandoa wawili kwa kusema:

‫على خري والربكة وعلى خري طائر‬


“Katika kheri na baraka na katika kheri ya kuwa na bahati nzuri na hadhi
yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

‫ وبارك هلما يف بنائهما‬,‫اللّه م بارك فيهما‬


“Ee, Allaah! Wabarikie kwa hayo, na uwabarikie wote wawili katika
mjengo wao.” (Atw-Twabaraaniy)
14-Zawadi Kwa Wanandoa: Siku
Ya Mwanzo Ya Ndoa

Zawadi Kwa Wanandoa

14-Siku Ya Mwanzo Ya Ndoa

‫ليلة الّز فاف‬

Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa, ni siku ambayo yenye athari kubwa
katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa
matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.

Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole
mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri
washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa
yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna
haja ya haraka.

Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko
ifuatayo:
15-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kumfanyia Upole na Kumlainisha
Mkeo

Zawadi Kwa Wanandoa

15-Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo

Fondling the wife

Mume anapoingia kwa mke wake katika siku hii muhimu katika m'Aaishah
ya ndoa mara nyingi hisia za khofu na wasiwasi za mwanamke zinakuwa
juu, hivyo basi ni juu ya mwanamme kukaa nae kwa upole na
kumbembeleza hadi nae ajihisi anaanza kuzoea hali hiyo na kup unguza
khofu na wasiwasi aliokuwa nao juu yako. He's like, ugomvi, matusi au
kupiga si mahali pake kabisa, na sio lazima kumuingilia kumuingilia usiku
ule ule, unaweza kusubiri hadi asubuhi au hata siku ya pili, mara nyingi
mwenye pupa huwa anakosea na matokeo yake yanakuwa ni mabaya (na
yenye kudu mu katika m' Aaishah mazima ya ndoa yenu).

Imepokewa kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd bin as-Sakan amesema:


“Nilimuendea Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) hali ya kuwa
amejipamba kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
nikamuondoa khofu. Baada ya muda kidogo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) akaja pembeni yake na kikombe cha maziwa, akayanywa kidogo
kisha akampa Bibi 'Aaishah nae akateremsha kichwa chake kwa kuona
haya. (Asmaa) nikamnyanyua ('Aaishah), nikamwambia: chukua kutoka
kwa mkono wa Mtume wa Allah. ('Aaishah) Akachukua na kuyanywa, kisha
(Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamwambia, “Wape marafiki
zako wa umri wako.” (Ahmad)

Na si neno kwa mke kumkatalia kidogo mumewe kwani katika hilo mtu
husisimkwa, na hujitayarisha, na kunapelekea kumjali zaidi na kumtaka. Na
kunanasihiwa kwa wanandoa kuwa ni vizuri wakavua nguo zao zote kama
vile mshairi anavyosema:

Na tahadhari kuingiliana kunako nguo kwani huo ni ujahili usiokuwa na


shaka!

I have no choice but to eat nacho – ee, rafiki yangu mkivue

Na uwe ni mchezaji nae ili asifadhaike.

Ni Sunnah mume kusema anapoingia kwa mkewe siku ya mwanzo:

O God, I ask You for its goodness and the goodness of


what You have created, and I seek refuge in You from its
.evil and the evil of what You have created for it
“Ee, Allaah nakuomba kheri yake na kheri aliyokuja nayo na uniepushe na
shari yake na shari aliyokuja nayo.” (Abu Daawuwd na Ibn Maajah)

Du'aa kama hii hutuliza hisia za mwanamke na Nafsi yake na hukaribisha


baraka, na huenda kwa hayo Allaah Akajaalia baraka katika usiku huu.
16-Zawadi Kwa Wanandoa:
Swalah Ya Sunnah Kwa
Wanandoa

Zawadi Kwa Wanandoa

16-Swalah Ya Sunnah Kwa Wanandoa

‫سّنة صالة الّز واج‬

Usiku wa mwanzo wa Mume na Mke si kwa ajili tu ya kujifurahisha


pekee na raha ya kuingiliana bali ni lazima kutekeleza amri za Dini na
katika hayo ni Swalah. Amesema Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa
sallam) :

‫ فإّن اهلل جا‬, ‫ وليأمرها أن تصلّي خلفه‬, ‫إذا تزّو ج أحدكم فكانت ليلة البناء فليصّل ركعتني‬
‫عل يف البيت خريا‬

“Atakapooa mmoja wenu na ikawa ni siku ya mjengo na aswali rakaa


mbili na amuamuru mke wake aswali nyuma yake, kwani Allaah
Atajaalia katika nyumba hiyo kheri.”

(Imepokewa na al-Bazaar kama ilivyo katika kashfu al-Astaar)


Mtume Amesema juu yake Swalah na amani:

‫ اللهم‬: ‫إذا دخلت املرأة على زوجها يقوم الّر جل فتقوم من خلفه فيصّليان ركعتني ويقول‬
‫ اللهم امجع بيننا ما‬, ‫ وارزقين منهم‬, ‫ اللهم ارزقهم مين‬, ‫بارك يل يف أهلي وبارك ألهلي ّيف‬
‫ وفّر ق بيننا إذا فّر قت إىل خري‬, ‫مجعت يف خري‬

“Atakapoingia mwanamke kwa mumewe, atasimama mwanamme na


mwanamke atasimama nyuma yake, na wataswali rakaa mbili na
atasema: Ee Allaah! Nibarikie mimi kwa ahli zangu na uwabariki
kwangu ahli zangu, ee Allah! Waruzuku wao kwangu na uniruzuku
mimi kwao, ee Allaah! Tuunganishe mimi na mke wangu katika
muunganisho wa kheri, na Utufarikishe

baina yetu kwa kheri pindi Utakapotufarikisha.” [Al-Bukhaariy na


Muslim]
17-Zawadi Kwa Wanandoa:
Unapomwingilia Mkeo

Zawadi Kwa Wanandoa

17-Kinachosemwa Unapomwingilia Mkeo

‫ما يقال عند اجلماع‬

Mume anaomba anapomuingilia mkewe kwa du'aa aliyofundisha


Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

‫بسم اهلل اللّه م جّنبنا الشيطان وجّنب الشيطان ما رزقتنا‬

“BismiLLaah, Ee Allaah, tuepushie sheitani na Umuepushe kwa kile


Utakachoturuzuku.” (Al-Bukhaariy na Muslim)
18-Zawadi Kwa Wanandoa:
Malipo Ya Kuingiliana

Zawadi Kwa Wanandoa

18-Malipo ya Kuingiliana

‫ثواب اجلماع‬

Katika kuingiliana hakupatikani kwa raha peke yake bali kunabeba


ndani yake malipo mtu anayolipwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
katika kufanya hivyo na mke wake au mume wake, amesema Abu
Dharr (Radhiya Allaahu 'anhu) :

“Hakika watu katika Maswahaba walimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa


sallam) : Ee Mtume wa Allaah wameondoka wenye uwezo (ahlu duthuur) na
malipo yote, huswali kama tunavyosali, hufunga kama tunavyofunga, na hutoa
sadaka katika bora ya mali zao. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
akawaambia, “Je, Allaah Hakuwajaalia katika ya kutoa sadaka? Hakika katika kila
tasbiyh (Subhaana-Allaah) ni sadaka. Na katika kila takbiyr (Allaahu Akbar) ni
sadaka, na kila tahliyl (La ilaaha illa Allaah) ni sadaka. Na kila tahmiid
(AlhamduliLLaah) ni sadaka. Kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni
sadaka vile vile na kumuingilia mkeo ni sadaka.” Wakasema Maswahaba na je,
katika kupata raha binafsi mmoja wetu analipwa??!. Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) akasema: “Je, mnaonaje lau mtu huyo angeingiza (tupu yake)
katika haramu, je, ingelikuwa ni shari juu yake (ya madhambi, maradhi,
adhabu)?, wakasema: ndio. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) : “Hivyo ndivyo atakapoweka (tupu yake) katika halali atalipwa.”
(Muslim)
19-Zawadi Kwa Wanandoa:
Adabu Za Kuingiliana

Zawadi Kwa Wanandoa

19-Adabu Za Kuingiliana

‫أدب اجلماع‬

Imepokewa vile vile kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu
'anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

‫ فإذا قضى حاجته قبل أن تقضي حاجتها فال يعجلها‬, ‫إذا جامع أحدكم أهله فليصدقها‬
‫حىت تقضي حاجته‬
“Atakapomuingilia mmoja wenu mkewe na amsadikishe (yaani wote wafikie
kilele cha ladha ya kitendo cha ndoa), atakapomaliza haja yake kabla ya mke
wake kumaliza ya kwake basi asifanye haraka hadi mke wake nae amalize haja
yake.” (Abu Ya'ala)

Tunajifunza katika hadithi hii mafundisho ya kisheria yenye kumtaka


mume amsubiri mke wake nae amalize haja yake, amshibishe na afikie
kilele kama alivyofika yeye. Mafundisho haya ya Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) yanatufundisha kujali hisia za mwanamke
na kuziheshimu.
20-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuoga Baina Ya Matendo Ya
Ndoa

Zawadi Kwa Wanandoa

20-Kuoga Baina Ya Matendo Ya Ndoa

Bathing between intercourse

'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu


'alayhi wa sallam) amesema: “Atakayemuingilia mke wake kisha
akataka kurejea tena katika tendo la ndoa na asafishe tupu yake.” (Atw-
Twabaraaniy).

Kadhalika imesimuliwa toka kwa Abu Rafi kuwa Mtume (Swalla


Allaahu 'alayhi wa sallam) siku moja aliwazungukia wake zake, akioga
kwa huyu na akioga kwa yule. Nikamwambia (Abu Rafi): Who is
worthy of Allah, who is worthy of worship? Akasema Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam): “Hi there, I won't save you.” (Abu Daawuwd
na Ibn Maajah). Katika hadithi nyingine Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) anasema:
If one of you comes to his family and then wants to return,
he should perform ablution between them as he does for
prayer
“Atakayemuingilia mkewe kisha akataka kurudi tena (katika tendo la tendo) na
atawadhe baina ya matendo mawili wudhuu wa Swalah.”

(Muslim, Abu Dawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

Katika kuchukua wudhuu, kukosha au kuoga ni katika jumla ya


kuchangamsha mwili na kuziibua upya nguvu za kiwiliwili. Na si
hivyo tu kunahakikisha usafi katika tendo la ndoa (homosexual).
21-Zawadi Kwa Wanandoa:
Adabu Za Mtu Na Ndugu Za Mke
Wake

Zawadi Kwa Wanandoa

21-Adabu Za Mtu Na Ndugu Za Mke Wake

‫أدب الّر جل مع أقارب زوجته‬

Katika jumla ya adabu ya mtu na ndugu za mke wake ni kutokutaja


maneno au kufanya vitendo vya aina yoyote ile vyenye kuashiria
mapenzi ya chumbani kama kubusu na mfano wa hayo, na hii ni katika
adabu ya kuishi nao. Imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib
(Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: nilikuwa ni mtu mudhaa-a, nikiona
haya kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa nafasi
ya mtoto wake kwangu, nikamuomba Miqdaad aniulizie.
22-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuharamisha Kuingilia Katika
Tupu Ya Nyuma

Zawadi Kwa Wanandoa

22-Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu ya Nyuma

‫حترمي نكاح الّد بر‬

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

‫نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أىن شئتم‬


“ Wake zenu ni konde zenu, basi ziendeeni konde zenu
mpendavyo.” (Al-Baqarah: 223)

Ilikuwa ni tabia ya Mayahudi wakisema: Mtu atakapomuingilia mke


wake mbele lakini kwa upande wa nyuma basi atazaliwa mtoto akiwa
ni kengeza; ikashuka Aayah hii:“Wake zenu ni mashamba
yenu.” (Muslim). Katika riwaya nyingine:

‫إن شاء جمّبية و إن شاء غري جمّبية غري أّن ذلك يف صمام واحد‬
“…na ukipenda ufanye staili ya kama anasujudu na ukipenda sivyo
hivyo yote ni sawa sawa...” (Muslim: Hadithi 1435)

Ilikuwa ni tabia ya Ahlul-Kitaab kutomuingilia mwanamke ila kiubavu


na katika hali ya mwanamke kujistiri. Na ilikuwa tabia ya baadhi ya
Answaar kuiga tabia zao hizo. Na wanaume wa ki-Quraysh walikuwa
wamezowea kufanya mapenzi na wake zao vilivyo, wakistarehe nao
kwa mbele, nyuma na kwa chali, (lakini bila ya kuwaingilia tupu zao za
nyuma). Walipohamia Muhajirina Madiynah alioa mmoja wao
mwanamke wa ki-Answaar; akataka kufanya nae mapenzi kwa mitindo
waliyozoea (huko Makkah) akachukizwa mwanamke yule na hilo, na
akasema: Hakika sisi tulikuwa tukiingiliwa kiubavu, fanya hivyo au
niepuke; kisa chao kikaenea, zikamfikia habari Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) na Allaah Akashusha:

‫نساؤكم حرث لكم‬


“Wake zenu ni konde zenu…” (Abu Daawuwd)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema vile vile:

“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo wa) Kwa mbele au (kwa mtindo
wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (utupu wa nyuma) na
(kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.”(At-Tirmidhiy)
23-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuoga Katika Chombo Kimoja

Zawadi Kwa Wanandoa

23-Kuoga Katika Chombo Kimoja

‫اإلغتسال من إناء واح‬

Inajuzu kwa wanandoa wawili kuoga pamoja katika sehemu moja,


imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesema:

“Nilikuwa nikioga mimi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi


wa sallam) katika chombo kimoja, inapishana mikono yetu ndani yake,
na ananianza kwa hilo hadi nasema: niachie … niachie. Akaendelea
kusema Bibi 'Aaishah wakiwa hivyo hali ya kuwa ni wenye
janaba.” (Muslim)
24-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuondosha Bikira

Zawadi Kwa Wanandoa

24-Kuondosha Bikira

‫فض غشاء البكارة‬

Utando wa bikira unatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine,


baadhi yao bikira zao ni khafifu hukatika na kuachia mara moja kwa kuanguka,
na baadhi nyingine ni ngumu. Hivyo basi anatahadharishwa mume katika
kufahamu na kujua kuwa ule utando wa bikira wenyewe ndio kipimo cha usafi
na utukufu wa mwanamke. Katika ada zilizo mbovu kabisa ni ile hali ya baadhi
ya wanaume kuondosha bikira kwa kutumia vidole vyao, na haya ni madhara
makubwa kwa mwanamke na humsababishia maudhi mengi.

Jambo jingine ambalo ni baya ni zile hila za kisheitani wanazotumia baadhi ya


wasichana wasiojitunza na ambao wanawahadaa waume zao siku ya mwanzo
ya harusi kwa hila zenye kufahamika na madaktari na makungwi.

Jukumu kubwa linaloonekana kwa waume wengi ni kuondosha utando wa


bikira siku ile ile ya mwanzo kwa njia yoyote na husubiri mke wake
ajisalimishe kwake kwa hilo. Na wakati mwingine msichana al-huyiyya (bado
hajamuona mwanamme) anaweza kukataa na baadhi ya wasichana hufikiri
kuwa ndoa ni mchezo na matembezi hivyo basi akimuona mwanamme amevua
nguo zake na uume wake umesimama akiwa ni mwenye pupa na jambo lake
huanza kuogopa na huenda akaupiga ukelele na hujaribu kujizuia na mume
wake na hii inarejea na uduni wa uzoefu wa wote wawili mume na mke na
kuwa na fikra mbovu kuhusu ngono.
25-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kumchezea Mke

Zawadi Kwa Wanandoa

25-Kumchezea Mke

‫مداعبة الّز وجة‬

Hakika katika jambo ambalo ni muhimu kwa mume kulichunga na


kulilinda ni kumchezea chezea mke wake na haswa kabla ya
kumuingilia, hili lina athari kubwa sana kati ya wanandoa wawili
katika mahusiano yao ya kiroho na ya kijinsi.

Katika kufikia kilele cha raha ya kiwiliwili kunahitaji kwa mwanamme


awe na diplomasia ili aweze kumpa mke wake hamu na matamanio ya
kweli, na ushiriki mzuri ulio kamili na mapenzi yaliyokita.

Mke mwenye hekima anaweza kwa diplomasia aliyokuwa nayo na


mapambo yake na usafi wa kiwiliwili chake kumvuta mume wake na
kumtamanisha. Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa
kiwiliwili vyao kwa urahisi na wepesi zaidi, mahaba siku zote
yanatimiza furaha.

Ama kumuingilia mwanamke bila ya kuwepo vitangulizi huwa ni


jambo lisilofaa na la kinyama la kutosheleza mahitaji ya mwanamme,
kisha haupiti muda mrefu kamaliza haja na kukaa mbali ya mwanamke
hali ya kuhema!.

Mwanamke siku zote hupendelea mumewe ashirikiane nae katika hisia


zake kwa upole na wema na acheze nae kwa muda unaotosha
kupandisha hamu na nyege zake. Na hivi vitangulizi vya jimai husaidia
kuwafikisha wanandoa wawili katika utulivu kamili na hivyo kufikia
kilele cha raha ya tendo la ndoa.

Kwa hilo na mengineyo Uislamu unahimiza suala hili la kuchezeana na


kumchezea mke, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

‫ مالعبة الّر جل امرأته و تأديب‬:‫ هلو ولعب إّال أن يكون أربعة‬, ‫كّل شيئ ليس من ذكر اهلل‬
‫الّر جل فرسه ومشي الّر جل بني الغرضني وتعليم الّر جل الّس باح‬

“Kila kitu katika lahau na mchezo si katika dhikri ya Allah ila iwe ni
kimoja katika hivi vinne: 1) Mwanamme kumchezea mke wake. 2) Mtu
kumfundisha farasi wake. 3) Na mtu kutembea katika kamba mbili za
juu au milingoti miwili. 4) Na mtu kujifunza kuogelea.” (At-Tirmidhiy)

Na katika kuchezeana suala muhimu ni upole na ulaini na kumsubiri


mkeo hadi amalize haja yake kwani wakati mwingine huchelewa, ni
bora kwa mwanamme ajipambe na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) :

‫ال يؤمن أحدكم حىت حيّب ألخيه ما حيّب لنفسه‬


“Hatoamini mmoja wenu hadi ampendelee nduguye lile
analolipendelea katika nafsi yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

na ukweli ni kwamba hakuna aliyekuwa karibu kufanyiwa hayo


isipokuwa ni mke.

Tukiulizana ni vipi mwanamme anafika kilele cha ladha ya jimai?


Utaona kwamba ufumbuzi unapatikana katika hali zifuatazo. Kuamini
kuwa tendo la Ndoa ni Ibada:
26-Zawadi Kwa Wanandoa:
Tendo La Ndoa Ni Ibada

Zawadi Kwa Wanandoa

26-Tendo La Ndoa Ni Ibada

‫الّنكاح عبادة‬

Uislamu umenyanyua hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya


kuwa ni ibada, ibada ambayo wana ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani
kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi na uchafu na
wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana,
kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana
mapenzi yenye kulandana.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) juu yake amani na salamu


anasema:

‫يف بضع أحدكم صدقة‬

“…na katika kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)


Tendo la ndoa ni sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika
ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa haja zake zinashibishwa na
ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya Allaah (Subhaanahu
wa Ta'ala).

Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) anasema: kila ladha husaidia ladha


ya siku ya mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:

Upande wa mwanzo ni kule kustarehe na kujifurahisha na kupata


utulivu wa macho.

Upande wa pili ni kule kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na


huko ni kuifikisha nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.
27-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kubusu Kabla Ya Kuingiliana

Zawadi Kwa Wanandoa

27-Kubusu Kabla Ya Kuingiliana

‫القبلة قبل اجلماع‬

'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesema:

“Hakika Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa


akiwabusu wake zake kisha akitoka kuelekea kuswali na hakuwa
akitawadha.”

(Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ahmad)

Tendo la kubusu lina athari muhimu sana katika mapenzi na


hukurubisha zile hisia za mapenzi na mwisho hupelekea kugandana
kwa kiwiliwili, na jinsi lilivyo muhimu ni kuwa mwenyewe Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa haliachi hata kama
amefunga saumu, kwani alikuwa akibusu na akiwakumbatia wake
zake hali ya kuwa amefunga.” (Al-Bukhaariy na Muslim) Ummu
Salama (Radhiya Allaahu 'anha) amesema: Hakika Mtume wa Allah
alikuwa akiwabusu wake zake hali ya kuwa amefunga.

Busu linakuwa katika hali nzuri na yenye kufidisha na kusisimua


likiwa ni ndefu na haswa linapokuwa ni mdomo kwa mdomo hali ya
kuwa wamefunga macho mawili na kufungua kidogo kidogo mara kwa
mara. Wakati huo inapokuwa miili imegandana na pumzi
kubadilishana hali zikiwa moto moto, ukianzia kuvuta kwa ndani
kabisa na macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa huruma. Yote haya
huzipa raha nafsi za wanandoa na ni vitangulizi vizuri kwa kutayarisha
mazingira mazuri ya kuanza kwa Jimai.

Kubusiana hakuishii katika midomo miwili tu, lakini huweza


kuendelezwa katika maeneo mengine ya kiwiliwili ambayo yanaweza
kusisimshwa na na hivyo matamaniwa yakasimama.
28-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuchezea Chezea Kinembe

Zawadi Kwa Wanandoa

28-Kuchezea Chezea Kinembe

‫دغدغة البظر‬

Kinembe ni moja katika maeneo muhimu sana ambayo yanaamsha


hisia za jimai kwa mwanamke. Kukichezea kwa mwanamme ni
muhimu sana ili kusisimsha hisia za kutamani kuingiliwa kwa
mwanamke. Jinsi ya kukichezea inatakiwa iwe kwa upole na uangalifu
mkubwa. Kinaweza kuchezewa kwa njia ya mkono au kwa njia ya
kichwa cha dhakari ya mwanamme, na baada ya hapo ndipo
anapoweza mwanamme kumuingilia mkewe na kukamilisha haja na
matamanio yao.

Hali kadhalika inapendeza zaidi kwa mwanamke kuendelea


kuchezewa kinembe hata baada ya kuingiliwa au Jimai kumalizika ili
kumsisimsha zaidi na hivyo kufikia kilelenikama bado hajafikia
alipokuwa akiingiliwa na mumewe.
29-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kutafuta Raha Bila Ya Jimai

Zawadi Kwa Wanandoa

29-Kutafuta Raha Bila Ya Jimai

‫االستمتاع دون مجاع‬

Je mwanamke akiwa katia udhuru, kwa kuwa ni mwenye hedhi,


mwanamme huruhusiwa kumchezea mkewe? Au amtelekeze na
kumtenga kabisa kwa sababu hiyo?

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ana msemo maarufu


kuhusu wanawake wenye hedhi, anasema:

‫اصنعوا كّل شيئ إّال الّنكاح‬

“Fanya kila kitu isipokuwa kumuingilia.”

(Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)


Na imepokewa kwa wake za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) kuwa Mtume“Anapotaka kustarehe na mke wake mwenye
hedhi basi hufunika tupu ya mwanamke.”(Abu Daawuwd). Na kutoka
kwa Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesema:“Alikuwa Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akimuamuru mmoja wetu akiwa na
hedhi ajifunge shuka kwenye tupu yake kisha humchezea.” (Al-
Bukhaariy na Muslim)

Mahusiano ya mke na mume hayaishii katika Jimai peke yake bali


yanakusanya kuona raha katika uke wa mke na hisia nyingine za
kibinaadamu kama vile kunusa, kukumbatia, na kuchezeana, michezo
mingine ya kuchekesha na kushikana shikana kwa aina zote mbali na
tendo lenyewe la Jimai. Na hii hufanikisha hamu na matamanio ya
kubadilishana baina ya wanandoa wawili. Kwa mwanamke mwenye
hedhi huku kutomaswatomaswa humsaidia kumpunguzia ule
usumbufu aupatao katika hedhi yake na lingine muhimu zaidi ni
kufahamu vile vile kuwa yeye si chombo tu cha kushibisha matamanio
ya kingono ya mumewe peke yake bali kuna mambo mengine amabayo
ni muhimu vile vile mbali na kule kushuka na kumwaga.
30-Zawadi Kwa Wanandoa:
Uhuru Wa Kuangalia Uchi

Zawadi Kwa Wanandoa

30-Uhuru Wa Kuangalia Uchi

Freedom to look at private parts

Baaadei Ya Majahili Hudhani Kuwa Kuanglia TuPu Ni Haramu Au


Makruhu, Na Kwamba MTUME (Swalla ALAHU 'A TheyyHi Wa
Sallam) Amekataza Hilo Na Kulitahadharisha Na Wanapoke A kwa
aisha kuwa Amesma: Sikupata Kuona Uchi Wa MTUME (Swalla
Allaahu 'Alayhi Wa Sallam) That's what happens. Hadithi hii
imebatilishwa na Haafidhw Ibn Hajar, kuwa ni uongo mtupu na
imezushwa.

Na ndivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu


'alayhi wa sallam) kuwa amesema: “Atakapomuingilia mmoja wenu
mke wake basi asimuangalie kwenye tupu yake kwani hiyo hupelekea
mtu kuwa kipofu.” Na hadithi hii ni Mawdhuw'(imezushwa) kama
alivyosema Ibn al-Jawziy na Abu Haatim alrRaaziy.

What kind of tunasema kuwa amepokea At-Tirmidhiy na Abu


Daawuwd na wengineo kutoka kwa Mu'aawiyah bin Hayda amesema:
nilisema: Ee, Mtume wa Allaah, uchi wetu, tunaingilia na
kuangalia? Akasema:
Guard your private parts, except from your wife or what
belongs to your right hand

“Hifadhi uchi wako ila kwa mke wako au kwa wale unaowamiliki
mkono wako wa kuume.”

(Abu Daawuwd, At-Tirmidhi na Ahmad)

Na hii ni dalili tosha ya kuruhusu kuangaliana uchi baina ya mke na


mume.
31-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuondosha Nguo Zote

Zawadi Kwa Wanandoa

31-Kuondosha Nguo Zote

‫التجّر د من املالب‬

Ukweli ni kuwa nguo zina nafasi yake katika kuonyesha uzuri na


kusisimsha, na kuonesha mandhari nzuri kwa wanandoa wawili. Vile
vile kama zilivyo nguo nzuri na zaidi, uchi huonyesha uzuri,
husisimsha na huvutia katika kufanya kazi ya kuamsha hisia na
matamanio.

Kama ilivyokuwa maarufu kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa


sallam) alivua nguo zake alipokuwa akioga sehemu moja na Bibi
'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) . Tunachoweza kutolea dalili hapa ni
neno lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Surat al-
Baqarah Aliposema:

‫هن لباس لكم وأنتم لباس هلن‬


“…Wao ni (kama) nguo kwenu (zilizokugandeni mwilini), na ninyi ni
(kama) nguo kwao…” (Al-Baqarah: 187)

Nako huku kuwa uchi kabisa kunapendezesha na kuwezesha kufikia


kilele za raha za kimwili azipatazo mtu, hivyo basi hufanikisha kufikia
lengo lililokusudiwa la kila mmoja wa wanandoa kuwa ni nguo kwa
mwenzake!
32-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuchezeana Kwa Kuangaliana!

Zawadi Kwa Wanandoa

32-Kuchezeana Kwa Kuangaliana!

‫املداعبة عن طريق الّنظر‬

Katika kuangalia kunaleta mvuto mkubwa katika moyo wa


mwanaadamu na kunaamsha hisia kali za kimapenzi. Baadhi ya
washairi wanaona kuwa kuangalia ni mshale unaoteka na kusibu lengo
na kuua. Anasema mmoja wao:

Nami ninaona lau kama muangaliaji atawindwa

kwa kuangalia kwake mwanamke atakuwa ameniwinda

na kulisemwa zamani: muonaji ni bora ya muhadithiwa.

Kule kuona kunahadithia hisia za moyo wa mtu, na huelezea undani


wa nafsi na kile ambacho nafsi imekibeba katika hisia za mapenzi
ambazo zinapelekea kumsisimsha mtu na kudumisha ndoa.

Na ilikuwa ikisemwa hapo nyuma mambo manne hayashibishwi ila na


mambo manne:Macho kwa kuona, mwanamke kwa mwanamme, Ardhi
kwa kupata mvua na masikio kwa kupata habari.
Kuangaliana kwa wanandoa kunapelekea kukubaliana, kuvuta hisia,
ambayo inapelekea katika mahaba na kuhurumiana. Hivyo tunaweza
kuema Macho ni chanzo cha mvuto na kilele cha ladha ya mapenzi.

Na inatakiwa muono huu wa kuangalia uwe sio wa kukazia bali wa


kuibia na kusinzia ili anaeonwa aingie haswa katika moyo. Antar kwa
ushujaa wake na ugumu wa moyo wake katika kuua maadui zake
anaelezea muono wa macho na athari yake kwa kusema:

Ee, wewe yule uliyetupa moyo wangu katika kupata

na kuufunika kwa mishale yenye sumu na kuuona kwake ugumu.


33-Zawadi Kwa Wanandoa:
Athari Za Sauti Na Harakati
Katika Kuchezeana

Zawadi Kwa Wanandoa

33-Athari Za Sauti Na Harakati Katika Kuchezeana

‫احلركة والّص وت أثناء املداعبة‬

Harakati zina athari kubwa sana katika kuonyesha uzuri wa


mwanamke na haswa zaidi ule wa kiroho, kwani harakati za
mwanamke zinachanganya akili ya mwanamme, na mshairi Umru al-
Qais anayo haya ya kusema:

Ikiwa kelele imeondoshwa katika nguo yake

inapelekea katika ulaini kusikokuwa na ukali

kama mchanga uliojikusanya wanatembea wazazi wawili juu yake

kwa jinsi walivyojifikiria kwa ulaini wa mshiko na wepesi wake.

Sauti ni chemchem ya mvuto wa hisia kali za ladha na kimapenzi, vile


vile ni chanzo cha kuzungumza maneno laini ya kimapenzi, na ndani
yake ni dekezo na sisimko, na sauti ya mwanamke katika kilele cha
ladha ya jimai inapendeza zaidi ikiwa ni laini yenye Naghma.
Mwanamke kwa uzuri wa harakati zake na uchangamfu wake na uzuri
wa sauti yake na utamu wake humvutia mwanamme na huteka moyo
wake. Hivyo basi kuchezeana kunawafikisha katika kilele cha ladha ya
tendo la Jimai.

Katika wanawake kuna ambao wanatoa sauti zao wakati wa Jimai na


hilo halina tatizo. Asyuuti ametaja katika kitabu chake (ad-Durrul al-
Manthuur) kuwa Muawiya bin Abi Sufyaan alimuita siku moja mke
wake (Fakhita), akaitikia mwitiko wa kusemea puani wenye matamanio
ndani yake, akaona haya na kuhisi vibaya. Muawiya akamwambia:
usijali, Wallahi wabora wenu ni huu mfano wako wenye kupiga ukelele
kwenye mapenzi, kunguruma na kuzungumzia puani!

Na katika yote haya ni msisimsho na furaha ndani yake.


34-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kulidekeza Jina La Mke

Zawadi Kwa Wanandoa

34-Kulidekeza Jina La Mke

‫ترخيم اسم الّز وجة‬

Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim kuwa Mtume (Swalla Allaahu


'alayhi wa sallam) alimuita 'Aaishah jina lake kwa kulidekeza na
kumuita 'Aaishu. Na lengo la mwito huu ni kuonesha mapenzi kwa
mke na kujikurubisha nae.

Hivyo basi ni juu ya waume kujifunza kutoka kwa kiongozi wetu pindi
wanapocheza na wake zao, kwani katika haya ni raha tupu kwa yule
atakaemudu kuifanya vizuri fani hii aliyotufundisha Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam). Na katika dekezo la namna hii ni kuonesha
mapenzi ya kweli na inapelekea katika ladha na kusisimsha shauku na
kuwafurahisha wote pamoja.
35-Zawadi Kwa Wanandoa:
Adabu Za Maisha Ya Ndoa

Zawadi Kwa Wanandoa

35-Adabu Za Maisha Ya Ndoa

‫آداب احلياة الّز وجية‬

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema katika Surat Ruum Aayah ya


21:

‫ومن آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها وجعل بينكم مودة ورمحة إن يف‬
‫ذلك آليات لقوم يتفكرون‬

“Na katika ishara Zake (za Kuonyesha ihsan juu yenu) ni kuwa
Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao,
Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya
zimo ishara kwa watu wanaofikiri.” (Ar-Ruwm: 21)

Katika Aayah hii kuna ishara katika misingi inayosimamisha maisha


mazima ya mke na mume ambayo itapelekea katika furaha. Furaha
ambayo itakuwa na misingi madhubuti ya mapenzi na
huruma, mawaddatan warahmah.
Ni juu ya wanandoa wawili kuujenga vizuri uhusiano wao hadi ufikie
katika sifa hii ya mapenzi (mawadda) wanapokuwa ni vijana, na
kuhurumiana (rahma) wanapokuwa ni watu wazima.

Na katika jumla za adabu ya maisha ya ndoa ni:


36-Zawadi Kwa Wanandoa: Tabia
Njema

Zawadi Kwa Wanandoa

36-Tabia Njema

‫حسن اخللق‬

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

‫وعاشروهن باملعروف‬

“ … na kaeni nao kwa wema…” (An-Nisaa: 19)

katika Aayah nyingine ya sura hiyo hiyo Allaah (Subhaanahu wa


Ta'ala) Anaendelea kututanabaisha

‫وأخذن منكم ميثاقا غليظا‬

“…Nao wanawake wamepokea kwenu ahadi thabiti (kuwa mtakaa nao


kwa uzuri).” (An-Nisaa: 21)
Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akielezea
fadhila za tabia njema anasema:

‫ وخياركم خياركم لنسائهم خلقا‬,‫أكمل املؤمنني إميانا أحسنهم خلقا‬

“Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na


mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia.”

(Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema tena:

‫ وأنا خريكم ألهلي‬, ‫خريكم خريكم ألهله‬

“Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora
kwa watu wangu wa nyumbani (ahli).”

(Ibn Maajah na Ad-Daarimy)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

‫ وإن‬, ‫ فإن ذهبت تقيمه كسرته‬, ‫إّن املرأة خلقت من ضلع وإّن أعوج شيئ يف الّض لع أعاله‬
‫ فاستوصوا بالنساء‬, ‫تركته مل يزل أعوج‬

Mwanamke Ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni


juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea
kupinda, nakuusieni (kuwafanyia wema) wake zenu.” (Al-Bukhaariy
na Muslim)

Si hayo tu aliyohimiza Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu


'alayhi wa sallam) kuhusu wanawake. Bali kwa umuhimu na unyeti wa
suala hili tunaona kuwa katika usia wake wa mwisho anatuuusia:

‫ واستحللتم فروجهّن بكلمة‬, ‫ أخذمتوهّن بأمانة اهلل‬, ‫اهلل اهلل يف النساء فإهّن ن عوان يف أيديكم‬
‫اهلل‬

“Allaah, Allaah, kwa wanawake, hao ni wasaidizi wenu walio kwenye


mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allah, na
imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) (Iijaab na Qubuwl).” (Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah na
Ahmad)

Na katika jumla ya tabia nzuri katika maisha ya ndoa ni kuacha


kumfanyia mke maudhi ya aina yoyote ile. Vile vile kumfanyia na
kumtendea mazuri, na kucheza nae na kuongea nae kwa upole. Hali
kadhalika kujali zaidi uadilifu katika mambo yake na kufuata siasa za
kati kwa kati katika muamala wako nae na haswa katika yale yenye
maslahi kwake na yale yenye kuhifadhi akhlaq zake kulingana na haja,
sehemu au tukio.
37-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kuishi Nae Kwa Wema Hata
Ikiwa Unamchukia

Zawadi Kwa Wanandoa

37- Kuishi Nae Kwa Wema Hata Ikiwa Unamchukia

‫املعاشرة باملعروف حىّت يف حال الكراهية‬

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

‫وعاشروهن باملعروف فإن كرهتموهن فعسى أن تكرهوا شيئا وجيعل اهلل فيه خريا كثريا‬
“ …na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache)
kwani huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu Ametia kheri
nyingi kwake.” (An-Nisaa: 19)

Katika hilo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

‫ال يفرك مؤمن مؤمنة إن كره منها خلقا رضي منها آخر‬
“Habughudhiki muumini mwanamme kwa tabia ya mke wake
akichukizwa na moja ( ya tabia) atapenda nyingine.” (Muslim na
Ahmad)

Hata hivyo hakuna binaadamu aliyekamilika, anayeweza kusifika kwa


ukamilifu wa tabia zote za kuigwa, na vile vile hakuna maisha yenye
furaha yaliyokamilika. Hivyo basi ni lazima yawepo mapungufu na
matatizo, ambayo yanahitajia suluhisho litakalofikiwa kwa ushirikiano
wa pande zote mbili (mume na mke) ili kutatua na kuyashinda.

Katika kuamiliana na matatizo yanayojitokeza kunahitaji subira,


uvumilivu na utulivu ili maisha yaweze kuendelea na mambo kuweza
kurejea kama yalivyokuwa kabla.

Na katika matengamano ya maisha haya ya ndoa ni kuishi na mke kwa


wema hata katika hali ya kuwa hata kama unamchukia. Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) anatufundisha:

‫ وال هتجر‬, ‫ وال تضرب الوجه وال تقّبح‬, ‫ وتكسوها إذا اكتسيت‬, ‫أن تطعمها إذا طعمت‬
‫إّال يف البيت‬
“Kumlisha unapokula, na kumvisha unapovaa, wala usimpige usoni na
kumharibu na usimtusi (kwa matendo yake na maneno yake) wala
usimhame kwenda nyumba nyingine (umhame kitanda tu).”

(Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad)

Na ni juu ya mwanamme yeyote kumtizama na kumuangalia


mwanamke kulingana na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) :

‫ارفق بالقوارير‬
“Wafanyieni wema vyombo vyenu (qawariira).” (Al-Bukhaariy)

Na usia huu unaohusu wema unakusudia upole na mazungumzo


mazuri na kuvumilia maudhi. Hali kadhalika kumfanyia uadilifu katika
hali zote.
38-Zawadi Kwa Wanandoa:
Uwastani Katika Wivu

Zawadi Kwa Wanandoa

38-Uwastani Katika Wivu

‫االعتدال يف الغري‬

Huu uwastani unaokusudiwa hapa ni kutoghafilika na mambo ambayo matokeo


yake huogopwa siku zote, na kutozidisha dhana na dhulma katika kuhesabu
mambo.

Amesema mbora wa viumbe juu yake Swalah na amani:

‫إّن من الغرية غرية يبغضها اهلل عّز وجّل وهي من غرية الّر جل على أهله من غري ريبة‬

“Hakika katika wivu ni wivu unaombughudhi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)


nao ni wivu wa mwanamme kwa mkewe katika kisichokuwa na shaka.” (An-
Nasaa, Ibn Maajah na Ad-Daarimy)
Swahaba 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya AAllaahu 'anhu) anasema:

‫ال تكثر الغرية على أهلك فرتمى بالسوء من أجلك‬

“Msizidishe wivu kwa wake zenu ukaangukia uovu kwako.”

Wivu unatakiwa na ni muhimu ili kulinda hadhi ya mtu na ikithibiti sehemu


yake basi inapendeza na kupongezwa na shsri'ah, katika hili Mtume wetu (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) ana haya ya kusema:

‫ وغيرة هللا تعالى أن يأتي الّرجل ما حّرم عليه‬,‫ والمؤمن يغار‬, ‫إّن هللا يغار‬
“Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huona wivu na muumini huona wivu
na Wivu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Unakuwa pindi mtu anapofanya
alichoharamishiwa.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Leo hii watu ambao hudhani kuwa wamestaarabika huchukuwa wake zao
wakiwa wamekamilika kwa mapambo yao huenda na kukesha na marafiki zake
katika sehemu za starehe na wakati mwingine humtoa kwa aliyemuomba acheze
na mke wake na hana wasiwasi kabisa, Je, huku si kufa kwa nafsi za wivu kwa
watu hawa?!

Suluhisho la amani la tatizo hili ni kutochanganyika wanaume na wanawake.


'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa siku moja kwa Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam) akasema: “Ni kitu gani bora kwa mwanamke? Hawakujibu
kitu na niliporejea nilimwambia Fatima: Je, ni kitu gani bora kwa mwanamke?
Akasema: “Asifanyiwe rehani mumewe. Nikalitaja hilo kwa Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) .”Akasema: “Huyo (aliyekuambia) ni fatima nae ni
sehemu yangu (damu yangu).” (Al-Bazaar)

Ibn al-Qayyim amesema: Asili ya Dini ni wivu, na asiyekuwa na wivu hana dini,
na wivu unalinda moyo na huo moyo unalinda kiwiliwili, hivyo basi huuzuia
moyo kufanya uovu na uchafu. Na kukosekana kwa wivu hufisha moyo hivyo
basi na kiwiliwili kizima hufa, hivyo anakosa kinga ya kujizuia na maovu na
machafu.

Mfano wa wivu ni kama ile nguvu inayozuia maradhi na kuukinga mwili, hivyo
kinga hiyo ikiondoka ugonjwa huingia sehemu ile ya mwili na hukosa cha
kuizuia na kuilinda, hivyo ugonjwa hukaa, na hapo ndipo penye maangamizi
yenyewe.
39-Zawadi Kwa Wanandoa:
Uwastani Wa Kutoa Katika
Matumizi

Zawadi Kwa Wanandoa

39-Uwastani Wa Kutoa Katika Matumizi

‫االعتدال يف النفق‬

Ni kutofanya Israafu na kutokuwa bakhili, bali kinachohitajika hapa ni


suluhisho la kati kwa kati nalo ni lile Analolisema Allaah (Subhaanahu
wa Ta'ala) :

‫وكلوا واشربوا وال تسرفوا إنه ال حيب املسرفني‬

“ … na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri). Lakini msipite kiasi


tu…” (Al-A'raaf: 31)

Na Maneno Yake Mengine Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):


‫وال جتعل يدك مغلولة إىل عنقك وال تبسطها كل البسط‬

“Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala


usiukunjue ovyo ovyo (utakuwa ni mwenye kulaumiwa ukifanya
hivyo)…” (Al-Israa: 29)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema:

‫ ودينار‬, ‫ ودينار تصّد قت به على مسكني‬, ‫ ودينار أنفقته يف رقبة‬, ‫دينار أنفقته يف سبيل اهلل‬
‫ أعظمها أجرا الذي أنفقته على أهلك‬, ‫أنفقته على أهلك‬

“Dinari utakayoitoa katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na


dinari utakayoitoa katika kumkomboa mtumwa, na dinari utakayompa
sadaka masikini, na dinari utakayoitoa kwa mke wako, bora ya dinari
yenye malipo makubwa (katika hayo) ni ile utakayotoa kwa ajili ya mke
wako.” (Muslim)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema: “Atakapotoa


mtu matumizi kwa mkewe, matumizi yaliyo katika hesabu itakuwa ni
sadaka yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Kitu muhimu kinachoangaliwa na Uislamu katika kutafuta riziki ni


kuwa riziki yako ni halali na chanzo chake ni halali ambayo haina
uovu, shaka wala shubha ndani yake. Hili ni kwa hali yoyote ilivyo ya
kimaisha na ugumu wake utakavyokuwa kwa kuingiliwa na mipenyo
ya sheitani.

Hapa hatuna budi kumnong’oneza mke mnong’onezo ambao


tunaufupisha katika haya: mume anaweza kupatwa na ufakiri hivyo ni
juu yake awe na subira, kwani wewe ndie uliyemchagua kwa uhuru
wako mwenyewe. Kisha elewa kuwa maisha ya kiuchumi ni yenye
kubadilika, siku moja ipo pamoja nawe yaani maisha ya kiuchumi ni
mazuri, lakini kumbuka vile vile kuwa siku nyingine maisha ya
kiuchumi yanaweza kuwa magumu.

Ni uzuri ulioje mtu kutokufanya maisha yake kuwa makuu. Ajitahidi


ayafanye mepesi yanayowezekana kuendeshwa bila matatizo yoyote na
hivyi kumwezesha kuhifadhi kinachobakia. Ubadhirifu ni utazaa
majuto, taabu na ubakhili. Bora ya mambo ni yale ya kati kwa kati.
Tumuombe Allaah Atuondoshee kujiona, kujifakharisha na israafu.
Aamiyn
40-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kujipamba Kwa Ajili Ya Mkeo

Zawadi Kwa Wanandoa

40-Kujipamba Kwa Ajili Ya Mkeo

‫التّزّين للمرأة‬

Hapana budi kwa wanandoa kujipamba na kuwa safi daima kila


mmoja kwa ajili ya mwenzake. Kujipamba huku ni kwa kuvaa vizuri na
kujitia manukato.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

‫حّبب إّيل من دنياكم الّنساء والّطيب‬


“Nimependezeshewa mimi katika dunia yenu wanawake na vitu vizuri
vilivyosalimika na uchafu.” (An-Nasaaiy)

Kujipamba kunarithisha mapenzi na hujenga na kukuza sababu zote


zinazopelekea katika kuzoeana. Kisha kumbuka, “Allaah Hupenda
yaliyo mazuri.” (Muslim na At-Tirmidhiy)
Ibn 'Abbaas (Radhi ya Allaah iwe kwake na baba yake) anasema: Mimi
napenda kujipamba kwa ajili ya mke wangu kama nilivyokuwa
napenda yeye ajipambe kwa ajili yangu.

Kujipamba ni haki ya wanandoa wote wawili mwanamme na


mwanamke. Ni vizuri sana tusilidharau jambo hili la kujipamba na
kuona si la muhimu kwani mwenye kuhitajia maisha ya furaha ya ndoa
na yenye matokeo mazuri hana budi kujishughulisha na kijipamba.
41-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kumsaidia Mke Katika Kazi Za
Nyumbani

Zawadi Kwa Wanandoa

41-Kumsaidia Mke Katika Kazi Za Nyumbani

‫مساعدة الّز وجة يف األعمال املنزيل‬

Amesema bibi 'Aaishah (Radhiya AAllaahu 'anha) :

‫ كان صلى اهلل عليه وسلم يكون يف مهنة أهله فإذا حضرت‬: ‫قالت عائشة رضي اهلل عنها‬
‫الّص الة خرج إىل الّص الة‬.
“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akiwasaidia
katika kazi za nyumbani na inapowadia muda wa Swalah alikuwa
akitoka kwenda kuswali.”

(Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Na alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), “Akitoa uchafu


katika nguo zake, na akikama mbuzi maziwa na akijuhudumia
mwenyewe.” (Ahmad)
“Na alikuwa yeye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akishona
nguo zake na kusafisha ndala zake.” (Ahmad)

Katika haya yote tunajifunza kutojikweza na tunahamasishwa kuwa na


tabia nzuri za kusaidia katika kutunza nyumba na familia.
42-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kukubali Kukosolewa Na Mke
Kwa Moyo Mkunjufu

Zawadi Kwa Wanandoa

42-Kukubali Kukosolewa Na Mke Kwa Moyo Mkunjufu

‫االستماع إىل نقد املرأة بصدر رح‬

Walikuwa wake wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)


wakijibizana wakati mwingine, na alikuwa akiwahama mmoja wao
hadi usiku.

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) anasema kuwa


kulikuwa na maneno baina yake na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) , akaambiwa 'Aaishah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) : “Ni nani utakaemridhia baina yangu na yako?” (kusuluhisha)
Je, utamridhia 'Umar? akasema 'Aaishah: Simridhii 'Umar kabisa,
'Umar ni mkali. Akasema tena Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) : “Je, utamridhia baba yako baina yetu?” akasema 'Aaishah:
ndio. Kisha akasema:” Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
akatuma mtu aitwe Abu Bakr”, kisha akasema: “Huyu ana jambo na
jambo lake ni kadhaa.’ Akasema 'Aaishah: kisha akasema tena:
muogope Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) , na useme haki tupu,
akasema: akanyanyua Abu Bakr mkono wake, akampiga pua yake hata
damu ikatoka- kisha akasema: huna mama Ee mtoto wa Ummu
Ruumaan, unasema haki na baba yako na haki hiyo asiiseme Mtume wa
Allaah. Anasema 'Aaishah: pua yake ikasimama utafikiri Swalah wawili
hali yakimwagiwa maji kutoka katika kifuko cha maji na mfano wake.
Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kumwambia Abu
Bakr: “Mimi sikukuitia hili.” Akasema 'Aaishah: kisha akasimama na
kuchukua jarida lililokuwa nyumbani, kisha akaanza kumpiga nalo
akageuka akamkimbia baba yake, akajificha nyuma ya mgongo wa
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) . Akaendelea kusema
'Aaishah: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamwambia:
“Nimekuapia ulipotoka, sisi hatukukuita kwa hilo
(unalolifanya).” (Imefanyiwa takhrijy na Al-Haafidhw Ad-Dimashqiy)

'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) anahadithia kuwa kuna siku moja


alikuwa ameghadhibika akamwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) : “Wewe si unadai kuwa ni Mtume wa Allah! Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akatabasamu, na akalivumilia hilo
kwa huruma na ukarimu.” (Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Mwanamke anaweza kumshupalia mumewe na akateleza katika haki


ya mumewe nasi tuna mfano mwema wa kuigwa kutoka kwa Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwani yeye kwetu ni ruwaza njema
na hakika ametufundisha jinsi gani ya kuamiliana. Katika misimamo na
matukio kama haya, mwanamke ni sawa na mwanamme kwa kauli
yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Hakika wanawake ni
ndugu wa wanaume.” (Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Ni bora zaidi kwa mwanamme awe ni mwenye kutumia akili zake


vizuri kwa hekima na busara na haswa zaidi katika maeneo na matukio
ambayo mwanamke atakuwa ameteleza na kupotea, ama akiyakabili
makosa kwa makosa basi matokeo yake ni kuzidi na kupanuka tofauti
hizi, na hili ni jambo lisilopendeza kabisa, na sio kwa maslahi ya
wanandoa wawili.
43-Zawadi Kwa Wanandoa:
Kujua Fiqhi Ya Wanawake

Zawadi Kwa Wanandoa

43-Kujua Fiqhi Ya Wanawake

Familiarity with the jurisprudence of women

I don't know what's going on, what's up with what I'm doing, what's
up, what's up, what's up, what's up, what's wrong with me, how much
hafahamu hukumu's za twahara na Swalah na hedhi…

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

O you who have believed, protect yourselves and your


families from a fire whose fuel is people and stones

“Enyi mlioamini! When the Prophet zenu na watu wenu, na moto


ambao kuni zake ni watu na mawe...” (At-Tahrym: 6)

Na ikitokea mwanamke hafahamu hukumu hizi za ki-Fiqh, au


mumewe hakuweza kumfundisha ni juu yake kuwauliza Ahlu-Dhikri
(wenye ujuzi) katika mabaraza ya ki-elimu yanayo jihusisha na
wanawake.

Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

Yes, the women of the Ansar did not prevent their modesty
from learning about religion

“Wabora wa wanawake ni wanawake wa ki-Answaar ambao


haikuwazuia haya katika kujifunza mambo ya Dini.” (Al-Bukhaariy na
Muslim)
44-Zawadi Kwa Wanandoa:
Asimgongee Mwanamme
Kumgongea Mke Wake Usiku

Zawadi Kwa Wanandoa

44-Asimgongee Mwanamme Kumgongea Mke Wake Usiku

The man should not let his family knock on me

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik:

The Prophet, may God bless him and grant him peace, did
not go to his family at night. He would enter in the
morning or evening
“Kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Alikuwa hagongi
kwa mkewe usiku, Alikuwa akiingia asubuhi sana au ishaa.” (Al-
Bukhaariy na Ahmad)

Kutoka kwa ibn Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) anasema kuwa:


On the authority of Ibn Omar, the Messenger of God, may
God bless him and grant him peace, descended on Al-Aqiq
and forbade the intercourse with women. Two men
disobeyed him, and both of them saw what he disliked.
“Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alishukia alghaqiiq
akakataza kugongewa wanawake, watu wawili wakamuasi (wakenda
kugonga kwao) na wote wawili waliona mambo
yaliyowachukiza.” (Ahmad)

Here is the story of the story of 'Abdullaah bin Rawaaha' of the story of
the day, the story of the story, the story of the safari akachelewa, none
of the nyumbani kwake pana waka taa, none of the people wake up to
the kitu pamoja nae, akaamua kuchukua upanga, akasema mkewe:
koma usinisogelee, ni mwanamke Fulani anani suka, akajiwa Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika hilo na akakataza wanaume
kuwagongea milango wake zao usiku. (Ahmad)
45-Zawadi Kwa Wanandoa: Baina
Ya Wakwe Na Mke Wa Mtoto
Wao

Zawadi Kwa Wanandoa

45-Baina Ya Wakwe Na Mke Wa Mtoto Wao

‫بني احلماة والكّنة‬

Uislamu umefaradhisha kuwepo kwa maisha mema na kutendeana


vizuri katika muamala familia, na akajaalia misingi ndoa ni mapenzi na
kuhurumiana. Hivyo basi hapana budi kuwasiliana na kuoneana
huruma pamoja na wengine ndani ya familia, na haswa zaidi jamaa
zake mume na jamaa zake mke.

Na ajitahidi sana mke kutokuufanya moyo wa mume wake kuwa


mgumu sana kwa ndugu za mume wake, na kufanya mambo mabaya
ili mume awachukie ndugu zake ni kumuasi Allaah na Mtume Wake
(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) . Kuvunja udugu ni jambo lenye
kuchukiza na huondosha mahusiano ya ki-dugu, na vile vile huufanya
moyo wa mtu kuwa ni mgumu na huvunja kabisa sababu za
kuwasiliana. Wake zetu ni taa za njiani na ni nuru ya maisha na wala
sio moto uunguzao au mwiba unaochoma. Ni juu ya wanandoa kusoma
Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) inayosema:
‫وقضى ربك أال تعبدوا إال إياه وبالوالدين إحسانا‬

“ …na Mola wako Amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu.
Na (Ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi”. (Al-Israa: 23)

Furaha ya ndoa inapatikana na kukua na inaendeelea kukua kadri mke


atakavyomsaidia mumewe juu ya wajibu wake na kudumisha
mahusiano yake (mke) nae na ya wengineo.

Mwanamke ni msaidizi wa mwanamme katika kumsaidia kumtii


Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na kuwafanyia wema, upole, na
kuwanyenyekea wazazi, ndugu, wake na waume wa watoto wao.

Uislamu unatahadharisha katika ufanyaji dhulma na udikteta na huu


ni mlinganio katika kusimamisha amani ya kudumu baina yake mzazi
wa kike au wa kiume na mke wa mtoto wao wa kiume (ambae ni kama
mtoto wake wa kuzaa) na inabidi kuamiliana nao kwa upole na kwa
ukarimu na hapo ndipo yatakaposimama mahaba na kutengemaa kwa
familia.

You might also like