You are on page 1of 36

‫ْش ِة َّالز رو َج ِة ِل َز رو ِ َِجا‬

َ ‫آ َد ُاب ِع ر‬
ADABU ZA MKE KATIKA
KUISHI NA MUMEWE

:‫أعده‬
‫حفظه الل‬- ‫اركٍ ب ِْن قَ ْذ ََلنَ ْال َم ْز ُر ْو ِعي‬
َ َ‫الشيخ أَحْ َمدُ ب ُْن ُمب‬
Imeandaliwa na : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru'iy -Allah amuhifadhi .
Tarjama : Abuu Thurayyah Ismail Seiph Mbonde .
Imekusanywa na: fawaidusalafiyatz.net

1
‫إليك يا أيتها الزوجة هذه اآلداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن‬
:‫ فمن ذلك‬, ‫عشرة‬

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki
zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki
zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki
(mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na
miongoni mwa hizo (adabu ni) :
.‫عليك بحسن الطاعة بالمعروف ففيها مالك الزوج ورضى الرب‬- ١
1- Jilazimishe kumtii (mumeo) kwa uzuri katika (yale) yasiyokuwa
ya haramu ,basi katika huko (kumtii mume) kuna kummiliki mume
na kumridhisha Mola Mlezi .

Maelezo ya mfasiri:
Adabu ya kwanza kabisa ambayo sheikh ameitaja nayo ni adabu ya
wajibu kwa mke kumtekelezea mumewe ni kumtii mumewe ,na
mwanamke kumtii mumewe maana yake ni mke kumtii mumewe kwa
kadri ya uwezo wake bila ya kujiingiza katika kupata mashaka mazito
au kujidhuru .

Na dalili ya hili kwanza kabisa katika Qurani ni kauli yake Allah -


aliyetukuka- :

ٍ ‫علَى بَ ْع‬
‫ض‬ َ ‫ض ُه ْم‬
َ ‫اللُ بَ ْع‬ َّ َ‫اء بِ َما ف‬
َّ ‫ض َل‬ ِ ‫س‬َ ِ‫علَى الن‬
َ َ‫الر َجا ُل قَ َّوا ُمون‬
ِ
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake ,kwa sababu Allah
amewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine
[٣٤ :‫]النساء‬
Ufafanuzi:
2
Allah ameyaweka majukumu usimamizi ni wa mwanamume kwa
maana anawajibika kumsimamia mkewe kwa kumuadabisha na
kumzuia ndani /asitoke ila kwa idhini yake na ni wajibu kwa mke
kumtii mumewe katika yote haya maadamu hajamuamrisha la haramu
.
Na dalili ya pili ni katika suna :
Kuna hadithi nyingi zinazojulisha uwajibu wa mke kumtii mume ,na
katika hizo ni kauli yake Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie- :

‫ وما أنفَقَت ِمن‬،‫ وَل تأذَنَ في بي ِته َّإَل بإذ ِنه‬،‫تصوم وزَ و ُجها شا ِهدٌ َّإَل بإذ ِنه‬
َ ‫يح ُّل لل َمرأ ِة أن‬
ِ ‫َل‬
ُ ‫ فإنَّه يؤدَّى إليه ش‬،‫أمره‬
‫َطره‬ ِ ‫ير‬ ِ ‫نَفَق ٍة عن غ‬

"Si halali kwa mwanamke kufunga (funga ya suna) na hali ya kuwa


mumewe yupo ila kwa idhini yake ,na wala asimruhusu (yeyote)
kuingia nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake , na (mke) hatoi
kile anachokitoa bila ya amri yake (mume) , ila hakika hali ilivyo
atalipwa nusu yake"
.‫رواه البخاري‬

Maana ya hadith:
Mwanamke haruhusiwi kufunga funga ya suna pindi mumewe
anapokuwepo ila kwa idhini yake kwa sababu mume ana haki ya
kustarehe naye muda wowote atapomuhitajia na hii ni dalili kuwa
kumtii mume ni wajibu ndiyo maana kukatangulizwa juu ya ibada ya
suna . Pia mke haruhusiwi kumruhusu yeyote katika kuingia nyumbani
kwake ila kwa idhini ya mumewe hata akiwa ni mwanamke .Na
mwanamke anapotoa sadaka kutoka katika mali ya mumewe bila ya
kuamrishwa na mumewe kwa uwazi lakini akawa anafahamu kuwa
mumewe hatomkataza kutoa kiwango kama hicho alichokitoa ,au ada

3
na mazoea yanajulisha kuwa kiwango kama hicho mume hawezi
kumkataza basi mwanamke huyo atapata nusu ya thawabu ,ama
akitoa kiwango kikubwa bila ya idhini yake ya wazi wala kimazoea
muda huo huyo mwanamke atapata madhambi .Vile vile katika faida
anayoipata mke pindi atapomtii mumewe ni kummiliki huyo mumewe
na kuzidi mapenzi yake kwake kwa sababu maumbile ya wanaume
wanapenda kusikilizwa na kupewa nafasi yao ya utawala ktk nyumba
.

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru'iy -


Allah amuhifadhi .

.‫القناعة كنزك في حياتك وراحة لقلبك في جميع أوقاتك‬- ٢


2- Kukinai /kutosheka ni hazina katika maisha yako na ni raha ya
moyo wako katika wakati wako wote.

Maelezo ya mfasiri :
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya pili katika adabu za mke
kuishi na mume nayo ni kukinai /kutosheka :
Na kukinai maana yake : Ni kuridhia kile alichokupa Allah ,na
kutokodolea macho vya wengine.
Amesema Allah aliyetukuka- :
‫س ِن‬ َ ً ‫صا ِل ًحا ِمن ذَ َك ٍر أ َ ْو أُنثَى َو ُه َو ُمؤْ ِم ٌن فَلَنُحْ يِيَنَّهُ َحيَاة‬
َ ْ‫طيِبَةً َولَنَجْ ِزيَنَّ ُه ْم أَجْ َر ُهم بِأَح‬ َ ‫ع ِم َل‬ َ ‫“ َم ْن‬
” َ‫َما َكانُواْ يَ ْع َملُون‬
" Wale waliofanya mema,wanaume au wanawake ,hali ya kuwa ni
waumini , tutawahuisha maisha mazuri ,na tutawapa ujira wao
(akhera) kwa sababu ya yale mazuri waliyokuwa wakiyatenda .
٩٧:‫النحل‬

4
Ufafanuzi : Mwenye kufanya mema atapewa maisha mazuri na baadhi
ya maswahaba-Allah awaridhie wamefasiri "maisha mazuri" hapa ni
kukinai/kutosheka .Rejea tafsir ya Twabariy .
Na katika sunnah kuna hadithi nyingi zinazohimiza kukinai lakini
miongoni mwa hizo ni kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah
zimfikie- :
َّ ُ‫ َوقَنَّعَه‬،‫ َو ُر ِزقَ َكفَافًا‬،‫"قَ ْد أ َ ْفلَ َح َمن أ َ ْسلَ َم‬
" ُ‫اللُ بما آت َاه‬
" Bila shaka amefaulu yule aliyekuwa muislamu wa kweli ,na
akaruzukiwa kinachomtosha ,na Allah akamfanya kuwa ni mwenye
kutosheka kwa kile alichompa "

‫َر َواهُ ُم ْس ِل ٌم‬


Ufafanuzi wa hadithi :
Bila shaka muislamu wa kweli amefaulu kwa kuepukana kwake na
ushirikina na ukafiri, na akapewa riziki inayomtosha isiyozidi wala
kupungua akawa na uwezo wa kutatua haja zake na yale ya dharura,na
Allah akamruzuku kutosheka kwa kile alichompa ambacho
kinamtosha.Na wanachuoni wengine wamesema mwenye kusifika na
sifa hizo zilizotajwa katika hiyo hadithi atakuwa amepata yale
anayoyataka ,na ameshinda kwa kupata anayoyataka duniani na
akhera .
Ewe mke kukiwa kukinai kuna daraja hili kwa waislamu wote, bila
shaka kukinai kwa mke katika maisha ya ndoa ni sababu kubwa ya
kupatikana utulivu katika maisha ya ndoa kwa sababu mke asiyekuwa
na tabia hii mzuri ya kukinai bila shaka atakuwa na tabia ya kukodolea
vya watu na kutamani vya wengine tena vile ambavyo vipo juu ya
uwezo wake !matokeo yake ni kumtia mume uzito na ikawa ndiyo
sababu ya kuchukiwa na mume au kuachwa kwa sababu mke
asiyekuwa na tabia ya kukinai ni mzigo usiobebeka .

5
Ewe mke tambua kuwa ukiwa na tabia ya kukinai na kutosheka
ulichonacho basi wewe ni tajiri ,kama alivyosema swahaba mtukufu
ibn Abbas- Allah amridhie-:
"‫"القناعة مال َل نفاد له‬
"Kukinai /kutosheka ni mali isiyomalizika "
.)١٦٩/٣ (:‫ذكره ابن عبد ربه في العقد الفريد‬
Kukinai kunafaida nyingi mno katika hizo ni kupata utulivu wa nafsi .

.‫ال تقع عينه منك على قبيح وال يراك إال في كل مليح‬- ٣
3- Lisikuone jicho lake katika ubaya na wala asikuone isipokuwa
katika uzuri /urembo .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi -anataja adabu ya tatu katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni hii : Mke anatakiwa ajiweke katika hali ya
kumfurahisha mumewe,awe kila anapomuona anafurahi kwa
kushikamana kwake na dini,kwa uzuri wake wa tabia,kwa kujipamba
/kujiremba kwake ,na hii ni sifa miongoni mwa sifa za mwanamke
mwema kama ilivyothibiti kuwa Mtumbe -swala na salamu za Allah
zimfikie- aliulizwa : Ni yupi mwanamke bora ?
akajibu:
‫ وَل تخالفُه في نف ِسها ومالها بما يكره‬، ‫ وتطيعُه إذا أمر‬، ‫تسره إذا نظر‬
ُّ ‫التي‬
Ni yule ambaye anamfurahisha (mumewe) pindi anapomtezama,na
anamtii pindi anapomuamrisha, na wala hamuasi (mumewe) kwa
kufanya machafu ,na wala (hamuasi) katika mali zake (mume) kwa
kuzitoa katika yale asiyoyapenda .
٣٢٣١ ‫أخرجه النسائي‬
6
Ufafanuzi wa hadith:
Huyu ndiye mwanamke bora ,hazina ya mume katika dunia na ndiyo
starehe yake bora na ndiye mbora wa wanawake ,na ndiye mwenye
baraka kwa mumewe ,na hizo zilizotajwa ni miongoni kwa sifa zake
kama vile kumfurahisha mumewe kidini ,kitabia na kimuonekano,
kama tulivyoeleza hapo juu na pia katika tabia zake ni kutotoa mali za
mume katika yale asiyoyapenda au ya haramu ,na wala hamuasi
mumewe kwa kutoka nje ya ndoa yaani kufanya machafu

Tanbih:
Bila shaka uzuri wa kwanza kabisa unaokusudiwa ni uzuri wa dini lakini
haina maana mwanamke ajiweke katika hali mbaya kwa mumewe bali
anatakiwa ajipambe na kutilia umuhimu usafi na kujipamba ,hebu
tumwangalie huyu mmoja katika wema waliopita pindi alipokuwa
akimuusia binti yake pindi alipomuozesha :
:‫ ما رواه سعيد بن يزيد‬،‫ومما يروى في وصية األب ابنته عند الزواج‬
Miongoni mwa yale yanayopokewa katika wasia wa baba kwa binti
pindi anapoolewa ni ule (wasia) alioupokea Sa'iid bin yaziid:
:‫ فقالت‬،‫ فأتته الجارية‬،‫أن أبا األسود الدؤ لي زوج ابنة له‬
:‫ فقال‬،‫ فأما إذا زوجتني فأوصني‬،‫ إني لم أكن أحب أن أفارقك‬،‫يا أبه‬
.‫ واعلمي أن أطيب الطيب الماء‬،‫إنك لن تنال ما عنده إَل باللطف‬
Kwamba Abuu Al-aswad Addualiy alimuozesha binti yake (basi) yule
binti akamjia (baba yake) na akasema: Ewe baba yangu hakika mimi
nilikuwa sipendi kuachana na wewe, na ama ukiniozesha (basi) niusie,
akasema (baba yake):
Hakika wewe hauto yapata yale yaliyopo kwake (mume) isipokuwa
kwa (kutumia) upole (ulaini), na tambua kwamba manukato mazuri
zaidi (ni) maji.
. ‫ إلى ابن أبي الدنيا بسند صحيح‬,219:‫ ص‬,‫عزاه ابن الجوزي في "أحكام النساء‬
7
Ufafanuzi :
Mke anatakiwa awe mpole na mlaini kwa mumewe na akiwa hivi basi
atapata heri nyingi na kufurahi katika ndoa yake, pia mke atilie
umuhimu sana kuusafisha mwili wake kwa kuoga ili mume asimchukie
kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka katika mwili wake, kuna
baadhi ya wanawake kutokana na kutotilia umuhimu usafi
husababisha waume zao kuwachukia ,na pengine ikawa ndiyo sababu
ya kutafuta mke mwingine ili apate utulivu, au wale wasiokuwa na
hofu ya Allah huingia katika uzinifu ! -Allah atukinge na hilo- ,kwa hiyo
ewe mke jitahidi ujiweke katika hali ya kuvutia kwa mumeo usije
ukawa ni sababu ya kuharibu ndoa yako .

.ً ‫خدمته في بيته بجعله جنة وراحة ال تجعليه مهربا ً ومالذا‬- ٤


4- Kumtumikia (mume) nyumbani kwake kwa kuifanya (nyumba)
kuwa ni bustani na (yenye) raha na wala usiifanye hiyo (nyumba)
kuwa ni sehemu ya makimbilio na sehemu ya kujihifadhi /kwa
muda"

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya nne katika adabu za mke
kuishi na mumewe ,nayo ni adabu ya kumhudumia mume na
kumtumikia .
Mke anawajibika kumtumikia mumewe, na majukumu ya kuitumikia
nyumba pia ni majukumu ya mke , Mtume - swala na salamu za Allah
zimfikie amesema :
ٌ‫ت بَ ْع ِلها وولدِه وهي مسؤولة‬
ِ ‫ والمرأة ُ راعيةٌ على بي‬، ....‫كلُّكم راعٍ وكلُّكم مسؤو ٌل عن رعيَّتِه‬
" ، ....‫عنهم‬

8
" Nyote ni wachunga na nyote ni wenye kuulizwa kuhusu wale
aliowachunga ...na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya
mumewe na wanae, na huyo (mwanamke) ataulizwa kuhusu hao "
.‫رواه ابن حبان‬
Mchanganuo:
Mke kumtumikia mumewe hili ni jambo la ada na limezoeleka katika
jamii mbalimbali kuwa wanawake hufanya kazi za ndani ,na ni wajibu
kwake kufanya hivyo kama walivyosema baadhi ya wanachuoni -Allah
awarahamu- .
Mke anatakiwa amtumikie mumewe na nyumba kwa ujumla mpaka
mumewe awe anatamani kuwepo nyumbani na pindi anapokuwepo
awe anahisi kama vile yupo katika bustani mzuri inayopendeza ,awe
anahisi raha ,na awe anatamani kuwepo muda wote na mke asiifanye
nyumba ikawa ni kama sehemu ya kukimbilia (kwa muda) au kupata
hifadhi kwa muda !, na ada ya wanawake kuwatumikia waume zao
ndivyo ada ya wanawake wa maswahaba,walikuwa wakiwatumikia
waume zao, na wala haifai kwa mke kukataa kumtumikia mumewe ,na
wala haifai kuchukua malipo maalumu kwa ajili ya huku kumtumikia
mumewe , na hapa nainukuu fatwa ya sheikh Fauzan- Allah
amuhifadhi- pale alipoulizwa -:
: ١٩٠ ‫السؤال‬
Swali la 190:
‫هل يجوز للزوجة أخذ أجرة من زوجها على ما تهيئه من الطعام ألكلهما؟‬
Je, anaruhusiwa mke kuchukua ujira (malipo) kutoka kwa mumewe
juu ya kile chakula anachomuandalia kwa ajili ya kula?
‫الجواب‬
Jawabu:
،‫المرأة يجب عليها أن تقوم بما جرت عادة النساء في بلدها بعمله في بيتها بدون أجرة‬

9
Mwanamke inawajibika juu yake ayatekeleze yale ambayo imejiri ada
(kawaida) ya wanawake katika mji wake kwa kufanya kwao (kazi)
ndani ya nyumba bila ya ujira (malipo),
.‫ألن المتعارف عليه في البلد كالمشروط‬
Kwa sababu lile lililozoeleka katika mji (fulani) ni kama liloshurutishwa.
.‫وقد جرت العادة في بالدنا بقيام المرأة بالطبخ ونحوه فهو واجب عليها‬
Na bila shaka yamejiri mazoea katika miji yetu (Saudia) mwanamke
kusimamia kupika na mfano wa hilo basi (kazi) hiyo ni wajibu juu yake.
.‫المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان‬
[ Al-muntaqaa min fatawaa Sheikh Al-fauzan ]
Maelezo kutoka kwa Mfasiri - juu ya fatwa ya sheikh- Allah
amuhifadhi
Mwanamke anawajibika kufanya kazi za ndani, haya ndiyo mazoea na
ada sehemu mbalimbali duniani kale mpaka sasa ,hata hapa kwetu
Tanzania ,na msingi wa kisheria kama alivyoeleza Sheikh unasema:
“ ‫”المعروف عرفا كالمشروط شرطا‬
“ Kinachojulikana kwa mazoea ni kama kilichowekewa sharti ”
Mfano ukimuoa mwanamke baada ya kumleta ndani akakwambia
sipiki, sifui.. mwambie: mazoea na ada ya sehemu zetu hizi kazi za
ndani ni kazi za mwanamke kwa hiyo unawajibika kuzifanya kwa
maana haya mazoea ni kama sharti. Kwa hiyo kauli inayosema kuwa
mwanamke ameolewa kwa ajili ya kazi moja tu ya kumstarehesha
mume! Hii kauli ni dhaifu kama alivyoeleza Sheikh Al-albaaniy - Allah
amrahamu - katika "Aadaabu Zzifaaf"
Na pia tendo la ndoa wote wanalihitajia na wote wanapata raha tena
kuna wanaosema kuwa mwanamke hustarehe zaidi!

.‫أوالدك تربيتك فإنه يراك من خالل تربيتك فحسن تربيتك دليل حسن عشرتك‬- ٥

10
5- Watoto wako ni malezi yako ,na bila shaka huyo (mume)
anakuona kupitia malezi yako ,basi uzuri wa malezi yako ni dalili ya
uzuri wa kuishi kwako kwa wema (na mumeo).

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh Allah -amuhifadhi- anataja adabu ya tano katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni malezi ya watoto : Anatakiwa mke
atambue kuwa pindi anapowasimamia vizuri wanae katika malezi basi
hilo humfurahisha mume na huko pia ni katika kuishi vizuri na mume
,na kuzidisha mapenzi ya mume kwake ,na hapa kuna haja ya kutaja
baadhi ya nukta zitakamzo msaidia mwanamke -kwa idhini ya Allah -
katika kuwalea watoto wake malezi sahihi :
1- Mke anatakiwa ajue kuwa yeye ni mama wa watoto na yeye ndiye
msingi katika malezi, kwa sababu yeye mara nyingi huchanganyika na
watoto kwa hiyo hupata fursa ya kuwaongoza ,kuwanasihi n.k.
2- Mke anatakiwa ajue yanayowajibika katika malezi na namna ya
kuwalea watoto .
3- Soma historia za wanawake wema waliopita ili ujue namna
walivyolea watoto wao mpaka wakafanikiwa kuwatoa wanachuoni
wakubwa walioijaza dunia elimu ,na maadili mema .
4- Ifanye shughuli hii ya malezi ndiyo mradi wako unaokushughulisha
na utoe juhudi zako zote katika hilo, weka mipango mbalimbali katika
malezi kwa sababu kuwalea kwako watoto wako katika malezi sahihi
ni sadaka yenye kuendelea baada ya kufa kwako.
5- Kithirisha kuwaombea dua na rudia rudia usichoke na haswa zile
nyakati ambazo hutarajiwa zaidi kujibiwa dua huwenda dua ikawa
ndiyo sababu ya kufaulu katika malezi yako , na kuwaombea dua
watoto ni kawaida ya mitume kuwaombea dua watoto wao ,na
miongoni mwa dua za nabii Ibrahimu ni hii:
"‫َام‬
َ ‫صن‬ْ َ ‫ي أ َ ْن نَ ْعبُدَ ْاأل‬
َّ ‫َواجْ نُ ْبنِي َوبَ ِن‬
11
"Na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu " .
6- Na katika majukumu yako makubwa zaidi ni kuwatamkisha watoto
na kupandikiza itikadi sahihi, na hata kama hawajafahamu katika umri
huo baadae watafahamu ,kama vile kuwatamkisha tamko la tauhid :
" ُ‫« ََل ِإ ٰلهَ ِإ ََّل هللا‬
Hukuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah
.
Na kuwatamkisha maswali matatu ambayo ni katika misingi ya itikadi
:
.‫ومن نبيك‬، ‫ وما دينك‬،‫َم ْن َربُّك‬
Nani muabudiwa wako ,na ipi dini yako,na nani Mtume wako ? .
7- Tambua kuwa kipindi cha utoto ni kipindi cha kupandikiza ,na kile
kinachopandikizwa muda huo ndicho kitachodhihiri baadae ukubwani
kwa hiyo kuwa ni kiigizo chema kwa watoto wako kwa sababu watoto
huiga kila wanachokiona .

.‫إياك والتبذير في المال والطعام وعليك بحسن التدبيروالتقدير‬- ٦


6- Tahadhari na kufanya ubadhirifu katika mali na chakula na
jilazimishe na upangiliaji /uendeshaja mzuri na ukadiriaji (mzuri) .
Maelezo ya mfasiri :
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya sita katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni kujiepusha na kutumia mali na chakula kwa
fujo ,na bila shaka uislamu umekataza ubadhirifu kwa maana utumiaji
ovyo kwa fujo kama alivyosema Allah :
.ً ‫َوَلَ تُبَذ ِْر ت َ ْبذِيرا‬
Na wala usitawanye (mali yako) ovyo kwa fujo .
ً ‫ان ِل َر ِب ِه َكفُورا‬
ُ ‫ط‬َ ‫ش ْي‬
َّ ‫ين َو َكانَ ال‬
ِ ‫اط‬
ِ َ‫شي‬ ِ َ‫ِإ َّن ْال ُمب‬
َّ ‫ذرينَ َكانُواْ ِإ ْخ َوانَ ال‬

12
Hakika wenye kutumia kwa ubadhirifu ni ndugu wa Mashetani .Na
Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi .

.٢٧-٢٦ : ‫اإلسراء‬
Na amesema Allah aliyetukuka-:
َ‫َو ُكلُوا َوا ْش َربُوا َو ََل تُس ِْرفُوا ِإنَّهُ ََل ي ُِحبُّ ْال ُمس ِْر ِفين‬

{Na kuleni na kunyweni .Lakini msipite kiasi .Hakika yeye (Allah)


hawapendi wapitao kiasi .

[٣١ :‫]األعراف‬
Na vilevile amesema Allah- alipokuwa akitaja sifa za waja wema :
‫َوالَّذِينَ ِإذَا أَ ْنفَقُوا لَ ْم يُس ِْرفُوا َولَ ْم يَ ْقت ُ ُروا َو َكانَ بَيْنَ ذَ ِل َك قَ َوا ًما‬
Na wale ambao wanapotumia hawatumia hawatumii kwa fujo ,na
wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo .
٦٧ :‫الفرقان‬.
Na katika sunnah ni kauli take Mtume- swala na salamu za Allah
zimfikie- :
ِ ‫ والبَسوا في‬، ‫ُكلوا وتصدَّقوا‬
‫غير إسرافٍ وَل َمخيَل ٍة‬
Kuleni na toeni sadaka na vaeni bila ya (kufanya) fujo wala kujigamba
.٢٥٥٨ ‫رواه النسائي‬
Mchanganuo:
Muislamu anakatazwa kufanya fujo na uharibifu katika matumizi ya
mali kama vile kuvaa,kula na matumizi mengine bali anatakiwa awe
mchumi yaani asiwe mbakhili na wala asitumie ovyo ,na mwanamke
ambaye atakuwa na tabia ya utumiaji ovyo kwa fujo na kupita kiasi bila

13
shaka huyu atakuwa haishi na mumewe kwa wema kwa sababu
kitendo cha kuwa na tabia hii ,mke huyu hufanya ubadhirifu katika
mali za mumewe ,na pia huwenda akawa ni sababu ya kumrudisha
nyuma mumewe katika maendeleo kwa kule kutumia kwake ovyo mali
kiwango ambacho lau angekiweka kingetumika katika matumizi
mengine ,kwa hiyo matumizi ya kupita kiasi yana madhara hapa hapa
duniani na pia ni haramu ,na kuna wanawake wengi wa kiislamu
wanaopika vyakula vingi mpaka vikabaki na baada ya hapo hutupwa
na huku ni katika kukanusha neema za Allah na sababu ya kutokea hili
ni mwanamke kutokuwa mchumi na mwenye makadirio mazuri katika
matumizi .

Na kuna wale ambao kila nguo wanayoiona wanaitaka ! kila mtindo


utokao wa viatu au nguo yeye anataka awe nayo !,bila shaka hii ni njia
ya kuingia katika utumiaji mbaya wa mali.
Ewe mke kuwa mchumi na mpangiliaji mzuri wa matumizi ya
nyumbani kwako kwa kufanya kwako hivyo ni katika kuishi kwa wema
na mumeo na ni sababu ya kuchangia maendeleo yake .

.‫إياك وإفشاء سره فإن أفشيت سره لم تأمني غدره وضيق صدره‬- ٧
7- Tahadhari na kusambaza siri zake (mumeo), basi kama
utasambaza siri zake hautopata amani kutokana na khiyana yake,
na dhiki/uzito wa kifua chake .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya saba katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutunza siri za mume yaani
kutunza siri za ndoa na huu ni wajibu kwa mume na mke , na mke pindi
atapokuwa anatoa siri za mumewe ajue kuwa kufanya kwake hivyo ni

14
sababu ya kumfanya kuondoa uaminifu wake kwa mumewe na
huwenda mumewe akamfanyia khiana kwa sababu ya kueneza kwake
siri za ndani ,na pia jambo hilo la kueneza siri za mume humfanya
mume kutokuwa na raha na huhisi dhiki katika kifua chake kwa sababu
huhisi kila anapopita habari zake zinajulikana! .
Na hukumu ya kutoa siri ndani za baina ya wanando wawili na haswa
zinazohusu kitandani ni haramu, na hata siri nyingine kama mume
atamwambia asizitoe na kuzieneza au akijua tu kwamba hili mume
wake hataki alifahamu yeyote ,na uharamu wa kusimulia ya kitandani
umethibiti katika hadithi ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-
pale alipowauliza baadhi ya waislamu je kuna yeyote anayefanya
jambo hilo yaani anayekutana na mumewe au mume na mkewe kisha
anasimulia ? ,baada ya kujibiwa kuwa wapo wanaolifanya hilo ,Mtume
-swala na salamu za Allah zimfikie- akasema -:

:‫ه َْل ت َ ْد ُرونَ َما َمث َ ُل ذَ ِل َك؟ فَقَا َل‬

Je munajua upi mfano wa huyo (mfanyaji wa hilo) ? akasema:


ُ ‫اس يَ ْن‬
‫ظ ُرونَ ِإلَ ْي ِه‬ َ َ‫الس َّك ِة فَق‬
ُ َّ‫ضى ِم ْن َها َحا َجتَهُ َوالن‬ َ ‫ش ْي‬
ِ ‫طانًا فِي‬ َ ‫ت‬ َ ‫ش ْي‬
ْ َ‫طانَ ٍة لَ ِقي‬ َ ‫ِإنَّ َما َمث َ ُل ذَ ِل َك َمث َ ُل‬
Hakika si vinginevyo mfano wa huyo ni mfano wa Shetani wa kike
aliyekutana na Shetani wa kiume barabarani ,na akakidhi haja zake
kwa (huyo Shetani wa kike) na hali ya kuwa watu wanamtezama.

٢١٧٤ ‫رواه أبو دادد‬

Ufafanuzi wa hadithi:
Hii na dalili wa uharamu wa kutoa siri za kitandani baina ya wanandoa
wawili na yale yote yanayohusu tendo la ndoa ,na dalili ya uharamu
wa hilo ni pale Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie- amemweka
15
mtu huyu katika daraja la mashetani wanaoingiliana na watu
wanawatezama ! .
Na hadithi nyingine inayojulisha uharamu wa hilo ni kauli yake Mtume
- swala na salamu za Allah zimfikie- :
ِ ‫ضي ِإلَى ْام َرأَتِ ِه َوت ُ ْف‬
ُ ‫ضي ِإلَ ْي ِه ث ُ َّم يَ ْن‬
‫ش ُر‬ َّ ‫الل َم ْن ِزلَةً يَ ْو َم ْال ِقيَا َم ِة‬
ِ ‫الر ُج َل يُ ْف‬ ِ َّ‫ِإ َّن ِم ْن أَش َِر الن‬
ِ َّ َ‫اس ِع ْند‬
‫ِس َّرهَا‬
{Hakika katika watu wenye daraja baya zaidi mbele ya Allah siku ya
kiama ni mwanamume anayekutana na mkewe na (mke) akakutana na
yeye kisha akaeneza siri yake } .
.) ١٤٣٧ ( ‫رواه مسلم‬
Mchanganuo wa hadithi:
Hii ni dalili kuwa ni haramu kuadithia mambo yanayotokea baina ya
wanandoa na hapa ametajwa mwanaume kwa sababu mara nyingi hili
hutokea kwa wanaume kama walivyoeleza baadhi ya wanachuoni .
Na aliulizwa sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
Inazidi kwa baadhi ya wanawake (tabia ya) kuhamisha mazungumzo
ya ndani na maisha yao ya ndoa pamoja na waume zao (huyapeleka)
kwa ndugu zao na rafiki zao ,na baadhi ya haya mazungumzo ni siri za
ndani (ambazo) waume hawapendi kuyajua yeyote ,basi ni ipi hukumu
juu ya wanawake ambao hufanya tendo la kueneza siri na kuzihamisha
nje ya nyumba au kwa baadhi ya wanafamilia ?
Sheikh akajibu kwa kusema:
‫إن ما يفعله بعض النساء ِمن نقل أحاديث المنزل والحياة الزوجية إلى األقارب والصديقات‬
، ‫ أو حالها مع زوجها إلى أح ٍد من الناس‬، ‫سر بيتها‬
َّ ‫ وَل يحل َلمرأة أن تفشي‬، ‫محرم‬
َّ ‫أمر‬
Hakika yale wanayoyafanya baadhi ya wanawake katika kuhamisha
baadhi ya mazungumzo ya nyumbani na Maisha ya ndoa kwa watu wa
karibu na marafiki ni jambo lililoharamu na wala si halali kwa
mwanamke kutoa siri za nyumba yake au hali yake na mume wake kwa
mtu yeyote.

16
‫زوجك جنتك أو نارك فحسن العشرة وجميل الصحبةوحسن الكلمة تضمن لك تلك الجنة‬- ٨
8- Mume wako ni pepo yako au moto wako ,basi ishi naye kwa
wema,na suhubiana (kuwa) naye kwa uzuri ,na kwa maneno mazuri,
(matendo hayo) yatakudhaminia pepo .

Maelezo ya mfasiri: Sheikh -Allah amuhifadhi-anataja adabu ya nane


katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni hii ambayo ni kama
vile inatilia nguvu adabu zilizopita nayo ni kuwa mke anatakiwa aishi
na mume wake kwa wema mpaka mumewe amridhie , na ajiepushe
na kumuudhi mumewe kwa sababu huyo mume ndiyo pepo yake au
moto wake!, ni nini maana ya maneno haya tusome hadithi hii :

:‫صن‬
َ ْ‫صيْن بن ِمح‬
َ ‫وروى اإلمام أحمد والحاكم عن ال ُح‬
Amepokea imamu Ahmad na Al-hakim kutoka ka Al-huswain bin
Mihswan :
- ‫ فقال لها النبي‬،‫ في حاجة ففرغت من حاجتها‬-‫صلى هللا عليه وسلم‬- ‫أن عمة له أتت النبي‬
-:‫صلى هللا عليه وسلم‬
Kuwa shangazi yake alimjia Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-
kwa ajili ya haja (fulani), alipomaliza haja yake, Mtume- swala na
salamu za Allah ziwe juu yake- akamuuliza
‫ ما آلوه (أي َل أقصر في حقه) إَل‬:‫كيف أنت له؟ "قالت‬:"‫ قال‬.‫"أذات زوج أنت"؟ قالت نعم‬
. ‫ما عجزت عنه‬
" Je una mume " ? ,akajibu:Ndio .(Mtume) akamuuliza (tena) : Upo
naye vipi ?, akajibu: Sipunguzi katika haki zake isipokuwa yale
niliyoyashindwa .
". ‫فانظري أين أنت منه فإنما هو جنتك ونارك‬:"‫قال‬

17
(Mtume) akasema: Basi angalia /chunguza upo naye vipi huyo
(mumewako) ,na hakika si vinginevyo huyo (mume ni) pepo yako na
moto wako .
".‫)ورجاله رجال الصحيح خال حصين وهو ثقة‬:"٤/٥٦٣(‫[قال الهيثمي في مجمع الزوائد‬
Kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- :
"...Hakika si vinginevyo huyo (mumeo) ni pepo yako na moto wako " .
Maana yake : Huyo mume ni sababu ya kuingia mke peponi kama
akitekeleza haki zake na mume akafurahi na kumridhia mkewe hiyo ni
sababu ya kuingia peponi ,na ni sababu ya kuingia kwake motoni kama
akizembea katika hilo kama vile akamkasirisha na kumfanyia ujeuri
n.k.

Mke ajitahidi katika kumtii na kumridhisha mumewe katika yale ya


halali awe karibu na mumewe katika dhiki na raha aitikie wito wake
pindi anapomuhitaji, akiishi hivi na mumewe basi ni sababu ya kuingia
peponi , na vile vile atahadhari na kumuasi mumewe na
kutomtekelezea haki zake kwa sababu kufanya hivyo ni katika sababu
za kuingia motoni, na kwa hadithi hii baadhi ya wanachuoni
wameeleza kuwa kumuasi mume na kumfanyia jeuri ni katika
madhambi makubwa .

TAHADHARI:
Wanawake wengi wameacha kuwaheshimu na kuwakirimu waume
zao na kuchunga haki zao ni kwa sababu ya kuathirika kwao na
maneno ya makafiri wa kimagharibi ya kudai usawa baina ya jinsia
mbili yaani wanaume na wanawake, au kauli yao:Mwanamke anaweza
! ,wanakusudia kuwa anaweza kusimamia yale majukumu ya
mwanamume !.

18
Wanawake wa kiislamu washikamane na dini yao ambayo miongoni
mwa mafundisho yake ni mke kumtii mume ,na kumuheshimu na
kumpa nafasi yake ya usimamizi wa nyumba akiwemo yeye mke.

.‫اشكريه على القليل وإياك وتكفير العشير فإن صاحبه متوعد بالسعير وبعد الخليل‬- ٩
9- Mshukuru huyo (mumeo) juu ya kichache na tahadhari na
kukanusha neema za mume, hakika mwenye kufanya hivyo ni
mwenye kuahidiwa adhabu na kutengwa mbali na Mwandani (wa
Allah yaani Mtume) .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh - Allah amuhifadhi - anataja adabu ya tisa katika adabu za mke
kuishi na mumewe, nayo ni adabu iliyokusanya mambo kadhaa :

Mosi :- Kumshukuru mume, maana yake ni hii: Mke anatakiwa


amshukuru mumewe kwa ulimi wake kwa kumsifu na kwa vitendo
vyake kwa kudhihirisha raha na furaha kwa kuwa pamoja na huyo
mumewe, na ayasimamie mambo ya mumewe na watoto wao, na
amtumikie huyo mumewe, na asimuache mumewe katika kipindi cha
matatizo yaliyompata, na asiyapekue makosa ya mumewe, na
amuitikie anapomuita, na ahifadhi siri zake, kwa kifupi asimshukuru
mumewe kwa maneno tu lakini vitendo vyake vikawa ni vibaya kwa
mumewe kwa sababu huku si kumshukuru mume, na kutomshukuru
mume ni sababu ya kukasirikiwa na Allah - aliyetukuka - na
kutoangaliwa kwa jicho la rahma, kama alivyosema Mtume - swala na
salamu za Allah zimfikie -:

.ُ‫وهي َل ت َست َغني عنه‬


َ ‫لزوجها ؛‬
ِ ‫ينظر هللاُ تبارك وتعالى إلى امرأةٍ َل تش ُك ُر‬
ُ ‫َل‬

19
"Allah - aliyezidi kheri na kutukuka - hamtizami mwanamke
asiyemshukuru mumewe, na hali ya kuwa yeye hajitoshelezi bila huyo
(mume) " .

‫ صحيح الترغيب‬.

Pili- Mke atahadhari na tabia ya kupinga wema wa mume kwa sababu


tendo hilo ni sababu ya kuingia motoni na kutengwa mbali na
mwandani wa Allah [yaani Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie
], kama alivyoeleza Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie - pindi
alipowahutubia wanawake siku ya eid akawaambia watoe sadaka na
akawaeleza kuwa yeye ameoneshwa kuwa wao ndiyo watu wengi
zaidi wa motoni, na wakamuuliza :

Kwa nini ewe Mtume wa Allah? akasema:


" ‫و ت َ ْكفُ ْرنَ ْالعَ ِشي َْر‬،
َ َ‫"ت ُ ْكثِ ْرنَ اللَّ ْعن‬
" Munakithirisha laana/matusi na munakanusha ihsani ya mume " .

‫ رواه البخاري‬.

‫ارضي بما يرضيه فيما فيه رضى هللا وال تكوني وقت رضاه ساخطة ووقت سخطه‬- ١٠
.‫راضية‬
10- Ridhia kwa yale anayoyaridhia (mumeo) katika yale ambayo
Allah anayaridhia, na wala usiwe mwenye kukasirika pindi mumeo
anapokuwa ni mwenye kuridhia, na wala usiwe ni mwenye kuridhia
pindi anapokuwa amekasirika .

20
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh- Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi (10) katika adabu za
mke kuishi na mumewe nayo: Mke anatakiwa ayaridhie yale
anayoyaridhia mumewe katika yale ambayo Allah anayaridhia mfano:
kama mume anaridhia kumuona mkewe ni mwenye kutabasamu basi
mke anatakiwa adhihirishe tabasamu mbele ya mumewe, mume
akiwa anaridhia kumuona mkewe amevaa nguo ya aina fulani basi
mke avae nguo hiyo. Kwa hiyo kila jambo ambalo mume analiridhia na
ndani yake kuna kupata radhi za Allah basi anatakiwa mke amfanyie
mumewe ama likiwa ni la haramu hatoruhusiwa kumridhisha mume
katika hili.

Vile vile mke anatakiwa ashirikiane na mumewe katika raha na shida


mfano kama mume atakuwa amepatwa na mtihani uliomkosesha raha
basi mke anatakiwa aoneshe kuwa hana raha kama mumewe, na wala
asioneshe hali iliyo kinyume na mumewe kwa maana akawa na furaha
na hali ya kuwa mumewe yupo katika majonzi, hali hii itapelekea
kupungua mapenzi ya mume kwa mke .
Pia mume anapokuwa na furaha na raha naye mke anatakiwa
adhihirishe furaha na raha ili ashirikiane na mumewe katika hiyo
furaha na raha hata kama yeye alikuwa hana raha .
Na hivi ndivyo walivyokuwa wanawake wa wema waliopita hebu
tusome tukio hili walikuwa wakishirikiana na waume zao katika hali
zote za raha na shida .
‫ ما يبكيك ؟‬: ‫بكى عبد هللا بن رواحة فبكت امرأته فقال لها‬
Abdullah bin Rawaahah alilia, basi mkewe (naye) akalia muda huo huo,
basi (Abdullah) akamuuliza huyo (mkewe) : Kipi kinakuliza ?
} ‫ إني ذكرت هذه اآلية { و إن منكم إَل واردها‬: ‫ رأيتك تبكي فبكيت قال‬: ‫قالت‬
(Mwanamke) akasema: Nimekuona ukilia basi na mimi nikalia,
akasema (Abdullah): Hakika mimi nimekumbuka aya hii :
21
{Na hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa atauingia huo (Moto)}
‫و قد علمت أني داخلها فال أدري أناج منها أنا أم َل‬
Na bila shaka najua kuwa mimi ni mwenye kuungia huo (moto kwa
kuuvuka) basi mimi sijui ni mwenye kuokoka kutokana na huo (moto)
au laa .
‫ التخويف من النار والتعريف بحال دار البوار‬: ‫المصدر‬
‫ ألبي الفرج عبد الرحمن بن أحمد بن رجب الحنبلي‬:‫المؤلف‬

Mchanganuo:
Hebu tazama huyu mwanamke – Allah amrahamu – alilia pindi
alipomuona mumewe akilia, bila shaka haya ni mapenzi makubwa
aliyokuwa nayo kwa mumewe kiasi ambacho anashirikiana naye
katika huzuni na raha .

.‫طاعة هللا سبب لأللفة والقرب فكوني على صالتك مقبلة وعلى عبادتك مداومة‬- ١١
11- Kumtii Allah ni sababu ya (kuleta) mshikamano na ukaribu, basi
kuwa ni mwenye kuzielekea swala zako ,na mwenye kudumu na
ibada zako

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na moja (11) katika
adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni : kukithirisha kuswali na
kudumu na ibada kwani kukithirisha kumcha Allah ni sababu ya
kuimarisha na kutunza mshikamano wao baina yake na mumewe , na
mwanamke ajue kuwa kukithirisha kwake kuswali na ibada mbalimbali
hiyo ndiyo sababu na siri ya kuwa mrembo mbele ya mumewe
,tunaweza kusema kuwa hii ndiyo siri ya urembo bila ya kutumia

22
mkorogo (kujichubua) , kama anavyosema ibn l-Qayyim- Allah
amrahamu- :
:‫ فقالت‬،‫وقد كان بعض النساء تكثر صالة الليل فقيل لها في ذلك‬
.‫إنها تح ِسن الوجه وأنا أحب أن يحسن وجهي‬
,Na kwa hakika baadhi ya wanawake walikuwa wakikithirisha kuswali
usiku basi akaambiwa (mmoja wao) katika hilo, (kwa nini wafanya
hivyo) akajibu: Hakika hilo hupendezesha uso na mimi napenda uso
wangu upendeze.
٣٢١ ‫ابن القيم روضة المحبين‬
Ufafanuzi wa maneno ya ibn l-Qayyim-Allah amrahamu:
Huu ndio urembo na uzuri halisi kwa mwanamke yaani ni dini ,na kila
anapozidi kushikamana na dini urembo wake huzidi ,na haina maana
kuwa mwanamke asijipambe kwa mumewe hapana ! bali kujipamba
kwa mume bila ya kushikamana na dini hakuna maana .
Pili: Hawa wanawake walikuwa wakijua kuwa kisimamo cha usiku
kinazipamba nyuso zao ,kama alivyosema ibn Kathir - Allah
amrahamu- katika kauli yake Allah-aliyetukuka :
ُّ ‫ِسي َما ُه ْم ِفي ُو ُجو ِه ِه ْم ِم ْن أَث َ ِر ال‬
.‫س ُجو ِد‬
{ Alama zao (zipo) katika nyuso zao kutokana na athari ya kusujudu } .
Akasema ibn Kathir- Allah amrahamu-:
‫ من كثرت صالته بالليل حسن وجهه بالنهار‬:‫وقال بعض السلف‬
Wamesema baadhi ya wema waliopita: " Mwenye kukithiri swala zake
za usiku uso wake hunawiri wakati wa mchana
.‫تفسير القرآن العظيم َلبن كثير‬

.‫حياؤك وحشمتك جوهرة ثمينة فكوني في نظره دائما ً جوهرة جميلة مصونة‬- ١٢

23
12- Aibu yako na heshima yako ni kito /jiwe lenye thamani, basi
kuwa katika mtezamo wake (mumeo) ni kito kizuri
kinachohifadhiwa .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi-anataja adabu ya kumi na mbili (12) katika
adabu za mke kuishi na mumewe ,nayo ni adabu ya kuwa na aibu na
kujiheshimu ,na akaifananisha adabu hii ni kama kito /jiwe lenye
thamani lililotunzwa .
Na bila shaka mwanamke mwenye aibu na kujiheshimu hawezi
akatoka nyumbani kwake bila ya dharura au haja, hawezi akayafanya
yale yanayopingana na sheria ya dini.
Na aibu maana yake ni:
" Ni tabia inayopelekea mtu kufanya mema na kujiepusha na
maovu/maasi " na aibu ni tabia njema, tena ni katika tabia ambayo
waislamu wanatakiwa wasifike nayo kama alivyosema Mtume - swala
na salamu za Allah zimfikie-:
‫اإلس َْال ِم ْال َحيَا ُء‬
ِ ْ ‫ َو ُخلُ ُق‬،‫ِين ُخلُقًا‬
ٍ ‫إِ َّن ِل ُك ِل د‬
"Bila shaka kila dini inatabia na tabia ya uislamu ni haya/aibu "
٩٤٠ ‫صححه األلباني في "الصحيحة‬
Ufafanuzi:
Yaani aibu ni tabia ambayo waislamu wanatakiwa wawe nayo na ni
tabia ambayo wengi waliokuwa wema katika waislamu wanasifika
nayo,
Na Mtume alikuwa ni mfano wa juu katika aibu kama anavyoelezea
Said Al-Khudriy - Allah amridhie:
‫وكان إذا كره شيئًا‬. ‫كان رسول هللا صلى هللا عليه وسلم أشدَّ حيا ًء ِمن العذراء في خدرها‬
. ‫صحابة في وجهه‬ َّ ‫عرفه ال‬

24
" Alikuwa Mtume - swala na salamu za Allah - ana haya/aibu mno
kuliko bikra katika kijumba chake. Na alikuwa anapochukia kitu
Maswahaba hufahamu katika uso wake.
.‫رواه مسلم‬
Uchambuzi:
Aibu inayosemwa vizuri ni ile aibu inayomzuia mtu kufanya
maovu/maasi na si aibu inayomzuia mtu kusoma dini au kuuliza,
kuamrisha mema na kukataza mabaya hii si aibu! bali huu ni unyonge
na uwoga,
sifa ya aibu anatakiwa kila muislamu asifike nayo lakini kwa
mwanamke ni zaidi kwa sababu aibu ni kawaida ya wanawake wema
tokea kale kama Allah alivyomuelezea yule binti aliyekuja kumuita
Nabii Musa baada ya kuwasaidia kunywesha mifugo yao:

ۚ ‫ْت لَنَا‬ َ ‫وك ِليَجْ ِزيَ َك أَجْ َر َما‬


َ ‫سقَي‬ َ ‫ع‬ُ ‫ت ِإ َّن أَبِي يَ ْد‬
ْ َ‫علَى ا ْستِحْ يَاءٍ قَال‬
َ ‫فَ َجا َءتْهُ إِحْ دَا ُه َما ت َْم ِشي‬
{ Basi mmoja katika wale mabinti wawili akamjia, hali ya kuwa
anatembea kwa haya/aibu. Akasema: Hakika baba yangu anakuita ili
akulipe ujira wa kutunyweshea (mifugo) }
Surat Al-qas'as': 25
Mchanganuo:
Yule mwanamke alikuja kumuita Nabii Musa hali ya kuwa ameweka
mkono wa gauni lake katika uso wake kwa haya/aibu na hii pia ni dalili
kuwa huo mkono wa gauni lake ulikuwa mpana kama wasemavyo
wanachuoni, na hii ni dalili kuwa wanawake tokea kale walikuwa na
tabia ya haya/aibu, na hii aibu na heshima kwa mke ni kama kito /jiwe
lenye thamani ,na mke akisifika na tabia ya aibu na kujiheshimu huwa
ni kama jiwe zuri lenye thamani lililohifadhiwa.
Ama wanawake wengi wa sasa wanaokithirisha kutoka majumbani,
wanaochanganyika na wanaume sehemu mbalimbali, wanaoongea na

25
wanaume au wanaopaza sauti katika mazungumzo yao, yote haya ni
alama ya kukosa aibu.

‫إال بأساليب لطيفة وإشارات‬, ‫كوني معظمة ألمره ال معارضة لطلبه مجادلة ألفكاره‬- ١٣
.‫خفيفة؛ لقصد تحقيق األفضل للحياة الزوجية‬
13- Kuwa ni mwenye kuzitukuza amri zake (mumeo na usiwe ni)
mwenye kupinga yale anayoyataka,(na usiwe) mwenye kujadiliana
na fikra zake ila kwa njia (ya) ulaini na ishara khafifu, kwa makusudio
ya kuthibitisha maisha bora ya ndoa .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na tatu (13) katika
adabu za mke katika kuishi na mumewe ,nayo ni adamu ya kuwa mtiifu
kwa mumewe ,na kutopinga yale anayoyataka maadamu hayaendi
kinyume na sheria ya Allah,na wala asijadiliane na mumewe kwa
kubishana naye ila kama itabidi kufanya hivyo basi anatakiwa mke
mtumie njia mzuri na ishara ya mbali, na kufanya hivyo ndiyo sababu
ya kuimarisha ndoa .
Hebu tujifundishe katika tukio lililotokea katika suluhu ya Hudaibiyah
,baada ya waislamu kuzuiliwa kuingia Makkah kutekeleza ibada ya
Umrah , Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-aliwaamrisha
waislamu wanyoe na wachinje vichinjwa vyao lakini hakuna yeyote
aliyetekeleza hayo waliyoambiwa ,na Mtume- swala na salamu za
Allah zimfikie- alirudia mara tatu lakini hawakufanya,basi Mtume-
swala na salamu za Allah zimfikie- aliingia kwa mkewe Ummu Salamah
na akamtajia hilo lililotokea kwa waislamu basi Ummu Salammah -
Allah amridhie- akasema:
،‫ أتحب ذلك اخرج وَل تكلم أحدا حتى تنحر بدنك (ذبيحتك) وتدعو حالقك فيحلقك‬،‫يا نبي هللا‬

26
Ewe Nabii wa Allah, je unapenda (watekeleze) hilo, (basi wewe) toka
na wala usimsemeshe yeyote mpaka uchinje ngamia wako (kichinjwa
chako) na umuite kinyozi wako na akakunyoa,
،‫فخرج رسول هللا وفعل بمشورتها فما كان من المسلمين إَل أن نحروا وحلق بعضهم لبعض‬
. ‫وبذلك حلت المشكلة‬
basi akatoka Mtume wa Allah - swala na salamu za Allah zimfikie- na
akaufanyia kazi ushauri wake (Ummu Salamah) ,basi ghafla waislamu
wakachinja (vichinjwa vyao) na wakanyoana , na kwa (ushauri wake)
ukapatikana ufumbuzi tatizo (hilo).

Faida katika tukio hili: Hapa tunapata faida kuwa mke anaweza
akamshauri mumewe na mume si vibaya kuuchukua ushauri wake bali
anatakiwa auchukue ukiwa mzuri ,na vile vile tunajifundisha kuwa
mke pindi anapomshauri mumewe anatakiwa atumie njia mzuri ya
upole na ulaini na kubembeleza kama alivyofanya Ummu Salamah-
Allah amridhie- .
Unajua kwanini unapojadiliana na mumeo unatakiwa utumie njia ya
upole,ulaini, na kubembeleza ? .
Kwa sababu mwanamume hapendi kutawaliwa na mwanamke siku
zote anapenda awe juu yake kwa hiyo unapotumia ukali,hasira yeye
huhisi kuwa unamvunjia heshima na kumdharau na kujiweka juu yake,
na hapo hatuchukua ushauri wako , na kama amekosea na ukamkosoa
kwa njia hii basi hatojirekebisha .

.‫ فاستري الذميمة وامدحي الجميلة‬,‫ال تفتخري عليه بخلة وال تذميه على خصلة‬-١٤
14-Usijifaharishe juu ya (mumeo) kwa jambo zuri na wala
usimuaibishe juu ya jambo (baya) ,na zistiri aibu (zake)na yasifu
mazuri .

27
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh- Allah amuhifadhi- anataja adabu ya (14) katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutojifaharisha juu ya mumewe,
kwa jambo fulani ulilokuwa nalo ili kujiweka juu ya mumewe ,na
kujitutumua juu yake mfano: akajifaharisha juu ya mumewe kwa mali
alizokuwa nazo, au akajifaharisha kuwa yeye ni mzuri sana hakustahiki
kuolewa na huyo mumewe ! ,bila shaka kauli hii ni haramu, au
akajifaharisha kwa neema mbali mbali ambazo Allah amemneemesha
,na hukumu ya kujifaharisha ni haramu kama alivyosema Allah-
aliyetukuka-:
ٍ ٍۢ ‫ٱللَ ََل ي ُِحبُّ ُك َّل ُم ْخت َا ٍۢ ٍل فَ ُخ‬
‫ور‬ َّ ‫إِ َّن‬
Hakika Allah Hampendi kila ajivunae,na ajifaharishaye .
.١٨ ‫سورة لقمان‬
Na makusudio ya kujifaharisha kuliko haramishwa hapa ni mtu kutaja
neema fulani katika neema ambazo Allah amemneemesha kwa njia ya
kujikweza na kujinyanyua kwa watu , na likiwa jambo hili ni haramu
kumfanyia mtu yeyote bila shaka mke kumfanyia mume licha ya kuwa
ni haramu bali lina madhara makubwa katika maisha ya ndoa kwa
sababu litamfanya mume amuone mkewe kuwa ni mwenye kujiona na
kujivuna !na mwisho wake ni ndoa kuvunjika .
Na vile vile mke anatakiwa asimlaumu mumewe juu ya aibu fulani
aliyokuwa nayo bali azistiri aibu zake na ayasifu yale mazuri yake
aliyokuwa nayo ,kwa maana mke awe na tabia ya kustiri makosa ya
mume yale madogo madogo ambayo hakuna mtu ambaye
ametakasika nayo isipokuwa Mitume , na mke anatakiwa ajue kuwa
hatopata mume mwenye tabia kama za Abuu Bakr Swiddiq -Allah
amridhie- kwa sababu yeye mwenyewe ucha mungu wake si kama wa
Asmau bint 'Umais- Allah amridhie- ambaye ni miongoni mwa wake
wa Abuu Bakr , ikiwa hali ni hii basi ni vipi anataka mume mwenye sifa
za mfano wa Abuu Bakr ? .

28
Na vile vile mke atambue kuwa ni lazima mumewe atakuwa na kasoro
japo moja kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie
-:
َّ ‫َطا ٌء َو َخي ُْر ْالخ‬
. " َ‫َطائِينَ الت َّ َّوابُون‬ َّ ‫" ُك ُّل اب ِْن آدَ َم خ‬

" Kila binadamu ni mwenye kukosea na wabora wa wenye kukosea ni


wenye kutubu" .
.‫رواه الترمذي‬

Na mshairi anasema :
!‫س َجاياهُ ُكلُّها‬ َ ‫َو َمن ذا الذي تُر‬
َ ‫ضى‬
.‫َكفى ال َمر َء نُبالً أ َ ْن تُعَدَّ َمعايِبُ ْه‬
Na ni nani (huyo) ambaye tabia zake zote ni zenye kuridhiwa .
Inamtosha mtu kuwa na utukufu kwa kuhesabika makosa yake .
Maana ya beti hii ya shairi:
Hakuna aliyekingwa na makosa kila mwanadamu ana sehemu fulana
ya makosa na mapungufu na tabia zisizoridhiwa ,lakini inatosha kwa
mwanadamu kuwa mtukufu zikiwa aibu zake ni chache zinazohesabika

.‫ال تبعدي عنه فينساك وال تقربي منه فيملك وكوني قريبة لطيفة وبعيدة حبيبة‬- ١٥
15- Usijiweke naye mbali (sana) akakusahau na wala usijisogeze
karibu naye (sana) akakuchoka, (bali) kuwa karibu naye na (kuwa)
mwenye huruma , na kuwa mbali naye (na hali ni) mwenye mapenzi.
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh-Allah amuhifadhi-anataja adabu ya (15) katika adabu za mke
kuishi na mumewe ,nayo ni adabu yenye kuzidisha mapenzi baina ya
wanandoa nayo ni hii:

29
Mke anatakiwa asijiweke karibu sana na mumewe mpaka akamchoka
haina maana kuwa ajitenge na mumewe kabisa isipokuwa anatakiwa
awe naye karibu kidogo si kila muda kwa sababu hili hupelekea
mumewe kumchoka na hapa kunadhihiri faida ya mwanamume kuwa
na mke zaidi ya mmoja , na mwanamke ataona faida ya ukewenza kwa
upande wake na hilo ni kwa sababu :
Pindi mwanamume anapokuwa na mke mmoja itamlazimu huyo
mwanamke siku zote awe na mumewe na pia itamlazima kila siku awe
amejipamba na kujiandaa kwa ajili ya mumewe lakini kama mumewe
atakuwa na mke zaidi ya mmoja hilo litampa nafasi ya kupumzika
baadhi ya siku yaani kile kipindi ambacho mumewe yupo kwa mke
mwenzie ,na pia hiki kitendo cha kutokuwepo na mumewe kwa muda
kitamuongezea hamu ya kukutana na mumewe baada ya kumkosa
kwa muda!.
Na vile vile mke anatakiwa asijitenge na mumewe kiasi ambacho
kikapelekea mumewe kumsahau na kumfanya mume awe katika shida
na dhiki na matokeo yake ni ndoa kuvunjika .

,‫إياك والمبالغة في الغيرة فتخرجي من الممدوح إلى المذموم فيشتعل الصدر بالهموم‬- ١٦
.‫ويتأجج البيت بالخالفات والشكوك‬
16- Tahadhari na kuzidisha katika wivu ukatoka katika (wivu) mzuri
na ukaingia katika (wivu) mbaya ,na kifua (moyo) kikajaa msongo wa
mawazo ,na nyumba ikawaka moto kwa mizozo na shaka .

Maelezo ya mtarajumu:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya 16 katika adabu za mke
kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kuwa na wivu wa kati na kati, kwa
maana mwanamke anatakiwa awe na wivu juu ya mumewe lakini huo
wivu uwe ni wivu usiochupa mipaka .
Kwa sababu wivu kwa viumbe umegawanyika sehemu mbili :
30
1- Wivu mzuri .
2- Wivu mbaya
Kama alivyoeleza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pale
aliposema:
، ‫إن من الغيرة غيرة ً يحبها هللا وغيرة ً يبغضها هللا‬
Bila shaka katika wivu kuna wivu anaoupenda Allah na kuna wivu
anaouchukia Allah,
‫فأما الغيرة ُ التي يحبها هللا فهي الغيرة ُ في ريبة‬
Ama wivu ambao Allah anaoupenda ni ule wivu katika (sehemu) yenye
shaka
) .‫أما الغيرة ُ التي يبغضها هللا سبحانه وتعالي فهي الغيرة ُ في غير ريبة‬
Ama wivu ambao anaouchukia Allah -utakasifu ni wake na ametukuka-
ni wivu katika (sehemu) isiyokuwa na shaka .
‫والنسائي وأحمد وغيرهم‬،‫ رواه أبو داود‬.
Wivu unatakiwa kisheria na haswa mwanamume kwa mkewe na pia
mke kwa mumewe lakini asichupe mipaka akaingia katika makosa ya
kumdhania vibaya mumewe kama vile kupekua simu yake ,na wala
mke asimpekue/chunguza mumewe katika kila analolifanya kwa
sababu akifanya hivyo bila shaka nyumba itawaka moto yaani
kutakosekana raha ya ndoa ,na wivu mbaya unatokana na udhaifu wa
imani na wasiwasi wa Shetani na maradhi ya moyo ,na wivu mbaya
una madhara mengi kama vile :
Kuingia katika usengenyaji,kujiingiza katika dharau,na kutomfanyia
wema mume, kumdhuru, kuwafanyia uadui ndugu wa mume
kutowapa haki zao,husuda,mafundo ya moyo, uchawi, kumpekua,
kupata maumivu ya nafsi na mwili, kufanya hila,na vitimbi, na pengine
humpelekea mtu kuua na hata huwenda ukampelekea katika makosa
mengine mengi .

31
Ama wivu wenye sababu huo ni wivu mzuri mfano mke akamuona
mumewe anaongea na mwanamke wa kando bila ya haja wala
dharura, tena ni mazungumzo ambayo yanaishara mbaya, bila shaka
hapa mwanamke ana haki ya kuwa na wivu kwa sababu ya hatari
inayohofiwa kutokana na mazungumzo haya.

.‫ال تخرجي إال بإذنه وال تصومي وتتصدقي تطوعا ً إال بعلمه‬- ١٧
17- Usitoke (nyumbani) isipokuwa kwa idhini yake na wala usifunge
(sunnah) na wala usitoe sadaka isipokuwa kwa kujua (mumeo) .
Maelezo ya mtarjumu:
Sheikh – Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na saba (17) b katika
adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutotoka ndani ya
nyumba ila kwa idhini ya mumewe na wala asifunge funga ya sunnah
na wala asitoe chochote katika mali yake isipokuwa mumewe
akimrumsu, na hili la mwanamke kutotoka nyumbani ila kwa idhini ya
mumewe au mlezi wake kama hajaolewa ni makubaliano ya
wanachuoni wote wa fiqih, kama yalivyokuja maneno kutoka katika
“Al-mausu’a l-fiqihiyyah” (19/107):
‫ منهيات عن الخروج … فال يجوز لها الخروج‬، ‫”األصل أن النساء مأمورات بلزوم البيت‬
.‫إَل بإذنه – يعني الزوج‬
Asili kuwa wanawake ni wenye kuamrishwa kulazimiana na majumba
,ni wenye kukatazwa kutoka.. basi haifai kwa huyo (mke) kutoka ila
kwa idhini yake- yaani mumewe .
‫ خرجت بإذن‬: ‫ لزيارة والد‬، ‫ وإذا اضطرت امرأة للخروج‬: ‫قال ابن حجر الهيتمي الشافعي‬
.‫ غير متبرجة‬، ‫زوجها‬
Amesema ibn Hajar Al-haitamiy Asshaafiy : Mwanamke akipata
dharula ya kutoka kwa ajili ya kumtembelea mzazi : Atatoka kwa idhini
ya mumewe na (atoke) bila ya kuonesha mapambo
:‫ونقل ابن حجر العسقالني عن النووي عند التعليق على حديث‬

32
Na ibn Hajar Al-‘asqalaniy amenukuu kutoka kwa Annawawiy pindi
(alipokuwa anaiwekea) maelezo hadith:
‫إذا استأذنكم نساؤكم بالليل إلى المسجد فأذنوا لهن‬
“Pindi wanawake zenu watakapokutakeni idhini ya kwenda msikitini
usiku basi wapeni idhini .
‫ لتوجه األمر إلى‬، ‫ استدل به على أن المرأة َل تخرج من بيت زوجها إَل بإذنه‬: ‫أنه قال‬
“‫األزواج باإلذن‬
kwamba yeye (Annawawiy) amesema : Imetumika dalili hiyo (hadithi)
kuwa mwanamke asitoke nyumbani kwa mumewe ila kwa idhini yake
,kwa sababu amri ya kutoa ruhusa imeelekezwa kwao (wanamume) “.
.‫انتهى النقل عن الموسوعة باختصار‬
Na pia mwanamke haruhusiwi kufunga funga ya sunnah kama
mumewe yupo ila kwa idhini ya mumewe ama zikiwa zile fungal
ambazo hujirudia rudia kila mwaka kama Arafah au Ashuraa inatosha
kule kutomzuia kufunga tu na wala si sharti ampe idhini,na dalili ya
kutoruhusiwa kufunga fungal ya suna ila kwa idhini ya mumewe ni
kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:
‫َل يحل َلمرأة أن تصوم وزوجها شاهد إَل بإذنه‬
” Si halali kwa mwanamke kufunga (sunnah) na hali mumewe yupo ila
kwa idhini yake ” .
.‫متفق عليه‬
Na vile vile mke haruhusiwi kutoa sadaka katika mali ya mumewe ila
kwa idhini yake ila kikiwa ni kitu kidogo ambacho inafahamika kwa ada
hiyo sehemu kuwa mume anaruhusu kitolewe, na dalili ya katazo la
hili ni kauli yake Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- katika
mazungumzo yake katika hija ya kuaga:
‫ ذلك‬:‫عام؟ قال‬ َّ ‫ وَل‬،ِ‫يا َرسو َل هللا‬: ‫ قيل‬.‫وجها‬
َ ‫الط‬ ِ َ‫بإذن ز‬
ِ ‫وجها َّإَل‬ ِ ‫َل تُن ِف ُق امرأة ٌ ِمن بَي‬
ِ َ‫ت ز‬
.‫ض ُل أموا ِلنا‬َ ‫أف‬

33
” Na wala mwanamke asitoe (chochote) katika nyumba ya mumewe
ila kwa idhini ya mumewe .
Kukasemwa: Ewe mjumbe wa Allah, wala chakula ? akajibu: Hicho
(chakula) ni bora zaidi ya mali zetu “

.‫كوني له عونا ً في الحياة ومشاقها وال تكوني عبء للحياة عليه‬- ١٨


18- Kuwa ni msaidizi kwa (mumeo) katika maisha na mashaka yake
na wala usiwe ni mzigo juu yake katika maisha .

Maelezo ya mfasiri:
Sheikh anataja adabu ya (18) katika adabu za mke kuishi na mumewe
na hii ni adabu ya mwisho katika hizi adabu alizoziandaa, na adabu
hiyo ni:
Mwanamke anatakiwa awe ni mwenye kumsaidia mumewe katika
maisha na misukosuko yake na shida mbalimbali, na wala mke asiwe
ni mzigo kwa mumewe kwa maana asimuongezee shida mumewe
kutokana na maneno yake, au tabia yake au kutompa utulivu
mumewe.
Mwanamke wa kiislamu anatakiwa awaige wanawake wema kama vile
bibi Khadija - Allah amridhie - ambaye alikuwa ni msaidizi mkubwa wa
Mtume - swala na salamu za Allah zimfikie - na haswa pale Mtume -
swala na salamu za Allah zimfikie - aliposhushiwa wahy na kujiwa na
Malaika alirudi kwa bibi Khadija - Allah amridhie - hali ya kuwa ana
hofu kwa hali iliyomtokea, basi bibi Khadija alimliwaza akamwambia
maneno yafuatayo:
‫ْف‬
َ ‫ضي‬ َ ‫ب ْال َم ْعد‬
َّ ‫ُوم َوت َ ْق ِري ال‬ ُ ‫الر ِح َم َوتَحْ ِم ُل ْال َك َّل َوت َ ْك ِس‬ ِ ‫اللُ أَبَدًا إِنَّ َك لَت‬
َّ ‫َص ُل‬ َّ ‫يك‬ ِ َّ ‫َك َّال َو‬
َ ‫الل َما ي ُْخ ِز‬
ِ ‫ب ْال َح‬
.‫ق‬ ِ ِ‫علَى ن ََوائ‬َ ‫ين‬ ُ ‫َوت ُ ِع‬
Hapana (usiogope) naapa kwa Allah, Allah hatokudhalilisha milele,
hakika wewe unaunga udugu na unabeba majukumu ya wasiojiweza,

34
na unawapa wale wasiokuwa nacho, na unakirimu wageni, na
unasaidia mambo ya haki”
.‫رواه البخاري‬
Kwa ajili hii ndiyo maana sheikh Fauzan - Allah amuhifadhi - alipokuwa
akielezea ujuzi na ufahamu wa bibi Khadija - Allah amridhie - baada ya
kumliwaza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alisema:

-‫صلى هللا عليه وسلم‬- ‫ فهي أول من طمأن الرسول‬-‫ رضي هللا تعالى عنها‬- ‫وهذا من فقهها‬
Na huu ni katika ufahamu wake (bibi Khadija) -Allah aliyetukuka
amridhie - na yeye ndiye wa kwanza kumtuliza Mtume - swala na
salamu za Allah zimfikie -
،‫وناصره وآنسه من هذه الوحشة‬
.‫وهذا موقف عظيم منها‬
na alimnusuru na kumliwaza kutokana na huu upweke na huu ni
msimamo mkubwa kutoka kwa (bibi Hadija).
.‫ شرح ستة مواضع من السيرة‬:‫المصدر‬
Hivi ndivyo anavyotakiwa awe mke kwa mumewe anatakiwa ajue hali
za mumewe mfano ajue kuwa : Mumewe amechoka, au amekwazwa
na nini au anahitaji nini ? ,ili amsaidie katika hilo ima kwa kumfariji,au
kumliwaza kwa maneno matamu mpaka akasahau shida zake ,au
kumpa ushauri n.k

Faida Zaidi tembelea : www.fawaidusalafiyatz.net


Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 1, 1443H ≈ September 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi.

35

You might also like