You are on page 1of 3

DUA WAKATI WA KULALA:

(Bismika Allahumma amuutu wa ahyaa)

MAANA YAKE:

(Kwa jina lako Ewe Allah, ninakufa{kwa kulala usingizi}na ninapata uhai {kwa kuamka})

KIARABU;

‫حيَا‬ ‫َأ‬ ‫ك اللَّه َأ‬


َ ‫م‬
ْ َ‫وت و‬
ُ ‫م‬ُ ‫م‬َّ ُ ِ ‫س‬
ْ ‫بِا‬

NYIRADI

Alikuwa Mtume (s.a.w) akitaka kulala usiku akivikusanya viganja vyake vya mikono kisha akivipulizia
na akivisomea Suratul-Ikhlas, na Suratul-Falaq, na Suratu Nnas, kisha akijipangusa kwa hivyo viganja
vyake katika mwili wake kiasi anachoweza, akianza kichwani na usoni na mbele. (Akifanya hivo mara
tatu)...

Mtume (s.a.w) amesema: (Ukitaka kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka umalize kwani Mwenyezi Mungu
ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi.

AYAT KURSIY;

[ Allahu la ilaha illa Huwa, Al-Haiyul-Qaiyum La ta'khudhuhu sinatun wa la nawm,lahu ma fis-


samawati wa ma fil-'ard Man dhal-ladhi yashfa'u 'indahu illa bi-idhnihi Ya'lamu ma baina aidihim wa
ma khalfahum, wa la yuhituna bi shai'im-min 'ilmihi illa bima sha'a Wasi'a kursiyuhus-samawati wal
ard, wa la ya'uduhu hifdhuhuma Wa Huwal 'Aliyul-Adheem.]

MAANA YAKE:

{Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na
usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye
kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao
hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda
mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu}.
(Suratul-Baqrah: 255).

KIARABU;

‫ض ۗ َمن َذا ٱلَّ ِذى يَ ْشفَ ُع ِعن َد ٓۥهُ ِإاَّل بِِإ ْذنِ ِهۦ ۚ يَ ْعلَ ُم َما‬
ِ ْ‫ت َو َما فِى ٱَأْلر‬ ِ ‫ٱهَّلل ُ ٓاَل ِإ ٰلَهَ ِإاَّل هُ َو ْٱل َح ُّى ْٱلقَيُّو ُم ۚ اَل تَْأ ُخ ُذهۥُ ِسنَةٌ َواَل نَوْ ٌم ۚ لَّهۥُ َما فِى ٱل َّس ٰ َم ٰ َو‬
‫ض ۖ َواَل يَـُٔو ُدهۥُ ِح ْفظُهُ َما ۚ َوهُ َو ْٱل َعلِ ُّى‬ َ ْ‫ت َوٱَأْلر‬ِ ‫بَ ْينَ َأ ْي ِدي ِه ْم َو َما خ َْلفَهُ ْم ۖ َواَل يُ ِحيطُونَ بِ َش ْى ٍء ِّم ْن ِع ْل ِم ِٓۦه ِإاَّل بِ َما َشٓا َء ۚ َو ِس َع ُكرْ ِسيُّهُ ٱل َّس ٰ َم ٰ َو‬
‫ْٱل َع ِظي ُم‬

Mtume (s.a.w) pia amesema: (Akiamka mmoja wenu kutoka usingizini kisha akarudi basi akikung'ute
kitanda chake kwa shuka lake mara tatu, na amtaje Mwenyezi Mungu, kwani hajui kilichokuja baada
yake. Na akilala aseme:

"Bismika Rabbi wa rada'atu jambi,wa bika arf'auh, fa in amsakta nafsi farhamha,wa in'arsaltaha fahfaz
bima tahfazu bihi ibadikas salihin"

MAANA YAKE:

''Kwa jina lako Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili yako nitaunyanyua, na ukiizuia
(ukiichukuwa) roho yangu, basi irehemu, na ukiirudisha basi ihifadhi, kwa kile unacho wahifadhi nacho
waja wako wema.''

KIARABU;

‫ َِإ ْن َأ ْم َس ْكتَ نَ ْف ِسي‬،ُ‫ َوبِكَ َأرْ فَ ُعه‬،‫ْت َج ْنبِي‬


ُ ‫ضع‬
َ ‫بِا ْس ِمكَ َربِّي َو‬
ْ َ‫ َوِإ ْن َأرْ َس ْلتَهَا فَاحْ ف‬،‫فَارْ َح ْمهَا‬
َ‫ بِ َما تَحْ فَظُ بِ ِه ِعبَادَكَ الصَّالِ ِحين‬،‫ظهَا‬

DUA YA KUAMKA USINGIZINI

"ALHAMDU LILLAHI LLADHI AHYAANA BAADA MA A-MAATANA WA ILAIHI NNUSSHUR''

MAANA YAKE:

Sifa njema zote zamstahiki Allah, ambae ametupa uhai baada ya kutufisha na ni kwake kufufuliwa.

KIARABU;

‫ْال َح ْم ُد هللِ الَّ ِذي َأحْ يَانَا بَ ْع َد َما َأ َماتَنَا َوِإلَ ْي ِه النُّ ُشو ُر‬

Ongeza kwa kusoma Dua Hii

Allahumma Inny As-aluka Ziyadatan fi Diin, Wa Barkatan fil Umr Wa Swihatan fil Jasad, Wa wasi'atan fi
Rizq, Wa Taubatan Kabla al Maut,Wa Shahadan In-dal Maut, Wa Afwan In-dal Hisaab, Wa Amaana
Minal Adhab, Wa Naswiiban Minal Jannah, Birahmatika Ya Arhama Rahimin.

MAANA YAKE:

Ewe mola wangu nakuomba ziada katika dini, na baraka katika umri, na afya katika mwili, na nafasi
katika rizki, na unikubalie toba na kutamka shahada kabla ya mauti, na unikinge na adhabu, na unipe
fungu katika pepo.

You might also like