You are on page 1of 3

DUA YA UPEPO MKALI

Allaahumma inniy as-aluka khayrahaa wa a’uwdhu Bika min sharrihaa

MAANA YAKE;

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri ya upepo huu, na najikinga Kwako na shari yake..

KIARABU;

ِّ َ‫ن ش‬
‫ـرها‬ ْ ‫م‬ َ ِ ‫ وََأعـوذ ُ ب‬،‫ـرها‬
ِ ‫ك‬ َ ْ ‫خي‬ َ ‫سـَألُـ‬
َ ‫ك‬ ‫َأ‬
َّ ‫اللّهُـ‬.
ْ ‫م ِإنَّـي‬

Dua Nyingine..

Allaahumma inniy as-aluka khayrahaa wakhayra maa fiyhaa, wakhayra maa ursilat bihi. Wa a’uwdhu Bika
min sharrihaa, washarri maa fiyhaa washarri maa ursilat bih

MAANA YAKE;

Ee Allaah nakuomba kheri yake na kheri ya kilicho ndani yake, na kheri ya iliyotumwa ndani yake. Na
najikinga Kwako kutokana na shari yake na shari iliyoko ndani yake na shari iliyotumwa nao[2]

KIARABU;

َ ِ‫ َوَأعـو ُذ ب‬،‫ـت بِه‬


ْ َ‫ َو َشـرِّ ما اُرْ ِسل‬،‫ َو َشـ ِّر ما فيهـا‬،‫ك ِم ْن َشـرِّ ها‬
‫ـت بِه‬ َ ‫اللّهُـ َّم ِإنَّـي َأسْـَألُـ‬.
ْ َ‫ َو َخيْـ َر ما اُرْ ِسل‬،‫ َوخَ يْـ َر ما فيهـا‬،‫ك خَ يْـ َرها‬

DUA YA RADI

SubhaanaLLadhiy yusabbihur-ra’-du Bihamdihi wal Malaaikatu min khiyfaatih

MAANA YAKE;

Ametakasika Yule Ambaye radi zinamsabihi kwa Himdi Zake na Malaika kwa kumkhofu[1]

KIARABU;

‫ َوالمالِئكـةُ ِم ْن خيـفَته‬،‫ ُس ْبـحانَ الّذي يُ َسبِّـ ُح الـ َّر ْع ُد بِ َح ْمـ ِد ِه‬.

DUA YA KUOMBA MVUA

Allaahumma Asqinaa ghaythan mughiythaa, mariy-aa, muriy’aa, naafi’an ghayra dhwaarun, ’aajilan
ghayra aajil

MAANA YAKE;
Ee Allaah Tunyesheleze mvua yenye kuokoa, nyingi yenye kustawisha, yenye manufaa isiyo dhuru, ya
haraka isiyochelewa..

KIARABU;

ِ ‫ عا ِجـالً غَـ ْي َر‬،ٌ‫ نافِعـا ً َغيْـ َر ضَّار‬،ً‫ ُمريـعا‬،ً‫ َمريئا‬،ً‫اللّهُ َّم اَ ْسقِـنا َغيْـثا ً ُمغيـثا‬
‫آج ٍل‬

Dua Nyingine

Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa

MAANA YAKE;

Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa kututeremshia mvua, Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa
kututeremshia mvua, Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa kututeremshia mvua[2]

KIARABU;

‫أغ ْثنـَا‬
ِ ‫ اللّهُ َّم‬،‫أغ ْثنـَا‬
ِ ‫ اللّهُ َّم‬،‫اللّهُ َّم أ ِغ ْثنـَا‬

DUA YA MVUA INAPONYESHA

Allaahumma swayyiban naafi’aa

MAANA YAKE;

Ee Allaah, Ijaaliye yenye kumiminika yenye kunufaisha..

KIARABU;

َ ‫اللّهُ َّم‬
ً ‫صيِّـبا ً نافِـعا‬

DUA BAADA YA MVUA

Mutwirnaa bifadhwliLLaahi wa Rahmatih

MAANA YAKE;

Tumenyeshelewa kwa fadhila za Allaah na Rehma Zake

KIARABU;

ِ ْ‫ُم ِطـرْ نا بِفَض‬


‫ـل هللاِ َو َرحْ َمـتِ ِه‬
DUA YA KUTAKA MVUA IKATIKE (wakati itakapoleta madhara)

Allaahumma hawaalaynaa walaa ’alaynaa. Allaahumma ’alal aakaami wadh-dhwiraab, wa butwuunil


awdiyah, wamanaabitish-shajar

MAANA YAKE;

Ee Allaah, Inyesheleze kwetu wala isiwe yenye kutuangamiza. Ee Allaah Inyesheleze kwenye vichaka na
milima na mabonde na kwenye mizizi ya miti.

KIARABU;

ِ ِ‫ َو َمنـاب‬،‫ َوبُطُـو ِن األوْ ِدي ِة‬،‫ب‬


ِ ‫ت ال َّش َج‬
‫ـر‬ ِ ‫ اللّهُ َّم عَلى اآل َك‬،‫اللّهُ َّم َحوالَيْنا َوال َعلَيْـنَا‬
ِ ‫ـام َوالظِّـرا‬

You might also like