You are on page 1of 4

Kuvaa Niqaab Ni Fardhi? Nini Hukmu Ya Mwanamke Kuvaa Suruwali?

SWALI:
Assalm aleikum warahmatullahi wabarakatu.
Insha Allaah Allaah atuongoze sote waisilamu tuwe wenye kuongoka.Swali langu ni kuhusu
hijab ya mwanamke.Nimefanya utafiti sana kuhusu jambo hili na wengine wanasema kuwa uso
wa mwanamke sio awra wengine wanasema ni awra.Na pande zote mbili wanatoa evidence ya
kusupport msimamo wao.Jambo hili limenitatiza sana naomba ufafanuzi zaidi.Pili je mwanamke
kuvaa suruali ambayo haimbani, haionyeshi umbo lake wala sio ya kitambaa chepesi na juu ya
suruali hiyo akavaa ngou au blauzi ya kufikia magotini inafaa?
JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah
na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa
sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji kwa swali lako zuri kuhusu kivazi cha mwanamke wa
Kiislamu.
Awali ya yote tungependa kuweka wazi masharti yanayohitajika kwa kivazi cha mwanamke wa
Kiislamu. Nadhani kubainisha kwetu huko kutaondoa utata mwingi na kutuweka sawa katika
baadhi ya nadharia. Masharti yenyewe ni kama yafuatayo kama yalivyodondolewa na
wanazuoni wetu kutegemea Qur-aan na Sunnah ya Bwana Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam). Nayo ni kama yafuatayo:
i)
Kivazi ni lazima kisitiri mwili mzima. Wanazuoni wanatofautiana kuhusu uso na
vitanga vya mikono. Kuhusu nukta hii Allaah Aliyetukuka Anasema: Na waambie Waumini
wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao
isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala
wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au
watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa
dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi
wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke.
Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote
kwa Allaah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa (24: 31).
Na Amesema: Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini
wajiteremshie nguo zao. H;ivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na
Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu (33: 59).
Wanazuoni wameafikiana kuwa ni wajibu kwa mwanamke kusitiri mwili wake mzima, tofauti
imepatikana katika kufunika au kutofunika uso na vitanga vya mikono.
ii)
Vazi lisiwe lenyewe ni pambo: Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Allaah (Subhaanahu
wa Taala) pale Aliposema: Wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika (24:
31).

Hii kwa ujumla inachanganya nguo kwa dhahiri zikiwa na mapambo yenye kuvutia wanaume.
Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Watu watatu hata usiwaulize
(kwani wameangamia): Mtu aliyetengana na Jamaah na akamuasi kiongozi wake na akafa
akiwa katika uasi; kijakazi au mtumwa aliyetoroka akaaga dunia; na mwanamke ambaye
mumewe hayupo (mjini) lakini kamuachia mahitaji yake yote ya dunia, naye akawa anaonyesha
mapambo baada yake. Hao usiwaulize kabisa (Ahmad na al-Haakim).
Kusudio la amri ya kuvaa jilbaab (nguo pana yenye yenye kufunika kiwiliwili vizuri) ni stara kwa
mwanamke, hivyo haiwezi kuingia akilini kuwa stara hiyo iwe tena ni mapambo na vivutio!

iii)
Nguo iwe nene isiyoonyesha kilichopo chini yake: Mtume (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Watu aina mbili ni wa motoni bado sijawaona:
Watu wenye viboko kama mikia ya ngombe wanapigia nayo watu, na wanawake
waliovaa lakini wapo uchi (wanaonyesha sehemu za miili yao ili kuonyesha uzuri wao au
wanavaa nguo nyepesi inayoonyesha vilivyomo ndani yake) wanatembea kwa
kuonyesha mapambo yao Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake
japokuwa harufu yake inasikika masafa kadhaa na kadhaa (Muslim).
iv)
Nguo iwe pana siyo inayobana hivyo kuonyesha maungo yake: Usaamah bin Zayd
(Radhiya Allaahu Anhuma) amesema: Alinivisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa
aalihi wa sallam) Qubtwiyah (nguo kutoka Misri) aliyopewa hadiya na Dihyah al-Kalbiy (Radhiya
Allaahu Anhu), nami nikamvisha mke wangu. Akaniambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam): Una nini, mbona huvai Qubtwiyah? Nikamwambia: Ewe Mtume
wa Allaah! Nimepatia mke wangu. Akaniambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa
aalihi wa sallam): Muamrishe ajaalie chini yake Ghulaalah (nguo ya ndani), kwani nahofia isije
ikaonyesha kiasi cha mifupa yake (Ahmad na Abu Daawuud). Kwa dada zetu Waislamu!
Haitoshi kusitiri nywele zenu na vifua vyenu kisha baada ya hapo mkawa mnavaa mavazi
yanayobana na mafupi yenye kuonyesha miguu yenu.
v)
Nguo zisitiwe manukato: Imepokewa na Abu Muusa al-Ashariy (Radhiya Allaahu
anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
Mwanamke yeyote anayepaka manukato, kisha akawapita watu ili wapate harufu yake (ya
manukato), ni mzinifu (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaaiy kwa Isnadi iliyo Hasan
[nzuri]). Al-Haythamiy katika az-Zawaajir ametaja kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa
kwa mwanamke kutoka nyumbani kwake akiwa amepaka manukato na amejipamba hata kama
mumewe amempatia ruhusa.
vi)
Isishabihiane (isifanane) na kivazi cha mwanamume: Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu
anhuma) amesema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani
wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifananisha na wanaume (alBukhaariy, Abu Dawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah).
Maana ya Hadiyth hii ni kuwa haifai kwa wanaume kujishabihisha na wanawake katika kivazi na
mapambo ambayo ni hasa kwa wanaume na kinyume chake. Amesema Abu Hurayrah
(Radhiya Allaahu anhu): Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)

amemlaani mwanamume anayevaa nguo za kike na mwanamke anayevaa nguo za kiume


(Ahmad na Abu Daawuud kwa Isnadi iliyo sahihi).
vii)
Isishabihiane na kivazi cha makafiri: Imekariri Shariah kuwa haifai kwa Muislamu
wanaume kwa wanawake kushabihiana na makafiri sawa katika Ibaadah zao, Iyd na sherehe
zao au katika mavazi yao hasa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
alimuona Abdillaah bin Amr (Radhiya Allaahu Anhuma) akiwa amevaa nguo fulani,
akamwambia: Hakika hii ni nguo ya makafiri, hivyo usivae (Ahmad, Muslim na an-Nasaaiy).
viii)
Isiwe ni kivazi cha fakhari (umaarufu na mitindo yenye kwenda na wakati): Hii ni kwa
mujibu wa Hadiyth ya Ibn Umar (Radhiya Allaahu Anhuma) aliyesema kuwa Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Yeyote mwenye kuvaa nguo ya kutaka
umaarufu hapa duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalilifu Siku ya Qiyaama, kisha Ataiwashia
moto (Abu Daawuud na Ibn Maajah). Nguo ya kutaka umaarufu na kujionyesha ni kila kivazi
kinachokusudia kutaka kujulikana na watu.
Tukirudia nukta ya kwanza kama tulivyotangulia kusema ni kuwa kuna tofauti baina ya wenye
kuunga rai hizi mbili kufunika uso na vitanga vya mikono au kutofunika, kila kimoja kina dalili
zake kutoka kwa Qur-aan na Sunnah. Rai hizo mbili zina vigogo nyuma yake kama kwa
muhtasari ufuatao:
Uso na vitanga vya mikono ni lazima vifunikwe: Hii ni rai ya Ibn Masuud (Radhiya Allaahu
Anhu), Imaam Ahmad na miongoni mwa wanazuoni wa zama zetu ni Ibn Baaz, Ibn Uthaymin,
Mawdudi na wengineo.Inafaa kutofunika uso na vitanga vya mikono: Hii ni rai ya Ibn Abbaas,
Ibn Umar (Radhiya Allaahu Anhum), Imaam Maalik na ah-Shaafiiy na miongoni mwa
wanazuoni wa zama zetu ni Imaam al-Albaaniy, Dkt. Al-Qaradhwaawiy, Dkt. Jamaal Badawiy
na wengineo.
Kwa maoni yetu tunaweza kuhitimisha mada hii kwa maneno mazuri yaliyoandikwa na
wanazuoni wetu mashuhuri katika karne ya 14 na 15 Hijri. Mmoja wao ni Allaamah Muhammad
Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy katika kitabu chake Jilbaab al-Mar-at al-Muslimah amesema:
Mwanamke amepewa ruhusa kutofunika uso na vitanga vya mikono lakini akitaka mwenyewe
kufunika (sehemu hizo mbili) hakatazwi na Shariah. La muhimu sana ni kuwa wafuasi wa
makundi haya mawili yenye miono tofauti yasiwe ni yenye kuzozana wala kukufurishana wala
kuwaona wengine wako katika makosa.
Na tunashauri kwa mwenye uwezo wa kuvaa Niqaab ikiwa haitamsobabishia matatizo na
kunyanyaswa katika jamii anayoishi, basi ni bora zaidi kufanya hivyo kwani ndivyo walivyofanya
wake za Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam).
Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho upate manufaa zaidi ya mas-ala haya:
Hijaab Ya Sheria Inahusu Kufunika Uso Na Miguu?
Ama kuhusu kuvaa suruali kwa mwanamke ni jambo ambalo litafahamika vyema ikiwa
tumefahamu masharti ya kivazi cha Kiislamu tuliyoyaeleza hapo juu. Hakika ni kuwa ni suruali
chache sana zinazovaliwa na wanawake ambazo hazibani wala kuwa na mapambo. Ni jambo

linalojulikana kuwa washoni (fashion designers) wa nguo za kike ni wananume ambao haja na
kusudio lao ni kutaka kuonyesha sehemu moja au nyengine nyeti ya mwanamke. Hivyo, uzuri
wa suruali za wanawake ni zile zenye kubana na kuvutia zenye kuonyesha umbile lake. Hakuna
katazo la kuvaa suruali ikiwa mshono wake ni tofauti na ule wa wanaume, na lau itakuwa kweli
halibani, halionyeshi umbile lake wala kilichomo chini yake sharti tu juu yake uvae jilbaab kwani
blauzi pekee haitoshi juu ya suruali au kuvaa koti refu. Kuvaa hijabu (Jilbaab) juu ya suruali hiyo
ya kike ambayo ni pana na isiyoonyesha ndani, kutamsaidia kutoonekana uchi wake hasa
anapopanda gari, kukimbia, kufanya mazoezi, na harakati zinginezo ambazo zinaweza
kusababisha vazi la juu kunyanyuka au kupanda wakati wa harakati hizo.
Na Allaah Anajua zaidi

You might also like