You are on page 1of 7

1

www.wanachuoni.com

Kushikamana Na
Uislamu Kweli Kweli

[Khutbah Ya Ijumaa]

'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Imetolewa na:

www.wanachuoni.com
2

www.wanachuoni.com

Himidi Zote ni Zake Mola wa walimwengu ambaye Katukamilishia Dini na


Akatutimizia neema na Akatujaalia kuwa Waislamu. Ninashahidilia ya
kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah Mmoja
Asiyekuwa na mshirika na wala hatuabudu kinyume Naye. Na nnashahidilia
ya kwamba Mtume Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake alietumwa kwa
walimwengu wote (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa Aswhaabihi wa at-Taabi´iyn) na watakaowafuata kwa
wema mpaka siku ya Mwisho. Amma ba´ad:

Enyi watu! Mmcheni Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Na shukuruni neema


Zake kwa kuwajaalia kuwa Waislamu. Na jua maana ya Uislamu mpaka
uweze kushikamana nao kwa Baswiyrah (elimu). Na usiwe katika wale
wanaodai Uislamu na huku wako dhidi yake.

Uislamu - kama wanavyosema wanachuoni - ni kujisalimisha kwa Allaah kwa


kumpwekesha (Tawhiyd), kujisalimisha Kwake kwa kumtii na kujiweka mbali
na ushirikina na washirikina (makafiri). Haya ndio mambo matatu hauthibiti
Uislamu isipokuwa kwayo.

Jambo la kwanza ni kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha,


kumuabudu Allaah Pekee Asiyekuwa na mshirika na kuacha 'Ibaadah
(kuabudu) kinyume Chake. Kwa kuwa wengi wanaojinasibisha na Uislamu
wana Shirki nyingi kwa kuwaabudu mawalii wa Allaah na watu wema ambao
wanajikurubisha kwao huku wanadai kwamba watawaombea mbele ya
Allaah na watawakurubisha kwa Allaah.

Shaytwaan amewafelisha wengi wanaodai Uislamu kwa majina yao na


wanaabudu kinyume na Allaah kwa matendo yao na Itikadi zao.

Jambo la pili ni kujisalimisha kwa kumtii. Anayejisalimisha kwa Allaah, na


kumtakasia 'Ibaadah Allaah na akamfuata Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), basi ni
wajibu kwake kutekeleza amri za Allaah na za Mtume Wake.

Anafanya vile alivyomuamrisha Allaah na Mtume Wake na kuacha vile


walivyomkataza. Ikiwa ataacha baadhi ya mambo ya wajibu au akafanya
3

www.wanachuoni.com

baadhi ya mambo ya haramu, basi haya ni katika yanayopunguza Uislamu


[wa mtu] au yanaungamiza kabisa.

Jambo la tatu - nalo ni muhimu sana ambalo wengi wameghafilika nalo [na
kuna watu] wanalikemea - ni mtu kujiweka mbali na washirikina na Dini yao,
na [mtu] aitakidi kuwa (dini zao) ni batili, mtu asiwapende, asiwanusuru,
kuwatetea, hili ni wajibu kwa Waislamu na ndio mila [Dini] ya Nabii Ibraahim
('alayhis Salaam). Ambaye tumeamrishwa kumfuata.

‫اَّلل َكفَ ْرنَا‬ ِ ‫ِيم َوالَّذِينَ َمعَهُ إِ ْذ قَالُوا ِلقَ ْو ِم ِه ْم إِنَّا ب َُر َءؤُا ِمن ُك ْم َو ِم َّما ت َ ْعبُدُونَ ِمن د‬
ِ َّ ‫ُون‬ َ ‫سنَةٌ فِي إِب َْراه‬ َ ‫َت لَ ُك ْم أُس َْوة ٌ َح‬
ْ ‫قَ ْد َكان‬
َ
ِ َّ ِ‫ضاء أبَدًا َحتَّى ت ُؤْ ِمنُوا ب‬
ُ‫اَّلل َوحْ دَه‬ ْ ْ
َ ‫بِ ُك ْم َوبَدَا بَ ْينَنَا َوبَ ْينَ ُك ُم العَدَ َاوة ُ َوالبَ ْغ‬
“Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibraahim na wale walio
kuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga
nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Allaah. Tunakukataeni; na
umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka
mtakapo muamini Allaah peke yake”.” (60:4)

Na Ibraahim ('alayhis Salaam) alijiweka mbali na baba yake pindi alipojua kuwa ni
adui wa Allaah.

‫ألواهٌ َح ِلي ٌم‬ َ ‫َّلل تَبَ َّرأ َ ِم ْنهُ إِ َّن إِب َْراه‬
َّ ‫ِيم‬ ِ ‫فَلَ َّما تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ َعد ٌُّو ِ ه‬

“Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Allaah, alijiepusha naye.


Hakika Ibraahim alikuwa mwingi wakuomba, mnyenyekevu, mvumilivu.”
(09:114)

‫سولَهُ َولَ ْو َكانُوا آبَاء ُه ْم أ َ ْو أ َ ْبنَاء ُه ْم أ َ ْو ِإ ْخ َوانَ ُه ْم أ َ ْو‬ َّ َّ‫اَّلل َو ْاليَ ْو ِم ْاْل ِخ ِر ي َُوادُّونَ َم ْن َحاد‬
ُ ‫اَّللَ َو َر‬ ِ َّ ‫ََل ت َِجدُ قَ ْو ًما يُؤْ ِمنُونَ ِب‬
‫ار خَا ِلدِينَ فِي َها‬ ُ ‫ت تَجْ ِري ِمن تَحْ تِ َها ْاأل َ ْن َه‬ ٍ ‫اْلي َمانَ َوأَيَّدَهُم بِ ُر‬
ٍ ‫وح ِ هم ْنهُ َويُد ِْخلُ ُه ْم َجنَّا‬ ِ ْ ‫َب فِي قُلُوبِ ِه ُم‬ َ ‫يرت َ ُه ْم أ ُ ْولَئِكَ َكت‬
َ ‫َع ِش‬
ْ
َ‫اَّلل ُه ُم ال ُم ْف ِل ُحون‬ َ
َ ‫اَّلل أ ََل ِإ َّن ِح ْز‬
ِ َّ ‫ب‬ ِ َّ ‫ب‬ ُ
ُ ‫ضوا َع ْنهُ أ ْولَئِكَ ِح ْز‬ ُ ‫اَّللُ َع ْن ُه ْم َو َر‬
َّ ‫ي‬ َ ‫ض‬ ِ ‫َر‬
“Huwakuti watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa
wanawapenda wanaompinga Allaah Mtume wake, hata wakiwa ni baba
zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika
nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na
atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa
daima Allaah awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio
Hizbullahi, Kundi la Allaah. Hakika Kundi la Allaah ndilo
lenye kufanikiwa.” (58:22)

Baadhi ya watu wanalingania kwa Allaah na wanaita watu katika Uislamu,


hawajui uhakika wa Uislamu. Na ukiwauliza nini maana ya Uislamu,
4

www.wanachuoni.com

hawatokujibu kwa jawabu lililo sahihi, kwa kuwa hawajajifunza, hawajasoma


nini maana ya Uislamu, hawajasoma 'Aqiydah sahihi iliyojengwa chini ya
msingi wa Qur-aan na Sunnah. Wanadhani kimakosa kabisa. Hii ndio faida ya
ujinga.

Uislamu umuhimu wake na uwajibu wake wa kuuwafunza watu, alikuja nao


Jibriyl kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), naye [Mtume] alikuwa amekaa na
Maswahabah wake.

“Walipokuwa wamekaa na Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), alijitokeza mtu haonekani
na uchovu wa safari na hapakuwa hata mmoja aliekuwa akimjua. Akakaa
mbele ya Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa adabu kabisa, mkao wa mtu mwenye
kutafuta elimu [mwanafunzi], akamwambia ewe Muhammad!: "Nambie nini
maana ya Uislamu? Akasema Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana mola
apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume
wa Allaah, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na
kwenda kuhiji kwa yule mwenye uwezo." Yule mtu (Jibriyl) akasema:
"Umesema kweli". Maswahabah wakashangazwa kuona anamuuliza kisha
anamwambia kasema kweli.

Yule mtu akasema: "Nambie nini maana ya Imaani? Akasema imani ni


kumuamini Allaah, malaika wake, vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya
Qiyaamah na kuamini Qadar; kheri na shari inatoka Kwake (Allaah)." Yule
mtu (Jibriyl) akasema umesema kweli.

Akauliza nieleze kuhusu Ihsaan? Akasema Ihsaan ni kumuabudu Allaah


kama vile unamuona na kama humuoni basi jua kuwa Yeye Anakuona.

Akasema (Jibriyl): “Niambie kuhusu Qiyaamah. Akajibu Mtume ( ‫صلى هللا عليه‬
‫)وسلم‬: “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji. Nijulishe alama
zake: Akajibu Mtume (‫)صلى هللا عليه وسلم‬: “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona
wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata
mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini)
wakishindana kujenga majumba ya fakhari. Kisha akaondoka (Jibriyl) na
nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Mtume (‫)صلى هللا عليه وسلم‬: "Ewe
'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: “Allaah na
Mjumbe wake wanajua zaidi.” Akasema Mtume (‫)صلى هللا عليه وسلم‬: “Ni Jibriyl,
alikuja kuwafundisha dini yenu”.”
5

www.wanachuoni.com

Hii ni dalili ya kwamba ni wajibu kwa mtu kujifunza Dini hii na kuiingia kwa
baswiyrah na kikweli kweli mpaka mtu awe Muislamu wa kweli. Si Muislamu
mwenye kufuata tu kichwa mchunga au mwenye madai tu.

Tumuogope Allaah katika Dini yetu, na hivyo ni kwa kumjua na kumfanyia


kazi na kuacha kwa yale Aliyokataza. Hiyo ndio natija yetu, mazuri yetu na
mafanikio yetu katika dunia hii. Anasema Allaah (Ta'ala):

َ‫اَّلل َح َّق تُقَاتِ ِه َوَلَ ت َ ُموت ُ َّن إَِلَّ َوأَنتُم ُّم ْس ِل ُمون‬
َ ‫يَا أَيُّ َها الَّذِينَ آ َمنُواْ اتَّقُواْ ه‬
“Enyi mlio amini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha; wala msife
ila nanyi ni Waislamu.” (03:102)

Shikamana na Dini hii mpaka yatakapokujia mauti, mfe katika Dini hii
mkutane na Allaah ilihali mko nayo.

َ‫طفَى لَ ُك ُم الدهِينَ فَالَ ت َ ُموت ُ َّن إََلَّ َوأَنتُم ُّم ْس ِل ُمون‬


َ ‫ص‬ َ ‫ي إِ َّن ه‬
ْ ‫اَّلل ا‬ ُ ُ‫صى بِ َها إِب َْراهِي ُم بَنِي ِه َويَ ْعق‬
َّ ِ‫وب يَا بَن‬ َّ ‫َو َو‬

“Na Ibraahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika


Allaah amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu,
wanyenyekevu.” (02:132)

Na hivyo ni kwa kujilazimisha na Dini hii na kuifanyia kazi, na kuacha


inavyoidhuru maisha yote ya Muislamu mpaka mauti yamkute naye yuko
katika Uislamu. Anayekufa katika Uislamu anaingie Peponi. Na anayekufa
katika kufru [dini zingine] na Shirki anaingia Motoni, na anayekufa katika
Uislamu naye yuko na madhambi makubwa ambayo ni chini ya Shirki, huyo
tunamuachia Allaah. Akipenda Atamsamehe na Akipenda atamuadhibu
kadiri ya madhambi yake kisha atamtoa Motoni baada ya kumuadhibu kisha
atamuingiza Peponi. Huu ndio Uislamu tunapaswa kuujua, kuusoma na
kushikamana nao.

Walikuwa watu wa Mji huu (Saudi Arabia) katika siku za mwanzo


wakiwafunza watu kwenye Misikiti Uislamu, Dini, wakiwahifadhisha hizi
hukumu mpaka wakashikamana nao. Ila leo hatuoni anaesimama kwa hilo
wala anaeliuliza, mpaka wengi miongoni mwa wanaojifunza (wanafunzi) na
wale wanaochukua Shahaadah, hawajui uhakika wa Uislamu. Ukiwauliza
nini maana ya Uislamu hawatokujibu, kwa kuwa hawakujishughulisha na
kujifunza, na hawajui uhakika wake mpaka wakaweza kushikamana nao kwa
6

www.wanachuoni.com

elimu na Baswiyrah na wakahadhari na yaliyo dhidi yake na yanayoyakhalifu


au kuyakata.

Mcheni Allaah Allaah enyi waja wa Allaah na jueni mambo ya Dini yenu
mpaka muwe imara kwa yale Aliyowateremshia Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala).

ِ ‫اَّلل َعا ِقبَةُ ْاأل ُ ُم‬


‫ور‬ ِ َّ ‫سكَ ِب ْالعُ ْر َو ِة ْال ُوثْقَى َو ِإلَى‬ ِ َّ ‫َو َمن يُ ْس ِل ْم َوجْ َههُ ِإلَى‬
َ ‫اَّلل َوه َُو ُمحْ ِس ٌن فَقَ ِد ا ْست َْم‬
“Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Allaah, naye akawa anafanya
wema, basi huyo hakika amekwishakamata fundo lilio madhubuti.
Na mwisho wa mambo yote ni kwa Allaah.” (31:22)

Enyi watu! Baada ya kujua neema ya Allaah juu yenu kwa Uislamu huu na
kujua uhakika wa Uislamu, ni juu yenu kumuomba Allaah uthabiti juu yake
(Uislamu). Wengi waliyokuwa wakiujua Uislamu na wakauingia wamepotea
na kuritadi kwa sababu ya fitnah ambayo imewakumba watu leo. Fitnah
ambayo inainga mpaka kwenye manyumba ya watu, wanaisikia na
kuishuhudia wenyewe.

Kwenye chaneli chavu mbali mbali, na kwenye intanet na vyombo mbali


mbali vya mda ambavyo vinawaweka utata na kuwazuia na Da'wah. Vyombo
hivyo vinawapoteza katika Uislamu mpaka wengine leo wanafikia kuwa
Mulhid (makafiri) baada ya wao walikuwa Waislamu, kuwa Madu'aat, baada
ya wao kujifunza wamepotea na wamekuwa wanajadiliana na Allaah na Dini
Yake.

Tusijiamini katika nafsi zetu kutofikwa na yaliyowafika wao (ambao


wamepotea). Ni juu yetu kuogopa fitnah na kumuomba Allaah uthabiti katika
Dini hii mpaka siku ya mwisho bila kukengeuka. Fitnah zimekuwa kubwa.
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katwambia kuhusu kwazo [hizo fitnah] ili
kutuhadharisha nazo, hivyo kwa kauli yake Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam):

"Uislamu ulianza ni kitu kigeni na utarudi kuwa ugeni kama ulivyoanza,


bishara nje kwa Ghuraabah."

Angalia, Muislamu anakuwa mtu mgeni ilihali kuna wanaodai Uislamu, vipi
kwa Makafiri? Ugeni! Na mgeni ni mtu ambaye yuko kwa watu ambao si
ndugu zake wala wa jinsia yake na hayupo kwenye Mji wake. Huu ndio
ugeni. Na [Uislamu] utarudi kuwa kitu kigeni kwenye Miji ya Waislamu.
7

www.wanachuoni.com

"... Bishara nje kwa Ghuraabah. [Maswahaba] wakauliza": Na ni kina nani


Ghuraabah ewe Mtume wa Allaah?" (Mtume) akasema: “Ni wale
wanaotengeneza wanapoharibu watu." Katika upokezi mwingine: "Ni wale
wanaotengeneza waliyoharibu watu."

Tuwe na khofu juu ya hilo, na tushikamane na Dini yetu tuwe na subira. Na


tuwe na khofu juu ya Dini yetu, watoto wetu, mabanati wetu na ndugu zetu
Waislamu, tuhadhari mambo haya.

Wala huwezi kushikamana na Dini hii vizuri isipokuwa pale utapojifunza na


kuijua. Utapojifunza elimu sahihi na ukashikamana na wanachuoni mpaka
ukashikamana nayo. Ama kujinasibisha tu bila ya kuijua hili halisaidii kitu na
mwisho wake ni kufikwa na fitnah, tunamuomba Allaah afya.

Mcheni Allaah enyi waja wa Allaah, tuwe tahadhari na Madu'aat waovu,


Madu'aat wapotofu, kuweni tadhari na shubuha (utata) ambao
unawababaisha watu leo katika vyombo mbali mbali.

Hakika haokoki mtu (na fitnah hizo) ila yule aliyemuwezesha Allaah na
akamjua Allaah ukweli wa kumjua na akaijua Dini ya Kiislamu uhakika wake
na akasubiria kwa hilo mpaka Akamchukua Allaah ('Azza wa Jalla).

Namuomba Allaah mimi na nyinyi atupe uthabiti katika Dini, na atukinge na


fitnah za dhahiri na zilizojificha.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, ahli zake na


Maswahabah zake wote.

You might also like