You are on page 1of 21

4.

Suurat An - Nisaai

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

76

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

4:22. Na nyinyi msioe wale wanawake ambao baba zenu wamepata kuwaowa, ila yale yaliyokwishapita. Kwa hakika hilo ni jambo la aibu na chukizo na ni njia mbaya kabisa. 4:23. Imeharamishwa kwenu nyinyi; Mama zenu na binti zenu na dada zenu na dada ya baba zenu na dada wa mama zenu na mabinti wa kaka zenu na mabinti wa dada zenu na mama ambao walikunyonyesheni nyinyi (maziwa ya matiti yao) na dada zenu wa kunyonya na mama wa wake zenu na binti zenu wa kambo ambao wako chini ya uangalizi wenu toka kwa wake zenu ambao nyinyi mmewaingilia na ikiwa nyinyi hamjawaingilia wao, basi, hakuana ubaya wowote kwa binti zao na (mmekatazwa pia) wake wa watoto wenu wa kiume ambao ni toka viunoni mwenu wenyewe na kuwa na madada wawili kwa pamoja (katika ndoa) ila yale ambayo tayari yamekwishapita. Kwa hakika Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma.

75

4. Suuratun Nisaai

4:13. Hii ndiyo mipaka ya Allah. Na yeyote anayemtii Allah na Mtume Wake Allah Atamfanya yeye kuyaingia mabustani ambayo hupita kwa chini yake mito humo wao wataishi. Na huko ndiko kufuzu kuliko kukubwa kabisa. 4:14. Na yeyote anayemuasi Allah na Mtume Wake na akachupa mipaka Yake yote Allah Atamfanya yeye aingie Motoni ambamo ataishi na kwa ajili yao iko adhabu kali yenye kudhalilisha.

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

4:15. Na wale wanaozini miongoni mwa wanawake wenu, basi, mchukue ushahidi wa wanaume wanne toka miongoni mwenu dhidi yao. Na wao wakitoa ushahidi, basi, wazuieni wao katika majumba hadi kiwafike wao kifo au Allah Awapatie wao njia nyingine. 4:16. Na wale wanaume na wanawake wanaofanya hayo (ya Liwati) miongoni mwenu, waadhibuni wao vikali. Na ikiwa wao watatubu na wakatengeneza, basi, waacheni wao. Kwa hakika Allah ni Mkubali-toba mno, Mwenye huruma. 4:17. Toba ambayo hukubaliwa na Allah kwa huruma Yake ni ya wale ambao hufanya mabaya kwa ujinga na wao wakatubu kwa haraka. Kwa watu hao Allah Huwaelekea na huruma Yake. Na Allah Yu Mjuzi mno, Mwenye hekima. 4:18. Na kuwa hapana toba kwa wale wanaoendelea kufanya mabaya mpaka pale kifo kinapomfikia mmoja wao ndo yeye asema; Sasa mimi ninatubu wala kwa wale wanaokufa wakiwa makafiri. Kwa ajili yao Tumewaandalia adhabu kali yenye kutiwa uchungu. 4:19. Enyi mliyoamini! Katu Si halali kwenu nyinyi kwamba muwarithi wanawake kwa nguvu. Na nyinyi msiwazuie wao kwa lengo la kuchukuwa baadhi ya vile mlivyowapa wao ikiwa ni mahari yao ila katika hali hii ya kuwa wao wafanye ya uzinifu bayana. Na muishi nao katika hali nzuri. Na ikiwa nyinyi mtawachukia wao, basi, inawezekana kabisa kwamba nyinyi mkachukia kitu na kumbe Allah Kajaalia katikacho mazuri mengi. 4:20. Na ikiwa nyinyi mnatamani kubadilisha mke mahali pa mwingine na tayari wewe umekwishampa yeye lundo la mali, basi, nyinyi msichukuwe katikayo kitu. Je! Nyinyi mtaichukua tena kwa kashfa na dhambi iliyo bayana? 4:21. Mtaichukuaje na hali ya kuwa tayari kila mmoja wenu amekwishajifunua mbele ya mwenzake na wao walichukua toka kwenu ahadi madhubuti? 74

4. Suuratun Nisaai

4:07. Kwa ajili ya wanaume lipo fungu katika vile ambavyo wazazi wao na ndugu wameacha nyuma yao na kwa ajili ya wanawake lipo fungu katika vile ambavyo wazazi wao na ndugu wameacha nyuma yao iwe ni urithi kidogo au mkubwa; Ni fungu lililokwisha kisiwa na kuamuliwa.

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

4:08. Lakini ikiwa wakati wa kugawa watakuja ndugu na yatima na wahitaji, basi, na wao muwape kidogo kutokacho na mseme nao maneno mazuri. 4:09. Na wao waogope, wale ambao kama wangeacha nyuma yao watoto walio dhaifu na wao pia wangekhofu kwa ajili yao. Basi, na wao wamuogope Allah na waseme maneno yaliyonyooka. 4:10. Wale wanaokula mali za yatima kwa dhuluma wao wanajaza matumbo yao Moto. Na hivi karibuni wao watauingia Moto uwakao vikali. 4:11. Allah-Subhaanahu wa taala Anakuamrisheni nyinyi kuhusu watoto wenu; Fungu la mtoto wa kiume ni sawa na fungu la watoto wawili wa kike. Basi, ikiwa kutakuwa na watoto wa kike tu zaidi ya wawili, basi, wao wana theluthi mbili (yaani 2/3) ya kile kilichoachwa. Na ikiwa kutakuwa na mtoto mmoja tu wa kike, basi, kwake yeye ni nusu (ya mali yote). Na kwa kila mmoja wa (wale) wazazi (wawili) wa marehemu ana sudusi (yaani 1/6) katika kile kilichoachwa ikiwa huyo marehemu ana mtoto. Lakini ikiwa hana mtoto na akaacha wazazi tu, basi, kwao wao mama ana theluthi (yaani 1/3). Lakini kukiwa na ndugu wengi wa kike na kiume, basi, mama ana sudusi (yaani 1/6; Na haya yatafanyika) baada ya kuzingatia wasia wa marehemu na kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu nyinyi hamjui ni yupi wao ndiye mwenye manufaa zaidi kwenu nyinyi; Huu ni mgawo uliokwishapangwa toka kwa Allah. Kwa hakika Allah Yu Mjua-yote, Mwenye hekima. 4:12. Na nyinyi mna nusu (yaani 1/2) ya kile walichoacha wake zenu ikiwa wao hawana mtoto. Lakini ikiwa wao wana mtoto, basi, nyinyi mna robo (yaani 1/4) ya walivyoacha baada ya kuzingatia wasia wao na kulipa deni. Na wanawake wana robo (yaani 1/4) ya vile mnavyoacha ikiwa nyinyi hamna mtoto. Lakini ikiwa nyinyi mna mtoto, basi, wao wana thumuni (yaani 1/8) katika vile mlivyoacha baada ya kuzingatia wasia wenu na kulipa deni. Na ikiwa mirathi inayogawiwa ni ya mwanaume au mwanamke asiye na mrithi; Hakuacha wazazi wala watoto lakini kwa upande wa mama yake ana kaka au dada, basi, kwa kila mmoja wao ipo sudusi (yaani 1/6). Lakini ikiwa hao kaka na dada ni wengi, basi, wao watagawana katika theluthi (yaani 1/3) baada ya kuzingatia wasia (wa marehemu) na kulipa deni; Hii ni Amri ya kisheria toka kwa Allah. Na Allah ni Mjua-yote, Aliye Mpole. 73

4. Suuratun Nisaai

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

Ina Aya 176

SUURATUN NISAAI (Imeteremshwa Makka) Allah kwa Jina la Aliye Mwingi mno wa upendo, Aliye Mwenye huruma ninaanza.

Ina Karaa 24

4:01. Enyi watu! Muogopeni Mola wenu nyinyi Ambaye Amekuumbeni nyinyi toka nafsi moja na Akaumba mwenza kutokayo na toka jozi hiyo (yaani Adamu na Hawa) Akaeneza wanaume wengi na wanawake wengi. Na Muogopeni Allah Ambaye kwa Jina lake nyinyi mnaombana na nyinyi muuenzi ule udugu. Kwa hakika Allah Yu Mwenye Kuwaona nyinyi wakati wote. 4:02. Na wapeni yatima mali zao na nyinyi msibadili vilivyo vichafu kwa visafi, wala msile mali zao kwa kuzichanganya na mali zenu. Kwani hilo Li dhambi kubwa kabisa. 4:03. Na ikiwa nyinyi mtakhofu ya kuwa hamtaweza kuwafanyia uadilifu wasichana yatima, basi, nyinyi oweni wale wanawake wengine ambao watawapendeza nyinyi; Wawili au watatu au wanne. Lakini ikiwa wewe utakhofu kuwa huwezi kuwaweka wake wawili kwa usawa, basi, owa mmoja tu au mateka (wajakazi) ambao wako chini ya himaya ya miliki zenu. Haya ni karibu na kukuweka wewe mbali kabisa na dhuluma. 4:04. Na muwape wanawake mahari zao kwa ridhaa. Lakini ikiwa wao kwa hiari ya nyoyo zao watakuachieni nyinyi katika hizo kitu, basi, mkile kwa upendo na furaha. 4:05. Na nyinyi msiwape wale wapumbavu mali zao mlizonazo ambazo Allah Amezijaalia kuwa ni njia ya nyinyi kujikimu na muwalishe wao kwazo na kuwavika wao na semeni nao maneno mazuri. 4:06. Na nyinyi muwapime yatima mpaka pale wao kuowa na ikiwa nyinyi mtawaona ya kuwa sasa wanaelewa mambo, basi, muwape wao mali zao na katu nyinyi msizile kwa ubadhirifu na kwa haraka mkichelea kukua kwao. Kwa yule ambaye ni muhitaji yeye ale kwa kiasi cha haja. Kisha pale nyinyi mnapowakabidhi wao mali zao, basi, chukueni ushahidi dhidi yao. Na Allah-Subhaanahu wa taala Yu Mwenye kutosha kwa hesabu. 72

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)


SUURATUN NISAA (WALE WANAWAKE)

Lan Tanaluu.

Maelezo mafupi; Sura hii iliteremshwa Madina. Ina Aya mia moja na sabini na sita, sehemu ishirini na nne maneno elfu tatu na arobaini na tano na herufi elfu kumi na sita na thelathini. Sura hii inajushughulisha zaidi na taratibu za kijamii na mahusiano ya kifamilia ambayo yalikuwa yanawakabili Waislamu baada ya vita vya Uhud. Sehemu kubwa ya Sura hii inashughulika na haki za wanawake na yatima na matatizo ya mahusiano ya kifamilia na ugawaji wa mali za marehemu yaani mirathi. Sura inaanza na msingi asili ya umoja wa binadamu na wajibu wa pande mbili wa mwanaume na mwanamke. Sehemu kubwa ya Sura hii imetengwa maalumu kwa sharia zinazohusu matatizo ya wakati wa amani na wakati vita. Aya zingine zinazungumzia juu ya uhusiano kati ya Waislamu na makafiri na wanafiki, Waislamu wanatahadharishwa dhidi ya njama za makafiri na wanafiki na wakashauriwa kujipanga vyema kwa ajili ya kujihami. Aya nyingine zinatia mkazo katika kumkubali na kumuamini Mtume wa mwisho na kujisalimisha kwake kwa unyenyekevu unaostahili maana bila ya yeye mtu hawezi kuwa Muislamu, Jambo hili liko wazi mtu hawezi kuaminika kwamba ni muumini wa Upweke wa Allah yaani Tauhidi mpaka kwanza yeye awaamini Mitume na manabii wote waliotangulia pamoja na huyu Mtume wa mwisho Muhammad-Swalallahu alayhi wasallam. Sura hii inatukumbusha kwamba watu wote Duniyani ni wenye hadhi sawa. Haki ya kila mmoja miongoni mwetu ni lazima iheshimiwe kwa ukamilifu wake. Uhusiano wa kidugu unatakiwa kupewa mkazo wa ziada na yatima walelewe kwa uadilifu katika majumba ya Waislamu na haki yao ya kumiliki mali ni lazima iheshimiwe na kulindwa. Kwa umuhimu wa wanawake ndani ya jamii, Sura nzima imeitwa kwa jina lao. Moja ya sifa za Sura hii ni kuwa kama mtu ataisoma sura hii mara saba mfululizo na msomaji akapuliza ndani ya maji baada ya kuisoma na maji hayo yakanywewa na mume na mke, basi, wao watapendana sana. Na inafahamika pia kuwa kama Sura hii itaandikwa kombe kwa zafarani iliyochanganywa na tezi ya kulungu na mtu anaesumbuliwa na mpapatiko wa moyo au ugonjwa wa ghamu akanywa kombe hilo basi bi idhnillah ugonjwa wake utapona.

71

3:199. Na kwa hakika miongoni mwa watu wa Kitabu wako ambao humuamini Allah na yale ambayo yameteremshwa kwenu nyinyi na yale ambayo yaliteremshwa kwao (yaani Taurati, Zaburi na Injili) mioyo yao ni yenye kunyenyekea kwa Allah na katu wao hawapokei bei ndogo kwa Aya za Allah. Hao ndiyo wale ambao tunzo yao I mbele ya Mola wao. Na Allah Yu Mwepesi mno katika hesabu. 3:200. Enyi mliyoamini! Kuweni na subira na mshindane na maadui zenu katika subira na muilinde mipaka ya nchi za Kiislamu na muendelee kumcha AllahSubhaanahu wa taala huenda nyinyi mkafanikiwa.

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

70

3:191. Wale ambao humkumbuka Allah (kwa nyiradi mbali mbali) wakiwa wenye kusimama, wenye kukaa au wenye kulalia mbavu zao na wakatafakari uumbwaji wa mbingu na ardhi na wakasema; Ee Mola wetu! Wewe Hukuviumba hivi bure; Utakasifu ni Wako Wewe tu, basi, Utuokoe sisi na adhabu ya Moto Jahanamu. 3:192. Ee Mola wetu! Kwa hakika Yeyote ambaye Wewe Utamfanya yeye auingie Moto, kwa hakika yeye Umekwishamfedhehesha. Na madhalimu hawatakuwa na wa kuwasaidia.

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:193. Ee Mola wetu! Sisi tulimsikia mpiga mbiu akiita watu kwenye imani ya kuwa mumuamini Mola wenu, na sisi tukaamini. Ee Mola wetu! Utusamehe sisi dhambi zetu na Utufutie sisi mabaya yetu na Utufishe sisi tukiwa miongoni mwa wale waliyo wema. 3:194. Ee Mola wetu! Utupe sisi vile ambavyo Wewe Umetuahidi sisi kupitia Mitume Wako na Usituaibishe sisi hiyo Siku ya Kiyama. Kwa hakika Wewe Si Mvunjaji ahadi. 3:195. Basi, Mola wao Akaisikia dua yao; Kwa hakika Mimi Sipotezi juhudi ya mfanya mema yeyote miongoni mwenu nyinyi iwe ni mwanaume au mwanamke, nyinyi ni wamoja miongoni mwenu, Na hivyo, wale ambao walihajiri na kutolewa majumbani mwao na wakateswa katika Dini Yangu na wakapigana na wakauliwa. Kwa hakika Mimi Nitazifuta dhambi zao zote na kwa hakika Mimi Nitawaingiza wao katika mabustani ambayo hupita kwa chini yake mito ni tunzo toka kwa Allah-Subhaanahu wa taala. Na kwa Allah tu ndiyo kwenye tunzo zilizo nzuri kabisa. 3:196. Basi, katu wewe usihadaike na mbwembwe za wale waliyo makafiri katika miji. 3:197. Ni starehe zenye kupita halafu mafikio yao ni katika Moto Jahanamu na ni kitanda kibaya kilioje! 3:198. Lakini wale wanaomuogopa Mola wao wao wana mabustani ambayo hupita mito kwa chini yake; Wao wataishi humo milele, ni cha kuwapendeza wao toka kwa Allah. Na vile vilivyo kwa Allah ni vizuri mno kwa ajili ya wale waliyo wema. 69

3. Suuratul Aali Imraan

3:183. Wale ambao walisema; Allah Ameahidiana nasi ya kuwa katu sisi tusimuamini Mtume yeyote hadi yeye Atuletee sisi amri ya sadaka ya kile ambacho moto utakiteketeza. Wewe sema; Mitume wengi walikujieni nyinyi hapo kabla yangu wakiwa na miujiza na hoja zilizo bainifu na ile amri ambayo nyinyi mnasema, basi, kwa nini nyinyi mliwauwa wao ikiwa nyinyi ni msemao kweli?

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:184. Basi, ewe mpendwa! Kama wao wakikupinga wewe, basi, hivyo ndivyo walivyopingwa Mitume kabla yako wewe; Waliwajia wao wakiwa na miujiza na hoja zilizo bainifu na sahifa na Vitabu vyenye nuru (yaani Taurati, Zaburi na injili) ambavyo tayari vimekwishapotoswa. 3:185. Kila nafsi itaonja mauti. Na nyinyi mtapata malipo yenu kikamilifu hiyo Siku ya Kiyama. Yeyote atakaeokolewa na Moto na kuingizwa Peponi, basi, yeye atakuwa miongoni mwa wale waliyofuzu. Na hayakuwa maisha ya Duniya ila ni vizuri vyenye kudanganya. 3:186. Kwa hakika nyinyi mtatahiniwa katika mali zenu na maisha yenu na kwa hakika nyinyi mtasikia matusi mengi toka kwa watu waliopewa Kitabu kabla yenu nyinyi na toka kwa wapagani. Lakini kama nyinyi mtavumilia na kumcha Mungu, basi, hilo ni jambo linalohitaji kuazimiwa. 3:187. Na kumbuka pale Allah Alipochukua ahadi toka kwa wale waliopewa Kitabu; Ni lazima nyinyi mkibainishe kwa watu na katu nyinyi msikifiche. Lakini wao wakakitupa nyuma ya migongo yao na wakachukua bei ndogo kwa kubadili nacho. Basi, ni biashara mbaya iliyoje ile waliyofanya! 3:188. Katu wewe usidhani ya kuwa wale wanaofurahia mambo wanayofanya na wale ambao hutaka kusifiwa kwa mambo wasiyofanya kuwa wao wako mbali na adhabu. Kwa ajili yao iko adhabu kali yenye kutiwa uchungu. 3:189. Na ni wa Allah tu ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allah-Subhaanahu wa taala Yu Muweza juu ya kila kitu. 3:190. Kwa hakika katika uumbaji wa mbingu na ardhi na katika ubadilikaji wa usiku na mchana, mna ishara kwa watu wenye kuelewa. 68

3. Suuratul Aali Imraan

3:175. Ni shetani ndiye huwatishia nyinyi waliyo rafiki zake, basi, nyinyi msiwaogope wao bali Mniogope Mimi tu ikiwa kweli nyinyi ni wenye imani.

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:176. Na (ewe mpendwa)! Usihuzunike kwa ajili yao wale ambao huukimbilia udanganyifu, wao hawatamdhuru Allah kitu. Allah Anataka kuwa Asijaalie nafasi yoyote kwa ajili yao huko Akhera. Na kwa ajili yao iko adhabu kubwa kabisa. 3:177. Wale waliyoununua ukafiri kwa imani katu wao hawatamdhuru Allah kitu. Na kwa ajili yao iko adhabu yenye kutiwa uchungu. 3:178. Na wale wasiyoamini katu wao wasidhani ya kuwa ule muda tunaowapa wao ni jambo zuri kwao. Kwa hakika Sisi Tunawaachia wao muda ili wao wazidi kulimbikiza dhambi zao. Na kwa ajili yao iko adhabu kali yenye kudhalilisha. 3:179. Allah Si wa kuwaacha Waislamu katika hali mliyonayo hata Yeye Ampambanue aliye mchafu na aliye msafi. Na Si stahiki Yake kuwa enyi watu! Yeye Akuacheni nyinyi kujua yale yasiyoonekana. Naam, Allah Huteua kutoka miongoni mwa Mitume Wake yeyote Anayemtaka. Basi, mumuamini Allah na Mitume Wake. Na ikiwa nyinyi mtaipokea imani na kumuogopa, basi, nyinyi tunzo iliyo kubwa kabisa. 3:180. Na wale waliyo mabakhili kwa vile ambavyo Allah Amewapa wao kwa Ukarimu Wake wasidhani kuwa hivyo ni vizuri kwao. Sivyo, ila ni kinyume chake na ni shari kwao. Hivi karibu vile walivyofanyia ubakhili vitakuwa ndio mikufu yao Siku ile ya Ufufuo. Na ni Allah tu Ndiye Aliye mrithi wa mbingu na ardhi. Na Allah Yu Mwenye Kuyajua yote yale mnayofanya. 3:181. Kwa hakika Allah Amekwishawasikia wale ambao walisema; Allah ni muhitaji na sisi ni matajiri. Hivi karibuni Sisi Tutaweka maneno yao na kule kuwauwa kwao Mitume kwa dhuluma katika maandishi na Sisi Tutasema; Ionjeni adhabu ya Moto (kwa ule uasi wenu). 3:182. Haya ndio malipo ya yale ambayo mikono yenu imetanguliza na Allah Si Mwenye Kudhulumu waja Wake. 67

3. Suuratul Aali Imraan

3:166. Na lile janga lilolowapata nyinyi siku ile yalipokutana majeshi mawili (la waislamu na lile la makafiri katika vita vya Uhud) ni kwa amri ya Allah; Na kwa hivyo Kuwaainisha wale waliyo waumini.

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:167. Na ili Yeye Awezeshe kutambulika kwa wanafiki. Na waliambiwa; Njooni mpigane katika njia ya Allah au kuwafukuza maadui. Wao wakasema; Lau sisi tungekuwa tunajua kupigana kwa hakika sisi tungekuwa upande wenu. Wao siku hiyo walikuwa karibu zaidi na ukafiri uliyo wazi kuliko imani. Wao husema kwa midomo yao yale ambayo hayamo katika nyoyo zao. Na Allah Yu Mwenye Kuyajua yote wanayoficha. 3:168.Wale ambao walisema kuhusu ndugu zao huku wao ni wenye kubaki nyuma; Laiti wao wangetutii sisi, basi, wao wasingaliuliwa. Wewe sema; Basi, mjizuilie kifo chenu nyinyi ikiwa nyinyi ni msemao kweli. 3:169. Na wale waliyouliwa katika njia ya Allah; Nyinyi msiwadhanie wao kuwa ni wafu! Hasha, wao ni hai wenye kuruzukiwa kwa Mola wao. 3:170. Ni wenye furaha kwa sababu ya yale ambayo Allah Amewapa wao kwa ukarimu Wake na wenye furaha kwa ajili ya wale walioshika nafasi zao; Ambao bado wao hawajajiunga nao ya kuwa hakutakuwa na khofu yoyote juu yao wala wao hawatahuzunika. 3:171. Wao wanafurahia neema za Allah na Ukarimu Wake na kwamba Allah-Subhaanahu wa taala Hapotezi malipo ya waislamu. 3:172. Wale ambao walimuitikia Allah na Mtume Wake baada ya wao kupata majeraha. Yapo malipo makubwa kabisa kwa wenye kufanya mema na Kumtukuza Yeye. 3:173. Wale ambao watu waliwaambia; Watu wamejikusanya dhidi yenu na hivyo nyinyi muwaogope wao, Lakini hilo likawazidishia wao imani na wakasema; Allah Anatutosha sisi na ni Mbora Aliyoje wa kupanga mambo! 3:174. Basi, wao wakarejea na neema toka kwa Allah na ukarimu Wake; Halikuwapata wao baya lolote na wakafuata radhi ya Allah. Na Allah Yu Mkarimu mno. 66

3. Suuratul Aali Imraan

3:157. Na kwa hakika ikiwa nyinyi mtauliwa katika njia ya Allah au mkifa, basi, msamaha wa Allah na huruma Yake ndiyo bora zaidi kuliko mali zote mnazokusanya (katika Duniya).

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:158. Na ikiwa nyinyi mtakufa au nyinyi kuuliwa kwa hakika ni kwa Allah tu ndiyo nyinyi nyote mtakusanywa. 3:159. Basi, ni kwa huruma toka kwa Allah ndiyo ewe mpendwa (Mtume Muhammad-Swallalahu alayhi wasallam)! Umekuwa mpole kwao. Na lau wewe ungekuwa mkali, msusuwavu wa moyo kwa hakika wao wangalisambaa kutoka duara yako. Basi, uwasamehe wao na uwaombee wao msamaha na uwashauri katika mambo yao. Na pale wewe unapoamua kitu, basi, umtegemee Allah. Kwa hakika Allah Anawapenda wale wenye kumtegemea. 3:160. Kama Allah Akikusaidieni nyinyi, basi, hapana yeyote wa kukushindeni nyinyi na ikiwa Atakuacheni nyinyi, basi, ni nani mwingine Atakaekusaidieni nyinyi tena? Na Waislamu wamtegemee Allah tu Peke Yake. 3:161. Na katu haifikiriki kuhusu Mtume yeyote kuwa yeye afiche kitu. Na yeyote atakaeficha yeye atakuja na kile alichokificha hiyo Siku ya Kiyama. Halafu kila nafsi ilipwe kikamilifu kwa yale iliyochuma na wao katu hawatadhulumiwa. 3:162. Je, Yule mwenye kufuata radhi ya Allah ni kama yule ambaye amechuma ghadhabu Zake na hatima yake ni Moto Jahanamu? Na ni mahali pabaya palioje kwa mtu kufikia! 3:163. Wao (hao wanaofanya yaliyo mema) kwa madaraja ni karibu na Allah. Na Allah Yu Mwenye Kuyaona matendo yao. 3:164. Kwa hakika Allah Amewaneemesha mno wale waliyo Waislamu pale Yeye Alipowatumia wao Mtume toka miongoni mwao ambaye huwasomea wao Aya Zake na kuwatakasa na kuwafundisha wao Kitabu na hekima na kwa hakika kabla ya hapo wao walikuwa katika upotovu uliyo bayana. 3:165. Inakuwaje! Pale nyinyi mnapopatwa na janga lolote, japo tayari nyinyi mmekwishawapatisha (wao) mara mbili mfano wake, nyinyi huanza kusema; Yanatoka wapi haya? Wewe sema; Haya yanatoka kwenu nyinyi wenyewe (kwa kule kuiasi kwenu ile amri ya Mtume!) Kwa hakika Allah Yu Muweza wa kufanya chochote Anachotaka. 65

3. Suuratul Aali Imraan

3:152. Na kwa hakika Allah Amekwishakuisadikisha ile ahadi Yake kwenu pale nyinyi mlipokuwa mkiwauwa makafiri kwa idhini Yake; Hadi pale nyinyi mlipovunjika moyo na kugombana kuhusu ile amri (ya Mtume) baada ya Allah kukuonyesheni nyinyi vile ambavyo nyinyi mnatamani (yaani ngawira). Miongoni mwenu wako wale ambao wanaitamani zaidi Duniya na miongoni mwenu pia wako wale ambao wanaitamani zaidi Akhera. Halafu Yeye Akakufanyeni nyinyi mgeuze sura zenu kutokao ili Yeye Apate kukutahinini nyinyi. Na kwa hakika Yeye Amekwishakukusameheni nyinyi. Na Allah Yu Mkarimu mno kwa wale waliyo waislamu.

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:153. Pale nyinyi mlipokimbia haraka bila ya kumuangalia yeyote nyuma yenu na huku Mtume Wetu akikuiteni nyinyi katika kundi jingine; Na hivyo Yeye Akakutieni nyinyi majonzi ikiwa ni malipo ya majonzi na Akakusameheni ili kwamba nyinyi msihuzunike kwa yale yaliyokuponyokeni wala juu ya yale yaliyokusibuni. Na Allah Yu Mwenye khabari ya yote mnayotenda. 3:154. Baada ya huzuni Yeye Akateremsha juu yenu nyinyi usingizi wa utulivu uliowapata kundi miongoni mwenu, wakati kundi jingine lilijawa na wasiwasi kwa dhana zao mbaya kuhusu Allah bila ya ukweli wowote na kwa dhana potovu kwa sababu ya ujinga tu, wakisema; Lau sisi tungekuwa na uwezo katika uendeshaji wa jambo hili! Wewe tangaza; Uendeshaji wa jambo hili U katika mamlaka ya Allah tu peke Yake! Wao wameficha katika nafsi zao yale ambayo wao hawathubutu kuyadhihirisha kwako wewe. Wao husema; Laiti sisi tungalikuwa na uwezo katika jambo hili katu sisi tusingaliuwawa hapa. Wewe tangaza! Hata kama nyinyi mgebaki katika majumba yenu, basi, wale ambao kifo kimeandikwa juu yao wangetoka na kwenda kwenye maanguko yao. Allah Alitaka kuyatahini yale yaliyokuwa katika nyoyo zenu. Na Allah Yu Mwenye Kuzijua vyema zile siri za nyoyo. 3:155. Kwa hakika wale waliyorudi nyuma siku ile yalipokutana majeshi mawili (katika vita vya Uhud) Aliwatelezesha wao shetani kwa sababu ya baadhi ya vitendo vyao. Na kwa hakika Allah Aliwasamehe wao. Kwa hakika Allah Yu Msameheji mno, Aliye Mpole. 3:156. Enyi mliyoamini! Katu nyinyi msiwe kama wale makafiri ambao walisema kuhusu ndugu zao pale wao wanaposafiri katika ardhi au wao wametoka katika vita vitakatifu ya kuwa; Laiti wao wangekuwa pamoja nasi katu wao wasingalikufa wala kuuliwa. Ili Allah Ajaalie hayo kuwa majuto katika nyoyo zao. Na Allah Hupa uhai na Husababisha kifo. Na Allah Yu Mwenye Kuyaona yote mnayofanya. 64

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:143. Na nyinyi mlikuwa mnakitamani kifo kabla ya kukutana nacho, basi, sasa mmekwishakiona kwa macho yenu. 3:144. Na Muhammad ni Mtume. Kumekuwepo na Mitume wengi kabla yake. Basi, je! Ikiwa yeye atatawafu au kuuliwa ndo nyinyi mtarejea nyuma na kuwa makafiri? Na yeyote anayerejea nyuma na kuwa kafiri kwa namna yoyote ile yeye hatomdhuru Allah, na hivi karibuni Allah-Subhaanahu wa taala Atawajaza wale wenye kushukuru.

3:145. Na hapana nafsi inayokufa ila kwa Kutaka Kwake Allah. Muda wa kila kiumbe umekwishaandikwa. Na yeyote anayetamani tunzo za Duniya Sisi Tutampa katika hizo na yeyote anayetamani tunzo za Akhera Sisi Tutampa katika hizo. Na hivi karibuni Sisi Tutawajaza wale wenye kushukuru. 3:146. Na wengi katika Mitume walipigana vita wakiwa pamoja na kundi la watu wema, wao hawakuwa wazembe kwa yale waliyokabiliana nayo katika njia ya Allah wao hawakudhoofu na wala wao hawakukata tamaa. Na Allah Huwapenda mno wale waliyo wavumilivu. 3:147. Na wao hawakusema kitu ila dua hii; Ee, Mola wetu! Utusamehe sisi dhambi zetu na uchupaji wetu mipaka katika mambo yetu, na Uziimarishe hatua zetu na Utusaidie sisi dhidi ya hawa watu walio makafiri. 3:148. Basi, Allah Akawapa wao tunzo za Duniya na tunzo zilizo bora kabisa za Akhera. Na Allah Anawapenda wale wenye kufanya matendo mazuri. 3:149. Enyi mliyoamini! Ikiwa nyinyi mtafuata msitari wa makafiri, basi, wao watakurejesheni nyinyi juu ya visigino vyenu na hivyo nyinyi kurejea wenye khasara. 3:150. Hali ya kuwa Allah Ndiye Mlinzi wenu na Yeye Ndiye Mbora wa wenye kusaidia. 3:151. Hivi karibuni Sisi Tutatia khofu katika nyoyo za makafiri kwa vile wao wamemfanyia Allah washirika ambao Yeye Hajatetremsha kwao hoja yoyote; Hao makazi yao ni Motoni. Na ni makazi mabaya yaliyoje ya wale waliyo madhalimu!

63

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:131. Na muuepuke Moto ambao umekwishaandaliwa kwa ajili ya wale waliyo makafiri. 3:132. Na nyinyi endeleeni na utii wenu kwa Allah na Mjumbe (Wake) kwa matumaini ya kuwa mtahurumiwa. 3:133. Na mkimbilie kwenye msamaha wa Mola wenu na Pepo ambayo upana wake ni sawa na mbingu na ardhi ambayo imeandaliwa kwa ajili ya wale waliyo wacha Mungu. 3:134.Wale ambao hutoa katika njia ya Allah wakati wa neema na wakati wa shida na wale wanaozuwiya hasira (zao) na wale wanaosamehe watu. Na watu wema ni vipenzi wa Allah. 3:135. Na wale ambao pale wanapotenda machafu au kudhulumu nafsi zao wao huomba msamaha kwa dhambi zao wakimkumbuka Allah; Na ni nani Anayesamehe dhambi kama Si Allah! Na wao hawanganganii yale waliyoyafanya hali ya kuwa wanajua. 3:136. Kwao wao malipo ni msamaha wa Mola wao na mabustani ambayo hupita mito kwa chini yake humo wao wataishi milele. Na ni tunzo nzuri ilioje ya wale wafanyao matendo mazuri! 3:137. Kwa hakika kumekwishakuwa na mifano kabla yenu nyinyi, basi, nyinyi msafiri katika ardhi na muone mwisho wa wale waliyopinga (Mitume wa Allah) ulivyokuwa. 3:138. Haya ni maelezo bayana kwa watu na mwongozo na ni maonyo kwa wale waliyo wacha Mungu. 3:139. Na nyinyi msiwe wazembe (katika kupambana na makafiri) wala msihuzunike na nyinyi ndiyo wale ambao mtashinda ikiwa nyinyi ni wenye imani. 3:140. Kama dhiki imekupateni nyinyi, basi, na wao pia wamekwisha pata dhiki mfano wake. Na hizo ni siku ambazo Sisi Huzigawa kwa zamu kwa ajili ya watu na hayo ni ili Allah Apate kuwaainisha wale ambao wameamini na kuwapa baadhi yenu nyinyi U-shahidi. Na Allah Hawapendi wale waliyo madhalimu. 3:141. Na ili Allah Awatakase wale ambao wameamini (kupitia hiyo mitihani) na Awaangamize wale waliyo makafiri. 3:142. Au ndo nyinyi mnadhani ya kuwa! Mtaingia Peponi kabla Allah Hajawatahini mashujaa miongoni mwenu nyinyi na Kuwatahini wale waliyo wavumilivu? 62

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:120. Pale linapokupateni nyinyi zuri lolote wao huudhika na kama nyinyi mkipatwa na baya hapo wao hufurahi kwalo, basi, kama nyinyi mtakuwa na subira na mkamuogopa Allah katu vitimbi vyao havitakudhuruni nyinyi kitu. Kwa hakika Allah Yu Mwenye Kuyazingira yote yale wanayofanya. 3:121. Na kumbuka ewe kipenzi! Pale wewe ulipoondoka nyumbani kwako asubuhi kwenda kuwapanga Waislamu katika vituo vyao kwa ajili ya vita. Na Allah Yu Msikia-yote, Mjua-yote. 3:122. Pale makundi mawili miongoni mwenu yalipopata woga, hali ya kuwa Allah Yu Mlinzi wayo! Na kwa Allah tu ndio waislamu wanapaswa kutegemea. 3:123. Na kwa hakika Allah-Subhaanahu wa taala Alikusaidieni nyinyi katika vita vya Badri wakati hamkuwa na uwezo wa kutosha (na mkashinda). Basi, mcheni Allah huenda nyinyi mkawa na shukurani. 3:124. (Kumbuka;) Pale wewe ulipowaambia waislamu; Je! Haikutosheni nyinyi kuwa Mola wenu Akusaidieni nyinyi kwa kuteremsha malaika elfu tatu? 3:125. Naam! Kama nyinyi mtavumilia na kumuuogopa Allah na makafiri wakakujieni nyinyi ghafla, basi, Mola wenu Atakuleteeni malaika elfu tano wenye kutambulika kwa vyeo vyao kukusaidieni. 3:126. Na Allah Hakuwapeni nyinyi huo ushindi ila ni kwa kukuridhisha wewe na ili kwamba nyoyo zenu zipate kutulia kwao. Na hapana msaada ila ni toka kwa Allah Aliye Mtenza nguvu, Mwenye hekima. 3:127. Ili kwamba Yeye Apate kufyeka sehemu ya makafiri na Awadhalilishe wao na hivyo wao warejee wakiwa wenye huzuni. 3:128. Jambo hili haliko mikononi mwako wewe; Aidha Yeye Awahurumie wao kwa kutubu kwao au Awaadhibu wao, kwa vile wao ni madhalimu. 3:129. Na ni miliki ya Allah-Subhaanahu wa taala tu vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Yeye Humsamehe yeyote Anayemtaka na Humuadhibu yeyote Anayemtaka. Na Allah Yu Msameheji mno, Mwenye huruma. 3:130. Enyi mliyoamini! Katu nyinyi msile riba zenye kuzidishwa zidishwa. Na muogopeni Allah ili nyinyi mpate kustawi. 61

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:112. Fedheha imetupwa kwao popote pale walipo ila kwa kamba ya Allah na kamba ya watu na wao wakastahili ghadhabu ya Allah na umevurumishwa umasikini juu yao. Hayo ni kwa sababu wao walikuwa wanazikataa Aya za Allah na wakiwaua Mitume kwa dhuluma na hayo ni kwa sababu wao waliasi na walikuwa wakichupa mpaka. 3:113. Wote Si sawa! Miongoni mwa watu wa Kitabu wapo wenye kusimama imara na wao huzisoma Aya za Allah nyakati za usiku na huswali. 3:114. Wao wanamuamini Allah na Siku ile ya Mwisho na huamrishana mema na hukatazana mabaya na hukimbilia yaliyo mazuri na hao ni miongoni mwa waliyo wema. 3:115. Na wale ambao watafanya mazuri, wao hawatanyimwa jaza yao na Allah Yu Mwenye Kuwajua waliyo wacha Mungu. 3:116. Kwa wale waliyo makafiri, mali zao na watoto wao hawatawaondolea wao kitu katika (adhabu ya) Allah. Na hao ndio watu wa Motoni wao humo wataishi. 3:117. Mfano wa vile ambavyo wao (hao makafiri) hutumia katika maisha ya hii Duniya ni mfano wa upepo wenye baridi kali ambao umelipiga shamba la watu waliodhulumu nafsi zao na hivyo kuliteketeza. Na Allah Hakuwadhulumu wao, naam! Wao ndiyo waliodhulumu nafsi zao.
3:118. Enyi mliyoamini! Katu nyinyi msiwafanye wasiyokuwa Waislamu kuwa wandani wenu, katu wao hawataacha kutafuta njia ya kuwadhuru nyinyi. Wao wanatamani sana yale yanayokutaabisheni nyinyi. Zimekwisha dhihiri chuki katika matamshi yao na walichoficha katika nyoyo zao ni kikubwa zaidi. Sisi Tumekwisha kubainishieni nyinyi Aya Zetu ikiwa nyinyi ni wenye hekima. 3:119. Tazama! Nyinyi ndio mnawapenda wao na katu wao hawakupendeni nyinyi japo nyinyi mnaviamini Vitabu vyote. Pale wao wanapokutana na nyinyi wao husema; Sisi tumeamini na pale wao wanapokuwa peke yao wao hukuumieni nyinyi vyanda kwa hasira dhidi yenu. Wewe sema; Kufeni na hasira zenu! Allah Yu Mwenye Kuyajua yote yaliyo nyoyoni.

60

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:102. Enyi mliyoamini! Mcheni Allah kwa uchaji Anaostahiki na katu nyinyi msife ila nyinyi ni waislamu. 3:103. Na kwa pamoja mshike kwa nguvu kamba ya Allah na katu nyinyi msigawanyike kati yenu. Na mzikumbuke neema za Allah zilizo juu yenu nyinyi pale palipokuwa na uadui miongoni mwenu nyinyi, basi, Yeye Akaunganisha nyoyo zenu kwa huruma Yake; Mkawa ndugu (katika Dini) na nyinyi mlikuwa kwenye ukingo wa shimo la Moto na Yeye Akakuokoeni nyinyi nao. Hivi ndivyo Allah Anavyokufafanulieni nyinyi Aya Zake huenda nyinyi mkapata uwongofu. 3:104. Na liwepo kundi miongoni mwenu nyinyi litakaloalika watu kwenye yale yaliyo mema na kuamrisha mambo ya haki na kukataza yale yaliyo mabaya. Na hao ndio wale watakaopata kustawi. 3:105. Na katu nyinyi msiwe kama wale ambao waligawanyika na kukhitilafiana miongoni mwao baada ya kuwajia wao hoja zilizo bayana. Na kwa ajili yao iko adhabu kubwa kabisa. 3:106. Siku ambayo baadhi ya nyuso zitakuwa nyeupe Pe na nyingine nyeusi tii. Halafu wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi tii (wataambiwa); Nyinyi mlikuwa makafiri baada ya kuikubali imani? basi, sasa ionjeni adhabu ikiwa ni malipo kwa ukafiri wenu. 3:107. Na kwa wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe Pe, wao watakuwa katika rehema ya Allah (yaani Peponi) wao wataishi humo. 3:108. Hizi ni Aya za Allah ambazo Sisi Tunazisoma juu yako wewe sawasawa. Na Allah Hapendi dhuluma kwa walimwengu.

3:109. Na kwa Allah-Subhaanahu wa taala ni milki ya vyote vilivyo mbinguni na vyote vilivyo katika ardhi. Na kwa Allah tu ndio marejeo ya mambo yote. 3:110. Nyinyi (waislamu) ndio umati uliyo bora mliyoinuliwa kwa manufaa ya watu. Nyinyi mnaamrishana yale yaliyo mema na mnakatazana yaliyo mabaya na mnamuamini Allah. Lau watu wa Kitabu nao pia wangeamini, basi, ingelikuwa bora kwao. Baadhi yao ni waislamu na wengi wao ni makafiri. 3:111. Wao hawawezi kuwadhuru nyinyi kitu ila adha tu! Na ikiwa wao watapigana nanyi, basi, wao watakupeni nyinyi migongo kisha wao hawatasaidiwa.

59

3. Suuratul Aali Imraan

(Juzuu ya nne : Q3:92-Q4:23)

Lan Tanaluu.

3:92. Katu nyinyi hamtoufikia wema mpaka kwanza nyinyi mtoe vile ambavyo nyinyi mnavipenda. Na chochote kile mnachotoa ni chenye kujulikana kwa AllahSubhaanahu wa taala. 3:93. Vyakula vyote vilikuwa halali kwa wana wa Israili ila vile ambavyo Yaaqub alijizuwiya mwenyewe kabla ya kuteremshwa kwa Taurati. Wewe sema; Ileteni Taurati (Torah) na muisome ikiwa nyinyi ni msemao kweli. 3:94. Kisha baada ya hapo! Yeyote atakayezua uwongo juu ya Allah-Subhaanahu wa taala, basi, hao ndio wale waliyo madhalimu. 3:95. Wewe sema; Allah-Subhaanahu wa taala tu Ndiye Kweli. Na hivyo nyinyi fuateni mila ya Ibrahimu aliyejitenga mbali kabisa na uzushi wote (wa kuabudu masanamu) na yeye hakuwa miongoni mwa washirikina. 3:96. Kwa hakika nyumba ya kwanza miongoni mwa zilizokusudiwa kwa ajili ya ibada za watu ni ile ambayo iko Makka iliyojaa baraka na mwongozo kwa walimwengu wote. 3:97. Humo mna ishara bainifu; Mahali aliposimama Ibrahimu. Na yeyote anayeingia huwa salama. Na kwa kumtukuza Allah ni wajibu juu ya watu kwenda kuhiji kwenye hiyo nyumba (ya al-Kaaba) kwa yule mwenye uwezo. Na yeyote anayekataa, basi, Allah-Subhaanahu wa taala ni Mkwasi juu mahitaji yote kwa walimwengu. 3:98. Wewe sema; Enyi watu wa Kitabu! Kwa nini nyinyi hamzikubali Aya za Allah na hali ya kuwa yote mnayotenda ni mbele Yake? 3:99. Wewe sema; Enyi watu wa Kitabu! Kwa nini nyinyi mnazuwiya wale ambao wameamini njia ya Allah mkitamani kuipotoa na hali ya kuwa nyinyi ni mashahidi kwa hilo? Na Allah Si mghafilika wa yote yale mnayotenda. 3:100. Enyi mliyoamini! Ikiwa nyinyi mtawatii baadhi ya watu wa Kitabu, basi, wao watakufanyeni nyinyi kuwa makafiri baada ya imani yenu.
3:101. Na iweje nyinyi mkufuru wakati Aya za Allah zinasomwa kwenu nyinyi na miongoni mwenu nyinyi yuko Mtume wa Allah? Na yeyote anayetafuta msaada wa Allah tayari yeye amekwishaongozwa kwenye njia yenye kunyooka.

58

QURANI TUKUFU
kanzul Iman
(Khazina ya Imani)

na Imam Ahmad Raza Qadri Rahmatullah Alayhi

Iliyotarjumiwa katika lugha ya Kiingereza na Prof. Sayyid Shah Faridul Haque

na kutarjumiwa katika lugha ya kiswahili na Maalim. Yusufu Rajabu Kanyama.

You might also like