You are on page 1of 4

CATHOLIC DIOCESE OF NAKURU LAY APOSTOLATE OFFICE COMMISSIONING RITE-CATHOLIC WOMEN

ASSOCIATION KUONGEZA NGUVU KATIKA IMANI

KIONGOZI-Baba Askofu/ Kasisi, wanawake walio

hapa mbele yako ni washiriki wakatoliki, waliohudhuria karakana za mafundisho ya chama cha
wanawake wakatoliki kwa muda wa wiki sita, kama inavyo ratibishwa na afisi ya kichungaji, idara ya
walei. Baada ya kuhojiwa na Baba paroko na kukubarika, nakuomba wapokelewe na kuidhinishwa katika
umoja wa chama cha wanawake wakatoliki.

ASKOFU/KASISIS-Basi ninyi wanawake wakatoliki,

jiwekeni chini yake Mwenyezi

Mungu mpingeni shetani na

mambo yake yote, naye atawakimbieni.

Mkaribieni Mungu, naye

atawabariki ninyi, na kwa nia yenu ya kukesha,

wekeni tumaini lenu lote, katika Baraka mtakayopewa wakati Kristu

atakapo rudi tena. AMINA.

ASKOFU/KASISI- Basi mbele ya jumuiya hii ya wakristo, yaka taeeni yafutayo.

- Je, uko tayari kutohusika na

matengano katika familia? NIKO TAYARI.

- Je, uko tayari kulinda na kuheshimu ndoa zenu na za wengine?

NIKO TAYARI.

- Je, uko tayari kujiepusha na ulevi, ulafi, fitina na masengenyo?

NIKO TAYARI.

- Je, uko tayari kujiepusha na ushauli wa waganga, hirizi, na wapiga ramli?

NIKO TAYARI.

ASKOFU KASISI - Nanyi Wasimamizi, Je, mko tayari kuwasaidia wanawake hawa kuepuka
na hayo yote na pia kutimiza wajibu wao katika chama na familia zao.

NIKO TAYARI.

ASKOFU KASISI - Kwa kutii ukweli wa Mungu zitakaseni roho zenu na kushuhudia Kristu katika maisha
yenu, na kama watoto wa Mungu wenye utiifu, msikubali kamwe kuzifuata tena tamaa mbaya
mlizozikataa sasa hivi, muutii ukweli wa Mungu, mkizitakasa roho zenu na kushuhudia Mungu wa kweli
baba wa Bwana wetu Yesu Kristu. AMINA.

KUBARIKI-BIBILIA> MISHUMAA> CHUMVI VITAMBAA.

ASKOFU KASISI- Ee Mungu unavitakasa vitu vyote

kwa neno lako, ubariki mishumaa hii+ na vitambaa hizi+ Bibilia hizi+ na chumvi hii+, na kila atakaye
Zitumia kama unavyo amuru, au unavyotaka WEWE, akuomba pamoja na kukushukuru apate afya
mwilini na usalama rohoni; kwako WEWE uliye asili ya Baraka zote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu
Bwana wetu.

AMINA

ASKOFU/KASISI- wanawake katika chama; pokeeni neno la Mungu.

Wote -

Tumshukuru Mungu

ASKOFU/KASISI- wanawake katika chama, pokeeni mwanga wa Kristu. AMINA

(wanawake wanawasha

mishumaa)

WOTE-Mwenyezi Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu.

ASKOFU KASISI- Mmepewa mwanga huu mpate

kuulinda, maneno na matendo yenu yaweze kuwa mwanga kwa wote mnaoishi nao; na pia wale mtakao
kutana nao; ambatana na Bwana Mungu wala usimwache

kamwe, nawe utafanikiwa mwishoni mwa maisha yako; na hivyo mwishoni huko mbinguni ninyi na
watakatifu wote muweze kumlaki Bwana. AMINA.
ASKOFU/ KASISI- ninyi ni chumvi ya ulimwengu; mumeitwa katika chama ili kuponya, kuhifadhi na kutia
ladha maisha ya imani; pamoja na wale wengine wote mtakao kutana nao; kwa Kristu Bwana wetu.
AMINA.

ASKOFU/KASISI- pokeeni vitambaa hivi kama ishara ya usafi wa mioyo yenu na cheo chenu katika chama
na familia. AMINA. vitambaa)

(wanawake wanafunga

ASKOFU KASISI- Je; unaahidi kushirikiana na kuwaheshimu wachungaji wako wa kiroho, viongozi wa
chama na Kanisa? Naahidi.

- Je; unaahidi kumshuhudia Bikira Maria mama wa Mungu na kueneza sifa zake?

Naahidi.

- Je; una amini kwamba baada ya kuvikwa kitambaa cha uanachama;

umemwaamua Kristu? Naamini.

ASKOFU KASISI- basi, mkiweke kila wakati kikiwa

Safi mkisaidiwa na wanawake wenzenu hadi uzima wa milele Mbinguni. AMINA.

Wanawake- ni naapa ya kwamba, nikishindwa kutimiza maagizo ya chama nitarudisha

kitambaa hiki.

- Ikiwa nitakosa mara ya kwanza; mara ya pili, nitakubali kushauriwa na chama

- Ikiwa nitakosa mara ya tatu, nitasimamishwa kuwa mwana chama kwa muda wa

miezi sita; na ikiwa nitazidi kukosa

nitapelekwa kwa kamati kuu ya parokia kwa ushauli zaidi. Ee mama Bikira Maria, na Mtakatifu Monika

mlezi wa chama cha wanawake uniombee niweze kutimiza nilio ahidi.

(kuchoma yale

nimeahidi kuachana nayo)

SALA-Ee Mwenyezi-Mungu; Mungu wangu, Mimi mtumishi wako nakuomba unisikie na kunitimizia ombi
langu; ninalo omba leo, kwa Kristo Bwana wetu. AMINA.

ASKOFU KASISI- Mwenyezi-Mungu awape neema ya


kutunza Yale yote mliopewa, tunawaweka ninyi mikononi mwake Baba Mwenyezi; na Mwanawe wa
pekee, na Roho Mtakatifu, ili mfanye jumuiya ya wakristu

KIAPO

Wanawake- ni naapa ya kwamba, nikishindwa kutimiza maagizo ya chama nitarudisha

kitambaa hiki.

- Ikiwa nitakosa mara ya kwanza; mara ya pili, nitakubali kushauriwa na chama

- Ikiwa nitakosa mara ya tatu, nitasimamishwa kuwa mwana chama kwa muda wa

miezi sita; na ikiwa nitazidi kukosa

nitapelekwa kwa kamati kuu ya parokia kwa ushauli zaidi. Ee mama Bikira Maria, na Mtakatifu Monika

mlezi wa chama cha wanawake uniombee niweze kutimiza nilio ahidi.

(kuchoma yale

nimeahidi kuachana nayo)

SALA-Ee Mwenyezi-Mungu; Mungu wangu, Mimi mtumishi wako nakuomba unisikie na kunitimizia ombi
langu; ninalo omba leo, kwa Kristo Bwana wetu. AMINA.

ASKOFU KASISI- Mwenyezi-Mungu awape neema ya

kutunza Yale yote mliopewa, tunawaweka ninyi mikononi mwake Baba Mwenyezi; na Mwanawe wa
pekee, na Roho Mtakatifu, ili mfanye jumuiya ya wakristu

ipendezwe nanyi; na Mungu mwenye rehema na neema ayalinde maisha yenu; na watakieni ninyi note
hekima ya Bwana wetu Yesu Kristu. AMINA.

Nendeni na amani ya Kristu Bwana wetu.

Wote-Tumshukuru Mungu.

You might also like