You are on page 1of 7

MAMBO 5 YATAKAYOKUSAIDIA KUONGEZA UFAHAMU JUU YA UTENDAJI WA

DAMU YA YESU

Katika ulimwengu wa roho nguvu za mtu huongezeka kwa kadiri mtu


anapofahamu jambo Fulani,yaani hii ni kusema kuwa ufahamu hukufanya kuwa
mwenye nguvu na kuwa na nguvu kutakufanya kutenda Makuu, Biblia inasema

𝒅𝒂𝒏𝒊𝒆𝒍 11:32
𝑵𝒂 𝒘𝒂𝒐 𝒘𝒂𝒇𝒂𝒏𝒚𝒂𝒐 𝒎𝒂𝒐𝒗𝒖 𝒋𝒖𝒖 𝒚𝒂 𝒉𝒊𝒍𝒐 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐 𝒂𝒕𝒂𝒘𝒂𝒑𝒐𝒕𝒐𝒔𝒉𝒂 𝒌𝒘𝒂
𝒎𝒂𝒏𝒆𝒏𝒐 𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒋𝒊𝒑𝒆𝒏𝒅𝒆𝒌𝒆𝒛𝒂; 𝒍𝒂𝒌𝒊𝒏𝒊 𝒘𝒂𝒕𝒖 𝒘𝒂𝒎𝒋𝒖𝒂𝒐 𝑴𝒖𝒏𝒈𝒖 𝒘𝒂𝒐
𝒘𝒂𝒕𝒂𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒉𝒐𝒅𝒂𝒓𝒊, 𝒏𝒂 𝒌𝒖𝒕𝒆𝒏𝒅𝒂 𝒎𝒂𝒎𝒃𝒐 𝒎𝒂𝒌𝒖𝒖.

neno kujua katika biblia humaanisha mahusiano au intimacy kwa kiingereza na


kujua huku kuchochewa na kuwa na ufunuo juu ya jambo Fulani,unapojua jambo
Fulani katika ufunuo unafanyika kuwa mtu mkuu anayetenda makuu hii ndio
sababu ukisoma mathayo 16:18 utaona ule ufunuo ambao petro alikuwa nao juu
ya Yesu ni nani ulimpa kuwa na nafasi ya kuwa mmoja wa wajenzi wa kanisa lenye
Nguvu ambalo malango ya kuzimu hayataliweza.

basi kwa msingi huo tunaweza kufahamu sasa ya kuwa kiwango cha utendaji kazi
wa damu ya Yesu hutegemeana na kujua kwa ufunuo ulionao,Damu ya Yesu ni
damu isiyo na ukomo katika utendaji wake na ni moja kati ya funguo kuu katika
Ufalme wa Mungu,ukomo wa nguvu za Damu ya Yesu ni matokeo ya ufunuo ulio
nao na kule kujua Damu ya Yesu.

kama kujua kwako kwa ufunuo wa Damu ya Yesu ni katika kusamehe dhambi basi
hutaweza kuitumia katika uponyaji hata kama umsikia na unafahamu kuwa damu
ya Yesu inaponya, ninachotaka kukuonesha hapa ni kuwa haitoshi wewe
kufahamu kuhusu damu,unahitaji kuijua kwa namna ya ufunuo( mahusiano +
ufunuo)

Mdo 19:11-20
𝑩𝒂𝒂𝒅𝒉𝒊 𝒚𝒂 𝑾𝒂𝒚𝒂𝒉𝒖𝒅𝒊 𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒌𝒖𝒕𝒂𝒏𝒈𝒂-𝒕𝒂𝒏𝒈𝒂, 𝒏𝒂𝒐 𝒏𝒊 𝒘𝒂𝒑𝒖𝒏𝒈𝒂 𝒑𝒆𝒑𝒐,
𝒘𝒂𝒌𝒂𝒋𝒂𝒓𝒊𝒃𝒖 𝒌𝒖𝒕𝒂𝒋𝒂 𝒋𝒊𝒏𝒂 𝒍𝒂 𝑩𝒘𝒂𝒏𝒂 𝒀𝒆𝒔𝒖 𝒋𝒖𝒖 𝒚𝒂𝒐 𝒘𝒂𝒍𝒊𝒐𝒑𝒂𝒈𝒂𝒘𝒂 𝒏𝒂
𝒑𝒆𝒑𝒐 𝒘𝒂𝒄𝒉𝒂𝒇𝒖, 𝒘𝒂𝒌𝒊𝒔𝒆𝒎𝒂, 𝑵𝒂𝒘𝒂𝒂𝒑𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒀𝒆𝒔𝒖, 𝒚𝒖𝒍𝒆
𝒂𝒏𝒂𝒚𝒆𝒉𝒖𝒃𝒊𝒓𝒊𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝑷𝒂𝒖𝒍𝒐. 14𝑾𝒂𝒍𝒊𝒌𝒖𝒘𝒂𝒌𝒐 𝒘𝒂𝒏𝒂 𝒔𝒂𝒃𝒂 𝒘𝒂 𝒎𝒕𝒖 𝒎𝒎𝒐𝒋𝒂
𝑺𝒌𝒆𝒘𝒂, 𝑴𝒚𝒂𝒉𝒖𝒅𝒊, 𝒌𝒖𝒉𝒂𝒏𝒊 𝒎𝒌𝒖𝒖, 𝒘𝒂𝒍𝒊𝒐𝒇𝒂𝒏𝒚𝒂 𝒉𝒊𝒗𝒚𝒐. 15𝒀𝒖𝒍𝒆 𝒑𝒆𝒑𝒐
𝒎𝒄𝒉𝒂𝒇𝒖 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒋𝒊𝒃𝒖, 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒂𝒎𝒃𝒊𝒂, 𝒀𝒆𝒔𝒖 𝒏𝒂𝒎𝒋𝒖𝒂 𝒏𝒂 𝑷𝒂𝒖𝒍𝒐
𝒏𝒂𝒎𝒇𝒂𝒉𝒂𝒎𝒖, 𝒍𝒂𝒌𝒊𝒏𝒊 𝒏𝒊𝒏𝒚𝒊 𝒏𝒊 𝒏𝒂𝒏𝒊? 16𝑵𝒂 𝒚𝒖𝒍𝒆 𝒎𝒕𝒖 𝒂𝒍𝒊𝒚𝒆𝒑𝒂𝒈𝒂𝒘𝒂 𝒏𝒂
𝒑𝒆𝒑𝒐 𝒎𝒄𝒉𝒂𝒇𝒖 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒓𝒖𝒌𝒊𝒂 𝒘𝒂𝒘𝒊𝒍𝒊, 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒘𝒆𝒛𝒂, 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒔𝒉𝒊𝒏𝒅𝒂, 𝒉𝒂𝒕𝒂
𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒐𝒌𝒂 𝒎𝒃𝒊𝒐 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒏𝒚𝒖𝒎𝒃𝒂 𝒊𝒍𝒆 𝒉𝒂𝒍𝒊 𝒘𝒂 𝒖𝒄𝒉𝒊 𝒏𝒂 𝒌𝒖𝒋𝒆𝒓𝒖𝒉𝒊𝒘𝒂.

utaona hawa vijana si kwamba hawakuwa na ufahamu juu ya jina la


yesu,ufahamu walikuwa nao na ndio sababu unaona wanasema “kwa jina la Yesu
yule anayehubiriwa na Paulo” ,kwa hiyo waliufahamu uweza wa jina la Yesu lakini
hawakuwa na kujua kwa ufunuo yaani hawakuwa na mahusiano na mwenye jina
wala ufunuo wa Jina la Yesu
vivyo hivyo unaweza kuwa na ufahamu wa damu ya Yesu lakini ukikosa kujua kwa
ufunuo hauwezi kupata maajabu yaliyo ndani ya damu ya Yesu
sasa tuangalie Damu ya Yesu

𝟏. 𝐃𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐘𝐄𝐒𝐔 𝐍𝐈 𝐃𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐍𝐎 𝐉𝐈𝐏𝐘𝐀

Neno agano Tafsiri yake ni makubaliano ya kimkataba baina ya pande mbili au


Zaidi na makubaliano haya yanakuwa na vipengele vya kiutekelezaji kati ya pande
hizo zinazoingia makubaliano.
lakini pia kila mkataba ili uwe imara, mbali na makubaliano nil lazima kuwepo kwa
Muhuli unaoonesha uhakika wa makubaliano,tunaweza tukasema Nguvu ya
mkataba ni Muhuri unaotambulika na chombo chenye Nguvu ya kisheria.

Damu ya Yesu ni Damu ya agano jipya ,damu yenyewe sio agano jipya isipokuwa
ndio Nguvu ya agano jipya

katika mambo ya kiroho Damu imetumika kama muhuri wa kila makubaliano kati
ya pande mbili,iwe kati ya Mungu na wanadamu au kati ya shetani na wanadamu.
hii ni kwa sababu ya ile Nguvu ya uhai iliyomo ndani ya Damu husika
Katika Agano la kale,Damu iliyotumika kuweka agano ilikuwa ni damu ya
Wanyama,ambayo nguvu yake ya kiutendaji ilidumu kwa mwaka mmoja na baada
ya mwaka ilihitajike kuweka agano tena,ndio sababu Biblia inasema agano la kale
ni agano Dhaifu kwa sababu hata damu yake ilikuwa dhaifu na kwa sababu hiyo
haikuwezekana kuleta utimilifu wa ahadi zile.

𝑬𝒃𝒓 8:7
𝑴𝒂𝒂𝒏𝒂 𝒌𝒂𝒎𝒂 𝒍𝒊𝒍𝒆 𝒍𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒏𝒛𝒂 𝒍𝒊𝒏𝒈𝒂𝒍𝒊𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒉𝒂𝒍𝒊𝒏𝒂 𝒖𝒑𝒖𝒏𝒈𝒖𝒇𝒖, 𝒏𝒂𝒇𝒂𝒔𝒊
𝒊𝒔𝒊𝒏𝒈𝒂𝒍𝒊𝒕𝒂𝒇𝒖𝒕𝒘𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒍𝒊𝒍𝒆 𝒍𝒂 𝒑𝒊𝒍𝒊. 𝑴𝒂𝒂𝒏𝒂, 𝒂𝒘𝒂𝒍𝒂𝒖𝒎𝒖𝒑𝒐, 𝒂𝒔𝒆𝒎𝒂….

kwa lugha rahisi ni wenzetu wa agano la kale hawakuweza kufurahia uzuri wa


ahadi za Mungu kikamilifu kwa sababu ya nguvu iliyosimamia makubaliano yao ya
kimkataba kuwa dhaifu na hii ndio sababu Pamoja na kuwa na agano bado shetani
aliwafunga katika mateso.
lakini sasa BWANA anasema

𝑬𝒃𝒓 8:8
𝑨𝒏𝒈𝒂𝒍𝒊𝒂, 𝒔𝒊𝒌𝒖 𝒛𝒊𝒏𝒂𝒌𝒖𝒋𝒂, 𝒂𝒔𝒆𝒎𝒂 𝑩𝒘𝒂𝒏𝒂,
𝑵𝒂𝒎𝒊 𝒏𝒊𝒕𝒂𝒘𝒂𝒕𝒊𝒎𝒊𝒛𝒊𝒂 𝒏𝒚𝒖𝒎𝒃𝒂 𝒚𝒂 𝑰𝒔𝒓𝒂𝒆𝒍𝒊 𝒏𝒂 𝒏𝒚𝒖𝒎𝒃𝒂 𝒚𝒂 𝒀𝒖𝒅𝒂 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐
𝒋𝒊𝒑𝒚𝒂;

Agano hili jipya ni makubaliano mapya kati ya Mungu na wanadamu ni


makubaliano ya kimkataba yaliyobeba ahadi zilizobora na kupigwa Muhuri na
damu yenye thamani na inayoshinda damu zote yaani Damu ya Yesu Kristo

𝒎𝒂𝒕𝒂𝒚𝒐 26:28
𝒌𝒘𝒂 𝒎𝒂𝒂𝒏𝒂 𝒉𝒊𝒊 𝒏𝒅𝒊𝒚𝒐 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒚𝒂𝒏𝒈𝒖 𝒚𝒂 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐, 𝒊𝒎𝒘𝒂𝒈𝒊𝒌𝒂𝒚𝒐 𝒌𝒘𝒂 𝒂𝒋𝒊𝒍𝒊
𝒚𝒂 𝒘𝒆𝒏𝒈𝒊 𝒌𝒘𝒂 𝒐𝒏𝒅𝒐𝒍𝒆𝒐 𝒍𝒂 𝒅𝒉𝒂𝒎𝒃𝒊.

Damu ya Yesu imelifanya agano jipya kuwa bora Zaidi na lenye uhakika wa
kiutekelezaji,maana yake chochote ambacho Mungu amekuahidi ya kwamba
atakupa unakuwa na uhakika ya kwamba utapokea. hii ni kwa sababu Nguvu
iliyonyuma ya ahadi hizo za kiagano ni Damu ya Mungu mwenyewe aliyekuahidi
lakini pia mjumbe na msimamizi si Malaika na mwanadamu kama ilivyokuwa
katika agano la kale Bali ni Yesu Kristo Mungu mwenyewe.

Kwa ule uthamani na Nguvu ya Damu ya Yesu kila agano ambalo limewekwa
kinyume chako na mashetani linavunjika ndio maana biblia inasema

𝑹𝒖𝒎 8:1-2 𝑺𝑼𝑽


𝑺𝒂𝒔𝒂, 𝒃𝒂𝒔𝒊, 𝒉𝒂𝒌𝒖𝒏𝒂 𝒉𝒖𝒌𝒖𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒂𝒅𝒉𝒂𝒃𝒖 𝒋𝒖𝒖 𝒚𝒂𝒐 𝒘𝒂𝒍𝒊𝒐 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝑲𝒓𝒊𝒔𝒕𝒐
𝒀𝒆𝒔𝒖. 𝑲𝒘𝒂 𝒔𝒂𝒃𝒂𝒃𝒖 𝒔𝒉𝒆𝒓𝒊𝒂 𝒚𝒂 𝑹𝒐𝒉𝒐 𝒘𝒂 𝒖𝒛𝒊𝒎𝒂 𝒖𝒍𝒆 𝒖𝒍𝒊𝒐 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝑲𝒓𝒊𝒔𝒕𝒐
𝒀𝒆𝒔𝒖 𝒊𝒎𝒆𝒏𝒊𝒂𝒄𝒉𝒂 𝒉𝒖𝒓𝒖, 𝒎𝒃𝒂𝒍𝒊 𝒏𝒂 𝒔𝒉𝒆𝒓𝒊𝒂 𝒚𝒂 𝒅𝒉𝒂𝒎𝒃𝒊 𝒏𝒂 𝒎𝒂𝒖𝒕𝒊.
maana yake ni hii hakuna hukumu itokanayo na adhabu ya kutotimiza vipengele
vya maagano ya mababu na mabibi na wahenga waliopita juu yao walio katika
agano la Kristo Yesu kwa kuwa Sheria ya agano la Roho wa Uzima( 𝐃𝐚𝐦𝐮 𝐲𝐚
𝐘𝐞𝐬𝐮: 𝐝𝐚𝐦𝐮 𝐧𝐢 𝐮𝐡𝐚𝐢 𝐧𝐚 𝐮𝐡𝐚𝐢 𝐧𝐢 𝐫𝐨𝐡𝐨) ulio katika Kristo Yesu umeniacha hutu
mbali na sheria ya Dhambi na Mauti.

kwa sababu hiyo huna haja ya kuogopa maagano ama laana kwa sababu
unapookoka na kuachilia damu ya Yesu sawa sawa kila agano linavunjika na kila
laana inafutwa,huku ikikuacha huru ukifurahia uzima wa milele.

2. 𝐃𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐘𝐄𝐒𝐔 𝐍𝐈 𝐃𝐀𝐌𝐔 𝐈𝐍𝐀𝐘𝐎𝐍𝐄𝐍𝐀 𝐌𝐄𝐌𝐀

𝑬𝒃𝒓 12:24 𝑺𝑼𝑽


𝒏𝒂 𝒀𝒆𝒔𝒖 𝒎𝒋𝒖𝒎𝒃𝒆 𝒘𝒂 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐 𝒋𝒊𝒑𝒚𝒂, 𝒏𝒂 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒏𝒚𝒖𝒏𝒚𝒊𝒛𝒘𝒂,
𝒊𝒏𝒆𝒏𝒂𝒚𝒐 𝒎𝒆𝒎𝒂 𝒌𝒖𝒍𝒊𝒌𝒐 𝒊𝒍𝒆 𝒚𝒂 𝑯𝒂𝒃𝒊𝒍𝒊.

Damu ya Yesu ni Damu inayo nena,hii inamaana zipo damu zisizonena na pia zipo
damu zinazonena mabaya.
katika aina za Damu damu za watu ni Damu ambazo huongea hata kama mtu
mwenyewe hajasema chochote damu yake huongea kwa sababu ndani ya damu
kuna nafsi ambayo ndio inayosukuma maongezi katika mwili
hivyo damu ya mtu inapomwagwa isivyosawa hulia na inanena mabaya mbele za
Mungu

ufunuo 6:9
𝑵𝒂 𝒂𝒍𝒊𝒑𝒐𝒖𝒇𝒖𝒏𝒈𝒖𝒂 𝒎𝒉𝒖𝒓𝒊 𝒘𝒂 𝒕𝒂𝒏𝒐, 𝒏𝒊𝒌𝒂𝒐𝒏𝒂 𝒄𝒉𝒊𝒏𝒊 𝒚𝒂 𝒎𝒂𝒅𝒉𝒂𝒃𝒂𝒉𝒖
𝒓𝒐𝒉𝒐 𝒛𝒂𝒐 𝒘𝒂𝒍𝒊𝒐𝒄𝒉𝒊𝒏𝒋𝒘𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒂𝒋𝒊𝒍𝒊 𝒚𝒂 𝒏𝒆𝒏𝒐 𝒍𝒂 𝑴𝒖𝒏𝒈𝒖, 𝒏𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒂𝒋𝒊𝒍𝒊 𝒚𝒂
𝒖𝒔𝒉𝒖𝒉𝒖𝒅𝒂 𝒘𝒂𝒍𝒊𝒐𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂𝒐. 𝑾𝒂𝒌𝒂𝒍𝒊𝒂 𝒌𝒘𝒂 𝒔𝒂𝒖𝒕𝒊 𝒌𝒖𝒖, 𝒘𝒂𝒌𝒊𝒔𝒆𝒎𝒂, 𝑬𝒆
𝑴𝒐𝒍𝒂, 𝑴𝒕𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊𝒇𝒖, 𝒏𝒂 𝑴𝒌𝒘𝒆𝒍𝒊, 𝒖𝒕𝒂𝒌𝒂𝒘𝒊𝒂 𝒉𝒂𝒅𝒊 𝒍𝒊𝒏𝒊 𝒌𝒖𝒉𝒖𝒌𝒖𝒎𝒖 𝒏𝒂
𝒌𝒖𝒊𝒍𝒊𝒑𝒂 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒚𝒆𝒕𝒖 𝒌𝒘𝒂 𝒉𝒂𝒐 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒂𝒐 𝒋𝒖𝒖 𝒚𝒂 𝒏𝒄𝒉𝒊?
hivyo basi wakati wowote unapomwaga damu ya Mtu isivyosawa unatakiwa
kukumbuka kuwa damu hiyo inazungumza kisasi kinyume chako na watu wa
damu yako
umewahi kukutana na familia ambazo wanakuwa na vifo mfulilizo,sehemu kubwa
ya aina hiyo ya vifo ni mapatilizo yatokanayo na umwagaji damu ambao unaweza
ukawa ulifanywa na mtu mwingine ndani ya familia.

aina nyingine ya Damu ni Damu za Wanyama,hii ni aina ya damu ambayo haisemi


chochote inapomwagwa kwa sababu haina nafsi bali inaweza kuwekewa maneno
na yule anae imwaga,huwa ninaziita Damu zilizo wazi.

𝑲𝒖𝒕 24:8 𝑺𝑼𝑽


𝑴𝒖𝒔𝒂 𝒂𝒌𝒂𝒊𝒕𝒘𝒂𝒂 𝒊𝒍𝒆 𝒅𝒂𝒎𝒖, 𝒂𝒌𝒂𝒘𝒂𝒏𝒚𝒖𝒏𝒚𝒊𝒛𝒊𝒂 𝒘𝒂𝒕𝒖, 𝒂𝒌𝒂𝒔𝒆𝒎𝒂, 𝑯𝒊𝒊
𝒏𝒅𝒊𝒚𝒐 𝒅𝒂𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐 𝒂𝒍𝒊𝒍𝒐𝒍𝒊𝒇𝒂𝒏𝒚𝒂 𝑩𝑾𝑨𝑵𝑨 𝒑𝒂𝒎𝒐𝒋𝒂 𝒏𝒂𝒏𝒚𝒊 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂
𝒎𝒂𝒏𝒆𝒏𝒐 𝒉𝒂𝒚𝒂 𝒚𝒐𝒕𝒆.

nguvu ya utimilifu wa yale maneno ni nguvu ya nafsi ya yule anayeongea wakati


akiimwaga hiyo damu.

sasa Basi Damu Ya Yesu Ni damu inayonena nayo kwa sababu ni damu iliyobeba
Nafsi ya Yesu na Biblia inasema damu ya Yesu inanena Mema, Tunapoipokea na
kuitumia ipasavyo kila maneno yaliyonenwa kinyume chetu hufutwa Kwa yale
maneno mema ya Yesu.
haijalishi ni maneno gani na yamenenwa katika mzingira gani,Damu ya Yesu
inapoachiliwa hufuta kabisa hayo maneno yaletayo laana juu yako.

Bwana MUNGU akubariki utakapoendelea kufuatilia mafundisho haya


kwa Maswali unaweza ukaandika hapa au tutumie Ujumbe +255757370010
𝗨𝗸𝗶𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗞𝘂𝘀𝗮𝗽𝗼𝗿𝘁 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝗞𝘄𝗮 𝗡𝗷𝗶𝗮 𝘆𝗮 𝘀𝗮𝗱𝗮𝗸𝗮 𝗡𝗮𝗺𝗯𝗮 𝘇𝗲𝘁𝘂 𝗻𝗶 𝗵𝗶𝘇𝗶
+𝟮𝟱𝟱𝟳𝟱𝟳𝟯𝟳𝟬𝟬𝟭𝟬
+𝟮𝟱𝟱𝟳𝟭𝟯𝟯𝟳𝟭𝟴𝟭𝟵

You might also like