Professional Documents
Culture Documents
Salam, Malkia! Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam!
Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika
huku bondeni kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho
yako ya huruma, Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa
tumbo lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu Bikira Maria.
Tendo la pili;
Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu;
Yesu anazaliwa Betlehemu.
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne;
Yesu anatolewa hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano;
Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Tendo la kwanza;
Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili;
Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu;
Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne;
Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano;
Yesu anakufa Msalabani.
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Tendo la kwanza;
Yesu anafufuka.
Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili;
Yesu anapaa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu;
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne;
Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano;
Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
Tendo la kwanza;
Yesu anabatizwa Mto Jordani.
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili;
Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.
Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu;
Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne;
Yesu anageuka sura.
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano;
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia.
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.