You are on page 1of 150

Very Matunda-0746194783

Kwanini muziki na pambano kuu?


Pambano kuu ni vita kati ya wema na uovu. Ambapo vita hii inapiganwa
ndani ya kila mmoja, Kristo akiwa kiongozi wa wema, huku shetani
akiwa kiongozi wa uovu.

Lengo la somo hili ni kuangalia muziki unahusianaje na hili pambano, je


ni silaha moja wapo ambayo tunaweza tukaitumia kulishinda hili
pambano kama tumeamua kuwa upande wa Kristo kiongozi wa wema.
Lakini je shetani naye anatumiaje muziki kama silaha ya kutuangusha
katika pambano hili.

Very Matunda-0746194783
1Wathesolenike 5:21
jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;
Prove all things; hold fast that which is good. (KJV)

Very Matunda-0746194783
1. Muziki ni nini?
2. Muziki unaundwa na nini?
3. Kwanini Mungu aanzishe muziki?
4. Je shetani ameuacha muziki kama ulivyoanzishwa na Mungu?
5. Wimbo ni nini?
6. Kuna tafauti gani kati ya wimbo na muziki?
7. Ni mambo gani ya kuzingatia katika uimbaji?
8. Muziki unamahusiano yeyote na ubongo, kama yapo ni yapi?
9. Sayansi inasemaje kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya muziki na ubongo?
10. Contemporary Christian music (CCM) ni nini?
11. Je muziki una lugha ya mwili (body language)?
12. Kati ya muziki na mashairi kipi cha muhimu?
13. Muongozo wa kanisa unaongeleaje kuhusiana na muziki?
14. Utajuaje muziki ulio sahihi na usio sahihi?
Vyote hivi tutaviangalia ndani ya somo hili la MUZIKI NA PAMBANO KUU.
Very Matunda-0746194783
Vitu tutakavyotumia katika kujifunza;

Biblia inasema, 2wakoritho13.1 “…Kwa vinywa vya mashahidi


wawili au watatu kila neno litathibitishwa.” Hivyo yote tutakayo
jifunza hapa yatathibitishwa na,
1. Biblia
2. Roho ya unabii.
3. Vyanzo vingine kama vile wanasayansi, wasanii, wanafalsafa,
wataalamu wa muziki n.k

Very Matunda-0746194783
Muziki ni nini?
ni tungo zenye kufuata mapigo flani ya kimi za kiafukuzi yenye
mahadhi ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti (urari wa sauti)
na mpangilio maalum wa maneno.
or
Is the art of arranging sounds in time to produce composition through
the elements of melody, harmony, rhythm, and timbre.
or
A series of sounds organized in time, employing melody, harmony,
tempo etc. usually to convey a mood.

ZINGATIA: unapoongelea muziki unaongelea mpangilio wa sauti


na sio mashahiri(lyrics).
Very Matunda-0746194783
Muziki asili yake ni wapi?
Sefania 3:17 Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;
Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa
kuimba

“Muziki ni wa asili ya mbinguni...Sauti ya muziki ni moja ya zawadi za Mungu


kwa wanadamu” 3Selected message 334.4-5

“Uimbaji ni sehemu ya ibada ya Mungu mbinguni, nasi tungejaribu, kwa nyimbo


zetu kumsifu, kukaribia. Kadiri iwezekenavyo, ulinganifu wa sauti za waimbaji wa
mbinguni.” Kutayarisha Njia Uk.236

muziki asili yake ni mbinguni na Mungu mwenyewe ndio muasisi wa muziki.


Very Matunda-0746194783
Kwanini Mungu aanzishe muziki?

Very Matunda-0746194783
Makusudi ya Mungu kuanzisha muziki.
1. Kutimiza makusudi matakatifu.
“Muziki ulitengenezwa kutumikia makusudi matakatifu, kuyainua mawazo hadi
kuwa kitu safi, bora na kilicho juu, na kuamsha rohoni hali ya ibada na shukrani
kwa Mungu.” DA pg.594

“UFUNDI wa sauti tamu za nyimbo takatifu ulikuzwa daima (katika shule za


manabii). Hakuna ngoma ya upuzi iliyosikika wala wimbo hafifu ambao ungemsifu
mwanadamu na kupotosha akili kumwacha Mungu: bali zaburi takatifu za sifa kwa
Mwumbaji zenye kulitukuza jina lake na kuyasimulia matendo yake ya ajabu.
Hivyo muziki ulifanywa kulitimiza kusudi takatifu na kuyainua mawazo kwa kile
ambacho kilikuwa safi, bora na kikuu pamoja na kuamsha rohoni uchaji na moyo
wa shukrani kwa Mungu.”Kutayarisha Njia Uk.236
Very Matunda-0746194783
2. Kumtukuza yeye Mungu.
Zaburi 68:32 Enyi falme za dunia mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo.

3. Silaha dhidi ya kukata tamaa.


“kama kungekuwa na kumsifu Mungu Zaidi, na kuhuzunishwa kidogo na mambo
ya kukatisha tamaa, ushindi mwingi ungepatikana.” Evangelism, pg.499
“Tunapojaribiwa, badala ya kusema tunavyojisikia, hebu kwa imani tuimbe wimbo
wa kumshukuru Mungu……wimbo ni silaha ambayo tunaweza kuitumia daima
kushinda hali ya kukata tamaa.” The ministry of Healing p.254. (1905)

4. To Impress Spiritual Truth.


“Muziki ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuufikia moyo na kweli za kiroho. Mara
nyingi kwa maneno ya wimbo mtakatifu, chemchem za toba na Imani hufunuliwa.”
Review and Herald, June 6, 1912
Very Matunda-0746194783
5. Kumfukuza na kumshinda adui.
“Naliona kuwa kumtukuza Mungu kwa njia ya nyimbo mara nyingi kulimfukuza adui, na
kumsifu Mungu kulimfanya adui ashindwe kutusogelea na kulitupatia ushindi.” G. White.
Letter 5,1850. ]
“ Wakati kristo alipokuwa mtoto kama watoto hawa hapa, alijaribiwa kutenda dhambi,
lakini hakujitoa kwa majaribu. Alipokuwa mkubwa alijaribiwa, lakini nyimbo ambazo
mama yake kuimba zilikuja katika akili yake, na aliinua sauti yake katika sifa…Mungu
anataka tutumie kila kitu ambacho mbingu imetupatia kwa ajili ya kumpinga adui..”
Evangelism 498.2
“Nyimbo zake [christ] za sifa zilionekana kuwaondosha malaika waovu, na, kama uvumba
uliofukizwa, zilijaza mahali pale harufu nzuri. Mawazo ya watu waliomsikia
yalipandishwa kutoka katika mambo ya kidunia, na kupelekwa nyumbani pa juu
mbinguni.” Evangelism499.1

6. Kuifanya kazi ya kupendeza (To Make Work Pleasant).


“Ifanye kazi yako kuwa ya kupendeza kwa nyimbo za sifa.” Child Guidance, p.148.
“ Kwa nyimbo za shukrani aliburudisha [christ] masaa yake ya kazi, na kuleta furaha ya
mbinguni kwa wale waliovalia kazi na kuvunjika moyo.” evangelism 498.3
Very Matunda-0746194783
7. Kufundishia
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na
kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa
neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16
“Ni njia bora kabisa ya kuhifadhi Neno la Mungu katika kumbukumbu kwa kurudia-
rudia wimbo ambao huleta nguvu na uwezo mkubwa mno. Unaweza kudhibiti na
kutawala mazoea mabaya; una uwezo wa kuzalisha fikra na kuamsha huruma,
kukuza mwafaka wa kiutendaji, na kuondoa huzuni na hofu-mambo ambayo
yanaharibu ujasiri na kupunguza bidii ya kazi.” E. G. White. Msifuni Bwana kwa
Nyimbo, uk.01

8. Kutupatia nguvu ya kutenda mema.


“Muziki unaweza kufanywa kuwa nguvu kubwa kwa ajili ya wema; lakini hatutumii
vizuri kipengele hiki muhimu cha ibada.” Ujumbe kwa Vijana Uk.280

Very Matunda-0746194783
9. Kuwa ibada.
“ kuimba, kama sehemu ya ibada ya dini, ni tendo la ibada sawa na sala.”
Kutayarisha Njia Uk.236
“Kama sehemu ya huduma ya dini, uimbaji ni tendo la ibada sawa na maombi.
Kwa kweli nyimbo nyingi ni maombi. ” Ujumbe kwa Vijana Uk.276

10. Kutubariki.
“muziki, usipotumiwa vibaya, ni mbaraka mkubwa; lakini ukitumiwa vibaya, ni
laana ya ajabu.” Kutayarisha Njia Uk.237

11. Njia ya kukaribisha uwepo wa Mungu kwa mwanadamu.


“ Tufanye yote katika uwezo wetu kutengeneza muziki ndani ya nyumba zetu, ili
Mungu apate kuingia.” Evangelism 500.1
“Kwa sauti ya kuimba, alikaribisha [christ] mwanga wa asubuhi.” Evangelism 498.3
Very Matunda-0746194783
12. Kushikilia ushirika wetu na Mungu.
Alikuwa [christ] na ushirika na mbingu katika wimbo; na pindi wafanya-kazi
wenzake walipolalamika kuchoka katika kazi, waliburudishwa na sauti tamu ya
muziki uliotoka midomoni mwake. Nyimbo zake za sifa zilionekana kuwaondosha
malaika waovu, na, kama uvumba uliofukizwa, zilijaza mahali pale harufu nzuri.
Mawazo ya watu waliomsikia yalipandishwa kutoka katika mambo ya kidunia, na
kupelekwa nyumbani pa juu mbinguni. Evangelism 499.1

“ Lazima kuwe na uhusiano hai na Mungu katika maombi, uhusiano hai na Mungu
katika nyimbo za sifa na shukrani.” Evangelism 498.1

Very Matunda-0746194783
Ni vitu gani vinaunda muziki?

Very Matunda-0746194783
Muziki unaundwa na vitu vitatu;
1. Melody (ghani).
tune; sequence of notes that makes up a musical phrase.
Mfululizo wa sauti yenye mlingano ambao hufanya wimbo.
2. Harmony (ulinganifu wa sauti).
a pleasing combination of elements, or arrangement of sounds; two or more notes
played simultaneously to produce a chord.
Muunganiko wa sauti linganifu mbili au zaidi zinazosikika kwa wakati mmoja.
“Melody ndio kitu cha muhimu; harmony inatumika tu kufurahisha sikio.”
Joseph Haydn, words worth dictionary of musical quotation p.15
3. Rthym.
orderly movement of music sounds and silences through time.
Rthym ni muhimu zaidi kwasababu melody bila rthym imekufa.
Very Matunda-0746194783
Mfano wa melody

Mfano wa harmony

Harmony sio lazima itengenezwe na sauti za ala za aina tafauti tafauti za muziki,
ala ya muziki ya aina moja inaweza ikatengeneza harmony.

Very Matunda-0746194783
Vyombo vya muziki.

❑STRING INSTRUMENTS (vyombo vya nyuzi).


Recorder, flute, Clarinet piccolo, oboe, col Anglia's. (Saxophone). Trumpet, Trombone,
Tuba, Hone and Corn tuba.(vinatengeneza Melody tu)

❑WIND INSTRUMENTS (vyombo vya upepo).


Violin, Viola, Cello, double bass, Harp, Piano. (vinatengeneza Melody na Harmony tu)

❑PERCUSSION INSTRUMENTS (vyombo vinavyo gongwa).


Drums Snare. (vinatengeneza Rhythmy tu)

Very Matunda-0746194783
String instrument;

HARP GITAR GRAND PIANO


Very Matunda-0746194783
Wind instrument;

Very Matunda-0746194783
Percusion instrument;

Very Matunda-0746194783
Uungu na muziki;
Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Zaburi 19:1

Je na muziki nao unahubiri na kumtangaza Mungu? Jibu ni ndio.


Ukumbuke tunavyosema muziki tunaongelea mpangilio wa sauti, hivyo tukisema
muziki unamtangaza Mungu tunamaanisha ule mpangilio wa sauti ndio
unaomtangaza Mungu na sio ujumbe unaotolewa na waimbaji.

Swali: mpangilio wa sauti unamtangazaje Mungu? Kwa wewe kusikia tuni za


sauti zilizopangiliwa unapata habari gani kumuhusu Mungu?

Very Matunda-0746194783
ZINGATIA; hatupaswi kutumia kazi za Mungu kuelezea asili ya Mungu
isipokuwa tunapaswa kutumia kazi za Mungu kuelezea utendaji kazi wa
Mungu, hivyo tutaungalia Muziki kwa jicho la utendaji kazi wa Mungu ilitujue
unamfunuaje Mungu.

Very Matunda-0746194783
Yohana 8:42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda
mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi
yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.
Yohana 9:4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni
mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
Yohana 8:50 Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na
kuhukumu.
Yohana 8:54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu;
anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu
Yohana 17:4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa
niifanye.
Yohana 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule
niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

Very Matunda-0746194783
1Yohana 4:14 Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana
kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

Kupitia mafungu hayo tunaona utendaji kazi wa kiungu ya kuwa;


BABA anatukuzwa na MWANA.
MWANA anatukuzwa na BABA.
MWANA hajitukuzi mwenyewe.

Very Matunda-0746194783
Yohana 16:7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa
maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu
Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie
kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote
atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 16:14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na
kuwapasha habari.
Yohana 16:15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba
atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

ROHO MTAKATIFU anamtukuza BABA na MWANA.


ROHO MTAKATIFU hajitukuzi mwenyewe.
ROHO MTAKATIFU hatukuzwi na BABA wala MWANA.
Very Matunda-0746194783
Utendaji kazi wa BABA, MWANA , na ROHO MTAKATIFU unafanana na utendaji
kazi wa MELODY, HARMONY, na RYTHM.
Melody ndio kiini cha muziki, harmony inawekwa kulingana melody ilivyo harmony
inamuinua melody(melody ya wimbo inaonekana ni nzuri) na baada ya melody
kuinuliwa melody inamuinua harmony(harmony nayo inasikika kuwa nzuri), huwezi
kusema harmony ni nzuri pasipo kuisikia melody kwanza. Ndivyo ilivyo kwa BABA na
MWANA, BABA ndio kiongozi katika mpango wa ukombozi MWANA anamuinua
BABA baada ya BABA kuinuliwa BABA anamuinua MWANA.
Rhythm katika wimbo haisikiki kwasababu rthym ni mwendo/speed ya melody, lakini
bila rthym hakuna melody hakuna harmony. Wakati rthym inafanya kazi kwa ajili ya
kupata melody na harmony nzuri zinazosikika, nyenyewe haisikiki, utendaji kazi
wake ni wa kimya, ila HARMONY na MELODY zinasikika. Ndivyo ilivyo kwa ROHO
MTAKATIFU hajawahi kuonenaka na kiumbe chochote kama ilivyo BABA na
MWANA, anafanya kazi yake katika ukimya, anamuinua MWANA na BABA, hajiinui
mwenyewe, anawaongoza watu kwa KRISTO na BABA bila yeye hatuwezi kumpata
BABA wala MWANA.
Hivyo muziki nao unahubiri na kumtangaza Mungu.
Very Matunda-0746194783
Patakatifu na muziki;

Zaburi 77:13 Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu
kama Mungu?
Psalm 77:13 Thy way, O God, is in the sanctuary: who is so great a God as our
God? (kjv)

Njia za Bwana zipo katika patakatifu hivyo kupitia huduma za hekaluni tutajua
Mungu anasema nini kuhusu muziki.

Very Matunda-0746194783
Mfumo wote wa hekaluni/patakatifu
unatuelekeza kwa KRISTO.
Kutoka25:8 Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao

Hekaluni/patakatifu ni sehemu ambayo uwepo wa Mungu wa uhakika usiokuwa na


mashaka kwa watu hata ambao hawamuamini Mungu ulikuwa unadhihirishwa, hivyo
kwa kuangalia miziki iliyokuwa inapigwa hekaluni tunapata kujua ni muziki wa aina
gani Mungu anauhitaji mahali popote palipo na uwepo wake.
Kama nyimbo za aina flani ndizo zilizopigwa hekaluni mbele ya uwepo wa Mungu ni
Dhahiri ya kwamba nyimbo za aina hiyo hiyo ndio zinapaswa kupigwa sehemu
yeyote ambayo inaaminika kuwa Mungu yupo, na aina hiyo hiyo ya nyimbo ndio
inapswa kusikilizwa na mtu yeyote anayeamini kuwa Mungu anakaa ndani yake.

Very Matunda-0746194783
“Mungu yuko juu sana na ni mtakatifu; na kwa mtu mnyenyekevu, anayeamini,
nyumba yake hapa duniani, yaani, mahali watu wake wanapokutana
kumwabudu, ni lango la mbinguni. Wimbo wa sifa, maneno ya watumishi wa
Kristo, ni njia alizochagua Mungu kutumia kuwaandaa watu kwa ajili ya kanisa
lililoko juu, kwa ajili ya ibada ya juu Zaidi ambapo hakitaingia kitu chochote
kichafu, kisichokuwa kitakatifu…” Ujumbe kwa Vijana Uk.250
Kanisani ni lango la mbinguni hii ikiwa ina maana tunapokuja kuabudu tunaenda
mbele za Mungu kupitia lango hili sawa na kuhani alivyokuwa anaenda mbele za
Mungu hekaluni, na nyimbo zinazopaswa kupigwa ni zile zinazotuanda kuweza
kujakushiriki ibada za mbinguni, kwa lugha rahisi nyimbo zinazopaswa kupigwa ni
zile zinazoendana na nyimbo za Mbinguni, ili tukienda mbinguni tuweze kushiriki
aina hizo za nyimbo.
Kama ambavyo wadhambi hawataenda mbinguni kwa sababu vitu
watakavyovihitaji huko havipo, ndivyo ambavyo wanaopenda muziki usioendana na
muziki wa mbinguni hawataenda mbinguni kwa sababu muziki watakaouhitaji huko
haupo.
Very Matunda-0746194783
Vitu vilivyokuwepo hekaluni/patakatifu vilikuwa vitakatifu kwasababu ya uwepo wa
Mungu uliokuwa mahali hapo, kwa mfano moto ulikuwa unawaka kwenye
madhabahu ya uvumba ulikuwa unawashwa na Mungu mwenywe na mawanadamu
hakuruhusiwa kuuwasha.
“Juu ya madhabahu hii kuhani alichoma uvumba kila asubuhi na jioni; pembe zake
ziligusishwa damu ya toleo dhambi, na zilinyunyuziwa damu siku ya upatanisho.
Moto katika madhabahu hii uliwashwa na Mungu mwenyewe na ulikuwa ni moto
matakatifu.” Wazee Na Manabii uk. 349

Swali: ni miziki ya aina gani ilikuwa inapigwa patakatifu mbele za Mungu?

Very Matunda-0746194783
Ili kujua ni miziki ya aina gani ilikuwa inapigwa patakatifu ni lazima tujue ni vyombo
gani vya muziki vilikuwa vinatumika kutengeneza muziki patakatifu(hekaluni), hii ni
kwasababu majina ya aina za miziki tunayotumia sasa hivi hayakuwepo kipindi hiko
ila vyombo vya muziki vilikuwepo.

1 Nyakati 25:1,6. Tena Daudi na Maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi
ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yedhuthuni, watakaotabiri kwa vinubi na
vinanda na matoazi. Hao wote waliamriwa na baba yao; waimbe nyumbani mwa
BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda na vinubi, kwa utumishi wa nyimbo ya
Mungu, Asafu; Yeduduni, na Hemani wakiwa wameamriwa na mfalme.”

Very Matunda-0746194783
2Mambo ya Nyakati 5:1-14 Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika
patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala
hawakuzishika zamu zao; tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani,
na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi
na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na
pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) hata ikawa, wenye panda
na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na
kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda,
wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za
milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, hata makuhani
hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa
kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.
Matoazi (chombo cha kupigwa), vinanda na vinubi(vyombo vya nyuzi/Kamba)
ndivyo vilivyotumika katika ibada za hekaluni.

Very Matunda-0746194783
Je matoazi(sio ngoma) ambayo yapo katika aina ya vyombo vya kupigwa
yalitumikaje?
Matoazi yalitumika kuashiria wakati wa kuimba ubeti mpya wala hayakutumika
kuimbia.
Hivyo kwa mujibu wa vyombo vilivyotumika hekaluni na aina ya utumikaje wake
muziki uliokuwa unatengenezwa hapo unaangukia katika aina ya muziki ambayo
tunaitambua leo kama classical music isiyo kuwa na aina yeyote ya ngoma ndani
yake.
Ngoma kwa aina zake ni kifaa cha muziki ambacho hakijawahi kutumika kufanya
ibada ya nyimbo mbele za Mungu hekaluni.
Melody na Harmony ndio zilizotawala katika muziki wa hekaluni huku rthym ya
wimbo ikiwa haitengenezwi na kifaa cha aina yeyote wala ilikuwa hasikiki,
isipokuwa ilikuwa inapatikana katika melody na harmony. Kwa lugha rahisi muziki
wa hekaluni ulikuwa hauna rhythm za kusikika kwa sauti kama vile beats n.k
Very Matunda-0746194783
Je shetani yupo kimya kwenye swala zima la muziki?
HAPANA!

“Shetani hana upinzani dhidi ya muziki, ikiwa anaweza kuufanya mfereji


anaoweza kuutumia kuzifikia akili za vijana. Jambo lolote linaloondoa akili za
vijana na kuzipeleka mbali na Mungu, na kuchukua muda ambao ungetumiwa kwa
ajili ya huduma ya Mungu linatimiza kusudi lake. Ukitumiwa vizuri, muziki ni
mbaraka lakini mara nyingi unatumiwa kama moja ya njia za shetani
zinazovutia ambazo anazitumia kunasa roho. Ukutumiwa vibaya, unawafanya
watu wasikouwa na kicho cha Mungu kuwa na kiburi, upuuzi, na upumbavu.
Ukiruhusiwa kuchukua nafasi ya kicho na maombi ni laana ya kutisha. ” Ujumbe kwa
Vijana Uk.279

Kama shetani naye anatumia muziki kutimiza agenda zake kwa kushika akili za
watu, ina maana muziki unaweza usitimize makusudi Mungu aliyoyakusudia.
Very Matunda-0746194783
Shetani na muziki;
Muziki Mungu alioufanya unaanza na
• Melody
• Harmony
• Rthym

Muziki Shetani anaoufanya unaanza na


• Rthym
• Harmony
• Melody

Shetani amefanya mapinduzi kile ambacho Mungu amekiweka kuwa cha kwanza
kuzingatiwa amekifanya kuwa cha mwisho na kile cha mwisho amekifanya cha
kwanza.
Very Matunda-0746194783
muziki unafanya kazi gani ukitumika vibaya?

Ukitumika vizuri Ukitumika vibaya

1. Unatimiza makusudi matakatifu. 1. Unatimiza makusudi machafu.


2. Silaha dhidi ya kukata tamaa. 2. Chanzo cha kukata tamaa.
3. Unanatisha ukweli wa kiroho 3. Unanatisha uongo wa kiroho
moyoni. moyoni.
4. Unamfukuza adui(shetani na 4. Unamkaribisha adui(shetani na
malaika zake) malaika zake)
5. Nguvu kubwa kwa ajili ya 5. Unawafanya watu wasio kuwa na
wema. kicho cha Mungu kuwa na kiburi,
6. Baraka upuuzi na upumbavu.
7. Unamtukuza Mungu. 6. Laana ya ajabu.
7. Unamdhalilisha Mungu.
Very Matunda-0746194783
WIMBO
Wimbo ni nini?
Kuna tafauti gani kati ya wimbo na muziki?
Mambo gani ya kuzingatia katika uimbaji?

“Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.” Zaburi 47:7

“Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa
roho, tena nitaimba kwa akili pia.” 1 Wakorintho 14 : 1

Kama kuimba kunatakiwa kuwe makini kiasi hiki, vipi kuhusu nyimbo
unazotakiwa kusikiliza?

Unapaswa usikilize nyimbo zilizoimbwa kwa roho na akili.

Very Matunda-0746194783
Wimbo(song)- a musical compostion with lyrics for voice or voices performed by
singing, OR, a short poem or other set of words set to music or meant to be sung.

Muziki wenyewe hauna mashairi (lyrics), unapoingiza mashairi kwenye muziki


unatengeneza wimbo, na hii ndio tafauti kati ya wimbo na muziki.

Mashairi lazima yaendane na muziki, chukulia mfano wa gari na mtu alafu gari
ndio muziki na mtu ndio mashairi.
Mtu lazima aendane na gari analolipanda ili aweze kuingia.
Kati ya gari na mtu kipi kinamuongoza mwenzie na kipi kinamfikisha mwenzie?
Mashairi yanatuongoza katika tafakari, muziki unafikisha tafakari zetu juu.

Very Matunda-0746194783
Mambo ya kuzingatia katika uimbaji.

1. Kuimba kutokana na kweli, hii ina maana ya kuimba kwa namna sahihi kutokana
na neno la Mungu.
Biblia inatuambia nini kuhusiana na kuimba kutokana na kweli?
“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba
katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na
kweli.” Yohana 4:23-24
“Kama sehemu ya huduma ya dini, uimbaji ni tendo la ibada sawa na maombi.
Kwa kweli nyimbo nyingi ni maombi. ” Ujumbe kwa Vijana Uk.276

Hivyo chochote tunachojifunza katika injili ya Yohana 4:23-24 kuhusiana na


ibada, kinatakiwa kutumika katika uimbaji.
Very Matunda-0746194783
Katika Yohana 4:23-24 tunajifunza kuwa;
i) Mungu anahitaji tumuabudu yeye
ii) lazima tumuabudu Mungu katika roho na kweli.
“mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na
kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;” Waefeso 5:19
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na
kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu
kwa neema mioyoni mwenu.” Wakolosai 3:16
Kwaiyo kama kuimba ni ibada,
✓Mungu anahitaji uimbe katika roho na kweli.
✓Mungu anategemea uimbe katika roho na kweli.
✓Mungu ameamuru uimbe katika roho na kweli.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umeimba kutokana na kweli.
Very Matunda-0746194783
Kama kuimba hakutakuwa katika kweli, uimbaji wako utakuwa ni;
▪ Uimbaji wa bure.
“Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.”
Mathayo 15:9
▪ Uimbaji wa kijinga wa kujitungia mwenyewe.
“Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada
mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa
ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.”
Wakolosai 2:13

Ellen white anasema “ wakati wanadamu wanapoimba kwa roho na ufahamu,


wanamuziki wa mbinguni huchukua muelekeo na kujiunga na wimbo wa shukrani.”
ujumbe kwa vijana, uk.277-278.
Very Matunda-0746194783
Mambo ya kuzingatia katika uimbaji.

2. Kuimba ukweli.
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana
na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu
kwa neema mioyoni mwenu.” Wakolosai 3:16
Ukiwa unaimba unafundisha.

3. Kuwa mkweli kuhusiana na unachokiimba.


“Mungu hutukuzwa kwa nyimbo za sifa kutoka moyo safi uliojazwa na upendo na
kicho kwake.” ujumbe kwa vijana, pg 278.

Very Matunda-0746194783
Ubongo na muziki;
Pambano ni katika ubongo wako. Kwanini? Kwasababu ubongo ndio kiini cha
wewe ni nani.
Ubongo unasehemu nne Frontal lobe, Parietal lobe, Occipital lobe na Temporal
lobe.
Lobes are large area of your brain that have a certain location and are associated
with a set of functions.
Biblia inazungumzia Prefrontal cortex ambayo ni sehemu ya Frontal lobe.
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni,
na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba
yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. Ufunuo 14:1

Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye
yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji
cha uso wake, au katika mkono wake.” Ufunuo 14:9
Very Matunda-0746194783
Frontal lobe
The frontal lobes are located directly behind the forehead(kipaji cha uso). The
frontal lobes are the largest lobes in the human brain and they are also the most
common region of injury in traumatic brain injury.

Function of frontal lobe.


• Voluntary movement.
• Decision making.
• Planning.
• Reasoning.
• Problem solving.
• Memory.
• Emotional control centre.
• Speech and language production.
• Motor skills.
• Forming personality.
• Filtering information.
Very Matunda-0746194783
Effects of damage of frontal lobe. Things that damage frontal lobe which
• Change in personality. are scientifically proved are,
• Speech problems. • Illegal drugs
• Difficulty problem solving. • Alcohol, caffine, nicotine certain food.
• Inability to plan a sequence of complex • Certain modern movies impair the
movements needed to complete multi- frontal lobe.
stepped tasks. • Modern television program.
• Loss of flexibility in thinking and • Certain kind of music.
persistence of a single idea or
behaviour (Perseveration).
• Reduced awareness/insight into
difficulties.
• Changes in social behavior.
• Inability to focus on a task and to filter
out distractions (Attention)
Very Matunda-0746194783
Ukiwa unaangalia runinga au filamu.
What cause alpha or beta wave in music?

Very Matunda-0746194783
Prefrontal cortex
is the one of the functional area of the frontal lobe, cerebral cortex which covers the
front part of the frontal lobe.

This brain region has been


implicated in executive function
relates to abilities to differentiate
among conflicting thoughts,
determine good and bad, better
and best, same and different,
future consequences of current
activites, working toward a
defined goal, prediction of
outcome, and expectation based
on action

Very Matunda-0746194783
Kwenye prefrontal cortex ndio sehemu
pekee ambayo vitu vifuatavyo vipo;
• Character (tabia).
• Spirituality (hali ya kiroho).
• Discernment (utambuzi).
• Will (matakwa).
• Choose (kuchagua).
• Obey (utii).
• Worship (ibada).

Kwaiyo hii ndio sehemu pekee ambayo kila mtu anaitaka, Mungu anaitaka na
shetani pia anaitaka, kama Ufunuo 14:1,9 inavyosema. Very Matunda-0746194783
“Njia ziendazo moyoni zinazopaswa kulindwa zinahusisha akili za kuelewa,macho ya
kuona na masikio ya kusikia kusudi shetani asije akawashinda; maana hizi ndizo njia
za rohoni. Kila mtu anatakiwa awe askari mlinzi mwaminifu wa macho yake,
masikio na akili zake zote, kama akitaka kuutawala moyo wake na kuzuia
mawazo mabaya yasiyofaa yasiuharibu moyo wake.” Kutayarisha Njia-1 Uk.185

Kila unacho sikia, ona, gusa, jaribu, nusa kinarekodiwa vizuri kwenye ubongo
(frontal lobe).

Swali, ni kiasi gani cha vitu vimerekodiwa vinavyo athiri tabia yako(character)?
au
ni kiasi gani cha vitu vibaya vimerokodiwa vinavyo athiri tabia yako?

Ndiyo maana Sulemani akasema “For as he thinketh in his heart, so [is] he: …”
proverb 23:7
Very Matunda-0746194783
Sayansi inasemaje kuhusu muziki na ubongo

Very Matunda-0746194783
Masaru emoto
Mwanasayansi wa kijapani alizaliwa tarehe 22/07/1943 na kufariki tarehe
17/10/2014 alifanya experiment juu ya matokeo ya muziki kwenye maji (effect of
music in water) na akaja na majibu ya alichokipata.

anasema “ beautiful music and word form crystalline structure from water
molecules. Discordant tones and negative music form chaotic patterns every
time.”

Very Matunda-0746194783
Love and gratitude
words

Very Matunda-0746194783
Thank you

Very Matunda-0746194783
Very Matunda-0746194783
You make me sick

Very Matunda-0746194783
I hate you

Very Matunda-0746194783
Mozart symphony
no.40 music

Very Matunda-0746194783
Tchaikovsky: swan lake
(suite)

Very Matunda-0746194783
Beethoven pastoral

Very Matunda-0746194783
Heavy metal music

Very Matunda-0746194783
Fikiria
The vibration energy we create in our thought, ideas, words and music. Affect the
very molecular structure of water.
Kumbuka kwamba
• Maji ni moja ya kitu muhimu katika Maisha yako(basic need).
• Maji yamechukua asilimia 70 ya dunia.
• Maji yanatengeneza asilimia 70 ya mwili wako.
Kama muziki na maneno yanafanya maji yawe hivyo, vuta picha ni nini ambacho
mwili wako unafanywa na miziki pamoja na maneno pale unaposikiliza miziki
isiyofaa na maneno yasiyofaa.

The molecular structure of water reflects our environment both internal and
external , and it will change the molecular makeup of your cells.
Very Matunda-0746194783
Ufanye nini kulinda frontal lobe, frontal cortex na
ubongo kwa ujumla?
Usisome, usisikilize, wala kuangalia chochote kinachoharibu tabia njema.

Neno la Mungu kupitia Ellen G White linasema, “those who would not fall a prey to
satan’s devices must guard well the avenues of soul; they must avoid reading, seeing,
or hearing that which will suggest impure thoughts. The mind must not left to dwell at
random upon every subject that the enemy of souls may suggest. The heart must be
faithfully sentineled, or evils without will awaken evils within, and the soul will
wander in darkness.” Adventist home 403.3

Very Matunda-0746194783
“Njia ziendazo moyoni zinazopaswa kulindwa zinahusisha akili za
kuelewa,macho ya kuona na masikio ya kusikia kusudi shetani asije
akawashinda; maana hizi ndizo njia za rohoni. Kila mtu anatakiwa awe
askari mlinzi mwaminifu wa macho yake, masikio na akili zake zote,
kama akitaka kuutawala moyo wake na kuzuia mawazo mabaya
yasiyofaa yasiuharibu moyo wake.” Kutayarisha Njia-1 Uk.185

Very Matunda-0746194783
Satan frontal cortex
“Mwanzoni Shetani alikuwa malaika mwenye kuheshimiwa mbinguni, kutoka kwa
Kristo. Kuonekana kwake kulikuwa kama malaika wengine, alikuwa mpole mwenye
uso wa furaha. Paji lake la uso lilikuwa refu na pana, likionyesha kuwa na
akili nyingi. Umbo lake lilikuwa kamilifu; lenye kupendeza na kutamanika. Lakini
wakati Mungu alipomwambia mwanae, “Tufanye mtu kwa mfano wetu,” Shetani
alimwonea Yesu wivu. Alitegemea kuhusishwa katika uumbaji wa mwanadamu, na
kwa vile haikuwa hivyo, alijawa na husuda, wivu na chuki. Alitamani kupata
heshima ya juu sana mbinguni nafasi ya pili kwa Mungu.” {EW 145.1}
“Nilionyeshwa kama shetani alivyokuwa awali, akiwa mwenye furaha na malaika
aliyetukuka. Kisha nilionyeshwa jinsi alivyo Sasa. Bado anayo Hali ya kifalme,
Mwonekano wake bado ni bora, kwa maana ni malaika aliyeanguka. Lakini
mwonekano wa uso wake umejaa hofu, wasiwasi, huzuni,chuki,hasira,uharibifu,
udanganyifu na kila Aina ya uovu. Uso huo ulikuwa mwema mwanzoni, nilitambua
kipaji cha uso wake kilianza kutoka kwenye Macho yake hadi kichwani.
Niliona kwamba alikuwa amezama kwa muda mrefu katika uovu kiasi kwamba
kila Aina ya sifa njema ilikuwa imeharibiwa na kila Aina ya Tania ya uovu
ilikuwa imekuzwa…
Very Matunda-0746194783
Macho yake yalikuwa ya kijanja yenye hila na yaliyoonyesha kupenya kwa ndani
sana. Umbo lake lilikuwa kubwa, lakini mwili wake ulikuwa mlegevu katika mikono na
uso wake. Kadri nilivyomtazama, kidevu chake kilikuwa kimeegemezwa katika
mkono wake wa kushoto. Alionekana kuwa mwenye tafakari sana. Uso wake ulikuwa
na tabasamu lililonifanya nitetemeke, lilikuwa limejaa uovu na hila za kishetani.
Tabasamu hili ni lile alilolivaa muda mfupi kabla ya kuthibitisha matokeo ya
madhara yake na kadri alivyoimarisha madhara yake katika mitego, tabasamu hili
liliendelea kuwa la kuchukiza.” {EW 152.3}

Swali
Aina gani ya muziki unapaswa kusikiliza?
Very Matunda-0746194783
Muziki unaopaswa kusikiliza unapaswa uwe
na sifa zifuatazo.
• Unatimiza makusudi Mungu aliyoyakusudia kupitia muziki.
• Umeimbwa katika roho na kweli.
• Usio haribu ubongo wala mifumo ya mwili.
• Usio na ngoma ndani yake (beats).
• Usiochochea kuchezesha sehemu za mwili(body movement).

Kwa kanisa kuzitambua sifa hizo, kanisa baada ya kuchunguza neno la Mungu
na roho ya unabii lilitoa msingi juu ya nyimbo na miziki unayopaswa
kuisikiliza na kujifungamanisha nayo. Kisha likataja aina ya miziki
unayotakiwa kujiepusha nayo yaani kutoisikiliza kwasababu miziki hiyo haina
sifa tajwa hapo juu.
Very Matunda-0746194783
Toleo la Kiswahili la Mwongozo wa Kanisa (2013)
“Muziki ni moja ya sanaa za hali ya juu sana. Muziki mzuri hautupatii furaha tu, bali
huziinua akili zetu na kukuza sifa zetu zilizo bora kabisa. Mara kwa mara Mungu
amekuwa akitumia nyimbo za kiroho kugusa mioyo ya wenye dhambi kuwaleta
katika toba. Kwa upande mwingine, muziki huvunja maadili na kututoa katika
uhusiano wetu na Mungu.” (Uk.165)

“Inatupasa kuwa waangalifu sana katika kuchagua muziki katika nyumba zetu,
mikusanyiko ya kijamii, shule, na makanisa. Tuni yo yote, aina ya jazi, rock au aina
mchanganyiko zinazohusiana na hizo, au lugha yo yote inayoelezea hisia za
kijinga au zisizokuwa muhimu vitaepukwa.” (Uk.165)

“Muziki wa kidunia au ule uletao mashaka kwa namna ulivyo, kamwe


usiingizwe katika ibada zetu.” (Uk.103)
Very Matunda-0746194783
Miziki aina ya jazzi, rock au aina mchanganyiko zinazohusiana na hizo kama vile
Pop, Regge, RnB, Hiphop n.k, ipoje?

Jazzi

Rock

Pop

RnB
Very Matunda-0746194783
Vitu vinavyofanana kwenye aina hizo za muziki.

• Aina zote zinamidundo (beats).


• Aina zote zinatumia ngoma.
• Aina zote zina chochea au hamasisha body movement na physical action.
• Aina zote zina haribu ubongo.

Hivyo miziki yenye sifa kama hizo hapo juu ni ya kuacha na kuepuka kuisikiliza.

Very Matunda-0746194783
“UFUNDI wa sauti tamu za nyimbo takatifu ulikuzwa daima (katika shule za
manabii). Hakuna ngoma ya upuzi iliyosikika wala wimbo hafifu ambao ungemsifu
mwanadamu na kupotosha akili kumwacha Mungu: bali zaburi takatifu za sifa kwa
Mwumbaji zenye kulitukuza jina lake na kuyasimulia matendo yake ya ajabu. Hivyo
muziki ulifanywa kulitimiza kusudi takatifu na kuyainua mawazo kwa kile ambacho
kilikuwa safi, bora na kikuu pamoja na kuamsha rohoni uchaji na moyo wa shukrani
kwa Mungu.” Kutayarisha njia, pg 236

“Mazoea mabaya na mwelekeo wa dhambi hutiwa nguvu na kuimarishwa na


burudani hizi. Nyimbo za dunia, kuyumbisha sehemu fulani za mwili(body
movement and physical action) kunakoashiria hisia za msisimuko wa mapenzi,
maneno na mwelekeo mwovu huathili mawazo na kushusha maadili. Kila
kijana mwenye mazoea ya kuhudhuria matamasha kama haya tabia zao
huchafuliwa…hakuna kitu kingine chenye mvuto mkubwa kinachotia sumu mawazo
yanayoharibu moyo wa kupenda mambo ya kiroho na kupunguza hamu ya utulivu
na furaha ya kweli maishani kama tamasha la burudani.”White (4T 1948,pg497)
Very Matunda-0746194783
Body language(lugha ya mwili)
is a type of nonverbal communication in which physical behaviors as opposed to
word, are used to express or convey the information.

Katika wimbo, kati ya muziki na mashahiri kipi cha muhimu sana?


Muziki peke yake unaweza kumshawishi(influence) msikilizaji?

Does it matter on how the person speaks?

Muziki peke yake una lugha ya mwili (body language).


Very Matunda-0746194783
Je Mungu aliumba muziki kushawishi mawazo yetu na hisia?

“Kama mawazo ni mabaya, hisia zitakuwa mbaya; na mawazo na hisia


zikiungwanishwa pamoja hufanyiza tabia ya maadili(moral character). Wakati
sisi tunaamua kwamba kama wakristo hatutakiwi kuzuia mawazo na hisia zetu,
tunaletwa chini ya ushawishi wa malaika wabaya, na kuwakaribisha uwepo wao na
udhibiti wao.” RH April 21, 1885,par.2
Hisia na mawazo unayopata kwa kusikiliza miziki na nyimbo ndio body language.
Mfano,

Kuna kiasi kikubwa cha lugha ya mwili(body language) kwenye muziki, kamwe
usimruhusu mtu yeyote akwambie kwamba ni mashairi tu ndio ya muhimu.
Very Matunda-0746194783
Motives
a reasoning for doing something especially one that is hidden or not obvious.
In music is a music fragment or succession of notes that has some special
importance or intesion.
Katika kila kipande cha muziki kuna motive.

PROFESSOR MARSHALL MCLUHAN


“the medium is the message: that is to say the music; it’s a melody, harmony, and
rhythm, all by itself disposes man to virtue or vice by moving the emotions. Therefore
the way in which move the passion should serve as a principle basis for
judgement on whether any given piece of music is good or bad.”

Very Matunda-0746194783
Beats(kiki).
a steady and regular pulse we hear in music. It’s the element of rhythm.
Muziki Mungu alioufanya unaanza na
• Melody
• Harmony
• Rthym

Muziki Shetani anaoufanya unaanza na


• Rthym
• Harmony
• Melody

Shetani amefanya mapinduzi kile ambacho Mungu amekiweka kuwa cha kwanza
kuzingatiwa amekifanya kuwa cha mwisho na kile cha mwisho amekifanya cha
kwanza.
Christian contemporary music (CCM).

Ni miziki ambayo maneno ya kikristo yanachukua nafasi (replace) ya


ujumbe wa kidunia(wordly text) lakini aina ya muziki inabaki kuwa ileile.

Aina hii ya muziki inathibitisha kwa yenyewe kwamba mashahiri ni bora


kuliko muziki, kitu ambacho sio sahihi.

Very Matunda-0746194783
Mfano wa Christian
Contemporary Music (CCM)
“ muziki, usipotumiwa vibaya, ni mbaraka mkubwa; lakini ukitumiwa
vibaya, ni laana ya ajabu. Husisimua, lakini hautoi ile nguvu na moyo
ambao mkristo huweza tu kuupata kwenye kiti cha neema akionyesha kwa
unyenyekevu wa moyo haja zake na akilia kwa machozi, na kuomba
kuongezewa nguvu za Mungu kumwezesha kushindana na majaribu
makali ya yule mwovu.” Kutayarisha Njia 237.4

“Shetani anaelewa ni kiungo gani cha mwili cha kushitua ili mwili
wote usisimke na kuchangamsha akili, kisha Kristo hatamaniki tena
moyoni.” 1T 496.1

“ Muziki umeharibiwa mara nyingi ili utumike kutekeleza makusudi


maovu, na kwa njia hiyo unakuwa moja ya vyanzo vikuu vya majaribu.”
Ujumbe kwa Vijana 275 Very Matunda-0746194783
“Wajumbe wa Mungu, wanapojibidisha kuwafikia watu,
hawapaswi kufuata/kuiga njia za ulimwengu. Kwenye
mikutano inayoendeshwa, hawapaswi kuwategemea waimbaji wa
ki-ulimwengu na matamasha ya maonyesho kuamsha
shauku/usikivu wa watu. Inawezekanaje kwa wale ambao
hawavutiwi na neno la Mungu, ambao hawajawahi kamwe
kulisoma neno lake kwa hamu ya dhati/kweli ya kuuelewa ukweli
wake, kutegemewa kuimba kwa roho na ufahamu?. . .
Inawezekanaje kwa kwaya ya mbinguni kujiunga na muziki
ambao ni wa mtindo tu? . . .” (9T pg.143-144)

Very Matunda-0746194783
“Nalionyeshwa kuwa yawapasa vijana kuchukua msimamo wa juu zaidi na
kulifanya neno la Mungu kuwa mshauri wao na kiongozi wao. Vijana
wana wajibu mzito ambao si wakuudharau… Nyimbo za upuzi na
mitindo wa uimbaji upendwao na wengi huelekea kuwapendeza…
Shetani anawateka nyara vijana. Aha, niseme nini kuwaongoza
kuukomesha uwezo wake wa kupumbazisha! Yu mpendezi mwerevu
anayewashawishi kwenda hata jehanam.” 1T 497.1

Very Matunda-0746194783
Vigezo unavyopaswa utumie kuchagua muziki
au wimbo wa kusikiliza.
1. Body language(lugha ya mwili)
Muziki/wimbo unaotaka kuusikiliza una lugha gani ya mwili(body
language)?
Unakutafakarisha kile kinachoimbwa au paka uamue mwenyewe kusikiliza
mashairi ndio labda unaweza kutafakari?
Unapousikia, mwili wako unakua katika hali gani?

“Shetani anaelewa ni kiungo gani cha mwili cha kushitua ili mwili
wote usisimke na kuchangamsha akili, kisha Kristo hatamaniki tena
moyoni.” 1T 496.1
Very Matunda-0746194783
2. Lyrics(mashairi)
Mashairi yana ujumbe gani?
Ujumbe wa mashairi upo sawa na neno la Mungu?
Mashairi yanatamkwaje?
Mashairi yanaendana na muziki?

“Sio sauti ya upayukaji inayotakiwa, bali lafudhi inayosikika, matamshi


sahihi, na maneno yanayoeleweka.” Ujumbe kwa Vijana Uk.278
“Baadhi wanafikiri kuwa wanavyopayuka zaidi ndivyo wanavyotoa
muziki mzuri; lakini kelele siyo muziki. Uimbaji mzuri ni kama muziki wa
ndege-ni laini na ni mtamu…Nyimbo ambazo kila neno linasemwa kwa
dhahiri, katika toni ya muziki, ndizo nyimbo ambazo malaika wanajiunga
nasi tunapoziimba.” Evangelism Pg.510
Very Matunda-0746194783
3. Beats(kiki)
Muziki unaotaka kusikiliza una beats au hauna?
“Shetani anaelewa ni kiungo gani
cha mwili cha kushitua ili mwili
wote usisimke na kuchangamsha
akili, kisha Kristo hatamaniki tena
moyoni.” 1T 496.1

“Mazoea mabaya na mwelekeo wa


dhambi hutiwa nguvu na
kuimarishwa na burudani hizi.
Nyimbo za dunia, kuyumbisha
sehemu fulani za mwili
kunakoashiria hisia za msisimuko
wa mapenzi, maneno na
mwelekeo mwovu huathili
mawazo na kushusha
maadili.”EGW (4T 1948:497) Very Matunda-0746194783
Tumia vigezo tulivyojifunza kuchagua miziki unayofaa
katika miziki ifuatayo;

Very Matunda-0746194783
Mfano wa miziki inayostahili;

Very Matunda-0746194783
wrong correct

Nyimbo no 173:

Nyimbo no 22:

Nyimbo no 130:
Very Matunda-0746194783
“Bwana amenionyesha kuwa mambo ambayo umeyaelezea kuwa
yanatokea huko Indiana, yatatokea muda mfupi kabla ya
kufungwa kwa mlango wa rehema. Kila jambo la kishenzi
litafanywa. Kutakuwepo makelele, pamoja na ngoma, muziki
na kucheza. Fahamu za viumbe wenye akili zitachanganywa kiasi
kwamba hazitaweza kufanya maamuzi sahihi. Na hayo
yataitwa matendo ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu kamwe
hajidhihirishi kwa njia kama hizo, yaani katika makelele na
zahama kana kwamba ni sauti za vichaa, (bedlam of noise). Huu
ni ubunifu wa Shetani ili kuficha mbinu zake kwa ujanja
akiwa na lengo la kuharibu nguvu ya ukweli wa wakati huu
ulio safi na wenye kuinua na kutakasa watu…
Very Matunda-0746194783
Ni bora zaidi kumwabudu Mungu bila muziki kuliko kutumia ala
(vyombo vya muziki) za muziki kufanya kazi ambayo
ilionyeshwa kwangu kuwa ingeletwa katika mikutano
yetu…..nguvu za mawakala wa shetani hujichanganya na
makelele na kuamsha misisimko….shetani anafanya kazi
katikati ya makelele na mchanganyiko wa muziki kama huo,
ambao kama ungeendeshwa vizuri, ungemsifu na kumtukuza
Mungu.Shetani anaufanya muziki kuwa na madhara
yanayofanana na sumu ya nyoka mwilini….. shetani
ataufanya muziki kuwa mtego kwa namna utakavyoendeshwa.”
Selected Messages, book 2, Uk. 36.2-3, 37.5, 38.1)

Very Matunda-0746194783
“Malaika wanazunguka nyumba moja ya makazi huko. Vijana
wamekusanyika humo; kuna sauti ya waimbaji na ala za muziki.
Wakristo wakusanyika humo, lakini hiki ni kitu gani unachosikia? Ni
wimbo, wimbo mfupi, mwepesi wa kipuuzi, unaostahili kuimbwa
katika holi ya densi. Tazama malaika safi wanaondoa taa zao, na
giza linatanda katika nyumba ile. Malaika wanaondoka katika eneo
lile. Huzuni inatanda katika nyuso zao. Tazama, wanaomboleza.
Niliona jambo hili likirudiwa rudiwa mara kadhaa miongoni mwa
watunza sabato… Muziki umechukua saa ambazo zilipaswa kutumiwa
kwa ajili ya maombi. Muziki ni sanamu ambayo wakristo watunza
sabato wanaiabudu. Shetani hana upinzani dhidi ya muziki, ikiwa
anaweza kuufanya mfereji anaoweza kuutumia kuzifikia akili za
vijana. Jambo lolote linaloondoa akili za vijana na kuzipeleka mbali
na Mungu, na kuchukua muda ambao ungetumiwa kwa ajili ya huduma
ya Mungu linatimiza kusudi lake.” Ujumbe kwa Vijana Uk.279
Very Matunda-0746194783
“Mazoea mabaya na mwelekeo wa dhambi hutiwa nguvu na kuimarishwa
na burudani hizi. Nyimbo za dunia, kuyumbisha sehemu fulani za mwili
kunakoashiria hisia za msisimuko wa mapenzi, maneno na mwelekeo
mwovu huathili mawazo na kushusha maadili.”EGW (4T 1948:497)

Very Matunda-0746194783
“Hebu na tukumbuke kuwa katika kila mkutano wa watakatifu hapa
duniani malaika wa Mungu wanakuwepo wakisikiliza shuhuda,
nyimbo, na maombi. Na tukumbuke kwamba sifa zetu zinajaliziwa na
kwaya ya malaika wa mbinguni.” Message to young people 97:297)

“Muziki unapaswa kuwa na uzuri, huruma, na nguvu. Hebu sauti ziinuliwe


kwa nyimbo za sifa na sala. Tumia, ikiwezekana, muziki wa ala na
hebu ulinganifu mtukufu wa sauti (harmony) upae kwa Mungu,
sadaka inayokubalika” 4T 71.1

Very Matunda-0746194783
“Nimeonyeshwa utaratibu kamili wa mbinguni, nami nimependezwa
mno nilipokuwa nikisikiliza uimbaji ulio kamili pale. Baada ya kutoka
katika njozi, nyimbo za hapa hazikunipendeza na sauti hazilingani.
Nimeona jamii za malaika, waliosimama mraba, kila mmoja akiwa na
kinubi cha dhahabu. Mwisho wa kinubi kuna chombo cha kubadilishia
sauti. Vidole vyao havikuenda kwa uzembe juu ya nyuzi, bali waligusa
nyuzi mbalimbali kutoa sauti mbalimbali. Palikuwa na malaika ambaye
siku zote aliongoza ambaye kwanza hupiga kinubi na kutoa sauti, ndipo
wote huungana naye kwa sauti kubwa ya uimbaji kamili wa mbinguni.
Hauwezi kusifiwa mno kupita vile unvyostahili. Ni sauti tamu, takatifu, ya
mbinguni, huku mionzi ya nuru ya sura ya Yesu iking’aa kutoka uso wa ila
mmoja, kwa utukufu usioelezeka.” Kutayarisha Njia Uk.236

Very Matunda-0746194783
“Maboresho makubwa yanaweza kufanywa katika uimbaji. Baadhi
wanafikiri kuwa wanavyopayuka zaidi ndivyo wanavyotoa muziki
mzuri; lakini kelele siyo muziki. Uimbaji mzuri ni kama muziki wa
ndege-ni laini na ni mtamu. Katika baadhi ya makanisa nimesikia solo
ambazo hazifai kabisa kwa huduma za nyumba ya Bwana. Noti
zinazovutwa sana na sauti za ajabu-ajabu zinazotumiwa katika
uimbaji wa “Opera” haziwafurahishi malaika. Malaika wanapenda
kusikia nyimbo sahihi za sifa zikiimbwa katika sauti asilia. Nyimbo
ambazo kila neno linasemwa kwa dhahiri, katika toni ya muziki,
ndizo nyimbo ambazo malaika wanajiunga nasi tunapoziimba.
Wanajiunga kuimba wimbo ambao unaimbwa kutoka moyoni na
unaimbwa kwa roho na ufahamu.” Evangelism Pg.510
Very Matunda-0746194783
“ Yeye ambaye ametupatia karama zinazotuwezesha kuwa watenda
kazi pamoja na Mungu, anatarajia watumishi wake wapalilie sauti zao, ili
waweze kusema na kuimba kwa namna ambayo wote wanaweza
kuelewa. Sio sauti ya upayukaji inayotakiwa, bali lafudhi inayosikika,
matamshi sahihi, na maneno yanayoeleweka. Hebu wote watumie
muda wa kutosha kuboresha sauti,ili kwamba sifa ya Mungu iweze
kuimbwa katika sauti iliyo wazi na laini, badala ya sauti yenye
mikwaruzo au ya juu sana inayoumiza masikio. Uwezo wa kuimba ni
karama ya Mungu; hebu itumiwe kwa utukufu wake. ” ujumbe kwa vijana
278

Very Matunda-0746194783
“ muziki uliumbwa kutimiza kusudi takatifu, kuinua mawazo yaelekee kile
kilicho safi, bora na kinachoinua, na kinachochea kicho na shukrani kwa
Mungu. Kuna tofauti kubwa kati ya desturi ya zamani na matumizi ya
sasa ya muziki! Wengi wanatumia karama hii kuinua nafsi, badala ya
kuitumia kumtukuza Mungu! ” Ujumbe kwa Vijana Uk.277

“Muziki unaweza kufanywa kuwa nguvu kubwa kwa ajili ya wema; lakini
hatutumii vizuri kipengele hiki muhimu cha ibada. Uimbaji unafanywa
kwa kushtukizwa au kukidhi matukio maalumu, na kwa nyakati zingine
wale wanaoimba wanaachwa kuimba kwa makosa, na muziki
unapoteza mvuto wake katika akili za wanaohudhuria.” Ujumbe kwa
Vijana Uk.280
Very Matunda-0746194783
“ukitumiwa vizuri, muziki ni mbaraka lakini mara nyingi unatumiwa
kama moja ya njia za shetani zinazovutia ambazo anazitumia kunasa
roho. Ukutumiwa vibaya, unawafanya watu wasikouwa na kicho cha
Mungu kuwa na kiburi, upuuzi, na upumbavu. Ukiruhusiwa kuchukua
nafasi ya kicho na maombi ni laana ya kutisha.” Ujumbe kwa Vijana
Uk.279

Very Matunda-0746194783
Kwanini Yesu hajaja mpaka sasa?
Ufunuo 7.1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne
za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari,
wala juu ya mti wo wote.

Ufunuo 7.2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye
muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika
wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,

Ufunuo 7.3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha
kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Very Matunda-0746194783
Nilimuuliza malaika aliyekuwa pamoja nami maana ya yale
niliyiyasikia na ambacho malaika wanne wanaenda kufanya.
Akaniambia ni Mungu anayezuia nguvu na amewapa malaika zake
majukumu juu ya vitu vyote juu ya nchi; kwamba malaika wanne, na
kwamba walikuwa karibu kuziachia pepo hizo na pepo nne zilipokuwa
tayari kuvuma, jicho la Yesu lenye neema liliangalia masalio
waliokuwa hawajawekewa muhuri, naye aliinua mikono yake mbele
ya Baba na kumsihi kwamba alimwaga damu yake kwa ajili yao.
Ndipo malaika mwingine akatumwa kuruka kwa kasi na
kuwaendea wale malaika wanne na kuwaagiza washikilie, mpaka
watumwa wake Mungu wawekewe muhuri na Mungu aliye hai
katika vipaji vya nyuso zao. EW 38.2

Very Matunda-0746194783
Ndugu wapendwa na dada zangu, acheni amri za Mungu na ushuhuda
wa Yesu kristo vidumu katika fikira zenu daima na ving’oe mawazo
ya kidunia na mifadhaiko ya kidunia ndani yenu. Yatafakarini hayo
daima wakati mnapolala na mnapoamka. Muishi na kutenda
mkionyesha kabisa marejeo ya Mwana wa Adamu. Wakati wa kutiwa
muhuri ni mfupi sana, kitambo tu kazi hiyo itakuwa imeisha. Huu ndio
wakati wa kuthibitisha wito wetu na kuchaguliwa kwetu, maadamu
malaika wanne wanashikilia pepo nne. EW 58.2

Very Matunda-0746194783
Hitimisho.
Muziki ni moja ya kitu ambacho kinaweza kukukosesha kutiwa muhuri wa
Mungu, na ni silaha ambayo shetani anaitumia kuwafanya watu
washindwe katika pambano kuu. Huu ndio muda ambao Bwana anatumia
kukupa maarifa juu ya nini ambacho unatakiwa kufanya kuhusiana na
muziki kabla kazi ya kutia muhuri kwa watu wake haijakoma.

Wagalatia 5.7 …ni nani aliyewazuia msiitii kweli?


Wagalatia 5.9 Chachu kidogo huchachua donge zima.
1Wakorintho 10:31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo
lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Very Matunda-0746194783
“ Vijana hukusanyika kuimba na, ingawa wanaojiita wakristo, mara nyingi
hawamheshimu Mungu na Imani yao kwa maongezi yao ya upuuzi
na uchaguzi mbaya wa muziki. Muziki mtakatifu hauna ladha nzuri
kwao. Nilielekezwa kutazama mafundisho ya wazi ya neno la Mungu
ambayo hupitwa bila kutiliwa manaani. Katika siku ya hukumu maneno
haya yote yatawahukumu wale ambao hawakuyatii. ” Ujumbe kwa
Vijana Uk.279

Very Matunda-0746194783
Muandaaji: Very Robert Matunda
Mawasiliano: 0746194783-What’s Up
0678390688-Normal call/Text

You might also like