You are on page 1of 2

KAMA HUJUI KUFA TAZAMA MAKABURI! Je umewahi kuona makaburi? Bila shaka jibu lako ni ndiyo.

Ukipita huku na kule katika maeneo mbalimbali utaona makaburi, wengine wanaweka misalaba katika makaburi hayo, lakini makaburi mengine hayana misalaba lakini hilo siyo hoja kwa sasa, Makaburi hayo unayoyaona ni kutujulisha kuwa kuna watu waliokufa na kuzikwa humo. Neno la Mungu linasema (Waebrania 9:27)mtu amewekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu. Unasikia matangazo ya vifo katika radio, umeona tangazo la TANZIA katika ubao wa matangazo, unasikia misiba huku na kule, umeona na kushiriki katika msiba mmojawapo hayo yote ni kukujulisha kuwa kuna mtu au watu wamekufa na kuiacha dunia hii. Ndugu yangu, unapoona makaburi hayo, matangazo hayo ya vifo, Misiba hiyo, au kuona watu hawa wamekufa unaona kama wewe utaendelea sana katika dunia hii, usijue kuwa huenda wewe ndiye utakayefuata, Mhubiri 9:12Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafula. Itafika mahali wewe nawe utalazimishwa kustaafu kuishi maisha maisha ya dunia hii, utakufa na kuzikwa kama wengine na kaburi lako litaonekana. Je, utakufa lini? Huenda ikawa leo, huna hakika ya kuimaliza siku ya leo kwasababu maisha yako hayako mikononi mwako. Kama ukifa katika hali ya dhambi uliyo nayo sasa utaingia katika moto wa milele. Yatengeneze mambo yako, yamkini Maneno haya unayasoma kwa mara ya mwisho kabla ya kustaafu kuishi kwako hapa duniani.baada ya kufa kwako utaenda katika adhabu ya milele au katika uzima wa milele. Mathayo 25:46Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. Unajifahamu ni mwenye dhambi, huu ni wakati wako wa kuokoka(2 Korintho 6:2 siku ya wokovu ndiyo sasa). Fuatisha Sala hii ya toba kwa imani toka ndani ya Moyo wako.

Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Naomba msamaha kwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Nipe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia leo. Asante kwa kunisamehe, na kuniokoa, katika Jina la Yesu. Amen. Tayari umesamehewa dhambi zako, na hata ukifa sasa utaingia katika uzima wa milele bila shaka. Huna budi kutafuta Kanisa ambalo linahubiri wokovu, ili ulishwe Neno la Mungu na kushiba kiroho, ili wakati wowote uwe na hakika ya kuingia katika uzima wa milele. Ubarikiwe na BWANA.

You might also like