Professional Documents
Culture Documents
1.sababu za kimazingira
Hapa vipo visababishi vingi vya kimazingira vitakavyo
sababisha kati ya zile sauti tuzisikie
▪ mzunguuko wa hewa bandani unapokua mdogo
husababisha
▪ amonia (mbolea) panapokua na mbolea ambayo
ikazalisha amonia kwa kiwango cha juu lazima kuku
wako watapiga chafya
▪ baadhi ya chakula kinapokua na ulaini ambao
unaweza ukawasumbua kuku kipindi wanakula na
vivumbivumbi vikaingia kwenye mfumo wa hewa sauti
tufazisikia
2.Magonjwa
Sababu hii ndo imenifanya niandike juu ya swala
hili tunaloliita mafua.kuna magonjwa ambayo kuku
akiyapata yanapelekea kuharibu mfumo wa hewa na
kutoa viashiria vya (mafua)
● infectious bronchitis (IB)(nimeupa jina kata
mayai)
● Infectious laryngotracheitis (ILT) (nimeupa jina
koo damu)
● Infectious coryza
● Mycoplasmosis
● Avian influenza
● ornitho bacteriosis
● dalili ya awali ya Newcastle (kideli) nk.
Yapo magonjwa mengi yanayohusishwa na mafua
nitaongelea 6 kati ya hayo amboyo nimekutana nayo
kwa wafugaji na nimeona yanaathari kubwa.
MATIBABU
Magonjwa ya virusi kutibika ni ngumu
Hapa tunachotibu ni zile dalili za ugonjwa
zinazoonekana (tunayoita mafua)
Dawa
Tylodox(tylosin & doxycycline) from Holland
Ilifanya vizuri kwa mfugaji nilipo itumia kutibu mafua
(Matumizi sahii ya dozi hukupa matokeo mazuri zaidi).
◇USHAURI
Kwa wafugaji tz nawaomba tumieni ile chanjo ya New‐
castle +infectious bronchitis (mnaiita chanjo ya New‐
castle ilichanganyikana na ya mafua) hiyo mnayosema
mafua ndo huo ugonjwa sasa athari zake ni kubwa.
●
2. Infectious laryngotracheitis (ILT) (nimeupa jina
koo damu)
Ugonjwa no 2 nimeupa jina hilo pia naushuhudia athari
zake kwa kuku unaharibu sana njia ya hewa na kuvilia
damu kwenye koo la hewa unapenda kuambatana
e.coli inapotokea maambukizi ya pili ya bacteria na
kugandisha ute unaokua kwenye njia ya hewa na
kuziba njia ya hewa na kupelekea kifo.
MATIBABU
¿Magonjwa ya virus hayana dawa kesi hii nimejaribu
kutibu kwa dalili kutumia dawa za kutibu mfumo wa
hewa bila mafanikio vifo bado vinatokea nimejaribu
kutibu e.coli kumbunguza vifo
USHAURI
ugonjwa huu unaleta hasara kubwa kwa wafugaji
virusi hawa hufa kwa urahisi na dawa za kukinga
maambukizi shambani
Zile zinazotumiwa kufanya usafi mabandani na
zinawekwa milangoni kabala ya kuingia bandani.
Nashauri kufanya spray ya mazingira yako shambani
kila mwezi kutoruhusu muingiliano wa watu shambani
kuweka maji yenye dawa mlangoni kabla ya kuongia
bandani.
3.infectious coryza
Niugonjwa wa mfumo wa upumuji mara nyingi watu
huujua kama ugonjwa wa kuvimbisha kichwa .
DALILI
•Uvimbe wa uso.
• Kutokwa na machozi
• Kupiga chafya.
•Kuhema kwa shida (Dyspnoea). •Kupoteza hamu ya
kula
uzalishaji wa mayai kupungua kati ya 10-40%.
MATIBABU.
DAWA
Streptomycin,
Dihydrostreptomycin,
sulphonamides,
tylosin, (tylodox)
erythromycin.
Flouroquinolones
USHAURI
ugonjwa huu unaleta hasara kubwa kwa wafugaji
virusi hawa hufa kwa urahisi na dawa za kukinga
maambukizi shambani
Zile zinazotumiwa kufanya usafi mabandani na
zinawekwa milangoni kabala ya kuingia bandani.
Nashauri kufanya spray ya mazingira yako shambani
kila mwezi kutoruhusu muingiliano wa watu shambani
kuweka maji yenye dawa mlangoni kabla ya kuongia
bandani
4.Mycoplasmosis
Huu ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji
hasa unapendelea kwenye kuku wa broiler na layers
pia wanapata wenye umri wowote ule .unaweza
kuambukizwa kwenye mayai kama kuku mama atakua
anaumwa basi kifaranga kinauwezekano kikatotolewa
na kupata maambukizi kwenye yai.ni ugonjwa wa
(bacteria)
Kisababishi cha ugonjwa
Mycoplasma gallisepticum
Ushauri.
●
5. dalili ya awali ya Newcastle (kideli)
Nimeona niliweke hili kama sababu moja wapo ya
chanzo cha hayo tunayoita mafua Newcastle (kideli)
pia inaathiri mfumo wa upumuaji hivyo kuku akiathirika
na Newcastle ataonyesha ishara za awali kama
anamafua.
Ushauri.
Unapopta tatizo kuhusu mafua jaribu kuita mtaalamu
aweze kubaini ni aina gani ya mafua na dawa gani ni
nzuri ya kutibu
Imeandaliwa na..
Vet.chuma.
0694258206
0622359072
Instagram:vet_chuma