You are on page 1of 9

PID

Maana ya PID
Pelvic Inflammatory Diseas
Ni maambukizi na uvimbe unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke
inaweza kuwa sehemu moja au zaidi, maeneo ambayo yanaweza kupata
maambukizi haya ni uterasi, ovari na milija ya falopio
Hivyo PID ni uvimbe
unaotokea katika mrija huo.
Maambukizi haya kutokea ikiwa bakteria
wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa
kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba
(Uterus), mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na kwenye
ovari (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).
Dalili za PID
• Maumivu ya tumbo, na mgongo
• Maumivu wakati wa kujamiiana au kukojoa
• Hedhi isiyo ya kawaida, au kuongezeka kwa
maumivu wakati wa hedhi
• Kubadilika kwa hali Ya kawaida ya uke hasa kuvuja
damu wakati wa kujamiiana
• homa, baridi, kichefuchefu au kutapika
PID husababishwa na nini?
• PID husababishwa na maambukizi ya bakteria
kutoka kwenye shingo ya kizazi kwenda kwa viungo
vingine vya uzazi vya mwanamke. Sababu za
kawaida za PID ni magonjwa ya zinaa (STIs), mara
nyingi kisonono au na UTI za Mala kwa mala
• Mara chache zaidi, maambukizi yanaweza
kusababishwa na utoaji mimba, kuingizwa kwa vifaa
cha uzazi wa mpango kama vile vitanzi nk.
UTAGUNDUA VIPI KAMA
UNA PID?
• PID inaweza kugundulika kwa uchunguzi wa uke na
swabs ukeni na shingo ya kizazi (vaginal and cervical
swabs) .
• Vipimo vingine ni pamoja na kipimo cha damu,
kipimo cha mkojo na ultrasound.
• Mara chache zaidi, laparoscopy (kwa kutumia
kamera kuangalia ndani ya tumbo lako) pale
inapohitajika.
MATIBABU
• PID inatibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotics kwa
angalau siku 14. Wakati wa matibabu, inashauriwa
usifanye ngono.
• Iwapo wewe au mpenzi wako mtagunduliwa kuwa
na magonjwa yamtatakiwakuibiwa kutibiwa.
• Pia unaweza kuwasiliana na wenzi wako wa awali
ulio wahi kufanya nao tendo la ndoa ili kuwajulisha
nao wanapaswa kuchunguzwa magonjwa ya zinaa.
FAIDA YA KUTIBU PID
MAPEMA
• PID inapopatiwa matibabu mapema, hupunguza kwa kiasi
kikubwa hatari ya matatizo kama vile
• kupungua kwa uwezo wa kuzaa,
• maumivu ya tumbo ya muda mrefu,
• mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi kama vile kwenye
mirija ya uzazi,
• kuharibika kwa mimba,
• kuzaa kabla ya wakati na Mtoto kufia tumboni
• Wanawake walio na dalili kali za PID (homa, kichefuchefu,
kutapika) na wajawazito wanaweza kuhitaji kulazwa
hospitalini ili kupatiwa matibabu kwa kina.
Jinsi ya kunikinga na PID
Matumizi ya kondom ni
muhimu sana.
Kuwa waaminifu Kwa wenzi
wenu.
Kupima Mala kwa mala
magonjwa ya zinaa wewe
na Mwenzi wako.

Imeandaliwa na Sabbath
Mashenene
Source Family planing
NSW

You might also like