You are on page 1of 8

PELVIC

INFLAMMATORY
DISEASE (PID)
Solly and Flory Corporation

2023
Solly & Flory Corporation
www.sollydaddy92@gmail.com
www.hadassah5464@gmailcom
0769 567 263 / 0753 907 403

UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Disease)


Ugonjwa wa PID ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi
haya hutokea ikiwa bacteria wanaoambukizwa kwa njia nya kujamiiana watasambaa
kutoka kwenye uke kwenda kwenye mrija wa mimba (Uterus), mirija ya uzazi
(Fallopian tubes) na kwenye Ovary (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

PID inasababishwa na nini?

Ugonjwa wa PID husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kisonono


(Gonorrhea), na pangusa (Chlamydia). Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema,
mlango wa kizazi huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bacteria wasiweze kuingia katika
viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.

Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa
kuingia hasa kisonono (Gonorrhea), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kasha
hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bacteria kuingia na kufika
juu kwenye viungo vya uzazi.

Jinsi unavyoweza kuambukizwa ugonjwa wa PID

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa wa PID. Njia
hizo ni pamoja na;

 Kama una ugonjwa wa zinaa na haujatibiwa.


 Kufanya ngono zembe isiyo salama (Yaani kulala na wanaume tofauti tofauti).

~1~
 Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi nje.
 Kama umeshawahi kuwa na historia ya kuugua PID kabla.
 Maambukizi ya nje ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo
salama (Post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (Miscarriage)
 Maambukizi ya nje ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua
(Postpartum Period).
 Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo
ya uzazi wa mpango.
 Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
 Kutumia sana vidole wakati wa kusafisha uke (Excess Vaginal Douching).

Dalili za PID

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa wa PID miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na;

 Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu.


 Kupata maumivu ya mgongo.
 Mwanamke kupata majimaji machafu sehemu za siri, majimaji haya
huambatana na harufu mbaya.
 Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
 Kupata maumivu/kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
 Kutokwa na damu bila mpangilio wakati wa hedhi.
 Kupata homa mara kwa mara.
 Kutokwa na damu nje ya siku zako za kawaida za kupata hedhi.
 Wakati fulani kupata kichefuchefu kama mwanamke mjamzito na kutapika.

Matibabu ya PID

Matibabu ya PID kwa kutumia dawa yataondokana mara moja lakini hakuna njia ya
kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na PID.
Matibabu ya PID yaweza kuwa;

~2~
A. Antibiotics za kutibu PID

Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako. Utasubiri siku
kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.

Dawa za PID zinazotolewa na daktari ni pamoja na; Metronidazole tabs,


Doxycycline tabs na Cefixime tabs.

B. Kuacha kushiriki ngono kwa muda

Acha kushiriki tendo la ndoa hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.

Madhara ya PID

PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji
yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke, vitu hivi vinaweza
kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. Madhara yanayoweza
kutokea ni pamoja na;

I. Mimba nje ya mirija (Ectopic Pregnancy)

PID ndiyo sababu ya mimba kutunga nje ya kizazi, mimba huweza kutunga nje ya
kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya
husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea
kwenye nyumba ya mirija ya uzazi. Mimba nje ya uzazi husababisha utokaji wa damu
usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

II. Ugumba

Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba, kushindwa kupata


ujauzito. Kadri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi ndivyo hatari ya ugumba
inavyozidi, kuchelewa kupata tiba ya PID pia huongeza hatari ya ugumba.

III. Maumivu sugu ya nyonga

PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu miaka mingi.


Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu

~3~
wakati wa tendo la ndoa na wakati yai linapondondoshwa (Ovulation).

IV. Tubo Ovarian abscess

PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya mirija ya
uzazi na ovary, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi
kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha.

Madhara ya PID kwa mjamzito

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa mama mjamzito endapo atashindwa


kupata tiba ya PID mapema;

 Kujifungua kabla ya wakati.


 Ujauzito kuharibika.
 Kujifungua mtoto mwenye maambukizi na wakati mwingine hufariki muda
mchache baada ya kujifungua.
 Kujifungua mtoto mfu.
 Kuziba kwa mirija ya uzazi.

Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa PID

Kuna njia kadhaa za kuzuia ugonjwa wa PID. Njia hizi ni pamoja na;

 Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa zinapoanza


kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mpenzi wako ana dalili za magonjwa
ya zinaa au anatembea na wanawake wengi.
 Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vipimo vya uzazi, pamoja na vipimo vya
maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI) hususani
kwa mgonjwa wa Chlamydia, ufanye vipimo mara moja kwa mwaka mara moja.
 Kutoshiriki tendo la ndoa mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara
baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingi ya uzazi imefunga vyema.
 Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni kuacha ngono zembe na kufanya
ngono salama.

~4~
Dawa za asili za PID
Zifuatazo ni dawa za asili ambazo unaweza kuzitumia kutibu ugonjwa wa PID
unapokuwa katika mazingira yako ya nyumbani;

Kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu ugonjwa wa


PID. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria wanaosababisha ugonjwa wa PID.

Matumizi.

Chukua kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara mbili, menya nusu yake (Punje 10
au 15), menya punje moja moja na kasha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na
kisu na kasha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe viwili kila unapoenda
kulala na kila unapoamka asubuhi kwa siku 7, baada ya hapo hautakuwa na
maambukizi tena ya PID.

Binzari ya manjano.

Binzari ya manjano pia ni mojawapo ya dawa ya asili ambayo hutumika kutibu


ugonjwa wa PID.

Matumizi

Chukua kijiko kimoja cha binzari ya manjano iliyosagwa, kisha koroga kwenye glass
yenye asali mbichi vijiko viwili na maji, baada ya hapo kunywa mchanganyiko huo wa
asali mbichi, binzari na maji, asubuhi na jioni kwa muda wa siku 7.

Baking soda.

Kama ukikosa kitunguu swaumu au binzari ya manjano unaweza kutumia baking soda
kama dawa ya kutibu maambukizi ya PID.

Matumizi

Chukua nusu kijiko au kijiko kimoja cha baking soda, kisha koroga kwenye glass
yenye maji ya vuguvugu, baada ya hapo kunywa mchanganyiko huo wa baking soda na
maji ya vuguvugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili.

~5~
Mbegu za mlonge

Vitamini, madini, na homoni muhimu zilizomo kwenye mbegu hizi huufanya mwili wako
kuwa na usawa unaohitajika kiafya na hivyo kukupa kinga dhidi ya magonjwa mengi
bila idadi ikiwemo PID.

Matumizi

Cukua punje 3 za mbegu za mlonge na uzimenye ganda lake la juu kila moja, kisha
tafuna zile mbegu zake za ndani, ukimaliza kuzitafuna kunywa maji ya kawaida glass
2 (nusu lita), usinywe maji ya baridi yaliyotoka kwenye friji. Fanya hivi kutwa mara
tatu.

Kielelezo 1: Kitunguu swaumu

Kielelezo 2: Binzari ya manjano

~6~
Kielelezo 3: Baking soda

Kielelezo 4: Mbegu za mlonge

Prepared by Mr Solima and Ms Florida

Solly & Flory

©2023

~7~

You might also like