You are on page 1of 8

Jarida la kilimo endelevu Afrika Mashariki Toleo la 65, Februari 2018

Fuata ratiba na chanjo sahihi katika Kilimo cha mbogamboga 2


ufugaji wa kuku Lishe kwa ng’ombe wa maziwa 7

Picha: IN
Umuhimu wa punda 8

Mpendwa mkulima
Mara nyingi wakulima na wafugaji
wamekuwa wakianzisha miradi mbalimbali
wakiwa na lengo la kupata mafanikio kwa
kiwango cha juu na kwa haraka.
Jambo hili ni jema sana kwa kuwa
kila mradi unaoanzishwa lengo ni kupata
mafanikio, huku mradi huo ukisaidia
kupunguza na hatimae kuondokana na
umaskini kabisa.
Pamoja na malengo hayo mema kwao
na jamii nzima, kuna baadhi ya mambo
Ni muhimu kuhakikisha kuku wanapata chanjo kwa wakati muhimu ambayo husahaulika kuzingatiwa
pale miradi inapoanza na hata kutekelezwa
Ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli Pamoja na hayo, wafugaji wengi
kwa kiwango kikubwa.
ambayo imekuwa maarufu sana nchini wamekuwa wakianguka kwa Baadhi ya mambo hayo ni uzingatiaji
Tanzania. Kazi hii imekuwa ikifanywa kutokufahamu na kutokuzingatia wa suala zima la afya ya binadamu pamoja
na watu wa kada zote bila kujali ni chanjo muhimu zinazohitajika kwa na wanyama, halikadhalika utunzaji wa
wakulima, wafugaji, wafanyabiashara kuku. mazingira.
au waajiriwa. Ni muhimu sana kufahamu na Ni dhahiri kuwa bila uwepo wa siha
Halikadhalika imekuwa ni chanzo kufuata ratiba sahihi ya chanjo njema, hatuwezi kusema kuwa mradi wako
uwe wa kilimo au ufugaji umefanikiwa
kikubwa cha kipato miongoni mwa zinazohitajika kwa kuku tangu
kwa kiasi kikubwa.
vijana wa rika zote. Hii ni kwa sababu wakiwa vifaranga. Pengine tunaweza kusema kuwa
ni mradi rahisi lakini wenye pato la mradi huo haukuwa na mafanikio kwa
uhakika wakati wote. Zaidi soma Uk 3 kuwa haukujali uzingatiaji wa afya ya
walaji, wanyama na hata mazingira
Tahadhari: Mlipuko wa Viwavi Vamizi yanayouzunguka.
Wakulima nchini Tanzania Ili kuhakikisha hayo yote yanafanyika,
wametakiwa kuchukua tahadhari ni vyema mkulima na mfugaji kabla
Picha: IN

juu ya mlipuko wa wadudu ya kuanzisha mradi wa aina yoyote


wanaoshambulia mazao ya nafaka akatafakari kwa kina, ni changamoto
wajulikanao kama viwavi jeshi (Fall zipi za kiafya kwa maeneo tajwa ambazo
Army Worm). anaweza kukutana nazo na ni kwa namna
MkM kwenye mtandao gani anaweza kukabiliana nazo!
Kwa mfano endapo ng’ombe au mbuzi
Njia ya mtandao yaani internet,
watashambuliwa na aina fulani ya
inawasaidia wale wote ambao hawana
Viwavijeshi hushambulia mazao kwa magonjwa unapaswa kufahamu ni njia
namna ya kupata machapisho ya
haraka mno gani salama utakayotumia kukabiliana na
Mkulima Mbunifu moja kwa moja,
kusoma kwenye mtandao na hata Tahadhari hiyo imetolewa hivi changamoto hiyo.
kupakua nakala zao wao wenyewe. karibuni na watafiti waandamizi Endapo ni uzalishaji wa mazao ni
wa kituo cha utafiti wa viuatilifu na muhimu kujua ni aina gani ya mbegu
mkulimambunifu.org wadudu TPRI mkoani Arusha.
http://issuu.com/mkulimambunifu pamoja na njia za kukabiliana na wadudu
Imeelezwa kuwa Tanzania na magonjwa utakazotumia.
http://www.facebook.com/mkulimam- imekuwa ikikumbwa na mlipuko wa
bunifu Katika toleo hili tunakueleza kwa
viwavi jeshi katika miezi ya April na
Mei. ufasaha namna unavyoweza kuzingatria
https://twitter.com/mkulimambunifu chanjo za kuku na hatimae kuwa na mradi
+255 785 496 036 Zaidi soma Uk 6 wenye ufanisi mzuri.

MkM, S.L.P 14402, Arusha, Simu 0717 266 007, 0785 133 005 Barua pepe info@mkulimambunifu.org, www.mkulimambunifu.org
Toleo la 65, Februari 2018
Kanuni za kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu
Dawa za asili zinafaa zaidi katika kukinga
bustani za mboga dhidi ya wadudu

Picha: MkM
waharibifu na magonjwa.

Patrick Jonathan

Kabla hujaamua kutumia madawa


ya kienyeji kwenye kilimo
chambogamboga, hakikisha unafanya
mambo yafuatayo katika shamba lako:
• Chagua eneo lisilokuwa na
magonjwa ya mboga unazotaka
kuzalisha.
• Hakikisha unatumia mbegu
bora, kwani baadhi ya magonjwa
hutokana na mbegu.
• Hakikisha kuwa vitalu, bustani na
Hakikisha bustani ya mboga ni safi wakati wote kuepuka wadudu na magonjwa
sehemu ya kuhifadhia mboga ni
safi. Zifuatazo ni baadhi ya kanuni za dawa kabla ya kuchanganya dawa
• Uchafu na magugu huvutia kutumia dawa za asili na maji, ili dawa iweze kutoka
magonjwa na wadudu waharibifu. • Epuka Kupiga dawa ya aina vizuri.
• Toa majani au mimea iliyoathiriwa moja mara kwa mara dhidi ya • Nguvu ya madawa pia
na ugonjwa, na uiteketeze au ugonjwa au mdudu wa aina moja. hutofautiana sana, katika uwezo
ifukie. Hii hufanya hivyo kwa wadudu wa kuua wadudu. Changua dawa
• Panda mazao muda unaotakiwa kujenga usugu dhidi ya dawa hizo. zinazofaa kufuatana na ugonjwa
ili kukwepa baadhi ya magonjwa • Epuka kupiga dawa wakati wa na wadudu.
ya msimu. upepo mkali au jua kali kwani Baadhi ya dawa za asili
• Epuka kupanda mboga za jamii kiasi kikubwa cha dawa kinaweza Kuna aina nyingi za dawa za asili
moja katika eneo moja kwa misimu kupotea hewani. zinazotumika nchini, na baadhi ya
mingi mfululizo. • Usipige dawa wakati wa mvua mimea inayotoa madawa ya asili,
• Changanya mazao au mimea (mara tu kabla ya mvua), kwani ambayo yameshajaribiwa Tanzania
ambayo inafukuza magonjwa maji ya mvua yataosha na ni pamoja na muarobaini (mbegu na
na wadudu kama vile mimea kupunguza nguvu ya dawa. majani), kitunguu swaumu, tumbaku,
inayotoa harufu. • Piga dawa wakati wa asubuhi hasa pilipili kali, pareto, n.k.
• Epuka kuchanganya mboga na kukinga magonjwa ya ukungu Muarobaini ni miongoni mwa mimea
baadhi ya mazao yanayovutia yapendayo unyevunyevu. michache ambayo mpaka sasa
wadudu au magonjwa, katika • Ili kuzuia wadudu, ni vizuri kupiga imefanyiwa utafiti wa kina. Mfano;
bustani yako. Mfano mazao kama dawa wakati wa jioni. Wakati wa Unaweza kuchanganya nusu kilo ya
mipapai na bamia huvutia inzi jioni dawa huua wadudu zaidi mbegu za muarobaini zilizotwangwa
wadogo weupe wanaoeneza kwani hukaa muda mrefu juu katika lita ishirini za maji na dawa
ugonjwa wa “ukoma wa nyanya”. ya majani kabla ya nguvu yake hii husaidia kuua wadudu mbalimbali
• Mwisho, tumia dawa za asili kuharibiwa na jua. wakiwemo funza wanaotoboa
na viwandani zisizokuwa na • Weka kiwango cha dawa kama matunda ya nyanya.
madhara ili kupunguza kuenea ilivyo elekezwa. Kiasi kidogo cha Ubora wa dawa za asili
kwa magonjwa na wadudu. dawa katika maji hufanya viini vya Madawa ya asili ni bora zaidi kuliko
Kanuni za kukinga magonjwa na magonjwa na wadudu kuwa sugu. dawa za viwandani, kwani sumu yake
wadudu kwa kutumia madawa • Nyunyiza dawa ya kutosha ni kidogo na hupungua haraka baada
Unalazimika kukinga mboga dhidi ya sehemu zote za mmea kwani ya kupiga dawa.
magonjwa na wadudu kwa kutumia baadhi ya wadudu au magonjwa Hivyo ni salama zaidi kwa mpigaji
madawa ya asili, pale mbinu nyingine hukaa na kushambulia sehemu ya dawa na mlaji wa mboga. Hivyo
ambazo zimetajwa hapo nyuma chini ya majani. kupendekezwa katika kilimo hai na
zinaposhindwa kuleta mafanikio. • Andaa vizuri bomba la kupigia hifadhi ya mazingira.
Mkulima Mbunifu ni jarida huru kwa jamii ya wakulima zwa na Biovision (www.biovision.ch) kwa Mpangilio Ibrahim Isack, +255 676 293 261
Afrika Mashariki. Jarida ushirikiano na Sustainable Agriculture Tan- Zenith Media Ltd
Mhariri Msaidizi Flora Laanyuni
hili linaeneza habari za zania (SAT), (www.kilimo.org), Morogoro. Mhariri Ayubu S. Nnko
kilimo hai na kuruhusu Jarida hili linasambazwa kwa wakulima Mhariri Mkuu Venter Mwongera
majadiliano katika nyanja bila malipo. Anuani Mkulima Mbunifu
zote za kilimo endel- Mkulima Mbunifu linafadhiliwa na Biovision - www. Sakina, Majengo road, (Elerai Construction
biovision. block) S.L.P 14402, Arusha, Tanzania
evu. Jarida hili linatayar- Ujumbe Mfupi Pekee: 0785 496 036, 0766
Wachapishaji African Insect Science for Food and 841 366
ishwa kila mwezi na Mkulima Mbunifu,
Health (icipe), S.L.P 30772 - 00100 Nairobi, KENYA,
Arusha, ni moja wapo ya mradi wa Piga Simu 0717 266 007, 0785 133 005
Simu +254 20 863 2000, icipe@icipe.org, www.icipe.
mawasiliano ya wakulima unaotekele- Barua pepe info@mkulimambunifu.org,
org
www.mkulimambunifu.org
Toleo la 65, Februari 2018
Chanjo muhimu na kinga za wadudu na magonjwa yanayoshambulia kuku
Kwa muda mrefu sana wafugaji wengi
wa kuku wamekuwa wakikumbana na

Picha: MkM
changamoto za wadudu pamoja na
magonjwa yanayoshambulia kuku. Hali
hii imekuwa ikisababisha hasara kubwa
inayowakatisha tamaa wafugaji

Amani Msuya

Katika Jedwali hili utaweza kufahamu


baadhi ya magonjwa na wadudu
wanaoshambulia kuku, ni namna ya
kukabiliana nao kwa urahis kabisa,
jambo litakalokuwezesha kuepukana
na hasara. Ni rahisi kuku kushambuliwa na magonjwa na kusababisha hasara wasipo chanjwa

2. Siku ya 7
Ugonjwa Utaratibu wa Kinga Vifaranga wapatiwe chanjo ya Kideri
Mdondo Kuku wote wachanjwe kila baada ya miezi mitatu. (Newcastle). Chanjo hii huchanganywa
Ndui Chanjo hii ni ya sindano, itolewe na mtaalamu kabla ya na maji safi katika eneo lenye kivuli
mvua za muda mrefu kuanza. kisha kupewa vifaranga kwa muda
wa masaa mawili, kisha toa maji hayo
Ukosefu wa Wapatie kuku majani mabichi au mchicha mara kwa mara.
na kuyamwaga mbali na eneo ambalo
Vitamin A Kama hakuna majani wapatie vitamini za kuku toka duka
kuku wengine wanaweza kuyafikia, au
la dawa za mifugo katika pumba au maji ya kunywa kama kuyachimbia. Baada ya hapo vifaranga
utakavyoshauriwa na mtaalamu. wapewe maji yenye mchanganyiko wa
Koksidiosisi Safisha banda kila siku na hakikisha hakuna unyevu vitamini.
sakafuni. Wapatie kuku dawa za kinga kama”Amprolium”
3. Siku ya 14
au Salfa kwa siku 3 mfululizo,mara wafikishapo umri wa Wapewe chanjo ya Gumboro(IBD).
siku 7. Chanjo hii pia huchanganywa katika
Viroboto, Mwagia majivu katika banda na hasa viota vya kutagia maji na kupewa vifaranga kwa muda
Chawa, Utitiri ili kukinga wadudu. Tumia dawa za dukani kama vile wa masaa mawili tu.
“Akheri Powder” na ‘Sevin Dust’ kumwagia kuku mwilini Baada ya hapo vifaranga wapewe
na katika mazingira. Paka mafuta ya taa kwa kutumia mchanganyiko wa vitamini. Kuku
unyoya wa kuku kwenye viroboto vinavyoonekana. waliokufa kwa ugonjwa huu, unaweza
kuwatambua kwa kuchana vifua vyao
Chanjo muhimu na ratiba yake kwa Chanjo na ratiba maalumu na hapo utaona vidoti vyekundu.
kuku 1. Siku 1
4.Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Ili kuweza kuwa na ufugaji wa kuku Baada ya vifaranga hutotoleshwa,
Rudia chanjo ya Kideri (Newcastle)
wenye tija. Ni muhimu kwa mfugaji ndani ya siku moja wapewe glucose
kwa muda wa masaa mawili. Glucose 5. Siku 28 (Mwezi)
kuhakikisha kuwa anafahamu na
huchanganywa katika maji na kupewa Rudia chanjo ya Gumboro IBD
kuzingatia chanjo na ratiba kwa kuku
vifaranga hawa na baada ya hapo 6. Siku 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
wake.
vifaranga wapewe mchanganyiko wa Kipindi hiki kuku wapewe
Endapo mfugaji atashindwa kuwapatia vitamini mfano ni Aminovit na OTC mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
kuku chanjo kwa kufuata ratiba hii ni plus.
dhahiri kuwa atakuwa katika hatari 7. Wiki ya 6-8
Pia hii huchanganywa na maji.
Kuku wapatiwe kinga ya Ndui (fowl
kubwa ya kupoteza mifugo hao kwani Vifaranga wawekwe katika eneo lenye pox). kinga hii sio rahisi kwa mfugaji
hawataweza kustahimili magonjwa. joto la wastani na safi. asiye na utaalamu kuwapa kuku,
tafuta mtaalamu wa mifugo kwa kazi
hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka
kinga hii.
8. Wiki ya 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama
Piperazzine na baada ya hapo unaweza
kurudia chanjo ya Newcastle.
Inaelndelea Uk 8
Chanjo ya kideri Dawa ya minyoo
Toleo la 65, Februari 2018
Jesca: Zalisha aina mpya ya maharangwe yenye madin
Jesca ni aina mpya ya maharagwe chuma na zinki ambayo ni madini
ambayo imefanyiwa utafiti na kituo cha muhimu katika mwili wa binadamu
utafiti Seliani Arusha, na inatarajiwa kwani husaidia kuongeza damu,
kusambazwa kwa wakulima katika ukanda na madini ya zinki husaidia kina
wa kaskazini mwa Tanzania mama kutokuzaa mtoto njiti( Mtoto
anaezaliwa kabla ya wakati wake).
Ayubu Nnko
Maharagwe haya yana madini ya
chuma kiasi cha kati ya 50% - 70% na
Maharagwe ni zao muhimu
madini ya zinki yatasambazwa. Na
katika kanda ya kaskazini na nchi
hivi karibuni katika ukanda wote wa
ya Tanzania kwa ujumla. Zao hili
kaskazini mwa nchi ya Tanzania, hasa
hutumika kama chakula kwa
katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro,
kutowelea vyakula mbalimbali kama
Arusha na Manyara.
ugali, wali, makande na vinginevyo,
Matayarisho na uzalishaji wa aina
huku majani yake yakitumika kama
hii ya maharagwe unafanyika kwa
mboga za majani.
kufuata kanuni na taratibu kama
Hivi sasa zao la maharagwe
ilivyo kwa uzalishaji wa aina nyingine
limeanza kuwa zao la bishara hasa
za maharagwe.
katika maeneo ambayo hayana mazao
ya kudumu ya biashara. Utayarishaji wa shamba
Majani ya mahagarafwe baada Shamba litayarishwe kwa kuondoa
ya kukauka yamekuwa ni chanzo magugu yote kwa kutumia jembe
muhimu cha kumuongezea mkulima la trekta, jembe la kukokotwa na
kipato, ambapo hufungwa na kuuzwa wanyama au jembe la mkono.
kwa bei ya juu kama chakula cha
Kupanda
mifugo.
Wakulima walio wengi wamekuwa Mkulima ahakikishe kuwa anapanda
wakipata mavuno haba kutokana mbegu bora zilizopendekezwa na
na sababu mbalimbali, moja wapo wataalamu, kulingana na kanda
ikiwa ni kutokununua mbegu bora ilivyoshauriwa na wataalamu. Shamba la maharagwe likitunzwa vyema mk
za maharagwe, kutokuzingatia Si vyema kupanda mbegu za
njia mbalimbali za matunzo kienyeji au kurudia rudia mbegu Mfumo wa uoteshaji
zinazopendekezwa, kutokufahamu ambazo zilikwishapandwa, kwani 1. Kilimo MSeto-Mahindi
namna ya kuwadhibiti wadudu na kwa kufanya hivyo utapoteza uhalisia • Nafasi kati ya mstari wa
magonjwa ya maharagwe. wa zao unalokusudia kuzalisha. mahindi ni sentimita 75 au
90.
Jesca Sifa za Jesca
• Panda mstari wa maharagwe
Katika makala hii tutaeleza namna • Aina hii ya maharagwe inastawi kati ya mistari miwili ya
nzuri ya kuzalisha maharagwe aina ya vizuri katika ukanda wa kati. mahindi.
Jesca ambayo yamefanyiwa utafiti na • Inavumilia magonjwa kama vile • Nafasi kati ya mashimo ya
kituo cha utafiti wa mazao na kilimo ndui, madoa pembe, na kutu maharagwe iwe sentimita
Seliani, kilichopo mkoani Arusha. • Inakomaa katika kipindi cha siku 15, kama nafasi ya mstari
Aina hii ya maharagwe 80-85. wa mahindi ni sentimita 75.
inayojulikana kama Jesca imefanyiwa • Inauwezo wa kuzalisha kati ya • Kama nafasi ya mstari wa
utafiti na kuongezewa madini ya magunia 10-12 kwa ekari moja. mahindi ni sentimita 90,
nafasi kati ya mashimo ya
Picha:MkM

maharagwe iwe sentimeta


10.
• Panda mbegu mbili za
maharagwe kwa kila shimo.
2. Kilimo kisicho cha mseto
• Panda Maharagwe kwa
kutumia kipimo cha
sentimita 50 kati ya mstari
wa maharagwe.
• Panda maharagwe sentimita
20 kutoka shimo hadi shimo.
• Katika kilimo kisicho
cha mseto, kama nafasi
zilizopendekezwa
zikizingatiwa, mkulima
atakuwa na idadi ya mimea
ipatayo 200,000 kwa hekari
Mbegu mpya aina ya Jesca inatarajiwa kuachiwa na kusambazwa kwa wakulima hivi karibuni moja.
Toleo la 65, Februari 2018
dini ya chuma na zinki kukabiliana na athari za kiafya
• Zingatia kilimo mzunguko. chandarua au turubai au mahali

Picha: MkM
Shamba ambalo maharagwe safi juu ya ardhi iliyofagiliwa
yalishambuliwa na magonjwa vizuri.
msimu uliopita, lisirudiwe • Piga kwa kutumia mti kuondoa
kupandwa maharagwe msimu mbegu katika ganda lake. Hii
unaofuata. Panda mazao mengine inaweza kufanyika yakiwa
katika shamba hilo kama vile sehemu ya kuanikia au kwa
mahindi au viazi, kwa muda wa kuweka kidogo kidogo kwenye
miaka miwili hadi mitatu. gunia.
• Panda aina bora za maharagwe • Baada ya kuyapiga ondoa
zinazostahimili magonjwa na takataka zote kwa mkono na
ukame. kupeta.
Kuzuia wadudu
1. Wadudu wa shambani
Maharagwe ya Jesca Kiafya
• Fanya kilimo cha mzunguko. Kama ilivyoelezwa hapo awali,
• Panda mapema mara maharagwe aina ya Jesca yamefanyiwa
msimu unapoanza. utafiti na kuongezewa madini ya
• Fanya kilimo mseto. chuma na zinki. Hii imefanyika
• Panda aina za mbegu za makusudi ili kuweza kusaidia
maharagwe zinazostahimili kuboresha afya ya walaji, hasa mama
wadudu. na mtoto.
• Unaweza kutumia dawa Inaelezwa kuwa nchini Tanzania,
upungufu wa damu huathiri asilimia
zifuatazo kwa maharagwe
58 ya watoto wenye umri wa miezi
yatakayotumika kama
6-9.
mbegu, Rogor, Karate, Halikadhalika asilimia 45 ya wanawake
Nimbicide ili kuzui inzi wa walio katika umri wa kuzaa (15-49)
maharagwe na wadudu hukabiliwa na upungufu wa madini
wa mafuta. Unaweza pia ya chuma, na hii inachukuliwa kuwa
a mkulima anauhakika wa mavuno yenye tija kutumia dawa za asili ni chanzo kikubwa cha upungufu wa
zinazofaa kuhifadhia damu mwilini.
3. Mbolea mbegu.
Maharagwe hustawi vizuri Athari za upungufu wa damu
na kutoa mazao mengi 2. Wadudu wa ghalani mwilini
• Vuna kwa wakati unaofaa. Upungufu wa damu mwilini
kama yakipata mbolea ya
• Kausha maharagwe vizuri. unaweza kuongeza athari za
kutosha. Mkulima anaweza
• Safisha ghala kabla ya vifo wakati wa kuzaliwa watoto,
kutumia samadi au mbolea za kuhifadhi. kuzaliwa njito (mtoto kuzaliwa kabla
chumvichumvi. • Kwa maharagwe ya chakula ya kufikisha siku zake), kuwa na
Tumia kiasi cha tani 2-4 za tumia Actelic Dust. uwezo mdogo wa kumbukumbu na
mboji au Samadi kwa ekari moja, • Kwa maharagwe ya mbegu kujifunza.
na uchanganye vizuri kwenye tumia Mwarobaini au Apron Makala hii imetayarishwa kwa
shamba wakati wa kulima. Star. kushirikiana na kituo cha utafiti
Endapo utatumia mbolea za wa kilimo Seliani Arusha na Shirika
Kuvuna
chumvi chumvi fuata maelekezo la CIAT(Tz). Kwa maelezo Zaidi
• Vuna maharagwe wakati
kama utakavyoelekezwa na yamekauka vizuri. unaweza kuwasiliana na Jovinus
wataalamu kabla ya kutumia. • Kama hayajakauka vizuri yang’oe Mbowe (SARI) +255682097870 na
Palizi na kuyaanika juu ya mkeka au Lazaro Tango(CIAT) +255 769539470.
• Hakikisha shamba halina magugu
Picha: SARI

wakati wa kupanda.
• Palizi ya kwanz ifanyike wiki
mbili baada ya kupanda, na ya
pili kabla ya maua kuchanua
kwa wale wanaotumia jembe la
mkono.
• Kwa wale wanaotumia dawa
za kuulia magugu, fuata kama
inavyoelekezwa na wataalamu
kwa usalama wa chakula na afya.
Kuzuia magonjwa
• Tumia mbegu safi ambayo
haina magonjwa. Ni muhimu kupepeta maharagwe ili kuondoa taka kabla ya kuhifadhi
Toleo la 65, Februari 2018
Namna ya kudhibiti kiwavi vamizi-Fall Armyworm (FAW)
Huyu ni mdudu vamizi (Spodoptera
frugipedra) asiye na mipaka ambaye asili
yake ni Amerika ya kitropiki hadi Argentina

Picha: IN
na maeneo ya Caribbean (Johnson 1987,
Pogue 2002).

Flora Laanyuni

Kiwavi vamizi hushambulia mimea


ya aina nyingi, yaani takribani mimea
80 na hupendelea zaidi nafaka kama
vile mahindi, uwele, mpunga, shayiri,
ngano na miwa.
Kiwavi huyu huruka hadi 100km
kwa siku na 2000km kwa maisha
yake.
Kiluilui ana hatua sita za ukuaji
na huishi siku 14 hadi 28. Jike hutaga
mayai mpaka 2000 katika maisha
Viwavijeshi huharibu mazao ya nafaka na kusababisha hasara kubwa kwa mkulima
yake na huwa na vizazi 6 hadi hadi
12 kwa msimu. huweka mashimo kwenye jani. machanga na kulazimika kurudia
Ugunduzi • Katika hatua ya nne hadi ya sita, kupanda upya,
Kiwavi vamizi aligunduliwa kuwepo kiluilui hufanya mashambulizi • Hushambulia majani, huzuia
Afrika mwanzoni mwa 2016 (Benin, makubwa ya jani na kuacha bua ukomaaji wa punje na uharibifu
Nigeria, Sao Tome na Togo). na kambakamba. wa mbelewele.
Katika baadhi ya maeneo wakulima • Aina hii ya kiwavi hushambulia • Matumizi holela ya viuatilifu
wamelazimika kupanda upya wakati wa usiku na mchana lakini huharibu mazingira na gharama
mahindi baada ya uvamizi wa kiwavi hasa asubuhi na jioni. ya uzalishaji.
huyu (FAW). Wakulima hupoteza • Mara nyingine kiluilui hutoboa • Kama kiwavi huyu asipo
maelfu ya hekari za mazao endapo hata toto la muhindi lakini pia dhibitiwa anaweza kusababisha
watavamiwa na mdudu huyu. hushambulia punje kama kiwavi hasara ya takribani 100%.
wa gunzi. (Tofauti na kiwavi wa
Utagaji wa mayai Kwa mfano;
gunzi anayeshambulia toto la
Mayai hutagwa wakati wa usiku • Zambia, wametenga kiasi cha
muhindi kutoka juu ya nywele
katika mafungu (cluster) ya 100 hadi dola milioni 3 mwaka 2017 kwa
yeye hushambulia kutoka
300 mpaka 1000 hadi 2000 kwa jike ajili ya kupanda upya maeneo
ubavuni).
mmoja). yalioadhirika.
• Kiluilui mkubwa huingia kwenye
Mayai hufichwa na utando • Serikali ya Ghana kiasi cha dola
bua la muhindi na kujificha (hii
(protective grey-pink scales of abdominal milioni 4 kwa mambo ya dharura.
humkinga dhidi ya viuatilifu).
bristles) • Serikali ya Rwanda imetumia
Mayai ni ya mviringo na hutagwa • Baadaye kuluilui huyo hukimbilia
askari wa jeshi kusaidia
chini ya jani na yai huanguliwa baada kwenye toto la muhindi, mmea
maangamizi ya wadudu hawa.
ya siku 2 hadi 5. unapoanza kutoa mbelewele na
Ushahidi huu unaonesha kuwa, kama
kuanza kulishambulia.
Kiwavi vamizi kipepeo (FAW) wakulima hawatapewa mbinu ya
Kipepeo hutokeza wakati wa usiku Madhara ya FAW kiuchumi kudhibiti hili tatizo litakua kubwa
na kuna tofauti kati ya dume na jike. Tangu avamie bara la Afrika, sana Afrika, hasa pale wakulima
Mabawa ya kipepeo dume huwa ameshasababisha hasara kiasi cha wanapojiamulia kutafuta mbinu zao
na alama ya pembe tatu nyeupe, kona takribani $13.383 milioni kwa mazao wenyewe.
ya pembeni na katikati. kama mahindi, mtama,mpunga na
Mbinu za udhibiti wa FAW
Mabawa ya kipepeo jike ni ya rangi miwa (CABI, 2017).
• Kilimo bora mfano kupanda kwa
ya kahawia yote na mabakamabaka. Hii ni ukiachilia mbali aina 80 ya
wakati.
mimea inayoushambuliwa na mdudu
Athari katika ukuaji wa mahindi • Matumizi ya mbegu kinzani
huyu. Pia mashamba ya mbegu.
• Katika hatua ya kwanza, kiluilui (tolerant/resistant varieties).
hula upande mmoja wa jani na Madhara ya FAW • Matumizi ya viumbe rafiki kwa
kuacha upande mwingine hali • Hushambulia mahindi machanga kuwaleta nchini mfano; Telenomus
angavu. mpaka hatua ya kukomaa. remus, Trichogramma. Sp na
• Kwenye hatua ya pili na ya tatu, • Anaweza kukata mahindi Diapetimorpha introit.
Toleo la 65, Februari 2018
Fahamu mahitaji muhimu kwa Ng’ombe ili wazalishe maziwa kwa wingi
Naitwa Vitalis Urio, ni msomaji wa
MkM na ninafurahia elimu inayotolewa

Picha:MkM
katika jarida hili. Ningependa kufahamu
ni mambo gani muhimu naweza kufanya
ili ng’ombe wangu wazalishe maziwa kwa
wingi?

Amani Msuya

Wafugaji walio wengi wamekuwa


wakitamani kuwa na ufanisi mkubwa
katika uzalishaji wa maziwa.
Jambo moja kubwa wanalokosea ni
kutokufuata kanuni na kuwapatia
ng’ombe virutubisho muhimu ili
waweze kuzalisha kwa tija.
Ni muhimu sana kuhakikisha
kuwa unawapa ng’ombe lishe kamili,
yenye nguvu, protini, na vitamini.
Tumia malisho bora
Kulisha ng’ombe kwa kutumia
aina yoyote ya malisho haitoshi
kukuhakikishia kuwa ng’ombe
anakuwa na afya nzuri na kutoa
maziwa ya kutosha.
Kama ilivyo kwa binadamu, Ng’ombe wanahitaji virutubisho na madini muhimu ili kuzalisha maziwa kwa wingi
ng’ombe anahitaji mlo kamili.
Malisho ni lazima yawe na uwiano Vyakula vya kutia nguvu calcium na phosphorous. Mimea ya jamii
sahihi wa viungo na virutubisho. Aina zote za majani ni chanzo kizuri ya mikunde na mengineyo isipokuwa
Mifugo inahitaji chakula cha vyakula vya kutia nguvu kwa nyasi yanatoa kiasi kikubwa cha
kitakachowapatia nguvu, protini, mifugo, endapo tu yatalishwa yakiwa calcium na madini mengineyo.
madini, na vitamin ili kujenga miili bado machanga. Pumba? Ndiyo lakini si kwa kiasi
yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Majani yaliyo maarufu kwa malisho kikubwa!
Wanyama wadogo wanahitaji ni pamoja na matete, ukoka, majani ya
virutubisho vya kutosha, ili wakue na Pumba aina ya Dairy meal ina kiwango
tembo, seteria na Guatemala. Majani ya kikubwa sana cha madini. Lakini
kuongeza uzito. mahindi au mtama ni chakula kizuri ina madhara kwa mifugo endapo
Ng’ombe wa maziwa wanahitaji sana kwa kuwapa nguvu mifugo. wanyama watalishwa kwa kiwango
virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha Vyakula vya kutia nguvu vilishwe kikubwa.
maziwa kwa wingi hasa katika kipindi kwa kiasi kidogo. Vyakula hivi
cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya Malisho yanayotokana na majani
vinaweza kutokana na aina zote za au nyasi kavu ni lazima yabakie
kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa nafaka, punje za ngano, au molasesi.
maziwa unakuwa juu. kuwa chakula kikuu kwa mifugo.
Vyanzo vya Protini Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6
Malisho ya kijani ni mlo mkuu kwa za pumba kwa siku kwa ng’ombe
mifugo Kanuni ya 1: Mimea michanga ina mwenye kilo 450.
kiasi kikubwa cha protini kuliko
Mlo muhimu na wenye virutubisho mimea iliyokomaa. Mahindi Ni lazima wapewe kwa kiwango
kwa mifugo ni majani. Malisho machanga pamoja na majani ya viazi kidogo sana, ambacho si zaidi ya kilo
bora ya kijani ni yale yanayoweza vitamu ni mahususi kwa protini. 2 kwa mara moja na kichanganywe
kumpatia ng’ombe wa maziwa na majani. Kuongeza kiwango
Kanuni ya 2: Mikunde ina protini
virutubisho muhimu vinavyohitajika nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, cha pumba kabla na wakati wa
mwilini. mabaki ya majani ya maharagwe, kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi
Malisho bora yanakuwa na sifa njegere, desmodium na lusina. Majani kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la
mbili muhimu; ni ya kijani kibichi yanayotokana na mimea kama lusina, mnyama lizoee.
na machanga, hii ina maana kuwa, calliandra au sesbania ina kiwango Wakulima wazoefu huongeza
majani ya malisho ni lazima yakatwe kikubwa cha protini pia.
na kuhifadhiwa yakiwa bado majani ya malisho na mbaazi
Ng’ombe wasilishwe kwa kutumia kwenye lishe ya mifugo. Wanaweza
machanga na kabla ya kuchanua. aina zote za jamii ya mikunde kwa hata kuacha pumba kwa muda au
Ni lazima mfugaji afahamu kuwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa kupunguza matumzi ya pumba
mimea ambayo imepoteza rangi yake mchanganyiko wa malisho ili
kuepuka matatizo ya kiafya. Aina kupitia njia hii.
halisi ya kijani, inaweza tu kuwasaidia
mifugo kuishi lakini haina virutubisho nyingine ya vyakula vyenye protini Utafiti unaonesha kuwa kilo 3 za
muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, ni mashudu ya pamba, mashudu ya malisho ya majani na chakula jamii
madini, protini na haiwezi kusaidia alizeti na soya. ya mikunde kama vile Desmodium au
katika uzalishaji wa maziwa. Madini majani ya viazi vitamu hutoa maziwa
Malisho yenye viwango vya sawa na kilo 1 ya pumba. Kwa hivyo,
Mifugo wanahitaji madini ya ziada. mfugaji anaweza kuokoa fedha
chini vya virutubisho ni lazima Ni lazima yapatikane muda wote,
yaongezewe kwa chakula cha ziada mfano kama jiwe la chumvi. Wanyama akalisha ng’ombe wake kwa kutumia
chenye virutubisho vya kutosha wanaokuwa, wenye mimba, na chakula cha jamii ya mikunde
kitakachoziba pengo la virutubisho ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji badala ya kununua aina nyingine ya
vilivyokosekana. kiasi kikubwa cha madini, mfano virutubisho.
Toleo la 65, Februari 2018
Ni muhimu kuzingatia afya na ustawi wa punda
Kwa miaka mingi punda amekuwa

Picha: MkM
mnyama aliye karibu sana na jamii zetu
hasa jamii za wafuugaji na wamekuwa
wakisaidia mambo mengi.

Ayubu Nnko

Moja wapo ya mambo ambayo punda


wamekuwa wakisaidia ni pamoja na
usafirishaji wa mizigo, shughuli za
kilimo, kufuata maji umbali mrefu
na shughuli nyinginezo nyingi za
nyumbani.
Pamoja na yote haya Punda
wamekuwa wakikumbana na
matatizo mengi kama kutokupewa
chakula cha kutosha na kwa wakati,
kukosa maji ya kunywa kupigwa,
uuaji na magonjwa ambayo
yanasababisha afya duni na kukosa
ustawi wa mnyama huyu.
Kama ilivyo kwa wanyama
wengine, punda nao wanahitaji Kama ilivyo kwa wanyama wengine ni muhimu punda kupatiwa chanjo ili kumkinga
kutunzwa vema kwa kupewa chakula dhidi ya magonjwa hatarishi kwa maisha yake.
bora kama nyasi na pumba pamoja na ya mwili na ya nje, ambayo kwa vidonda vinavyosababishwa
maji safi na yakutosha. na kutokuwa na matandiko
kiasi kikubwa huathiri afya kwa
Magonjwa na tiba kuzorotesha ukuaji, kupungua kwa au matandiko yaliyo na ubora
Punda hupata magonjwa mbali mbali damu mwilini pamoja na matatizo mdogo.
ikiwemo maumivu makali ya tumbo, mengine ya akili kama kuzunguka. • Si vema kumfanyisha kazi Punda
minyoo, pepopunda, vidonda, na Ni muhimu kuzingatia matumizi mwenye mimba zaidi ya miezi
ndorobo. minane au kabla hajafikisha miezi
Hivyo punda huhitaji kutibiwa bora na matunzo ya punda ikiwa ni mitatu baada ya kuzaa.
pale anapoonekana kuwa mgonjwa pamoja na; • Hakikisha Punda ana banda la
na baada ya kufanyiwa uchunguzi na • Punda abebeshwe mzigo
kupumzikia akiwa hafanyi kazi
dakitari wa wanyama na kupatiwa kutegemeana na umri na uzito na kulala nyakati za usiku.
tiba sahihi ili kuendelea kujali afya wake.
zao. • Punda apunguzwe kwato zake Kwa maelezo Zaidi juu ya ufugaji na
Chanjo zinapokua sana. matunzo bora ya Punda, unaweza
Kwa kawaida punda hupatiwa chanjo • Punda awekewe matandiko kuwasilianana na MAWO kupititia
ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, maalum kabla ya kuwekewa Bw. Johnson Lyimo kwa simu +255
ili kuweza kuzuia minyoo ya ndani mzigo mzito ili kumkinga na 755869619

Inatoka Uk. 3..... Chanjo na kinga muhimu kwa kuku


Fuata njia hizi kudhibiti magonjwa Mambo ya kujiepusha nayo katika chanjo kama umeme, sola au
ya kuku ufugaji wa kuku jenereta.
• Tunza hali ya usafi ndani ya banda Ni ukweli usiopingika kuwa katika • Kutibu kwa mazoea bila
na kudhiditi kusiwe na unyevu. ufugaji kuna baadhi ya mambo kuwasiliana na Afisa Mifugo.
• Badili matandazo kila wafugaji hufanya, lakini hayakupaswa • Kutembelea mabanda ya jirani bila
yanapochafuka. kufanyika. Yafuatayo ni mambo ya kuchukua tahadhari.
• Vyombo vya maji visafishwe kila kujiepusha nayo katika ufugaji:-
Madhara ya kuacha banda chafu
siku • Epuka Kuacha banda likiwa chafu.
Katika ufugaji jambo kubwa na
• Jitahidi uepuke kufuga kwa • Kuleta na kuingiza kuku wageni
muhimu ni kuzingatia usafi, bila usafi
njia huria ili kuku wako bila kujua historia ya chanjo
hata uwe unawapatia chakula cha aina
wasiambukizwe magonjwa walipotoka.
gani kuku hawawezi kufanya vizuri.
kirahisi • Epuka kuuza kuku wagonjwa.
• Epuka kufuga kuku wako pamoja • Epuka kuchinja kuku wagonjwa.
na bata na kanga.Hawa ni wabebaji • Epuka kununua kuku wagonjwa.
wa vimelea vya magonjwa ya • Epuka kutupa kuku waliokufa
kuku japo wao hubaki salama. porini.
Picha: MkM

• Zingatia ratiba za chanjo kwa • Epuka kununua chanjo kwa


magonwja yasiyo na tiba kama wauzaji wanaofahamika kuwa
kideri na mengineyo ya virusi hawana nishati inayotakiwa
kutumika katika uhifadhi wa Tumia wataalamu kuchanja kuku wako

You might also like