You are on page 1of 12

Mkulima Mbunifu

Jarida la Kilimo Endelevu Afrika Mashariki Toleo la 118 Oktoba 2023


Yaliyomo
Mwelekeo wa mvua za vuli na Maziwa mtindi
Wakulima Singida na kilimo ikolojia
3
6

tahadhari kwa wakulima/wafugaji

Kuhifadhi nafaka kwa njia sahihi 9


Uvunaji wa maji ya mvua 11

Mpendwa Mkulima
Kuna mzee mmoja aliwausia wanawe
kuwa, “mkitaka mali mtaipata
shambani”. Hii ni sahihi na kwa hakika
wakulima na wafugaji wamekuwa
mstari wa mbele katika kuthibitisha
kuwa mali hupatikana shambani kwani
hata uwe na shughuli nyingine yeyote ya
uzalishaji ni lazima utakula kilichotoka
shambani ili kuweza kuishi.
Wakulima hawa wanajitahidi katika
Picha:MkM shughuli zao za uzalishaji, ikiwa ni
pamoja kuzalisha mazao kwa wingi na
kwa njia salama na kuhudumia mifugo
yao kwa hali mali ili kufikia mafanikio
Kulingana na taarifa za Mamlaka ya wanashauriwa kupata ushauri ambayo wamekusudia.
Hali ya Hewa (TMA) katika msimu zaidi kutoka kwa maafisa ugani Hata hivyo pamoja na juhudi
huu wa mvua za vuli kunatarajiwa nyingi hizo, wakulima wanakutana na
kwa matumizi sahihi ya taarifa za
kuwepo kwa El-Niño ambayo italeta changamoto mbalimbali zinazozuia
utabiri wa hali ya hewa.
mchango mkubwa katika mvua za kufikia malengo yao kwa asilimia 100.
• Watumiaji wa taarifa hii Changamoto ambazo zinawakabili
msimu wa 2023. wanashauriwa kufuatilia utabiri wakulima na wafugaji katika shughuli
wa saa 24, siku 10, mwezi pamoja za uzalishaji ni pamoja na magonjwa
Mvua hizi za vuli 2023 zinatarajiwa na tahadhari kila zinapotolewa na
kuwa za juu ya wastani hadi wastani na wadudu ambayo huathiri mifugo na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. mazao wanayozalisha.
katika maeneo mengi ya pwani ya
• Wakulima wanashauriwa kuandaa Hili ni tatizo kubwa kwa kuwa huathiri
kaskazini na ukanda wa ziwa Victoria.
Aidha, kwa maeneo ya nyanda za mashamba, kupanda, kupalilia na uzalishaji kwa kiasi kikubwa sana.
Juu kaskazini mashariki na maeneo kutumia pembejeo husika kwa Mifugo kufa au kupunguza uzalishaji,
machache ya mashariki mwa ziwa wakati na kuchagua mbegu na mazao kuteketea, matumizi makubwa
Victoria mvua zinatarajiwa kuwa za mazao sahihi. ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na hali
wastani hadi juu ya Wastani. • Matumizi sahihi ya mbinu bora na hiyo, na kadhalika..
Mvua za Vuli, zinatarajiwa kuanza teknolojia za kuzuia maji shambani, Mkulima Mbunifu tunajitahidi
wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2023 mmomonyoko na upotevu wa kuwapa wakulima na wafugaji taarifa
katika maeneo ya magharibi mwa ziwa rutuba, vinashauriwa. sahihi za kilimo na mipango kazi ili
Victoria na kusambaa katika maeneo • Wafugaji wanashauriwa kutumia kuepuka changamoto hizo.
mengine mwezi Oktoba, 2023. mbinu bora za ufugaji ili kutunza Kwa msimu huu wa mvua za vuli
Kwa kawaida mvua za hizi huisha malisho na kuvuna maji ya mvua zinazotarajiwa kunyesha maeneo
mwezi Disemba, hata hivyo msimu kwa matumizi ya baadae. mengi ya nchi, ni rai yetu kwa wakulima
huu mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuhakikisha wanapata taarifa sahihi na
• Wavuvi na wafugaji wa samaki
kuendelea hadi Januari, 2024. kufuata ushauri unaotolewa na watabiri
wanashauriwa kuimarisha
wa hali ya hewa pamoja na wataalamu
Angalizo/Ushauri miundombinu ya uvuvi na ufugaji wa kilimo na ufugaji.
• Wakulima, wafugaji na wavuvi wa samaki.

Kwa uhitaji wa jarida hili wasiliana +255 717 266 007 Wasiliana na MkM,
http://www.facebook.com/mkulima_mbunifu
nasi kwa kutupigia simu au kwa http://twitter.com/mkulima_mbunifu S. L. P 14402, Arusha,
anwani kwa kupitia barua pepe, https://www.instagramu.com/mkulima_mbunifu Simu: 0717 266 007, 0762 333 876,
mkulimambunifu.org Barua pepe:
facebook, tovuti na sanduku la posta theorganicfarmer.org info@mkulimambunifu.org
kama zilivyoonyeshwa hapa; infonet-biovision.org
www.mkulimambunifu.org
Toleo la 118 Oktoba 2023

Faida na matumizi ya mbolea ya kijani


Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao
ambayo yanapandwa ili kuongeza

Picha:IN
rutuba kwenye udongo.
Brighton Shalua
Mazao ya mbolea ya kijani ya
jamii ya mikunde (ambazo ni zile
zinatengeneza mbolea ya naitrojeni
kutoka kwenye naitrojeni iliyopo
kwenye hewa) zinaweza kuwapa
wakulima wadogo faida nyingi sana
ikiwa ni pamoja na:
• Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni
kwa ajili ya udongo.
• Zinaongeza tani nyingi za viumbe
hai kwenye udongo, hivyo basi, Mbolea ya kijani hujumuisha upandaji wa mimea funika katika shamba kama viazi vitamu
kuongeza udongo wenye rutuba, ambapo husaidia kulinda na kuongeza rutuba
uwezo wa kutunza maji, kiasi cha
virutubisho, uwezo wa kuvunjik • Mazao ya mbolea ya kijani kwa kiasi kidogo katika mashamba
vunjika na muundo wa udongo. yanaweza kutoa kipato kwa kuuza ya wakulima (au tayari imekwisha
• Mazao ya mbolea ya kijani kuni, chakula au malisho (labda na kutumiwa tena)
yanapelekea kwa urahisi mbegu). • Zaidi ya yote, mbolea itarejesha
usafirishaji wa virutubisho kwa • Yanasaidia watu kuacha njia hatari takriban asilimia 98 ya naitrojen
mimea. za kienyeji, kama vile kuchoma katika shamba lakini mazao ya
• Mazao ya mbolea ya kijani hayana mabaki ya mazao au kuachilia mbolea ya kijani, yataongeza kiasi
gharama zaidi ya manunuzi wanyama kipindi cha kiangazi na chote kinachotakiwa cha naitrojen
yambegu. kula kila kinachoonekana. mpya katika mfumo.
• Mazao ya mbolea ya kijani zinatoa • Baadhi ya mbolea ya kijani
kivuli kwenye udongo mpaka miezi • Mkusanyiko wa mbolea huitaji
yakichanganywa na nafaka za maji. Hii ina maanisha kwamba
kumi na moja kwa mwaka, sababu
msingi, zinaweza kuzuia magugu inaandaliwa sehemu iliyo karibu na
ambayo ni ya muhimu zaidi katika
hivyo basi kuzuia gharama za vyanzo vya maji lakini katika umbali
nchi zenye hali ya hewa kwa ajili ya
utunzaji wamaji kwenye udongo uendeshaji wa kupalilia. kidogo na pale inapotengenezwa.
na viumbe hai. Mlinganisho wa mbolea Mazao ya mbolea ya kijani
• Kivuli kinachotokana na hii mimea Kutokana na kwamba utengenezaji yanapandwa ili kusaidia maji ya
inazuia udongo kutopotea kwa njia wa mbolea ni teknolojia ambayo mvua kutumika kwa vitu vingine
ya upepo na maji. inashauriwa kwa ajili ya miradi ya lakini pia hupandwa katika
• Mazao ya mbolea ya kijani maendeleo katika nchi za dunia ya eneo ambapo yanahitajika na
yanapelekea kupatikana kwa tatu, itakua ni vizuri kulinganisha yatatumiwa.
malisho yenye wingi wa protini utengenezaji wa mbolea na matumizi • Mbolea haiwezi kutumika kama
kwa wanyama na ni muhimu zaidi ya mazao ya mbolea ya kijani. chanzo cha chakula iwe ni kwa
yanapopatikana katika kipindi cha • Mbolea haiozeshi tu vitu wanyama au kwa binadamu lakini
miezi ya mwisho ya kiangazi (kama mbolea ya kijani hutumika kama
vilivyotokana na viumbe hai
vile malisho katika kipindi cha chakula kwa wanyama na hata kwa
ambayo tayari inayo, ilhali mbolea
mwaka huu ni kikwazo kwa ufugaji binadamu.
ya kijani yanaweza yakaongeza
wa wanyama kwa njia za kienyeji).
• Baadhi ya mazao ya mbolea ya zaidi ya tani arobaini ya vitu Kwa mawasiliano zaidi wasiliana
kijani ni chakula cha binadamu, vitokanavyo na viumbe hai kwa na Charles Bonaventure kwa simu
hasa maharage ya kuliwa, njegere hekari moja. Vitu vitokanavyo na namba 0717343723 cbonaventure@
na mbegu. viumbe hai mara nyingi huwa ni echonet.org

Mkulima Mbunifu ni jarida huru kwa jamii ya Mpangilio: Cathbert Msemo 0652 731 123
wakulima Afrika Mashariki. Jarida hili linaeneza Mhariri: Erica Rugabandana
habari za kilimo hai na kuruhusu majadiliano Mhariri Msaidizi: Flora Laanyuni
katika Nyanja zote za kilimo endelevu. Jarida
Anuani: Mkulima Mbunifu
hili linatayarishwa na Mkulima Mbunifu, Aru-
Sakina, Majengo road, (Elerai Construction Block)
sha, ni mojawapo ya mradi wa mawasiliano ya
wakulima unaotekelezwa na Biovision (www. S.L.P 14402, Arusha, Tanzania
biovision.ch) kwa ushirikiano na Sustainable Wachapishaji: African Insect Science for Food Ujumbe mfupi pekee: 0785 496 036, 0766 841 366
Agriculture Tanzania (SAT), (www.kilimo.org), and Health (ICIPE), S.L.P 30772 – 00100 Nairobi, Piga simu: 0717 266 007, 0762 333 876
Morogoro. Jarida hili linafadhiliwa na Biovision Kenya, Simu: +254 20 863 2000, icipe@icipe.org, Barua pepe: info@mkulimambunifu.org
Foundation www.icipe.org www.mkulimambunifu.org

2 Mkulima Mbunifu
Toleo la 118 Oktoba 2023

Namna ya kutayarisha maziwa mtindi


Maziwa ya mtindi ni maziwa
mabichi ya ng’ombe yaliyoganda

Picha:IN
na mara nyingi yanakuwa na hali
ya uchachu. Maziwa haya hutumika
kama kinywaji au kiambaupishi
katika mapishi mbalimbali.
Brighton Shalua
Mahitaji
• Maziwa mabichi safi na salama
• Kimea cha maziwa
Vifaa vinavyohitajika
• Sufuria / Keni safi ya kuchemshia
maziwa.
• Chombo (container) ambacho
utaweza kuhifadhi mtindi
unaoendelea kuchachuka
(fermenting) na kiwekwe katika
hali ya usafi ili kuwezesha vijidudu maji yanayochemka mpaka yafikie kwa muda Fulani. Kwa nyuzi joto
hatari visiweze kuwepo na mtindi nyuzi joto la sentigredi 850C na 25-300C unaweza kutambua kwa
uendelee kufanya kazi vizuri. kuyaacha yakiendelea kuchemka kuhisi joto la chombo husika kuwa
Chombo hiki kifunikwe kwa kwa dakika 30. Hakikisha unakuwa chini kidogo na joto la kawaida la
mfuniko safi. makini kuangalia maziwa yako mwili.
• Safisha vyombo hivi viuri na usuuze na kuyakoroga wakati wote 3. Weka kimea (Starter Culture)
kwa maji ya moto kabla ya kuanza yanapokuwa yanachemka. Na kwa kiwango sahihi (kama
kutumia. kama utakuwa na kipima joto basi ulivyoshauriwa na mtaalam)
• Na kama utaweza kupata kipima utaweza kutambua kama maziwa kwenye lita zako za maziwa
joto cha kupikia (Cooking yako yamefikia nyuzi joto 850C. zilizopo katika chombo safi
thermometer) basi unaweza 2. Yaondoshe kutoka kwenye jiko ulichokitayarisha kwa ajili ya
kukitumia pia. na yaache yapoe mpaka kufikia kuvundika (incubation) na ukoroge
nyuzi joto 25-300C. Hivyo kuwa na vizuri kwa dakika 3-5.
Namna ya kutayarisha mtindi 4. Funika chombo na ukiweke sehemu
bafu la maji ya baridi litasadidia
1. Chemsha maziwa kwa kupooza joto hili sawasawa na ya joto la wastani (kuvundika) kwa
kutumbukiza sufuria yenye haraka na kuhitaji tu kukorogwa masaa 16-18 ili kuwezesha bakteria
maziwa ndani ya sufuria lenye waliomo katika mchanganyiko huu
waweze kukua (joto linalopasa
kutumika likaribie nyuzi joto 25-
300C ikiwezekana)
Picha:IN

5. Baada ya masaa 16 pima mtindi


wako kama uko tayari kwa
kuangalia uchachu unaouhitaji
katika mtindi wako na nyamanyama
zilizojitengeneza na kujiridhisha
kua mtindi wako uko tayari.
6. Pooza mtindi wako katika jokofu ili
yagande vizuri na kama hutaweza
kuhifadhi kwenye joto la kiwango
cha chini (jokofu) basi itakulazimu
kutumia kwa siku moja tu.
Dozi ya culture
• 1Packet ni kwa lita 500-600 za
maziwa.
• 1kijiko cha chai (wastani) ni kwa
lita 100
• ½ kijiko cha chai ni kwa lita 50
• ¼ kijiko cha chai kwa lita 20- 25
• 1/8 kijiko cha chai kwa lita chini ya
20

Mkulima Mbunifu 3
Toleo la 118 Oktoba 2023

Tumia mfumo wa kilimo ikolojia kuzalisha chakula salama

Picha:MkM
Siku ya Chakula Duniani Mbegu asili kiafya, kama vile kisukari, unene
inaadhimishwa Oktoba 16 kote Kwa kuhifadhi aina mbalimbali za uliokithiri, na utapiamlo. Kukuza
duniani. Wakati kama tunatathmini mimea na wanyama ili kuboresha na kuhimiza mbinu za kilimo cha
hali ya usalama wa chakula ikiwa afya ya mkulima mwenyewe na ya ikolojia kunaweza kusaidia kufanya
ni pamoja na kuzalisha chakula cha familia kwa ujumla. udongo kuwa na tija zaidi, kupunguza
kutosha, kinachotoa lishe kwa jamii Katika kipindi cha miaka kadhaa, matumizi ya kemikali za kilimo na
nzima na pia kilicho salama kwa kama hamsini hivi, tumepoteza uchafuzi wa mazingira, na kuongeza
afya ya binadamu. asilimia kubwa ya mbegu zetu za aina mbalimbali za mazao. Hili
asili na hivyo kutegemea kwa kiasi nalo linaweza kufanya kilimo kuwa
Daudi Manongi kistahimilivu zaidi hasa wakati tabia
kikubwa mbegu mpya zinazonunuliwa
Kilimo ikolojia ni mbinu ya kilimo madukani. Hii inamaanisha kwamba nchi nchi inapobadilika.
ambayo mara nyingi ni kilimo wakati mkulima hana hela za kutosha Anza kidogo nyumbani
kinachotumia kiasi kidogo cha hawezi kununua mbegu na pembejeo Kila wakati, Mkulima Mbunifu
pembejeo za nje ama kemikali zingine na kuzalisha mazao ya kutosha. inawahimiza wakulima kutumia
zinazonunuliwa madukani. Kilimo Hii inaadhiri upatikanaji wa lishe na mbinu za kilimo ikolojia mashambani.
ikolojia inalenga kudumisha na madini muhimu kwa ukuaji unaofaa, Mkulima anaweza kuanza katika
kubadilisha mahusiano ya kijamii, hasa kwa watoto na akina mama. Ni eneo ndogo kama vile bustani la
kuwawezesha wakulima na kuongeza vyema wakulima kutunza mbegu asili jikoni kufanya majaribio ya mbinu
mnyororo wa thamani. Inaruhusu inayoweza kustahimili mashambulizi mbalimbali. Hii inakuwezesha kujua ni
wakulima kukabiliana na mabadiliko ya wadudu na magonjwa. mbinu gani zinaleta matokeo mazuri
ya hali ya hewa, matumizi endelevu Mazao kama ulezi, mhogo, zaidi kabla ya kulima eneo kubwa.
na kuhifadhi maliasili na bayoanuwai. viazi vitamu, mtama na mengine Kwa kufanya hivyo, unajihakikishia
Yaani, wakulima wanazalisha mazao yamekuwa yakichangia sana kwa upatikanaji wa chakula, hasa mboga-
ya chakula na ya thamani ya juu ili usalama wa chakula. Tunapopoteza mboga, nyakati zote za mwaka na
kikidhi mahitaji ya lishe na pia kupata utofauti katika mlo kunahusishwa msimu baada ya msimu. Na hauhitaji
hela kutokana na mauzo. moja kwa moja na mambo hatarishi hela ama pembejeo nyingi kuanzisha
bustani la jikoni. Hii ni njia moja ya
kujenga uzoefu wako na maarifa
katika kilimo ikolojia.
Picha:IN

Kuwawezesha wakulima
Kilimo ikolojia kiweze kutumika kwa
kiwango kikubwa, inahitaji kuungwa
mkono na serikali, watunga sera na
suhrikiano wa wadau katika sekta ya
kilimo. Kwa kuwawezesha wakulima
wadogo, mabadiliko hayo yanaweza
kutokea kwa haraka zaidi, matokeo
kuonekana na marekebisho muhimu
kufanywa.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana
na Daudi Manongi kwa simu
0769861063

4 Mkulima Mbunifu
Toleo la 118 Oktoba 2023

Teknolojia ya utengenezaji wa makaa ya mawe ya kupikia


Teknolojia ya utengenezaji wa Chati inayoonyesha hatua za uzalishaji/ utengenezaji wa makaa
briketi za makaa ya mawe ya kupikia bora ya mawe ya kupikia katika mbalawala women organization
ni teknolojia iliyofanyiwa utafiti na
wataalamu wa makaa ya mawe CHANGANYA
wa Tancoal Energy Limited katika Andaa SAGA KUPATA UKUBWA KUPUNGUZA JOTO
chenga UNAOTAKIWA NA HEWA CHAFU
mgodi wa Ngaka kwa kushirikiana za makaa
na Mbalawala women organization
mnamo mwaka 2014.
ANZA KUFYATUA
Fredrick Katulanda BRIKETI (MAKAA
Utafiti huo ulikuwa wa kimaabara na
pia ulihusisha kuhusu upatkanaji wa
malighafi ya msingi na malighafi za KAUSHA KWA KUTUMIA JUA (SIKU
BRIKETI ZA MAKAA
nyongeza (additives) katika maeneo MBILI HADI 3) AU KAUSHA KWA KU-
YA MAWE TAYARI
TUMIA TANURU LA KUKAUSHIA HASA
ya karibu na mradi. KWA MATUMIZI
KIPINDI CHA MVUA (SAA 8)
Pia, vipimo vya utafiti wa maabara
vilionyesha mafanikio mazuri.
Teknolojia ya briketi za makaa bora ya UMBO DUARA OVALI NDOGO NDOGO
mawe ya kupikia ni rahisi kutengeneza
na kutumia. Makaa ya mawe ya Matumizi ya makaa ya mawe ya jiko lako chini na kasha washa.
kupikia yaweza kuwa mbadala wa ya kupikia • Waweza kutumia Maranda ya
nishati iliyozoeleka ya kuni na mkaa mbao.
• Yanatumika kama chanzo cha
utokanao na miti. • Waweza pia kuwasha kwa kutumia
moto kwa matumizi ya kupikia
Hivyo, nishati hii mbadala ya vipande vichache vya mkaa wa
majumbani, katika taasisi kama
makaa ya mawe ya kupikia ikitumiwa, miti uliowaka
shule, magereza, hospitali n.k. Na
itasaidia sana katika kupunguza • Weka makaa yako na uyaache
pia kwa vikundi vya wajasiriamali
uharibifu wa misitu utokanao na yakolee moto kwa muda wa dakika
na wauzaji wa vyakula kama
matumizi ya kuni na mkaa wa miti. chache.
mamalishe, wauza chips na
MWO tunatengeneza briketi za • Makaa yatakuwa yamewaka na
wengineo.
maumbo ya aina mbili. Maumbo kuwa rangi nyekundu kuanzia
• Yanatumika pia katika viwanda
haya huruhusu mzunguko wa upepo chini, na yatakuwa tayari kwa
kwa kuyeyushia vyuma.
/ hewa katika makaa ili kurahisisha kupikia
• Yanatumika katika masuala ya
uwakaji kirahisi. Aina ya kwanza ni
ufugaji kama chanzo cha joto
umbo la duara (round honey comb) Matokeo baada ya kuwasha
hususani katika ufugaji wa kuku.
ambazo hutumika zaidi katika majiko makaa
• Yanaweza kutumika pia katika
makubwa ya taasisi. Aina ya pili ni • Makaa yanatoa
tanuru la kuchomea taka.
ile yenye umbo dogo la ovali (oval moshi kidogo na harufu
shape) ambazo hutumika zaidi katika Faida za kutumia
kidogo mwanzoni
majiko madogo ya nyumbani. makaa ya mawe ya
kupikia unapowasha, baada
Sifa za makaa ya mawe ya ya dakika chache
kupikia ya ngaka • Ni gharama nafuu
ukilinganisha na yakishawaka moto,
• Yametengezewa kwa kiwango cha hakuna moshi
mkaa wa miti.
joto la wastani linalokaribiana na
• Kwa kuwa moto wala harufu.
mkaa wa miti.
wake unawaka kwa • Moto wa
• Moto wake unawaka kwa muda
muda mrefu, hivyo makaa huendelea
mrefu, kwa saa 3-4.
hutumika kupikia kuwaka kwa muda
• Ni imara (magumu hayavunjiki
vyakula vingi kwa
vunjiki kwa urahisi) wa masaa 3-4.
sikubila kuongeza mkaa
• Yana muonekano mzuri • Hadi kuwa jivu na
mwingine jikoni.
• Ni rafiki kwa mazingira, hupunguza kuzima kabisa ni wastani wa saa
ukataji miti ovyo. 8.
• Ni rahisi kutumia. Kumbuka:
• Ni rahisi kusafirisha kutokana na
uimara wake. Wakati wa kuwasha moto ni muhimu
kufungua mlango wa kutolea jivu
Namna ya kuwasha makaa ya kuruhusu hewa ipite kuchochea
mawe ya kupikia
• Weka vijiti vidogo vidogo katikati Inaendelea Uk. 7. »»

Mkulima Mbunifu 5
Toleo la 118 Oktoba 2023

Wakulima Singida wakubali kilimo ikolojia


Kilimo ndio uti wa mgongo. Kwa

Picha:MkM
mujibu wa takwimu za asilimia tisini
ya wananchi wa Tanzania maisha yao
wanategemea kilimo, tena kilimo
cha chakula kwa ajili ya familia zao
huku kila kaya ikihesabiwa inakula
gunia moja kwa mtu mmoja.
Amini Nyaungo
Tanzania ina aina nyingi ya kilimo
kwa wanaojishughulisha na kilimo,
hii inatokana na ikolojia ya eneo
husika, huku kilimo cha kiikolojia
kwa mkoa wa Singida kikionekana
kupendwa zaidi baada ya kupata
elimu kutoka katika jarida la Mkulima
Mbunifu ambapo husambazwa kwa
wanakikundi kila mara moja kwa yake baaada ya msimu kuisha asili ambazo zinaendana na kilimo
miezi miwili. kwani hachomi masalia ya mazao cha kiikolojia yaani mbolea ambazo
bali anayaacha yaoze na baadae hazitumii kemikali hivyo mazao yake
Kilimo cha ikolojia ni nini?
kupata mbolea. yanakuwa salama.
Hiki ni kilimo kinachofuata utaratibu
• Lakini pia anahifadhi mbegu Ameeleza kuwa anatumia bangi
bora wa kilimo ambapo hakitumii
kwa kutumia ghala ambapo ya mbwa, mabilingali na majani ya
kemikali katika mazao yake huku
hazibunguliwi na wadudu na miti kwa ajili ya kutengeneza viatilifu
kikifuata mbinu za kilimo ambazo
msimu wa kilimo ukifika anazitoa kwa ajili ya kuua wadudu badaya
haziathiri udongo.
na kupanda. ya kutumia mbolea za viwandani
Baada ya kupata elimu hiyo
• Kupitia kilimo cha kiikolojia ambazo zina kemikali na zikitumika
ya kilimo cha kiikolojia wakulima
shamba lake linapata rutuba kwa katika vyakula mfano mbogamboga
mbalimbali kutoka mkoani Singida
kufuata kanuni za kilimo hiki hasa zinaweza kuleta madhara kwa walaji.
wameelezea namna walivyokipokea
kwa kutochoma masalia ya mazao, “Mimi nafarijika sana kukifahamu
kilimo hicho.
lakini pia uhifadhi wa mbegu ni kilimo cha kiikolojia kwani
Mkulima Madai Njou kutoka
kwa njia za asili ambazo ni bora, kimenifanya nitumie mbolea za asili
kijiji cha Unyangwe Halmashauri ya
salama na hazitumii madawa. ambazo natengeneza mwenyewe
Wilaya ya Ikungi yeye amesema kuwa
Rehema Joel Mbula mkazi wa kwa ajili ya kuua wadudu lakini
amenufaika na kilimo hicho kwa
Ilongero anasema kuwa katika nimefurahi kufahamu na kujionea
mambo yafuatayo:
shamba lake anatumia mbolea za mwenyewe kuwa mbolea ya ng’ombe
• Shamba lake halijapoteza rutuba
ni mbolea nzuri sana’’
Zaina Nkungu kutoka kata ya Msisi
ameongeza kuwa hakuna kilimo bora
na rahisi kama kilimo ikolojia kwani
unaweza ukafanya kilimo mseto na
ukafanikiwa kupata mazao mengi
kwa msimu mmoja.
“Elimu ya Kilimo ikolojia
imetusaidia kulima mazao mengi
kwa wakati mmoja na katika eneo
moja na tukapata mavuno mengi na
yenye ubora na soko la uhakika kwani
mazao yanakuwa salama.’’
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya
Singida Salumu Athuman ameeleza
kuwa wakulima wanazalisha kwa
njia hii ya kilimo ikolojia kwa ukubwa
Picha:IN

wake kwani wanaona ni kilimo rahisi


na kinachohifadhi mazingira.

6 Mkulima Mbunifu
Toleo la 118 Oktoba 2023

«« kutoka Uk.5 ... makaa ya mawe

moto, na pia washia jiko nje ya


nyumba hadi likolee na makaa
kuwa rangi nyekundu ndipo
waweza kuweka au kupikia ndani
ya chumba.
Usiwashe jiko ndani ya
nyumba.
Jiko zuri la kutumia ni
lile linalotunza joto, na liwe
limetengenezwa kwa kuwekewa
udongo kwa ndani, liwe na
matundu sehemu ya chini kwa
ajili ya kupitisha hewa.

Picha:MkM
Joto la makaa ya mawe ya
kupikia ni la wastani limepimwa
na wataalam halitoboi sufuria.
Unaweza kutumia yoyote kupikia
huhitaji kununua sufuria maalum.
“Tunza mazingira kwa kutumia
ulezi, vitunguu, viazi vitamu, viazi makaa bora ya kupikia ya ngaka.”
Salum amesema kuwa yeye
kama Afisa Kilimo anawafundisha lishe pamoja na dengu.
na kuwaelekeza namna ya kufanya Kila zao lina muda wake na KIKUNDI CHA MBALAWALA
kilimo mseto ambacho ni moja ya kwa mujibu wa Afisa kilimo Salum Mbalawala women organization
aina za kilimo ndani ya kilimo cha (MWO) ni shirika lisilo la kiserikali
Athumani anasema kuwa kuna baadhi
(NGO) lililopo katika mkoa wa
kiikolojia. ya mazao hayahitaji mvua nyingi kama Ruvuma wilayani Mbinga kijiji cha
Kwa upande wa Afisa kilimo wa vile dengu hivyo mara zote linalimwa Ruanda, eneo la Senta D.
Halmashauri ya Ikungi Boniface baada ya kuvuna au inapokaribia Mwo ni matokeo ya juhudi za
Barnaba yeye amebainisha kuwa kuvuna zile mvua za mwisho mwisho Tancoal EnergyLimited katika
kilimo cha ikolojia kina maana kubwa ndio zoa hili linalimwa. kuiweesha jamii inayoizunguka
kwa watanzania kwani kilimo hiki Kwa mazao mengine inatendana mgodi wa makaa ya mawe wa
kikiendelezwa kinaweza kusaidia Ngaka. MWO imeundwa na vijiji
na msimu wa mvua ulivyo basi vya Ruanda na Ntunduwaro, kwa
kuondoa baa la njaa kwa familia unaweza kulima na kupanda na kushirikiana na Tancoal Energy
kwani ni kilimo rahisi kinacholeta ukafanikiwa katika kilimo husika. Limited.
mazao mengi. Msimu wa kilimo mkoani Singida
“Hichi kilimo ni muhimu sana Lengo kuu la Mbalawala
ni kuanzia mwezi wa kumi na moja Women Organization
sisi maafisa kilimo tunafanya kazi
kwenda mwezi wa kumi na mbili Kuwawezesha wanawake kupata
kubwa kuwaelemisha lakini pia
ambapo ndio mvua za awali zinaanza fursa ya ajira katika miradi
tunawashukuru Mkulima Mbunifu mbalimbali kupitia uwepo wa
lakini matayarisho ya shamba
kwa kutoa elimu hii kupitia majarida mgodi wa makaa ya mawe wa
yanaanzia mwezi wa kumi na moja.
yake kwani wakulima wakikizingatia Ngaka.
Endapo wewe mkulima au mgeni
kilimo hiki wanaweza wakapata Mbalawala inajihusisha na miradi
katika eneo hili unataka kulima mbalimbali ikiwemo;
mavuno mengi yenye ubora na
salama wakakuza pato la familia kuna wakazi ambao wanakodisha • Uzalishaji wa briketi za makaa
pamoja na walaji kupata mlo kamili mashamba yao kwa msimu mmoja ya maweya kupikia.
safi na salama.’’ ambapo ekari moja elfu thelathini • Huduma ya chakula na usafi.
(30,000) au Elfu Hamsini (50,000) • Kitalu cha miti.
Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa
viwango vya bei vinatokana na ardhi • Shamba la bustani.
ambayo ina wakulima wengi na • Huduma za kifedha (Fahari
shughuli kubwa ni kilimo na alizeti ni ambapo kuna aina mbili ya ardhi
huduma &M-pesa)
zao kuu linalolimwa mkoa huu lakini mbuga na kichanga. Kwa maelezo zaidi unaweza
wakulima wake wanalima mazao Kwa maelezo zaidi wasiliana na kuwasiliana na Mbalawala
mengine. Afisa kilimo wilaya ya Singida Women Organization kwa simu
Moja ya mazao wanayolima ni Bwana Salum athumani kwa simu namba 0765 471 757/0754 285
887
pamoja na mahindi, mtama, uwele, namba 0755874414

Mkulima Mbunifu 7
Toleo la 118 Oktoba 2023

Kuandaa shamba kwa ajili ya msimu wa kilimo cha mahindi


Mahindi ni zao kuu la chakula linalo
limwa katika mikoa mbalimbali
nchini hasa katika maeneo ya

Picha:IN
kitropiki. Ili kupata mavuno bora na
yenye tija zao hili linahitaji kulimwa
katika udongo wenye uchachu
yaani pH 6 hadi 6.5 na hustawi zaidi
kwenye maeneo yenye mwinuko wa
2500
Flora Laanyuni
Zao hili linahitaji maandalizi sahihi
kabla ya kuanza kulima ili kuwepa
kupata mavuno bora.
Kuna kanuni tano za msingi za
kuzingatia
I. Kutayarisha shamba
Ni vyema mashamba yaandaliwe
mapema kabla ya msimu wa kupanda
Ni vyema mkulima akahakikisha anaanda shamba mapema kwa ajili ya msimu ujao
haujaanza ili kumpa mkulima fursa wa kilimo
ya kupanda kwa wakati unaotakiwa.
Kuna njia mbalimbali zinazotumika e. Hupunguza wadudu waharibifu. Mbegu za asili ni bora zaidi kutumia
kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi kwani zina sifa zote zilizotajwa hapo
ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki II. Kupanda kwa wakati
Ni muhimu kupanda mahindi kwa juu.
na kulima. Shamba linaweza kulimwa
kwa kutumia: wakati husika kwani kutasaidia Namna sahihi ya kupanda
• Jembe la mkono. Wengi wanatumia kuhudumia kwa ufasaha, kuepukana Idadi ya mimea katika eneo ni
• Jembe la kukokotwa na wanyama na changamoto za magonjwa na muhimu kwani ikizidi
kama ng’ombe ukame lakini pia kupata mavuno bora.
a. Mazao hupungua.
• Kulima kwa kutumia Power tillers Kama mvua itanyesha nyakati na
• Matrekta majira yale yale ni vyema mkulima b. Mmea hukosa rutuba ya kutosha
Matumizi ya trekta, power tillers na ukahakikisha unapandaa kwa wakati na kuwa hafifu.
jembe la kukokotwa na wanyama husika kulingana na majira ya msimu c. Mabua mengi hayatazaa.
yanapunguza nguvu kazi kwani katika eneo lako. Idadi ya mimea nayo ikipungua
vinachimbua udongo na kuufanya Mara nyingi ni wiki moja hadi mbili kwenya eneo husababisha mavuno
kuwa tifutifu (kufanya isiwe na kabla ya mvua kuanza kunyesha kwani kupungua hivyo panda mbegu
mabonge makubwa, wala isiwe kwa kuwahi ama kuchelewa kunaweza katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na
vumbi vumbi). Hii husaidia: kukasababisha mbegu kuharibiwa na wataalamu.
• Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini joto, wadudu, kuoza, kuliwa na panya,
kirahisi ndege au hata wanyama wengine, Nafasi za kupanda
• Udongo kuweza kuhifadhi maji wadudu,panya,ndege na wanyama 75cm x 30cm
• Udongo kuwa na hewa wengineo. 75cm x 60cm
inayohitajika na mimea 90cm x 25cm
• Ukuaji mzuri wa mimea hivyo Faida za kupanda mapema/
wakati 90cm x 50cm
kuongeza mavuno
Ni muhimu kuandaa shamba a. Mahindi yanapata mvua ya kutosha Tumia mbolea ya asili
mapema kabla ya mvua za kwanza. hadi kukomaa. Mahindi hustawi na kuzaa vizuri
Shamba lilimwe kina sm 15-20 b. Magonjwa kama yale ya majani iwapo yatapatiwa mbolea pamoja
kwenda chini. Baadhi ya udongo (streak ugonjwa wa milia)
na matunzo mengine ya kilimo bora.
huwa mgumu kulimika baada ya mvua hayatatokea au yatakuwa kidogo.
c. Mbolea uliyoweka itayeyuka Ukipanda mbegu bora bila kutumia
nzito, kwa hiyo shamba litayarishwe mbolea ni kazi bure.
vizuri na kulimwa kabla ya mvua. pamoja na mahindi yastawi vizuri.
Mbolea za asili kama samadi,
Faida za kuandaa shamba III. Kuchagua mbegu bora mboji na majani mabichi, mbolea
mapema Mbegu bora ni zile zilizozalishwa na hizi hua na virutubisho vya kutosha
b. Baada ya kuvuna, udongo bado ni kutunzwa kwa njia sahihi na ambazo; ambavyo huhitajika katika uzalishaji
mlaini hivyo hulimika kwa urahisi a. Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
wa chakula.
kwa kutumia jembe lolote. b. Huzaa mazao mengi.
c. Masalia yatakayofunikwa udongoni c. Hustahimili magonjwa na mkame. Kwa wasiliano zaidi wasiliana na
huoza mapema. d. Ni nzima na hazijapasuka. Afisa kilimo wilaya ya Arusha, Bi.
d. Husaidia kupunguza magugu. e. Zimekaushwa vizuri. Lucy Mvungi kwa simu 0755565621

8 Mkulima Mbunifu
Toleo la 118 Oktoba 2023

Hifadhi nafaka kwa njia sahihi kuepuka upotevu


Ni wazi kuwa wakulima wengine • Liwe na uwezo wa kuhifadhi mazao
wamevuna nafaka mbalimbali yaliyokusudiwa.
kama vile maharage na mahindi Aina ya maghala bora
katika msimu huu wa mavuno hivyo
wasipokuwa makini na kuhifadhi 1. Sailo au bini
kwa usahihi mavuno yote yatapotea Haya ni maghala yanayojengwa kwa
kwa kuharibiwa na wadudu, panya, dhana ya kutokuwepo na mzunguko
au hata ukungu unaotokana na wa kawaida wa hewa ndani ya
unyevu. nafaka iliyohifadhiwa na kusababisha
wadudu waharibifu na vimelea vya
Eliudi Letungaa magonjwa kutoweza kusitawi na
Ili kuepukana na hasara ni muhimu kuharibu nafaka.
kuhakikisha unahifadhi mazao
yako katika njia salama kama 2. Mapipa
unavyoshauriwa na Mkulima Mbunifu Mapipa yenye mifuniko imara
hutumika kuhifadhi nafaka kwa
au wataalamu wa kilimo.
dhana ya kutokuwa na hewa
Kabla ya kuhifadhi hakikisha
ndani ya mahindi. Pipa likijazwa
mazao yako yamekauka vizuri mahindi na kufungwa sawasawa
kwa kung’ata punji ambayo huwa hakuna hewa inayoingia na hakuna
ngumu na hukatika kwa mlio mkali, Nafaka zikihifadhiwa kwenye pipa lisilo- mdudu anayeweza kuishi ndani
kumimina kwenye chombo au sakafu, pitisha hewa kama hili haiwezi kuathiriwa yake, na hata punje za nafaka hufa
ambapo hutoa mlio mkali kama wa na wadudu wala kuingia uchafu wowote baada ya kuhifadhiwa kwa muda
kuumiza sikio, kutumia chumvi yaani hivyo inashauriwa kuwa nafaka
kuchanganya mahindi na chumvi kiasi Hatua za kuchanganya inayotegemewa kwa ajili ya mbegu
kisha mimina kwenye jagi la kioo, na • Tandika turubai safi kwenye sakafu isihifadhiwe ndani ya pipa.
kama chumvi itang’ang’ania kwenye katika sehemu isiyokuwa na upepo.
punje basi hazijakauka au kutumia • Pima nafaka kwa kutumia debe au 4. Maghala ya nyumba
kipima unyevu ambacho huonyesha kwa kutumia mizani ili kupata uzito Hifadhi hii hufanyika katika
unyevu wa asilima 13.5. wa kilogramu 100 (madebe sita) chumba au nyumba maalumu na
• Weka nafaka kwenye turubai maghala haya huhifadhi mazao
Kutayarisha nafaka kabla ya yaliyofungashwa kwenye magunia.
na funika pua na mdomo kwa
kuyahifadhi Uwezo wa kuhifadhi hutegemea
kitambaa safi ili kuzuia dawa
Kabla ya kuweka nafaka kwenye isiingie mwilini. wingi wa mazao.
vifungashio au kuhifadhi ghalani, • Fungua pakiti ya gramu 200 ya
inabidi kuchukua tahadhari ya kuzuia dawa ya asili na mimina juu ya kilo
uharibifu utokanao na wadudu au 100 za nafaka.
wanyama kama panya ndani ya ghala. • Anza kuchanganya dawa nanafaka
Hakikisha ghala la kuhifadhia kwa kutumia beleshi au koleo
nafaka ni safi, lisilovuja na ikibidi mpaka mahindi yote yatakapopata
changanya mahindi na viuwadudu. dawa.
Viuwadudu hivyo vinaweza kuwa vya • Fungasha kwenye magunia safi
asili vinavyotokana na mimea kwa ya kilo 100 tayari kwa kuhifadhi
mfano mwarobaini au pareto. Aidha ghalani au waweza kuhifadhi
ni muhimu kutenga kiasi cha nafaka kwenye kihenge, silo au bini.
itakayotumika kwa kipindi kisichozidi • Nafaka zipangwe kimadaraja
miezi mitatu baada ya kuvuna. Hii kwenye ghala. (Maguniua
ni kwasababu katika kipindi hiki, yasiwekwe moja kwa moja
mashambulizi ya wadudu huwa ni ya sakafuni, mbao huweza
kiwango cha chini sana. kutangulizwa sakafuni kwanza).
Kuchanganya kiuwadudu na Ghala bora la kuhifadhia
nafaka nafaka
Wakati wa kuchanganya kiuwadudu Ghala bora ni chombo chochote kile
na nafaka ni muhimu kuandaa vifaa au jengo lolote lililo imara na lenye Unaweza ukahifadhi nafaka kwa kutumia
kama vile, turubai isiyokuwa na sifa zifuatazo; mifuko maalumu ya kuhifadhia kama PICS
matundu, sakafu safi ya sementi, • Liwe na uwezo wa kuzuia wadudu, ambazo hupatikana sokoni
debe la kupimia nafaka, beleshi au panya, mvua na unyevu kutoka
koleo, dawa ya kuhifadhia na kifaa chini. Kwa maelezo zaidi wasiliana Afisa
au kitambaa safi cha kufunika pua na • Liwe na nafasi ya kutosha kuweka kilimo wilaya ya Arusha, Bi. Lucy
mdomo. mazao, kukagua na kutoa. Mvungi kwa simu 0755565621

Mkulima Mbunifu 9
Toleo la 118 Oktoba 2023

Matumizi ya mabaki ya mimea mara baada ya kuvuna


Mabaki ya mimea katika

Picha:IN
kilimo cha kutotifua ardhi
Hiki ni kilimo cha kisasa,
kinachotumiwa zaidi na wakulima
wa mashamba makubwa ambazo
hazitifuliwi. Kilimo hichi kinajumuisha
kuacha mabaki ya mazao shambani
na kupanda mazao mapya moja kwa
moja kwenye udongo uliokatwa.
Kilimo cha bila kutifua ardhi
kinahitaji mbinu tofauti ili kuhifadhi
mavuno mengi, kama vile mazao ya
kufunika na kurutubisha udongo na
matumizi ya dawa za asili ili kufikia
sifa bora za udongo.

Ni muhimu kuhakikisha unafunika udongo kwa kuacha masalia ya mimea shambani mara Kilimo bila kutifua ardhi kina
baada ya mavuno faida nyingi kwenye udongo:
• Mabaki ya mazao juu ya uso wa
Mabaki ya mimea ni nyenzo za sehemu ya kikaboni ya udongo. udongo yanawajibika kwa kupooza
mazao kama vile mashina, majani na • Ufyonzwaji bora wa matone udongo, kuongeza unyevu wa
mizizi, ambayo huachwa shambani ya mvua ambayo hupunguza udongo na kuzuia uvukizi.
baada ya kuvuna. • Mabaki ya mazao hulinda udongo
uwezekano wa mmomonyoko.
kutokana na mmomonyoko wa
Mbali na mabaki haya kutumika
Erica Rugabandana udongo na hutumika kama chanzo
wakati wa kilimo mkulima anaweza cha kikaboni.
Hapo awali, wakulima walichukulia pia kujumuisha katika usimamizi • Huzuia matumizi kukanyaga
mabaki ya mazao kuwa takataka, wa shamba lake, kulima mazao ya udongo na kuepelekea kugandana
ambayo kwa kawaida iliharibiwa kwa kufunika yaani mbolea ya kijani. kwa udongo. Hii inafanya iwe
kuchomwa moto. Mbolea ya kijani hurutubisha rahisi kwa mimea kuchipua na
Hata hivyo, uchomaji huu udongo kwa kuongeza malighafi za kukuza mizizi kwa kina. Kwa
haupendekezwi kwa sasa na kikaboni, udongo kuboresha shughuli hiyo, husababisha kupungua kwa
haitumiwi na wakulima na badala yake zake za uzalishaji, hutoa ufikiaji bora usumbufu kwenye udongo
wakulima hupanda wakati mabaki ya wa virutubisho. • Gharama za kilimo kama
mimea yanaingizwa kwenye udongo Pia ina athari nzuri kwenye vile nguvu kazi, gharama za
au kufanya kilimo cha kulima kidogo udongo mzito na mchanga na mashine/matrekta na mafuta
au kutokulima kabisa, ambapo inapendekezwa pia kutumika katika zimepunguzwa.
mabaki ya mazao huachwa juu ya uso udongo uliorutubishwa kwa mbolea Makala hii ni kwa hisani ya mtandao
wa ardhi na upandaji unafanywa bila wa AGRIVI
ya madini ya kemikali za viwandani.
kutifua udongo.
Matumizi ya mabaki ya mazao
Picha:IN
kwenye udongo
Kusudi kuu la kutumia mabaki mazao
ni kuboresha udongo. Mabaki ya
mimea husaidia wakati wa kulima
kwa kuongeza virutubisho kwatika
udongo na kuzuia kushuka kwa
nitrojeni. Wakulima wanaosimamia
mashamba yao kwa utaratibu huu,
wanategemea faida zifuatazo za
mabaki ya mazao:
• Virutubisho vilivyosindikwa
huondolewa na mmea unaokua
• Kudumishwa au kuongezeka kwa
vitu vya kikaboni vya udongo
ambavyo hutoa substrate kwa Maandalizi ya shamba ni pamoja na kuacha masalia ya mabaki ya mimea kama mabua
vijidudu vya udongo na kuongeza shambani ili kuendelea kufunika udongo na kuongeza rutuba

10 Mkulima Mbunifu
Toleo la 118 Oktoba 2023

Uvunaji wa maji ya mvua na umwagiliaji


Ni mbinu ambayo inazuia au mazao au kunywa.
kukusanya maji ya mvua yasitiririke Matayarisho ya

Picha:IN
hovyo na badala yake yaweze uvunaji maji ya mvua
kutumika hapo baadaye kwa yanapaswa kufanyika
shughuli mbalimbali ikiwepo mapema kabla ya
unyweshaji wa mifugo, matumizi ya msimu wa mvua kuanza
nyumbani kama kufua, kumwagilia ili mvua zinaponyesha
mashamba. “Maji ni uhai, Maji ni uweze kuvuna maji
chakula” Asibaki mtu nyuma. Hii ni na kuyahifadhi kwa
kauli mbiu ya siku ya chakula duniani matumizi hayo
October mwaka 2023 baadaye. Kumbuka
maji ya mvua
Flora Laanyuni yanaweza kutuzwa kwa Unaweza kutengeneza kisima cha kukinga maji ya mvua moja
Uvunaji wa maji ya mvua hufanywa muda mrefu bila ya kwa moja toka kwenye paa la nyumba
zaidi katika hali ya hewa kame au kuharibika.
yenye nusu ya ukame, kwani maeneo Maji ya mvua • Hatua ya kwanza ni kuanza
haya yana kiwango cha chini cha yanaweza kuvunwa na kutumiwa kuchimbia nguzo kwa ajili ya
maji kwenye udongo. Hii kwa wakulima wenye maeneo yenye kufunga turubai. Turubai linapaswa
ukame na siyo wakati wa kiangazi tu. kubonyea katikati ili kutengeneza
Vifaa vinavyohitajika tumbo ambalo litaruhusu
Ili kuvuna maji mkulima anapaswa kuyapokea maji yanayovunwa.
kuandaa vifaa vifuatavyo; Chimbia nguzo yako kiasi cha
• Turubai moja nusu mita na kuacha mita moja na
• Tanki la kuhifadhia maji nusu ikiwa juu, ambayo itahusika
• Nguzo 4 za miti zenye urefu wa kufungia turubai lako.
mita mbili (2) • Hatua ya pili ni kutoboa tundu katika
• Bomba la Plastiki lenye ukubwa wa turubai lako. Tundu linapaswa
¾ kuwa na ukubwa wa kuruhusu
inasababisha upungufu wa maji kwa
wanadamu, wanyama na mimea. Eneo la uvunaji maji bomba ambalo litaruhusu
Kuna njia tofauti ambazo maji ya Baada ya kukamilisha vifaa mkulima kuchukua maji yanayokusanyika
mvua yanaweza kuvunwa. kutumia anapaswa kuhakikisha anachagua katika turubai wakati wa mvua
mikakati ya usimamizi wa udongo eneo linalofaa kwa uwekaji mtego kunyesha na kuyahifadhi ndani ya
ambao unawezesha kuvuna moja kwa wake wa kuvunia maji. Sehemu za tanki.
moja maji ya mvua ndani ya udongo. muinuko na eneo la kilimo liwe katika • Hatua ya tatu ni kuweka tanki
Hii inazuia maji kutiririka na huongeza mteremko kwa sababu itakuwa la maji chini ya turubai au eneo
upenyezaji kwenye mchanga. rahisi kufikisha maji bondeni kutoka ambalo bomba lako litafika ili
Inawezekana pia kuvuna mvua kwenye tanki kwa kutumia njia ya kuyakusanya maji na kuyahifadhi
kwenye sehemu moja na kuihifadhi mteremko (gravity). kwaajili ya matumizi baadae.
mahali pengine. Kwa mfano, kukinga
maji ya mvua kutoka juu ya dari na Hatua za utengenezaji Uvunaji maji zaidi
kuyahifadhi ndani ya tenki. Maji Baada ya kukamilisha upatikanaji wa Ukihitaji maji zaidi inakupasa kuwa
haya hutumiwa zaidi kwa kumwagilia vifaa na kuchagua eneo. na matanki zaidi ili mvua zinapokuwa
kubwa uweze kuvuna maji mengi
zaidi kadri ya wingi wake na ukubwa
wa ujazo wa matenki yako.
Unaweza kuandaa tanki la maji kwa
saruji, kwa kulijenga juu au kuchimba
shimo chini lenyewe uwezo wa
kuhifadhi maji mengi. Changamoto
ya tanki la saruji inaweza kuwa ni
gharama kubwa za ujengaji na uvutaji
maji kutoka ndani ya tanki hilo kwa
Picha:IN

ajili ya kumwagilia.
Kwa wasiliano zaidi wasiliana na
Afisa kilimo wilaya ya Arusha, Bi.
Maji yanaweza kuvunwa moja kwa moja toka kwenye paa la nyumba na kuingia kwenye
Lucy Mvungi kwa simu 0755565621
tenki maalumu za kuhifadhia maji

Mkulima Mbunifu 11
Toleo la 124
116 Disemba
Sikiliza vipindi vya kilimo ikolojia
Juni 20232023

JINA LA RADIO JINA LA NAMBA YA SIKU YA KIPINDI MARUDIO YA KIPINDI


Kama ilivyo ada Mkulima KIPINDI KUBIPU

Mbunifu imeendelea SIKU MUDA SIKU MUDA

kushirikiana na wadau wengine RADIO KILIMO NA 784105727 IJUMAA 2:30-3:00 JUMATATU 2:30-3:00 USIKU
kuhakikisha inakufikishia taarifa MWANGAZA MWANGAZA USIKU

sahihi za kilimo hai. Kwa mantiki RADIO


STANDARD FM
KILIMO NA
JAMII
784105733 JUMAMOSI 1:00-1:30
JIONI
JUMATANO 1:30-2:00 USIKU

hiyo, usiache kusikiliza vipindi


RADIO UTUME KILIMO NA 784105788 ALHAMISI 2:30-3:00 JUMAPILI 1:00-1:30 JIONI
vya kilimo hai vinavyoletwa MKULIMA USIKU
kwako na shirika la Farm Radio RADIO HABARI JUKWAA LA 784105711 JUMAMOSI 3:00-3:30 JUMATANO 3:00-3:30 USIKU
International kupitia stesheni NJEMA MKULIMA USIKU

mbalimbali za radio. RADIO SAUTI YA JICHO LA


784105718 JUMAMOSI
1:30-2:00
JUMATANO 12:00-12:30 JIONI
INJILI MKULIMA USIKU

Tafuta masoko kabla ya kuanza uzalishaji


Mkulima anatakiwa kutafuta soko la na soko analolitegemea kwa zao Mkulima anaweza akauza
mazao yake kabla hajaanza shughuli analolizalisha. mazao yake katika masoko yasiyo
ya uzalishaji shambani. Utafiti wa Hivyo, wakati unapanga zao gani rasmi. Kikawaida, ni rahisi sana
soko humwezesha mkulima kupata unataka kuzalisha, fikiria kuhusu kuyafikia masoko haya kwani
taarifa sahihi kuhusu mambo yafuatayo: soko lisilo rasmi huwa
mbalimbali ya uzalishaji na uuzaji • Wengine wanazalisha nini ni pamoja na kuuza
wa zao husika. • Je kuna uhitaji wa bidhaa mazao mlangoni mwa
yako shamba (shambani
Flora Laanyuni • Soko linahitaji nini? au nyumbani kwa
Kupitia utafiti wa soko mkulima • Matarajio gani ya mkulima) na uuzaji
huweza kupata taarifa za mambo ubora yako katika wa kando ya
yafuatayo: eneo la soko barabara. Masoko ya
• Mazao yanayohitajika zaidi na • Mahitaji gani ya vijijini, uuzaji katika
walaji. kisheria unatakiwa maeneo ya mjini
• Masoko yaliyopo kwa kila aina ya kutimiza. Kwa mfano, na masoko ya jumla
zao. huwezi kuzungusha na rejareja ni masoko
• Bei za soko kwa zao husika. maziwa bila ya kibali. rasmi.
• Viwango vya ubora kwa kila aina ya Bei Muda wa kuuza
zao. Mkulima anapotafuta soko la mazao Mkulima lazima aamue juu ya muda
• Aina mbalimbali za wateja yake ni muhimu sana kutafakari juu halisi wa kuuza mazao yake. Katika
wanaoweza kununua mazao. ya bei itakayotozwa. Ni muhimu sana biashara, muda wa kuuza huwa
• Muda muaafaka wa kuuza mazao. kupata majawabu ya maswali yafua- na maana kubwa juu ya faida za
Mambo ya kuzingatia wakati tayo: na uzalishaji. Yapo mazao ambayo
kutafuta masoko • Utatoza bei sawa na wengine? huuzwa mara tu baada ya kuvunwa
• Utafanya nini kama kutatokea kwani uhifadhi wake ni mgumu na
Kutafuta soko la mazao ni kutafuta
mshindani? yapo mazao yanayoweza kuhifadhika
mnunuzi wa mazao yaliyozalishwa na
• Je, inafidia gharama zako za kiurahisi huweza kuuzwa kwa muda
mkulima. Soko linalotafutwa ni lile uzalishaji na kukuachia faida?
ambalo mkulima anaweza akauzwa tofauti wenye bei nzuri zaidi.
• Kuna bei tofauti kulingana na
mazao yake kwa faida. viwango tofauti? Vipimo sahihi
Kutafuta soko la mazao ni kutafuta • Unaweza kutengeneza faida? Wakati wa kuuza mazao, mkulima
mteja anayeweza kununua mazao Ni muhimu sana kwa mkulima lazima azingatie vipimo sahihi na
kwa bei nzuri zaidi. Kikawaida, soko kujua maeneo tofauti na bei ambazo vinavyokubalika nchini. Vipimo
lina wateja wanaoweza kununua anaweza toza kama atauza mazao vitumikazo hutofautiana na aina ya
mazao kwa bei tofauti, utafutaji wa yake huko. Mkulima anaweza zao linalouzwa. Vipo vipimo vya ujazo
soko huhusisha kumtambua mnunuzi kutumia mitandao ya kijamii, ambavyo hutumika hasa kupimia
mwenye uwezo wa kulipa kwa bei kusikiliza redio na televisheni pamoja mazao yaliyo katika ya uzito ambacho
kubwa zaidi kwa zao linalotakiwa na kusoma magazeti kwa lengo la ni kilogramu.
kuuzwa. kujua bei zinazotozwa katika masoko Mfano, mkulima anauza magunia
Wakati wa kutafuata masoko ya husika. Mkulima pia anaweza kufanya manne ya mahindi kwenye soko
mazao mkulima anatakiwa kuzingatia na mawasiliano na wanunuzi hivyo lisilo rasmi. Kipimo atakachokitumia
mambo yafuatayo: kujua bei halisi ya kuuzia mazao yake. ni kilogramu. Atalazimika kupima
Bidhaa Mahali pa kuuzia mazao uzito wa kila gunia ili kujua uzito wa
Kwa vile soko hutafutwa pale Mkulima lazima ajue wapi atauzia pamoja wa magunia yote manne.
mkulima anapotaka kuanza mazao yake. Hii inahusisha pia namna Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
kuzalisha, ni muhimu sana kwa gani mkulima ataweza kulifikia soko Lukas Rwechoka kwa simu
mkulima kutambua nini atakizalisha lake. 0754886888

+255 717 266 007


mkulimambunifu.org, http://www.facebook.com/mkulima_mbunifu
theorganicfarmer.org http://twitter.com/mkulima_mbunifu
infonet-biovision.org https://www.instagramu.com/mkulima_mbunifu

Haki zote zimehifadhiwa ©2023 Mkulima Mbunifu Mkulima Mbunifu

You might also like