You are on page 1of 8

HAIIBA TIMAMU TEA!

CHAI YA AJABU KUTOKA HERBAL IMPACT

NI KITU GANI CHA AJABU JUU YA HII CHAI TULIYOCHAGUA KUIITA HAIIBA
TIMAMU TEA?

Na. Juma Killaghai

PINGILI YA UTI WA MGONGO YAPONA!

Mimi nilikuwa mtu wa kwanza kabisa kushuhudia maajabu ya hii chai. Niilibuni hii chai kama
jaribio la kutibu pingili yangu ya mwisho ya uti wa mgongo (karibu na kiuno) ambayo ghafla
ilikuwa imeanza kunipa maumivu makali, haswa mida ya asubuhi baada ya kuamka.

Siyo siri, nachukia mno dawa za kifamasia. Kutokana na kutozipenda dawa hizo niliamua
nichukue kwanza sheria mkononi, na iwapo itashindikana ndipo nijisalimishe kuzitumia! Kwa
sababu kitaaluma mimi ni mkemia mtafiti wa vitu asili vyenye uhai (organic natural products
research chemist) niliamua kufanya utafiti.

Kama ilivyo ada hatua ya kwanza ya utafiti wowote ni utafiti wa nyaraka (literature review).
Kimsingi utafiti wangu uliishia katika hatua hii, kwani kupitia nyaraka mbalimbali stahiki
niliweza kubaini mimea kadhaa ambayo ilikuwa na mwelekeo wa kuweza kunitatulia tatizo
langu. Baada ya tafakuri ya kina niliamua kubuni mchanganyiko wa mimea hii katika muundo
ambao mtumiaji angetumia kama chai.

Kama nilivyotangulia kusema, nikawa mtu wa kwanza kabisa kuitumia hii chai. Maajabu! Ndani
ya siku tatu za matumizi maumivu yale ya pingili yalitoweka na hadi leo sijui yalikopotelea. Huu
ni karibu mwaka wa tano sasa! Kufuatia matokeo haya ya kustaajabisha niliamua kuiita chai hii
HAIIBA TIMAMU TEA

HAPA CHINI NITAELEZEA VISA VINGINE VICHACHE VYA KWELI AMBAVYO


NADHANI VINAHALALISHA KUIITA CHAI HII KUWA NI CHAI YA AJABU!

1. MKE WANGU APONA MAUMIVU SUGU YA KICHWA!

Baada ya kupona maumivu ya pingili yangu ya uti wa mgongo, nilipata hamasa ya kuishawishi
familia yangu kutumia chai iliyonitibu. Baada ya siku chache mke wangu alinipa siri yake ya
muda mrefu. Alisema kuwa alikuwa akikabiliwa na maumivu ya kichwa ya muda mrefu na
alikuwa amejaribu matibabu mbalimbali ya hospitali bila kuniambia lakini haikuwa imemsaidia.
Aliniambia kuwa baada ya mimi kuwahamasisha watumie HAIIBA TIMAMU TEA aliamua
kujaribu japo kwa shingo upande lakini alishangaa kuwa baada ya siku chache maumivu yote
yalikuwa yametoweka!

2. ARUDIA KULA NYAMA NYEKUNDU!


Siku moja alikuja rafiki yangu mmoja akadai kwamba kila alipokuwa akila nyama nyekundu
alikuwa anapata maumivu makali kwenye viungo (joints) haswa kwenye vifundo vya vidole.
Nilimwambia kuwa uwezekano mkubwa ni kuwa alikuwa anakabiliwa na ugonjwa wa jongo
(gout). Kwa kuwa rafiki yangu huyu anafahamu kuwa nafanya tafiti za tiba mbalimbali
zinazotokana na mimea na viumbe hai vingine aliniuliza iwapo nilikuwa na dawa. Nilimjibu
kuwa nilikuwa nimebuni chai fulani inayoitwa HAIIBA TIMAMU TEA ambayo pengine
ingeweza kumsaidia. Siku chache baadaye alinifuata akaniambia kuwa baada ya kutumia CHAI
niliyompa tatizo lake lilikuwa limekwisha na alikuwa ameanza kula tena nyama nyekundu bila
kuathiriwa na maumivu makali ya viungo.

3. NAONA RIZKI YANGU IMEFIKIA UKINGONI!

Siku moja rafiki yangu mwingine, bwana Chake Bakari Nyumba (kaniruhusu nimtaje na nitoe
namba yake ya simu kama kuna mtu anataka kufanya ithbati ya haya maelezo), alinipigia simu
akidai kwamba anahisi riziki yake duniani imekwisha. Nilipomuuliza ni kwa nini anasema hivyo
alijibu:

“Wala sijui hata ninaumwa nini. Najisikia hovyo kabisa. Siwezi kula chochote!”

Nilimwambia ajaribu chai ya HAIIBA TIMAMU. Baada ya siku chache nilimpigia simu
kuumuliza alikuwa anaendeleaje akanambia kuwa alikuwa mzima kabisa! Namba ya simu za
bwana Chake Bakari ni 0754415161/0715159159

4. HALI NI MBAYA WALA SIJUI NINACHOUMWA!

Jirani na ofisini kwangu mtaa wa Mosque, Kitumbini (mkabala na msikiti wa Sunni) liko duka la
vyombo vya nyumbani la KD Sundries. Duka hili liko kwenye kona ya mitaa ya Mosque na
Mshihiri. Ni duka maarufu kwa vyombo vya kila aina vya nyumbani.

Mmoja wa wafanya kazi wa duka hilo anayeitwa Rajab Bakari Amani ni rafiki yangu wa muda
mrefu (kanipa ruksa nimtaje na kutoa namba yake ya simu iwapo kuna mtu atataka kuhakiki
taarifa hii). Siku moja, mida ya saa 4 hivi asubuhi, nikiwa ndio kwanza nimefika mjini nilipita
nje ya duka la KD Sundries nikiwa njiani kuelekea ofisini kwangu.

Nilimkuta Rajab akiwa ameketi nje ya duka huku akiwa amejikunyata (mida hiyo duka lao bado
lilikuwa halijafunguliwa). Nilisimama kumsabahi na kumuuliza ni kwa nini alikuwa katika hali
ile.

“Brother, hali yangu ni mbaya sana, wala sijui naumwa nini! Karibu wiki ya tatu sasa”

Alinambia.

“Hospitali umekwenda?”

“Nimekwenda lakini sijaona matokeo yoyote ya maana!”


“Du! Sasa mbona umekuja kazini kama hali ndiyo hiyo?”

Nilimuuliza.

“Sasa kaka nitafanya nini? Si unajua kazi zetu hizi? Muhindi hawezi kukuelewa hata siku moja
kuwa umelala nyumbani, hasa kwa sababu haielweki utalala mpaka lini!”

“Kuna dawa fulani hivi, labda nikupe uijaribu”

Nilimwambia.

“Kaka utakuwa umeniokoa kaka!”

Nilimpatia Rajab pakiti moja ya chai ya HAIIBA TIMAMU nikampa maelekezo jinsi ya
kuitumia. Maajabu! Siku iliyofuata nilikutana na Rajab akiwa mchangamfu na akanambia kuwa
hakuwa anajisikia kuwa na tatizo lolote!
Namba ya simu ya Rjabu ni: 0712242557

5. BABA KAWEZA KWENDA MJINI!

Kuna jamaa yangu mmoja ni mtaalamu wa shughuli za usafi na bustani. Huyu tumekuwa naye
kwa miaka kadhaa tukishirikiana kila ninapopata kazi za kandarasi zinazohusiana na shughuli za
usafi na bustani.

Huyu jamaa yangu siku moja alinifuata akaniambia kuwa alikuwa anataka kusafiri kwa siku
chache kwenda kijijini kuwasalimia wazazi wake. Aliniambia kuwa nimpatie chai ya HAIIBA
TIMAMU ampelekee baba yake akaijaribu kwa kuwa kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa
na matatizo mengi ya kiafya.

Nilimpatia huyu jamaa yangu pakiti mbili za hii chai tukaagana. Siku chache baadaye huyu
jamaa yangu alirejea kutoka kijijini. Nilishangaa kuwa alikuwa akitabasamu kila mara aliponiona
kinyume na kawaida yake. Siku mbili baadaye udadisi ulinizidi nikaamua kumuuliza
kilichokuwa kinaendelea.

“Baba alienda mjini!”

Aliniambia.

“Kwani huwa haendi mjini?”

Nilimuuliza kwa mshangao.

“Anakwenda lakini ni lazima afuatane na mtu. Alishashindwa kwenda mwenyewe siku nyingi
zilizopita!”

“Sasa imekuwaje?”
Nilimuuliza.

“Baada ya kuitumia hiyo chai yako si kafunga safari peke yake hadi Moshi mjini na kurudi!”

“Du!”

Nilipigwa na mshangao. Pamoja na kwamba miye mwenyewe ndiye mtengenezaji wa hiyo chai
nilikuwa napata tabu kuamini nilichokuwa nakisikia!

6. SHEMEJI USIPONISAIDIA SIJUI WAPI PENGINE PA KWENDA!

Siku moja nilirejea nyumbani kiasi cha saa 4 usiku huku nikiwa nimechoka sana. Nilifadhaika
nilipoona kuna mgeni, kwani nilijua kuwa suala la kuoga na kupumzika mara moja halikuwepo
tena. Mgeni mwenyewe alikuwa ni rafiki ya mke wangu ambaye alikuwa anaishi mtaa wa tatu
kutoka pale kwetu. Baada ya kusabihiana mke wangu alinitaka tuingie chumbani. Huko
chumbani aliniambia kuwa shoga yake alikuwa amekaa muda mrefu akinisubiri kwa imani
kwamba ningeweza kumsaidia.

“ Kwani ana shida gani?”

Niliuliza.

“Anasema anaumwa. Naona ni bora umsikilize mwenyewe”

“Sasa wewe umemwambia kuwa mimi naweza kumtibu”

Niliuliza.

“Mimi sijamwambia. Ila kang’ang’ania kwa sababu kipindi kile ulimpa ile dawa ya jino
ikamsaidia”

“Du! Sasa itakuwaje? Anyway hebu ngojea nimsikilize”

Nilisema.

Rafiki yake mke wangu aliniambia kuwa alikuwa ana muda wa juma zima anajisikia mwili wote
unamuuma, kichwa kimekaa hovyo hovyo kabisa na kwa ujumla hana amani kabisa.

“ Sisi tunatibiwa katika vituo vya afya vya AAR. Nimezunguka vituo vitatu tofauti sijaona
tofauti yoyote. Shemeji usiponisaidia sijui wapi pengine pa kwenda!”

Aliniambia.

Nilimwambia asubiri nikalelekea chumbani. Alikuwa ameniweka kwenye mazingira magumu


kweli kwa kule kujenga kwake imani kuwa mimi ndiye niliyekuwa msaada pekee. Wakati
natafakari cha kufanya mke wangu aliingia.
Nilimwangalia kwa mfadhaiko.

“Huyu rafiki yako ananipa mtihani kweli! Sasa tutampa nini? Labda jaribu kumpa hizo pakiti
mbili za TIMAMU TEA zilizobaki hapo”

Nilimwambia.

Siku mbili baadaye nilimuuliza mke wangu.

“Hivi shoga yako anaendeleaje?”

“Bwana we! Nilisahau kukwambia. Anakushukuru sana! Bukheri wa afya”

7. HEDHI ISIYOKATA!

Kwa kumalizia nielezee visa vitatu vilivyoletwa na jamaa watatu tofauti ambao walidai kuwa
wake zao wanasumbuliwa na kutokwa na hedhi isiyokata! Niliwashauri kuwa siyo sahihi
kutafuta dawa za ‘KIENYEJI’ bila kwanza kupata vipimo vya kisasa ikajulikana wanaumwa
nini.
Kwa nyakati tofauti kila mmoja alirejea na kuniambia kuwa wake zao wamefanyiwa vipimo na
kugundulika kuwa wana saratani za shingo ya uzazi.

“Nimesikia kuwa una dawa!” Ilikuwa ni kauli ya kila mmoja.

“Kiukweli miye dawa ya ugonjwa huo sina. Hata hivyo iko dawa moja hivi ambayo
mchanganyiko wake pengine inaweza kusaidia. Hata hivyo itabidi mgonjwa akubali kuitumia
kwa muda mrefu”

Yalikuwa ndio majibu yangu kwa kila mmoja.

Maajabu! Kila mmoja kwa wakati wake alitoa taarifa kuwa hedhi iliyokuwa inamtoka mkewe
mfulululizo ilikuwa imekata na maumivu yametoweka. Saratani imepona? Hilo miye sijui.
Ushauri niliompa kila mmoja ni kuwa kama hali ya uchumi inaruhusu mgonjwa aendelee na
matumizi ya TIMAMU TEA kwa walau miezi sita zaidi mfulululizo.

Ukitafakari kwa undani kunaweza kusiwe na maajabu yoyote katika huu uwezo wa HAIIBA
TIMAMU TEA. Magonjwa mengi ya kimfumo yanasababishwa na upungufu wa virutubisho
mbalimbali vinavyohitajiwa na mwili ili kuimarisha siha. Mimea iliyotumika kuandaa chai hii
ina utajiri mkubwa sana wa hivi virutubisho. Orodha kamili ya virutubisho hivi ni:

1. AMINO ACIDS (VIJENZI VYA PROTINI)


• Arginine;
• Histidine;
• Isoleucine;
• Leucine;
• Lysine;
• Methionine;
• Phenylalanine;
• Threonine;
• Tryptophan; na Valine.

2. VITAMINI NA MADINI
• Carotine (Vitamin A);
• Thiamin (Vitamin B1);
• Riboflavin (Vitamin B2);
• Niacine (Vitamin B3);
• Vitamin C;
• Calcium;
• Copper;
• Iron;
• Magnesium;
• Phosphorous;
• Potassium;
• Zinc;
• Chromium; na
• Manganise.

3. VIZUIA VIOKSIDISHAJI (ANTI OXIDANTS)


• Curcumin;
• Catechines;
• Polyphenols;
• Flavonoids; na
• Piperine
4. Viua vijidudu
• Cinnamaldehyde.

Sasa ukisoma nyaraka za kitafiti utabaini kuwa viini lishe hivi vinatajwa kuwa ni msaada
mkubwa kwa matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na:

• Kudhibiti maumivu ya viungo;


• Kudhibiti uchovu na kuondoa hali ya kujisikia homa mara kwa mara;
• Kudhibiti mfuro wa seli (inflammation);
• Kuimarisha kinga za mwili;
• Kusawazisha kiwango cha lehemu (cholestrol) mwilini kuwa cha kawaida;
• Kudhibiti kasi ya kuzeeka;
• Kuboresha usagaji wa chakula tumboni;
• Kuboresha siha ya mfumo wa damu na utendaji wa ini;
• Kusafisha ngozi na kuhifadhi mnyumbuko wake;
• Kupeleka virutubisho muhimu kwenye ngozi;
• Kuimarisha siha ya macho;
• Kuzuia kuongezeka kwa seli za saratani;
• Kuzuia seli za kawaida za mwili kubadilika na kuwa seli za saratani;
• Kuuchochea mwili wako kuangamiza seli za saratani kabla hazijasambaa mwilini;
• Kuzuia uundwaji wa mishipa ya ziada ya damu kwa ajili ya kufikisha virutubisho vya ziada
katika seli za mwili zenye saratani;
• Hupunguza shinikizo la damu;
• Kupunguza uwezekano wa kupata shambulizi la moyo (heart attack);
• Kupunguza uwezekano wa mishipa ya fahamu kupoteza utando wa nje unaokinga sehemu ya
ndani na kwa hivyo kuifanya ifanye kazi kwa ufanisi (multiple sclerosis);
• Kuongeza uzalishaji wa nyongo;
• Kuzuia uharibifu wa lehemu nyepesi mwilini kutokana na mwingiliano na oxygen;
• Kupunguza madhara ya kisukari cha ukubwani;
• Kupunguza dalili za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer’s disease);
• Kuharakisha kupona kwa majeraha;
• Kupunguza madhara ya baridi ya yabisi;
• Kupunguza kasi ya ongezeko la virusi vya ukimwi;
• Kukinga dhidi ya uharibifu wa ini;
• Kukinga dhidi ya sumu na makovu kwenye mapafu;
• Kukinga dhidi ya ugonjwa wa ngozi kuchuja rangi, yaani, vitiligo; na
• Kusafisha kinywa dhidi ya bakteria wasiotumia oksijeni (anaerobic bakteria)

Chai hii inaweza kukusaidia pia kama unahisi kuwa unakabiliwa na moja wapo ya hali hizi. Hivi
sasa inapatikana Dar es Salaam pekee, katika ofisi zetu zilizoko Mosque Street, No. 1574/144
(mkabala na msikiti wa Sunni), Kitumbini. Jitihada zinafanyika pia ili kabla ya mwisho wa
mwaka huu iwe inapatikana walau katika miji yote iliyo makao makuu ya mikoa Tanzania
nzima. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba
0754281131/0686281131/0655281131.

KWA WALIOKO DAR ES SALAAM

Kama unaishi Dar es salaam unaweza kuja hapa ofisini kwetu mtaa wa Mosque, kwa ajili ya
kupata chai ya Timamu. Tuko Kitumbini, mtaa wa Mosque. Mtaa huu unaitwa Mosque kwa
sababu kuna misikiti miwili mikubwa inayoongozana (Ibaadh na Sunni); ambayo
imetenganishwa na duka la tamu-tamu la Taj Mahal Sweet Mart.

Mtaa huu pia ni maarufu sana kwa MGAHAWA WA MIAKA MINGI SANA UNAOITWA NEW
ZAHIR RESTAURANT (Tazama picha. Jengo lenye canopy yenye mistari myekundu.). Iwapo
utalazimika kuuliza ili ufike Mosque Street, basi waambie hao unaowauliza ni mtaa iliko NEW
ZAHIR RESTAURANT. Ukiweza kufika NEW ZAIHIR RESTAURANT utaiona hiyo misikiti
miwili tuliyoitaja iliko. Kama hukuiona wewe mwenyewe uliza! Ni hapo jirani kabisa.

Sisi tunatazamana na huo msikiti wa Sunni (wenye minara ya kijani). Aidha tuko jirani kabisa na
duka maarufu la vifaa vya usafi na bidhaa nyingine za majumbani la ZANZIBAR STATE
TRADING CORPORATION. Ukiona mabango ya TRIPLE A TAILORING SERVICES yafuate,
utakuwa tayari umefika. HERBAL IMPACT, TRIPLE A TAILORING SERVICES NA NEOBIZ
tunachangia eneo la ofisi.

JINSI YA KUFIKA
1. kwa wanaotokea maeneo ya Mbagala, Kurasini na Temeke ambao wakija mjini kituo chao cha
mwisho cha daladala ni Stesheni, basi waje mpaka barabara ya Samora liliko tawi la NBC
SAMORA. Mtaa wa Mosque unaanzia NBC Tawi la Samora na kupandisha kuelekea juu hadi
mtaa wa Libya. Ili kufika ofisini kwetu, ukitokea hapo NBC Samora utavuka kwanza mtaa wa
India, kisha mtaa wa Indira Gandi. Hapo utakuta hiyo misikiti mikubwa miwili inayoongozana.

2. Kwa wanaokuja mjini kwa njia za Morogoro na Ali Hassan Mwinyi, kituo cha basi cha
kushukia ni AKIBA. Baada ya kuteremka tembea hadi kwenye maungio ya Morogoro Road,
ingia Morogoro Road na uifuate kama vile unaelekea Bandarini zinakoegeshwa Boti za kwenda
Zanzibar. Endelea mbele ambapo utavuka mitaa ya Libya na kisha Jamhuri mpaka
utakapokutana na tawi la benki ya NMB la Morogoro Road likiwa mkono wako wa kulia. Hapo
kata kulia kuingia mtaa wa Mshihiri. Ukiendelea mbele kidogo utakutana na mtaa wa Mosque
unakatiza na kushoto kwako utaiona hiyo misikiti miwili.

3. Kwa wanaokuja na barabara za Nyerere au Uhuru hadi Mnazi Mmoja. Ukifika mnazi mmoja
vuka mataa hadi liliko tawi la benki ya NBC la Mnazi mmoja. Hapo utakuwa uko mtaa wa
Jamhuri. Shusha moja kwa moja na huo mtaa hadi utakapokuta kituo cha mafuta cha Puma.
Mbele kidogo ya hicho kituo ni mtaa wa Mosque unakatiza. Ukifika hapo kwenye mauongio ya
Jamhuri na Mosque, tazama kulia kwako utaona hiyo misikiti miwili.

4. Kama unataka kuja na gari lako Mwenyewe ni bora uende hadi Samora avenue uingie Mosque
Street kwa kutokea hapo tawi la NBC Samora. Au kama unatokea barabara ya Nkrumah au
Uhuru, ukishafika Clock Tower ingia mtaa wa India,vuka mtaa wa Aggrey (kuna kituo cha
mafuta cha GAPCO) na barabara utakayokutana nayo ikikatisha ni Mosque. Hapo kata kushoto
na baada ya kuvuka Mtaa wa Indira Gandi utaiona hiyo misikiti miwili mkono wako wa kulia.

You might also like