You are on page 1of 4

IFAHAMU SARATANI YA DAMU ( LEUKEMIA)

* JINSI YA KUTAMBUA KUWA NINA SARATANI YA DAMU (LEUKEMIA)

❇️Dalili za Saratani ya Damu

▪️Dalili za saratani ya damu hutofautiana kulingana na aina ya saratani ya damu. Kuna aina
tano tofauti za saratani ya damu ambazo kila moja inazo dalili, tiba na matokeo tofauti ya
matibabu na muendelezo na matokeo ya ugonjwa. Ambazo ni kama zifuatazo kwa majina ya
kitaalamu

1. Leukaemia (Leukemia)

2. Lymphoma

3. Myeloma

4. Myelodisplastic syndrome na,

5 Myeloproliferative Neoplasms.

Hapa tutaongelea zaidi aina ya kwanza na aina zake, yaani LEUKEMIA.

❇️DALILI ZA LEUKEMIA( zinazonekana kuwapata wagonjwa wengi)

✔️ Homa na kuhisi hali ya baridi( kutetemeka)

✔️ Kutoka Jasho sana hasa usiku

✔️ mwili kuchoka sana na kuwa dhaifu

✔️ kupata maambukizi ya magonjwa nyemelezi mara kwa mara

✔️ kupungua uzito bila sababu maalum

✔️ kupoteza hamu ya kula

✔️ kupata shida ya kupumua

✔️ kuvimba tezi sehemu mbalimbali za mwili

✔️ kuvimba ini pamoja na bandana na hisia ya kujaa tumbo

✔️ kupata michubuko ya ngozi isiyoelezeka au damu kuvia chini ya ngozi


✔️ damu kutoka ndani ya pua mara kwa mara

✔️ kuwa na alama alama nyeusi au nyekundu kwenye ngozi( viashiria vya mgando wa damu
chini ya ngozi)

✔️ maumivu ya misuli na mifupa na misuli kukaza hata wakati wa mapumziko.

✔️Vivimbe vya tezi za shingo, kwapa, tumboni na kwenye nyonga za miguu visivyokuwa na
maumivu

✔️Kuhisi uchovu wa mwili muda wote

SEHEMU YA PILI

IJUE LEUKEMIA:

JE LEUKEMIA NI NINI?

Leukemia ni Saratani inayoshambulia chembechembe za damu, ni saratani inayoathili mfumo


( kiwanda) wa kutengeneza seli mbalimbali za damu unaofahamika kama ULOTO
unaopatikana ndani ya mifupa pamoja mfumo wa tezi za mwili, ambapo baada ya mabadiliko
hasi husababisha uzalishaji wa haraka uliopindukia wa seli za damu usio sahihi. Kwa kawaida
huathili seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga ya mwili, ingawa pia huathili seli nyekundu
na zinazohusika na mgando wa damu.

Watu wanaokuwa kwenye mazingira yenye kiwango cha juu cha mionzi na kemikali yenye
sumu ya ki- Hydrokaboni ya Benzini wanao uwezekano mkubwa wa kupata aina tofauti za
Leukemia kama ilivyo kwa wavutaji sigara na aina za tumbaku, watu ambao wamewahi kupata
tiba ya kemikali katika kutibu maradhi mbalimbali na watu waliorithi magonjwa mbalimbali
ikiwemo yanayo athili mfumo wa damu.

❇️ AINA ZA LEUKEMIA

🔳Kuna aina mbalimbali za Leukemia. Madaktari huzitofautisha kilingana na sehemu


zinakoanzia na kuhusisha kama:-

▪️zinazoanzia na kuhusisha ULOTO (bone marrow) -huitwa Myeloid au,

▪️Tokana na mfumo wa tezi- huitwa Lymphoid

▪️Au jinsi gani kwa haraka saratani inavyo inavyokua na kuleta athali ( acute leukemias)
▪️Au jinsi gani saratani hukua taratibu na athali zake kuonekana baada ya muda mrefu
kupita ( Chronic Leukemias). Hata hivyo dalili za saratani hizi hutofautiana kulingana na aina
ya saratani husika.

MATIBABU YA LEUKEMIA NA JINSI YA KUZUIA MADHARA YATOKANAYO NA


DAWA.

Matibabu anayopata mgonjwa wa Leukemia hutegemea na aina ya Leukemia aliyonayo mtu,


hali yako kiafya wakati ugonjwa unagundulika na umri wako.

Hakikisha unaufahamu vizuri ugonjwa wako, aina za matibabu na dawa zilizopo na jinsi gani
itakavyogusa na kuleta athali kwenye mwili wako na maisha yako. Ufahamu juu ya saratani
kwa ujumla, matibabu yake na maudhi madogo madogo yatokanayo na matibabu unayopata
yatakusaidia kushirikiana bega kwa bega na wataalamu wako wa afya ili kuboresha hali ya
afya yako wakati wa matibabu na baada ya matibabu. Kumbuka siku zote kuwa kila mgonjwa
huwa na njia zake tofauti za matokeo yatokanayo na matibabu anayopata na hivyo
kutofanana kwa kila mgonjwa.

🔳Mambo muhimu ya kukumbuka kila unapoonana na Daktari wako.

Mara baada ya kuufahamu vizuri aina ya ugonjwa wako, utatakiwa kushirikiana na watoa
huduma wako wote wanaokuhudumia, ili kufikia muafaka kuhusu stahiki ya huduma na
matibabu yako ili kufikia matokeo change.

▪️kumbuka kuandika maswali au dukuduku lako ili umwulize Daktari wakati wa kliniki yako, na
aidha andika majibu kwa ufasaha kuepuka kusahau

▪️ongea na Daktari kuhusu jinsi gani unavyojisikia na kila dalili unayoona au kuhisi

▪️ongea na uliza kuhusu maudhi au madhara yatokanayo na matibabu na ni aina gani ambayo
utatakiwa kutoa taarifa kwa watoa huduma wako mara moja.

▪️Uliza ni jinsi gani utaweza kutuliza au kuondoa maudhi na madhara yatokanayo na matibabu

▪️Uliza kuhusu taarifa mpya zilizopo zinazohusu majaribio mbalimbali ya tiba ya Leukemia

▪️Uliza maswali kwa weredi na kuhakiki umeelewa vizuri ulichoelekezwa na watoa huduma
wako

▪️Pata taarifa sahihi kwa kutumia lugha nyepesi kwako ya mawasiliano na ikiwezekana pata
hata michoro kama ni muhimu na lazima katika kurahisisha uelewa wako
▪️Wakati mwingine ambatana na ndugu wa karibu atakaye kuwa msaada na njia ya
kumbukumbu na usikivu kwako

▪️Kama kuna gharama zitokanazo na matibabu omba ushauri toka kwa watoa huduma yako
jinsi ya kupunguza gharama hizo

▪️Ni muhimu sana kutumia dawa zako kama maelekezo yalivyo, lakini ni muhimu kuwaeleza
watoa huduma wako kama imetokea kuwa uliruka au hukutumia dawa kama ilivyopangwa, pia
wafahamishe kama kuna aina yoyote ya maudhi madogo madogo ya dawa yaliyosababisha
ukashindwa kutumia dawa zako kwa mpango

▪️Angalia kama watoa huduma wako hawashirikiani nawe katika kutatua changamoto
mbalimbali za matibu unazopitia, fikiria kuomba mbadala wa watoa huduma wengine watakao
kusaidia.

ASANTE SANA.

You might also like