You are on page 1of 1

ALAMA TISA (9) ZA LAANA

Zifuatazo ni alama TISA(9) zinazo dhihirisha kwamba unaishi chini ya laana katika maisha
yako.
1. MAGONJWA YA AKILI; pale mtu anapopatwa na matatizo ya kiakili au msongo wa
mawazo, hii ni dalili mojawapo kudhihirisha kuwa mtu huyo yuko chini ya laana. Na wakati
mwingine unakuta kuna watu kadha wa kadha katika familia au ukoo wanapatwa na tatizo hilo la
msongo wa mawazo hapo ni wazi kuna tatizo la laana katika Ukoo au familia.
2. MAGONJWA YA MUDA MREFU NA YA MARA KWA MARA; kama mtu anaumwa
ugojwa kwa muda mrefu na mara nyingine unaodoka na kumrudia tena au muda mwingine
unaitwa ugojwa wa kurithi. Na wakati mwingine unaenda kwa daktari haoni ugonjwa baada ya
kufanya vipimo vya kisayansi ni wazi mtu mwenye matatizo ya jinsi hiyo anaishi chini ya laana.
3. UGUMBA NA UTASA; Mtu mke au mume ambaye ana matatizo ya kutopata mimba au
kuzalisha hii ni dalili ya wazi kabisa kuwa kuna uwezekano mkubwa akawa yuko chini ya laana.
4. TABIA YA KUHARIBIKA KWA MIMBA MARA KWA MARA; mwanamke ambaye ana
sifa ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara kila wakati anapokuwa mjamzito, hii ni dalili ya
wazi kuwa mtu huyo yuko chini ya laana.
5. MATATIZO SUGU YA HEDHI; mwanamke ambaye ana matatizo sugu ya hedhi, mara kwa
mara haoni siku zake kwa wakati, anatokwa na damu nyingi kupita kawaida,NK. Hii ni dalili ya
wazi kabisa kuwa mtu huyo yuko chini ya laana.
6. KUVUNJIKA KWA NDOA NA UMOJA WA FAMILIA; pale ambapo uhusiano na umoja
wa wanafamilia unavunjika na kuwapo na uhasama baina ya ndugu kwa ndugu, na ikiwa kuna
historia ya ndoa za wanafamilia kuvunjika mara kwa mara, hii ni dalili ya wazi kuwa watu hawa
wako chini ya laana nzito.
7. UMASIKINI ULIOKUBUHU; pale mtu anapokuwa kwenye dimbwi zito la umasikini kwa
muda mrefu, na familia imejaa umasikini wa muda mrefu; yaani yeye kila siku ni ombaomba tu.
Hata akijitahidi kufanya shughuli fulani ya kujipatia kipato kwanza ndiyo matatizo
yanaongezeka. Ni wazi mtu huyo yuko chini ya laana.
8. AJALI ZA KILA MARA; mtu ambaye kila wakati anapata ajali, iwe kuteleza, ajali za vombo
vya mto kila wakati, uharibifu wa vitu kila wakati, kila wakati wewe unaumia tu kwa ajali zisizo
kuwa na kikomo, ni wazi mtu wa namna hiyo ni mtu aliye chini ya laana.
9. HISTORIA YA WATU KUJIUA NA VIFO VISIVYO VYA KAWAIDA KATIKA
FAMILIA AU UKOO AU KABILA; pale ambapo kuna historia katika familia, koo au kabila
kuhusu watu wa familia au koo au kabila kupatwa na vifo vya ajabu au kujitoa uhai wenyewe hii
ni dalili mbaya kuwa kuna laana kati yenu. Mfano halisi ni kabila moja hapa nchini Tanzania
kutoka katika mikoa ya nyanda za juu kusini, watu wa kabilia hili wanasumbuliwa na laana hii
kutokana nakile kilichofanywa na wazee wa zamani

You might also like