You are on page 1of 3

ELEZA AINA ZA USAMPULISHAJI NI KUTOLEA MIFANO.

A) Sampuli /sampling

Sampuli ni ndogo na huwa kiwakilishi tosha katika ukusanyaji wa data kutoka kwa jamii pana.
Data inayokusanywa hapa huwa kiwakilishi mwafaka cha jamii lengwa.(Field, 2005)
Aina za sampuli
a. Sampuli kutegemea fursa(opportunity sample)-Wale ambao ni rahisi kuhojiwa.
b. Sampuli nasibu(random sampling)
c. Sampuli nasibu tabakishi(stratified random sample)-hukuwezesha kupata aina ya watu
unaowahitaji.
d. Sampuli kusudio(purposeful sample)
e. Sampuli mgao (quota sample)
f. Sampuli tajwa. (snowball sample)
Uzuri wa mbinu hii.

a. Wakati huwa mfupi kwa kuwa hurejelea tu sehemu ndogo ya sampuli.


b. Gharama yake iko chini kwa sababu sampuli lengwa ndiyo inayohusika.
c. Sampuli husika huwa na wakati bora wa kujieleza.
d. Mtafiti huweza kukongamana vilivyo na walengwa.
e. Rasilimali(muda na fedha) hutumika kiasi na pia mzigo wa kazi huwa mwepesi.
f. Hutoa matokea kwa usahihi ambayo yanaweza kuthibitiwa kihesabu.

Ubaya wa mbinu hii.


a. Huenda sampuli lengwa isitoe msimamo thabiti wa jamii lengwa.
b. Kutopata data ya kutosha kwa kusababishwa na kukosekana kwa utangamano kati ya
wawakilishi husika.
c. Mapendeleo ambayo huathiri matokeo.
d. Kiwango duni cha elimu kati ya sampuli husika.
e. Hali ya kimaisha na misimamo ya kimaisha inayosukumwa na tamaduni za jamii husika.
B) Upimaji (Measurement)

Hii ni mbinu ya ukusanyaji wa data ambapo mtafiti huikusanya data kwa kupima. mtafiti
hutumiavifaa maalum vya Upimaji huku akirekodi matokeo.
Mbinu hii huweza kutumika katika hali mbalimbali kama ifuatavyo.

a. Zamani ili mtoto ajiunge na shule ya msingi, aliweza kujipima kwa kutumia mkono
wake juu ya kichwa. Iwapo alijigusa sikiobasi iliaminika kuwa alikuwa tayari
kujiunga na shule ya msingi.
b. Fundi mshona-nguo ni lazima aitafute data ya vipimo vya mteja wake kabla ya
kumshonea nguo.
c. Masorovea hutumia vifaa mbalimbali vya upimaji ili kubaini kiwango cha shamba
linalonunuliwa au kutatua migogoro ya mashamba.
d. Ili wahandisi waweze kuzigenga barabara au majumba ya maghorofa nilazima
waweze kuchukua data katika mbinu hii ili kuhakikisha kuwa wanachotarajia
kukitekeleza kitakuwa swari.

Ubora wa mbinu hii.

a. Kuna mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mtafiti na mtafitiwa.


b. Data inayokusanywa ni tendeti.
c. Huchukua muda chache kwa kuwa mtafiti na mtafitiwa/kitafitiwa huingiliana moja
kwa moja.
d. Muda huwa mchache mno.

Kasoro za mbinu hii

a. Kukosekana kwa vifaamaalum vya matumizi.


b. Wakati mwingine huwa ghali kutokana na viambajengo mbalimbali.
c. Kukosekana kwa mataalam faafu wa kuvitumia vifaa hivi.
d. Baadhi ya viombo hivi kutengemea kawi au nguvuza umeme na ambazo hazikadiriki.

Marejeleo

a. Adam, J na Kamuzora, F (2008) Research Methods for Business and Social Studies.
Morogoro:Mzumbe Book Project.
b. Bowern, C(2008) Linguistic Fieldwork: A Practical Guide. New York:Palgravw-
Macmillan.
c. Kothari, C.R(2004) Research Methodology: Methods and Techniques. New
Delhi:New Age International.
d. Msokile,M (1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, Nairibi:EAEP
e. Mulokozi, M.M.(1983) “Utafiti wa Fasihi Simulizi” Katika TUKI Makala ya Semina
ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili 111:Fasihi. Dar es Salaam:TUKI Kur. 1-25.
f. Ongechi,N.O.L Shitemi,na K.I. Simala (wah) (2008)Nadharia katika Taaluma ya
Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Eldoret:Moi Univesity Press.
g. Pons,Valdo (Mh) (1992) Introduction to Social Research. Dar es Salaam:Dup.
h. Sewangi, S.S. and Madulla J.S.(eds)(2007) Makala ya Kongamano la Jubilei ya
TUKI(Vol.1 and 11) Dar es Salaam:TUKI.
i. Siiimala K.I.(mh) (2002) Utafiti wa Kiswahili. Eldoret:MoiUniversity Press.
j. K.W.Wamitila(2004)Chemichemi za Kiswahili,Longhorn Printers(Kenya)Ltd,
Nairobi, Kenya.
k. J.Habwe na A. Matel (2006)Darubini ya Kiswahili.,Phonex Publishers, Nairobi.
l. L.Sanja na M.Kusino(2006) Kurunzi ya Kiswahili K.C.S.E. Kitabu cha marudio,
Focus Publishers Ltd,Nairobi.
m. F.Waititu na Wenzake(2004) Kiswahili Fasaha Kidato cha Tatu,Oxford University
Press, East Africa Ltd. (Kenya)

You might also like