You are on page 1of 10

CHUO KIKUU CHA MOI

BEWA KUU

KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA KIJAMII

IDARA. :KISWAHILI NA LUGHA NYINGINE ZA KIAFRIKA.

JINA. :HELLEN.M.NYAMWEYA

NAMBARI YA USAJILI:MS/KIS/5467/21

KOZI. : RESEARCH METHODS

MSIMBO WA KOZI: KIS 895

MHADHIRI :PROF. MOSOL KANDAGOR

KAZI. : a) Mbinu za kukusanya data.

Uchunguzi nyanjani

Uchunguzi shirikishi/Usoshirikishi.

MWAKA. :2020/2021

MUHULA. :KWANZA

TAREHE. : 03/03/2022
1)DHANA YA UTAFITI

Utafiti ni uchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi katika kutafuta taarifa juu ya Jambo fulani.

Utafiti hutumika kuanzisha au kuthibitisha ukweli, Kuthibitisha matokeo ya kazi ya awali


kutatua matatizo mapya au yaliyopo kuendeleza nadharia mpya pia upanuzi wa kazi ya zamani.

Utafiti hujumuisha kazi ya ubunifu ambayo hufanywa kwa misingi ya utaratibu ili kuongeza
maarifa ya elimu mfano; Ujuzi wa wanadamu.

Utamaduni na jamii.

Maatumizi ya ujuzi wa kuunda maombi mapya.

1.1. AINA ZA UTAFITI

a) Utafiti wa msingi

b) Utafiti wa matumizi

UTAFITI WA MSINGI

Ni utafiti unaolenga kupata maarifa au mawazo mapya juu ya tabia ya viasili vinavyoweza
kubadilika kukiwepo hali fulani.

Utafiti wa namna hii huzingatia sana kutumia matokeo yake kwa kutatua tatizo. Mfano; kufanya
Jambo ambalo halijawahi kufanywa ili kupata jibu.

UTAFITI WA MATUMIZI

Ni utafiti unaojihusisha na Kuthibitisha mambo muhimu katika jamii.

1.2. UTARATIBU WA UTAFITI


1.2.1. Ainisha mada ya utafiti- Chagua mada moja utakayo ishughulikia baada ya kusoma kazi
kadhaa za watangulizi katika uwanja unaotaka kushughulikia. Kwa mfano; sababu ambazo
zinaawafanya wanafunzi wengi kuwa watukutu shuleni katika nyakati hizi tunazo ishi

1.2.2 Fafanua tatizo la utafiti- Changanua tatizo ambalo umelichagua kwa undani ili kulielewa
zaidi kabla ya kuanza kulishughulikia na baada ya kusoma kazi kadha za kinadharia katika
uwanja huo.

1.2.3. Eleza madhumuni na malengo ya utafiti- Tambua Jambo ama sababu la kufanyia utafiti ili
kumfanya mtafiti kuangazia suala moja na lifaalo katika kazi yake.

1.2.4. Eleza nadharia tete zitakazoongoza utafiti wako- Tambua njia au mwelekezo utakao
utumia katika kazi uliyo ichagua kati ya zingine.

1.2.5. Jadili machapisho yaliyoshughulikia suala hilo na onyesha dosari na mapengo yake-
Mtafiti anapaswa kuangalia kazi iliyofanywa mbeleni ili kulitambua Jambo ambalo bado
halijaangaziwa na watafiti waliomtangulia.

1.2.6. Onyesha namna utafiti wako utakavyorekebisha dosari na kuziba mapengo hayo na
matarajio yako- Angalia Kama jawabu lako litaleta suluhisho na kuziba pengo zilizoko .

1.2.7. Eleza mbinu na njia za utafiti zitakazotumika, pamoja na usampulishaji wa watafitiwa au


wa data iwapo utahitajika- Njia inayotumiwa katika utafiti huchangia zaidi katika kumwezesha
mtu kufanya utafiti wa kutegemewa.

1.2.8. Eleza nadharia za kiuchambuzi utakazotumia kuchambua data zako- Njia zitumikazo
katika uchambuzi pia husaidia sana katika kuifanya kazi yako kuwa ya kuaminika.

1.2.9. Onesha ratiba ya utafiti- Panga kazi yako ukianzia na Jambo utakalo lifanya kuanzia la
kwanza hadi la mwisho ili kuwa na mwelekeo wa kazi yako unao onekana.

1.2.10. Onyesha makisio ya bajeti ya utafiti-, bajeti iwiane na ahughuli zitakazo fanyika- Mtafiti
anapaswa kuhakikisha amepiga bajeti ya pesa aatakazo hitaji katika kazi yake ili kujipanga
kuzipata pesa hizo.

1.2.11. Weka orodha ya marejeleo- Mtafiti anapaswa kuorodhesha nakala ambazo aatarejelea
katika kuandika na kufanya utafiti wake

1.2.12. Ambatisha maswali, vidadisi na zanaa nyingine za utafiti atakazozitumia- Vifaa


vitakavyo tumika katika utafiti zinapaswa kuwekwa pamoja ili Mtafiti kuianza kazi yake.

2)DHIMA YA UTAFITI (KIJUMLA)

Umuhimu wa utafiti kaatika taaluma ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali ni Kama ifuatavyo;
a) Utafiti na kujisomea

Utafiti huu utakuwa na umuhimu kutumika Kama rejeleo muhimu katika tafiti za baadaye
kuhusiana na ushairi wa kimapokeo na ule wa kisasa kwa mfano.

Vilevile, utafiti huu hutumika Kama kitabu ama rejeleo kwa wanafunzi wa ngazi za shahada ya
kwanza, uzamilifu katika taaluma za fasihi ya Kiswahili.

b) Kitamaduni

Utafiti huu utaonesha masuala ya kiutamaduni katika jamii za mwambao na jamii za bara. Kwa
kuzibaini tamaduni hizo itakuwa rahisi kwa msomaji na Mtafiti ama mhakiki yeyote yule
kuzielewa kwa undani pale aanapotaka kutumia tamaduni hizo katika maandishi yake.

c)Kinadharia

Katika ngazi ya elimu ya sekondari,utafiti huu utakuwa na umuhimu kwa watunzi sera na
mitaala ya elimu kwamba, wanapotunga mitaala hiyo kuhusu fasihi ya Kiswahili kwa ujumla na
ushairi mahususi wazingatie mambo gani yanayopaswa kuigizwa katika mitaala hiyo.

d)Kihistoria

Utafiti huu utakuwa sehemu mojawapo ya muendelezo wa maendeleo ya historia ya Kiswahili


tangu kupatikana kwa uhuru mpaka kufikia leo.

Baada ya kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika, historia ya ushairi wa kiswahili ilianza kuwa na
mgogoro wa ushairi wa kiswahili na sasa tunaandika kuhusu mambo yatokanayo na mgogoro
huo.

Humwezesha mtafiti kupata suluhisho la kilele la Jambo lililompa msukumo kufanya kazi yake.

Hutupa habari zote tunazohitaji kuhusu mada ya utafiti wa elimu.

Humsaidia Mtafiti kugundua ujuzi, maarifa au Kanuni mpya zinazosaidia kueleza nadharia mpya
za kielimu.

Humwezesha mtafiti kupima na kukadiria mafanikio.mfano; Tafiti zenye lengo la kuona ubora
wa mihtasali mipya, vitabu vipya, njia mpya za ufundishaji na masomo mbalimbali na hatimaye
kufanya marekebisho ili kufikia kiwango kinachohitajiwa.

Humwezesha mtafiti kuweza kupata mbinu za kutatua matatizo yaliyotokea na uwekaji wa


malengo ya baadae ya kielimu.

DHIMA YA UTAFITI ( KIELIMU)


a) Humwezesha mtafiti kupata taarifa muhimu kuhusu suala linalotafitiwa.

b) Kazi ya utafiti huongeza hazina ya maarifa katika uwanja unaohusika.

c) Kipima-joto Cha hali, fikira, Mitazamo, matarajio ya jamii ya watafitiwa.

d) Kuchangia katika kujenga na kuendeleza fani za fasihi simulizi na fani nyinginezo.

3)UKUSANYAJI WA DATA

Ukusanyaji wa data hutawaliwa na mambo mane;

i) Uwanja wa taaluma unaohusika- Hii ni sehemu ambayo inashughulikiwa na mtafiti katika kazi
yake ya utafiti.

ii)Lengo la utafiti- Ni lile Jambo ambalo mtafiti anataka kupata suluhisho kwalo kutokana na
utafiti anao ufanya.

iii)Uwezo wa nyenzo alizonazo mtafiti - Vifaa ambavyo mtafiti amevichagua kufanya kazi yake
ya utafiti pia huweza kudhihirisha iwapo kazi iliyofanywa ni ya kuaminika au la.

iv)Muda alio nao mtafiti- Iwapo mtafiti ana muda wa kutosha wa kufanya kazi yake, basi
ataifanya kazi yake kikamilifu na kwa makini kuhakikisha kuwa utafiti wake Ni wa kuaminika.

3.1. NJIA KUU ZA UTAFITI

.Utafiti wa maktabani/ wa nyaraka

.Utafiti wa uwandani

.Utafiti wa maabarani/ studioni.

3.1.a. Utafiti wa Maktabani/Nyaraka

Nyaraka asilia.

Nyaraka rasmi za kiserikali

Nyaraka binafsi (barua, shajara, mjadala, kumbukumbu, vyeti n.k)

3.1.b. Nyaraka Fuatizi

Nyaraka rasmi/ za serikali

Nyaraka binafsi (vitabu, kumbukumbu, ripoti, magazeti n.k)

3.1.c.Utafiti wa Uwandani
Mbinu za Utafiti

Kushuhudia

Kushiriki

Mahojiano

Mijadala ya vikundi lengani.

Kutumia vidadisi na majedwali.

MBINU ZA KUSHUHUDIA

Kushuhudia ni mbinu ya kuangalia tukio linapotendeka na kukusanya taarifa zake.

Namna za Ushuhudiaji

a) Uchunguzi na upimaji -Mtafiti awe na vifaa vinavyohitajika kwa kazi hiyo.

b)Ushuhudiaji fungemno .

c)Ushuhudiaji funge- Unatoa uhuru zaidi.

d)Ushuhudiaji lengani.- Mtafiti huangalia tukio katika mazingira yake asilia bila majedwali.

e) Ushuhudiaji huru/ Usiofunge- Hufanywa kwa siri na mtafiti bila mtafitiwa kufahamu na bila
mpangilio wa wazi.

3.2 MBINU ZA KUKUSANYA DATA

Data inaweza kukusanywa kwa njia mbalimbali Kama vile;

a) Kusikiliza

Mkusanyaji anaweza kusikiliza wasanii katika jamii wakitamba, kusimulia au kuimba tungo zao.

b)Kushiriki

Mkusanyaji data anaweza kujiunga na jamii kwa Kushiriki katika ngoma, soga, na masimulizi ya
hadithi na tanzu zingine.

UMUHIMU WA KUSHIRIKI

.Mtafiti huja karibu zaidi na jamii na hupata habari za kuaminika moja kwa moja.

.Mkusanyaji hupata hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na
watendaji hivyo kuelewa zaidi mada ya utafiti.
.Hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii.

.Ni rahisi kwa mkusanyaji kuuliza maswali kuhusu kipera kinachowasilishwa.

.Kushiriki ni njia bora ya kukusanya habari kutoka kwa watu ambao hawajui kusoma na
kuandika.

UDHAIFU WA KUSHIRIKI

.Huchukua muda mrefu kwani Kushiriki katika utendaji ni kazi.

.Huenda mtafiti akatekwa na yaliyomo na kusahau kurekodi.

.Ugeni wa mtafiti huweza kuleta wasiwasi miongoni mwa washiriki na wakakosa kutenda Kama
kawaida.

.Hii ni njia ghali ya utafiti kwani inamhitaji mtafiti kusafiri mbali ili Kushiriki katika utendaji.

c)Kurekodi (Filamu, Video)

Mkusanyaji anaweza kusikilizana na watu na kuwarekodi katika vinasa sauti , kanda na video.

d) Kutazama

Mkusanyaji anaweza kushuhudia kwa macho fasihi fulani ikiendelezwa bila Kushiriki.

UMUHIMU WA UTAZAMAJI

.Ni rahisi kwa mtafiti kurekodi kwa vile hashiriki katika utendaji.

.Mtafiti hupata habari za kutegemewa zaidi hasa pale anapotumia kinasa sauti kurekodi.

.Utendaji wa wahusika hauathiriwi kwani hawafahamu kuwa mtafiti anawaona, hivyo basi
kuaminika.

UDHAIFU WA UTAZAMAJI

.Wanajamii wanaweza kumshukuru mtafiti kuwa anawapeleleza na hivyo kusitisha uwakilishaji


wao.

e) Kutumia Hojaji

Hojaji ni fomu yenye maswali yaliyochapishwa ili kukusanya habari fulani.

Hojaji huandaliwa na mkusanyaji wa data na kutumwa kwa mhojiwa atakaye jaza . Kuna hojaji
wazi na funge.

UMUHIMU WA HOJAJI
.Gharama ya chini.

.Yaweza kutumika katika mahojiano.

.Huokoa muda kwani mtafiti aweza kuituma na kuachia mhojiwa kujaza.

.Hupata habari za kuaminika na kutegemea.

UPUNGUVU WA HOJAJI

.Utata wa maswali husababisha majibu yasiyo sahihi.

.Si nzuri kwa wasiojua kusoma na kuandika.

.Kutopata sifa za uwasilishaji Kama vile kiimbo, toni na ishara.

.waojiwa kukataa kuijaza kutokana na sababu mbalimbali.

f) Kurekodi Katika Kanda za Sauti.

UMUHIMU WA KUREKODI

.Kuweza kudumu na kufikia vizazi Vingine.

.Sifa za uwasilishaji/uhai Kama vile toni na kiimbo kuhifadhiwa.

.Mkusanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.

.Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.

.Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.

UDHAIFU WA KUREKODI

.Chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.

.Hakiwezi kunasa uigizaji.

.Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa .

.Ghali na kuhitaji kununua kifaa na kumbidi mtafiti kusafiri.

g)Mahojiano

Kuhoji wanao fahamu mengi kuhusu utafiti.

UMUHIMU WA MAHOJIANO

.Kuweza kungamua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.


.Kuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.

.Kuweza kupata sifa za uwasilishaji.

.Ni rahisi kurekodi.

.Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.

UDHAIFU WA MAHOJIANO

.Huhitaji muda mrefu.

.Mhojiwa kutotoa habari kwa kutomwamini mtafiti kwa ugeni wake.

.Kikwazo cha mawasiliano- Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.

.Ghali kwa gharama ya usafiri.


MAREJELEO.

Ehtridge, D.E. (2004) "Research Methodology in Applied Economics." John Wiley & Sons
p.24.

Quinn,. P.M. (1990) Qualitative Evaluation and Research Methods.

Nyandemo,S.M (2007) Research Methodology, Methods and Approaches. Richmonds Designers


and Printers.

Mugenda,O and Mugenda A.M (1999) Research Methods. Nairobi:Acts press.

Fox, W. & Bayat, M. S (2007) "A Guide to Managing Research" . Juta publications, p.45.

You might also like