Professional Documents
Culture Documents
Hellen's Prof Kandagor Assignment
Hellen's Prof Kandagor Assignment
BEWA KUU
JINA. :HELLEN.M.NYAMWEYA
NAMBARI YA USAJILI:MS/KIS/5467/21
MWAKA. :2020/2021
MUHULA. :KWANZA
TAREHE. : 03/03/2022
Tuki; Inaeleza kuwa vifaa vya tafsiri ni vyombo ambavyo hutumika kutoa andiko au maelezo
fulani kutoka lugha moja hadi nyingine.
Ni vyombo vya kutafsiri au kuhawilisha mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi
lugha nyingine
Mills na Tilden wakinukuliwa na Beck na Cable (1998) Wanadai ya kuwa hakuna namna
mkalimani atakwepa kutumia vifaa vya kiteknolojia , bali yampasa mkalimani kuhakikisha
anatumia vizuri vifaa hivyo na kwa uangalifu mkubwa.
1)TARAKILISHI/TAFSIRI KOMPYUTA
SEHEMU ZA TARAKILISHI
Kiwambo(Skrini)
Bao kuu
C.P.U(Bongo kuu)
Ugawi wa umeme
Kiendeshi (CD)
Baobonye
Puku
1)TARAKILISHI
Hivyo Kompyuta Kama Kompyuta kwa hakiki haifanyi kazi bila kupewa maelekezo.
Hii inabadilisha kabisa kabisa Imani kuwa Kompyuta inafanya kazi kuliko binadamu na
kwamba Ina uwezo wa juu kuliko hata ubongo wa binadamu!
Neno Kompyuta kwa kimombo 'computer' linatokana na neno 'computing' likiwa na maana
ya kukokotoa au kuchanganua hesabu kama; kujumlisha, kugawanya, kutoa na kuzidisha.
Kompyuta Ina historia ndefu kutoka katika kipindi Cha kabla ya kuzaliwa kwa Kristi ambako
watu mbalimbali Kama Charles Babbage.
Lakini kifaa Cha kwanza kabisa ambacho kinafanana kiutendaji na Kompyuta ya leo hii
kiligunduliwa mnamo karne ya 20 (kati ya mwaka (1940-1945) ingawa nadharia ya
Kompyuta na mashine mbalimbali zilizo fanana nayo zilikuwapo hapo mwanzoni
Kompyuta inaweza kuelezewa kuwa imepitia hatua kadhaa katika kufikia ubora iliyonayo
sasa.
Mfano wa Kompyuta hizi ni Konrad Zuse's electromechanical au" Z machines " au Z3(1941),
Atanasoff- Berry computer (1941), Colossus Computer(1944) ambayo ilitumika kwa ajili ya
shughuli za Siri katika jeshi la Uingereza na ilitumika katika kupata taarifa za Siri za jeshi la
Ujerumani katika kupata taarifa za Siri za jeshi la Ujerumani katika vita vya pili vya dunia,
Harvard.
Hata hivyo teknolojia hii ya vacuum tubes ilitumika mpaka mwishoni mwa miaka ya 1950 na
mwanzoni mwa miaka ya 1960 kulizinduliwa teknolojia mpya inayofahamika Kama
"transistor technology".
Kompyuta zilizotumia teknolojia hii ziliweza kufanya kazi kwa urahisi zaidi, hazikuwa ghali
sana, zilitumia umeme mdogo zaidi na ziliweza kufanya kazi kwa uhakika zaidi kuliko zile za
mwanzo
Kumbuka kuwa Kompyuta za mwanzo zilikuwa na ukubwa sawa na chumba kikubwa Cha
nyumba!.
Teknolojia hii ndiyo imesababisha kuzaliwa kwa Kompyuta ambazo ni ndogo zaidi kuweza
hata kubebwa katika kiganja Cha mkono!.
Hii ni sababu ya kuundwa kwa kifaa kijulikanacho Kama microprocessor ambacho ndicho
Kama ubongo wa Kompyuta.
Kifaa hiki kina umbo mdogo sana lakini kina jumla ya zaidi ya transistor (sakiti ndogondogo
zinazofanya kazi kwa ushirikiano) milioni moja!.
Electronic kifaa Cha Tafsiri ya lugha hutegemea akili ya bandia kuchakata maneno na
kuyatafsiri katika lugha mpya.
Huweza Kusaidia hadi lugha 170 na vinaweza kulishwa habari kwa njia anuwai.
I)Tafsiri ya sauti- Kifaa kile hutumia spika na kadi ya kumbukumbu kurekodi ujumbe
ii)Tafsiri ya picha- Mtu huchapisha maneno /picha Kisha kifaa hutumia kamera kuyaona
1)Huwezesha watu Kuwasiliana kwa urahisi nje ya nchi- Kutembelea nchi zingine na
kuelewa lugha yao.
2) Kupanua biashara yako- Ni ngumu kuanzisha tawi katika nchi nyingine iwapo hakuna mtu
ofisi yako anayezungumza lugha ya nchi hiyo.
2) PROGRAMU ZA KUTAFSIRI
Naanza kwa kuchagua lugha ambayo nataka kutafsiri kwenye orodha iliyopo
Basi mimi kuchagua lugha ambayo nataka kuwa na Tafsiri kutoka kwa orodha sawa ya lugha
zilizopo.
Kisha mimi kuandika neno ,Mimi kushinikiza kwenda na mimi kupata Tafsiri!.
Na kama sijui jinsi ya kuandika, naweza kubonyeza kipaza sauti na kusema neno na Tafsiri
ya Google itanipa tafsiri yake.
Naweza hata kubofya kamera na programu itafsiri moja kwa moja maneno yaliyoandikwa
kwenye karatasi au Skrini
Duolingo
Mfano; Programu hii ya kijani ni Duolingo . Kwa hiyo, baada ya kuunda akaunti ,anaweza
kuingia , bonyeza kitufe kwenye kona na Kisha bofya kwenye "plus cours".
Kwa 'default', itakuwa kwa watu wanaozungumza lugha ya kiingereza , lakini ikiwa unapita
chini, utaweza kutafuta na kuchagua lugha yako.
Mchakato halisi wa kutafsiri hufanyika ndani ya Smartling na zana iliyojengwa katika tafsiri
ya msaada wa Kompyuta (CAT)
Pamoja na CAT ya Smartling, Muktadha wa kuona hutolewa kila wakati kwa watafsiri, na
kuwezesha watafsiri kuelewa ni nini maudhui wanayotafsiri na jinsi maneno yao yanavyofaa
katika muktadha huo.
Mara tu Tafsiri yenyewe imekamilika, watafsiri wanaweza kuhamia haraka kwa shukrani ya
kazi inayofuata kwa uelekezaji otomatiki
Smartling pia inafanya kazi ya kufanya kazi ya waatafsiri wa kibinadamu iwe rahisi
iwezekanavyo pia.
i)Muktadha wa kuona- Watafsiri wanaweza kukagua kazi yao moja kwa moja, kwa muundo
wowote.
viii) Utunzaji wa tag rahisi- Inatumia ujifunzaji wa mashine kuweka vitambulisho kwa
usahihi.
ix) Utaratibu wa moja kwa moja- Programu inaweka yaliyomo kusonga na inasababisha moja
kwa moja tafsiri iliyokamilishwa kwa hatua inayofuata.
x) Ujanibishaji unaotokana na data- Programu sio tu! Inawapa wateja data ya wakati halisi
juu ya mchakato wao wa kutafsiri, lakini pia ni busara ya kutosha kuwafanyia maamuzi.
xi) Muktadha wa kuona- Watafsiri wanapaswa kuona maneno kwa muktadha ili kutoa kazi ya
hali ya juu. Bila hivyo, uzoefu wa mtumiaji wa mwisho unateseka.
3) UJUZI/MAARIFA
MAARIFA- Ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu kwa kutumia
elimu au ujuzi. Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao au ukatokana na mangamuzi ya
maisha yakiwa pamoja na kusoma, kusikia au kutenda, pia huhusisha ufahamu na uelewa.
a)Awe mahiri wa lugha mbili zinazohusika- Kuwa mahiri ni kujua vizuri nyanja mbalimbali
za isimu ya lugha husika Kama vile; fonolojia( matamshi), fonolojia (maumbo),
Sintaksia(muundo).
e)Awafahamu watu, jamii na utamaduni wao- Mitazamo kuhusu watu, Mitazamo kuhusu
wanyama.
a) Awe mwaminifu kwa matini na kwa Mwenye matini; Yaani asipotoshe habari au kusema
uongo.
d)Aelewe/ kuelewa taratibu za kazi na kuzifuata. Mfano; bei ya kutafsiri kwa ukurasa au kwa
maneno.
Uhusiano wake na tafsiri- humsaidia mtafsiri kuelewa mifumo ya lugha mbalimbali na jinsi
lugha hizo zinavyotumia vipengele vyake vya kiisimu kutolea taarifa mbalimbali.
a) Ni njia ya mawasiliano kati ya watu au jamii mbili zinazotumia lugha tofauti mfano;
maelezo mbalimbali ya jinsi ya kutumia bidhaa mbalimbali Kama redio na simu.
b) Ni nyenzo ya kuelezea utamaduni kutoka jamii moja kwenda jamii nyingine mfano;
kupitia dini- Tafsiri ya Biblia au Kuruani.
d)Ni kazi ya ajira Kama kazi nyingine , hivyo huweza kumpatia mtu kipato.
UTANGULIZI
CHANGAMOTO
c) Data za kutafsiri huitaji huhitaji utafitiwa kina kuhusu lugha mbalimbali ili kutunga
kamusi faafu za kuzipa mashine hizi uwezo.
d) Mashine za tafsiri hazina uwezo wa kufanya tafsiri zinazohusu lugha nyingi za ulimwengu
ambazo hazina data.
g) Lugha nyingine zipo hatarini kupotea na hivyo, harakati za kutunga data katika lugha hizi
zinaweza kukabiliwa na matatizo hasa iwapo juhudi hazitafanywa kuokoa lugha hizi.
k) Mchakato wa tafsiri huhitaji tajriba au ujuzi na uzoefu ambao mashine Kama tarakilishi
hazina
l) Kubadilika kwa lugha pia huathiri tafsiri ya sentensi kwa sababu lugha zote za ulimwengu
hubadilika kulingana na wakati, msamiati uliopo huzeeka na mwingine mpya kuzuka na
kuanza kutumiwa na katika hali hii tafsiri ya tarakilishi hukabiliwa na upungufu iwapo
hakutakuwa na juhudi za kufanya mabadiliko ili kuzifanya mashine hizo ziendane na miundo
ya lugha zinazohusika.
m) pia changamoto ya ubora wa tafsiri wa taarifa zilizofanyiwa tafsiri kwa njia ya mashine
Kama vile changamoto za misamiati huzuka iwapo wataalamu wa tafsiri watachelewa kubuni
misamiati ya kurejelea teknolojia mpya.
HITIMISHO
Imebainika katika makala haya kwamba ingawaje utandawazi umekuja na manufaa mengi
kwa huduma za jamii ikiwamo utoaji wa huduma za tafsiri, Kuna pia changamoto nyingi
ambazo zimeandamana na manufaa hayo. Imebainika kwamba vifaa mbalimbali vya tafsiri
vimekabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimewalazimu watafsiri na wasaidizi wao
kupanga mikakati ya kuyasuluhisha . Mikakati hii imekuwa na gharama ambayo watafsiri na
wasaidizi wao wanalazimika kumudu ili kufanikisha kaazi yao. Baadhi ya changamoto
ambazo zimeibuliwa na utandawazi ni zile zinazotokana na tamaduni. Imebainika kwamba
watafsiri na wasaidizi wao sharti wafahamu utamaduni wa matini asilia pamoja na waandishi
wao ili kufanikisha tafsiri zao.
Changamoto ya dini nayo inalazimu wafasiri kufanya utafiti kuhusu dini iliyoathiri matini
asilia ili kuwasaidia kuelewa matini asilia. Changamoto nyingine ni zile zinazotokana na
Kuwepo kwa teknolojia mpya ambayo imekuwa ala muhimu katika mchakato wa tafsiri.
Vilevile, wafasiri wanatakiwa kupata mafunzo ya kila mara ili kuinua kiwango chao Cha
maarifa na ujuzi unaoendana na mabadiliko katika teknolojia mpya kuhusiana na utoaji wa
huduma za tafsiri.
MAREJELEO
Mwasoko, H.J.M na wenzake. (2003). Kitangulizi Cha Tafsiri. Nadharia na Mbinu. Dar es
Salaam: TUKI.
BEWA KUU
JINA. :HELLEN.M.NYAMWEYA
NAMBARI YA USAJILI:MS/KIS/5467/21
Uchunguzi nyanjani
Uchunguzi shirikishi/Usoshirikishi.
MWAKA. :2020/2021
MUHULA. :KWANZA
TAREHE. : 03/03/2022
1)DHANA YA UTAFITI
Utafiti ni uchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi katika kutafuta taarifa juu ya Jambo
fulani.
Utafiti hujumuisha kazi ya ubunifu ambayo hufanywa kwa misingi ya utaratibu ili kuongeza
maarifa ya elimu mfano; Ujuzi wa wanadamu.
Utamaduni na jamii.
a) Utafiti wa msingi
b) Utafiti wa matumizi
UTAFITI WA MSINGI
Ni utafiti unaolenga kupata maarifa au mawazo mapya juu ya tabia ya viasili vinavyoweza
kubadilika kukiwepo hali fulani.
Utafiti wa namna hii huzingatia sana kutumia matokeo yake kwa kutatua tatizo. Mfano;
kufanya Jambo ambalo halijawahi kufanywa ili kupata jibu.
UTAFITI WA MATUMIZI
1.2.1. Ainisha mada ya utafiti- Chagua mada moja utakayo ishughulikia baada ya kusoma
kazi kadhaa za watangulizi katika uwanja unaotaka kushughulikia. Kwa mfano; sababu
ambazo zinaawafanya wanafunzi wengi kuwa watukutu shuleni katika nyakati hizi tunazo
ishi
1.2.2 Fafanua tatizo la utafiti- Changanua tatizo ambalo umelichagua kwa undani ili
kulielewa zaidi kabla ya kuanza kulishughulikia na baada ya kusoma kazi kadha za
kinadharia katika uwanja huo.
1.2.3. Eleza madhumuni na malengo ya utafiti- Tambua Jambo ama sababu la kufanyia utafiti
ili kumfanya mtafiti kuangazia suala moja na lifaalo katika kazi yake.
1.2.4. Eleza nadharia tete zitakazoongoza utafiti wako- Tambua njia au mwelekezo utakao
utumia katika kazi uliyo ichagua kati ya zingine.
1.2.5. Jadili machapisho yaliyoshughulikia suala hilo na onyesha dosari na mapengo yake-
Mtafiti anapaswa kuangalia kazi iliyofanywa mbeleni ili kulitambua Jambo ambalo bado
halijaangaziwa na watafiti waliomtangulia.
1.2.6. Onyesha namna utafiti wako utakavyorekebisha dosari na kuziba mapengo hayo na
matarajio yako- Angalia Kama jawabu lako litaleta suluhisho na kuziba pengo zilizoko .
1.2.8. Eleza nadharia za kiuchambuzi utakazotumia kuchambua data zako- Njia zitumikazo
katika uchambuzi pia husaidia sana katika kuifanya kazi yako kuwa ya kuaminika.
1.2.9. Onesha ratiba ya utafiti- Panga kazi yako ukianzia na Jambo utakalo lifanya kuanzia la
kwanza hadi la mwisho ili kuwa na mwelekeo wa kazi yako unao onekana.
1.2.10. Onyesha makisio ya bajeti ya utafiti-, bajeti iwiane na ahughuli zitakazo fanyika-
Mtafiti anapaswa kuhakikisha amepiga bajeti ya pesa aatakazo hitaji katika kazi yake ili
kujipanga kuzipata pesa hizo.
1.2.11. Weka orodha ya marejeleo- Mtafiti anapaswa kuorodhesha nakala ambazo aatarejelea
katika kuandika na kufanya utafiti wake
a) Utafiti na kujisomea
Utafiti huu utakuwa na umuhimu kutumika Kama rejeleo muhimu katika tafiti za baadaye
kuhusiana na ushairi wa kimapokeo na ule wa kisasa kwa mfano.
Vilevile, utafiti huu hutumika Kama kitabu ama rejeleo kwa wanafunzi wa ngazi za shahada
ya kwanza, uzamilifu katika taaluma za fasihi ya Kiswahili.
b) Kitamaduni
Utafiti huu utaonesha masuala ya kiutamaduni katika jamii za mwambao na jamii za bara.
Kwa kuzibaini tamaduni hizo itakuwa rahisi kwa msomaji na Mtafiti ama mhakiki yeyote
yule kuzielewa kwa undani pale aanapotaka kutumia tamaduni hizo katika maandishi yake.
c)Kinadharia
Katika ngazi ya elimu ya sekondari,utafiti huu utakuwa na umuhimu kwa watunzi sera na
mitaala ya elimu kwamba, wanapotunga mitaala hiyo kuhusu fasihi ya Kiswahili kwa ujumla
na ushairi mahususi wazingatie mambo gani yanayopaswa kuigizwa katika mitaala hiyo.
d)Kihistoria
Baada ya kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika, historia ya ushairi wa kiswahili ilianza kuwa
na mgogoro wa ushairi wa kiswahili na sasa tunaandika kuhusu mambo yatokanayo na
mgogoro huo.
Humwezesha mtafiti kupata suluhisho la kilele la Jambo lililompa msukumo kufanya kazi
yake.
Humsaidia Mtafiti kugundua ujuzi, maarifa au Kanuni mpya zinazosaidia kueleza nadharia
mpya za kielimu.
ii)Lengo la utafiti- Ni lile Jambo ambalo mtafiti anataka kupata suluhisho kwalo kutokana na
utafiti anao ufanya.
iii)Uwezo wa nyenzo alizonazo mtafiti - Vifaa ambavyo mtafiti amevichagua kufanya kazi
yake ya utafiti pia huweza kudhihirisha iwapo kazi iliyofanywa ni ya kuaminika au la.
iv)Muda alio nao mtafiti- Iwapo mtafiti ana muda wa kutosha wa kufanya kazi yake, basi
ataifanya kazi yake kikamilifu na kwa makini kuhakikisha kuwa utafiti wake Ni wa
kuaminika.
.Utafiti wa uwandani
Nyaraka asilia.
3.1.c.Utafiti wa Uwandani
Mbinu za Utafiti
Kushuhudia
Kushiriki
Mahojiano
MBINU ZA KUSHUHUDIA
Namna za Ushuhudiaji
b)Ushuhudiaji fungemno .
d)Ushuhudiaji lengani.- Mtafiti huangalia tukio katika mazingira yake asilia bila majedwali.
e) Ushuhudiaji huru/ Usiofunge- Hufanywa kwa siri na mtafiti bila mtafitiwa kufahamu na
bila mpangilio wa wazi.
a) Kusikiliza
Mkusanyaji anaweza kusikiliza wasanii katika jamii wakitamba, kusimulia au kuimba tungo
zao.
b)Kushiriki
Mkusanyaji data anaweza kujiunga na jamii kwa Kushiriki katika ngoma, soga, na
masimulizi ya hadithi na tanzu zingine.
UMUHIMU WA KUSHIRIKI
.Mtafiti huja karibu zaidi na jamii na hupata habari za kuaminika moja kwa moja.
.Mkusanyaji hupata hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na
watendaji hivyo kuelewa zaidi mada ya utafiti.
.Kushiriki ni njia bora ya kukusanya habari kutoka kwa watu ambao hawajui kusoma na
kuandika.
UDHAIFU WA KUSHIRIKI
.Hii ni njia ghali ya utafiti kwani inamhitaji mtafiti kusafiri mbali ili Kushiriki katika
utendaji.
d) Kutazama
Mkusanyaji anaweza kushuhudia kwa macho fasihi fulani ikiendelezwa bila Kushiriki.
UMUHIMU WA UTAZAMAJI
.Ni rahisi kwa mtafiti kurekodi kwa vile hashiriki katika utendaji.
.Mtafiti hupata habari za kutegemewa zaidi hasa pale anapotumia kinasa sauti kurekodi.
.Utendaji wa wahusika hauathiriwi kwani hawafahamu kuwa mtafiti anawaona, hivyo basi
kuaminika.
UDHAIFU WA UTAZAMAJI
e) Kutumia Hojaji
Hojaji huandaliwa na mkusanyaji wa data na kutumwa kwa mhojiwa atakaye jaza . Kuna
hojaji wazi na funge.
UMUHIMU WA HOJAJI
.Gharama ya chini.
UPUNGUVU WA HOJAJI
UMUHIMU WA KUREKODI
UDHAIFU WA KUREKODI
g)Mahojiano
UMUHIMU WA MAHOJIANO
.Kuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.
UDHAIFU WA MAHOJIANO
Ehtridge, D.E. (2004) "Research Methodology in Applied Economics." John Wiley & Sons
p.24.
Fox, W. & Bayat, M. S (2007) "A Guide to Managing Research" . Juta publications, p.45.