You are on page 1of 8

JINA………………………………………………………….…..NAMBA……………….

DARASA…………
KISWAHILI
102/2
KARATASI YA PILI
LUGHA
21/2 SAA
1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
Cheo na madaraka ni dhamana ambayo haina thamani yoyote ile kama haikutumika kwa manufaa ya jamii.
Kutumia madaraka uliyokabithiwa vibaya inapotarajiwa yatumiwe kwa kuleta stawa na fanaka, heri na fahari
kwa watu unaowatumikia na taifa zima siyo hasa murua wa madaraka; wala si wajibu madaraka kutumiwa
kama sumaku ya kuvutia rushwa na mambo maovu kama hayo. Mara nyingi watu watu wenye madaraka
wanaoyatumia kwa njia isiyofaa huwa wapofu wa kweli uliopo kwamba utumiaji mbaya wa vyeo huweza
kupanguza au kuondoa kabisa imani ya raia kwa viongozi wao; na kwa kuwa serikali ndio huwapa wakuu hao
madaraka hayo – bila shaka kwa nia njema – raia huondoa imani kwa serikali yao.

Tatizo kubwa jingine, ambalo si mbali sana na hilo ni utumiaji wa fedha ya serikali kwa njia ya kufuja.
Malalamiko mengi sana yanayopokelewa yanaonyesha kuwa iktisadi haifuatwi na watenda kazi wa serikali
katika matumizi ya fedha. Ni wazi kuwa watenda kazi hawa wa serikali huandama fahari na anasa katika
utumizi wa fedha za serikali. Wao buchukua maisha katika hali ya juu ambayo harija yake huenda sambamba
kabisa na hali ya chini ya uchumi wa nchi. Inapokidhi kabisa kuwa na gari la shilingi chini ya milioni moja,
watu hawa huongeza shilingi milioni moja kutoka kwa mfuko wa serikali, wanaona fahari kuwa na gari la
shilingi milioni mbili. Inapohitajika kuandaa karamu ndogo tu, karamu kubwa huandaliwa na hugharinu
mapesa mengi ya serikali. Aste,aste hazina ya serikali huanza kupungukiwa kwa ukosefu wa uwekevu katika
matumizi ya fedha ya serikali. Matokeo makuu ya tatizo hili ni kudhoofisha hali ya uchumi na hivyo kuhini
mipango mingine fedha ya maendeleo kwa ufujaji kama huo. Jambo la maana kwa nchi maskini kama hii ni
watu hasa viongozi kuelewa umaskini wan chi yao na kukata koti kadiri ya kitambaa walicho nacho. Ni
muhimu serikali kutambua budhara ya fedha ya wananchi iliyofanywa na wakuu hawa. Pia kuwe na
zinazofungamana na matumizi ya fedha na zifuatwe, serikali inafaa pia kupunguza gharama katika mambo
mengi. Wakati umefika kwa kila mtumishi wa umma kuubeba mzigo wake kwa kugharamia maovu yake ili
kama wanavyosema, “kuwa funzo kwake yeye na wengine wenye tabia kama yake.

MASWALI
a) Ipe habari uliyoisoma anwani mwafaka (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
b)
i) Onyesha jinsi wenye vyeo hutumia vibaya madaraka yao (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………..
ii) Ni nini matokeo yao matumizi mabaya ya mamiaka (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 1

………………………………………………………………………………………………………
………
c) Kulingana na mwandishi ni namna gani ambapo cheo chaweza kukosa thamani. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
……….
d) Mwandishi anamaanisha nini anaposema “ ….kukata koti kadiri ya kitambaa walicho nacho” toa mifano.
(alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
……….
e)
i) Taja njia mbili alizopendekeza mwandishi ambazo zinafaa kuchukuliwa kutatua matatizo aliyotaja
katika kifungu hiki. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
ii) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika kifungu. (alama 2)
a) Sumaku…………………………………………………………………………………

b) Iktisadi………………………………………………………………………………….

2. UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata.
Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA)
barani Afrika. Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa ni za kimagharibi kama vile kijerumani, kifaransa na
kiingereza. Idadi kubwa ya waafrika, hasa wanaoishi vijijini, hawazifahamu lugha hizi.
Uamuzi wa Shirika la Microsoft wa kutumia lugha ya Kiswahili katika programu za kompyuta kuanzia
mwaka 2005 ni mchango mkubwa. Kuzinduliwa kwa mradi huu ni tuko la kipekee kuimarisha teknolojia
sehemu za mashambani. Mradi huu umewawezesha wananchi takribani milioni 150 wa janibu za Afrika
Mashariki kufaidi huduma za tarakilishi.
Utekelezaji wa mradi huu halikuwa jambo jepesi. Kwanza, ilibidi shirika la Microsoft chini ya uongozi
wa Bill Gates kulishawishi bodi lake la wakurugenzi. Bodi liliposhawishika lililofuatia lilikuwa kuteua
maneno 700000 ya kimsingi ya kiingereza ambayo yangetafsiriwa kwa Kiswahili.
Hatua iliyofuata ilikuwa ya kutafuta ushirikiano na dola pamoja na mashirika ya kibiashara na taasi za
kielimu ulimwenguni. Ilipobainika kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yangehamasisha uwekezaji katika
vituo vya mtandao vijijini, ushirikiano katika kuendesha mradi huu uliafikiwa bila shida. Mradi huu ulichukua
muda wa miezi 18 kukamilika. Uliwashirikisha wahusika katika uwanja wa teknolojia ya habari, mawasiliano,
elimu, biashara na idara za Kiswahili katika vyuo vya Afrika Mashariki. Vyuo vikuu hivi ni pamoja na Dar
es salaam, Nairobi, Kenyatta na Makerere.
Wataalamu walioshirikishwa walisaidia katika kubuni faharasa ya istilahi za Kiswahili 3000. Hizi ni zile
ambazo zinafaa kwa matumizi ya kompyuta ya kawaida nay a kila siku.
Mradi huu umeshangiliwa na wakereketwa na wapenzi wa Kiswahili katika Nyanja zote. Wasomi,
wanamuziki, watalii, wafanyabiashara, wanasiasa, wafuasi wa dini mbalimbali na wakulima; wote
wamefurahia hatua ya Kiswahili bila kuingizwa kwenye mtandao.

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 2

Watu ambao walikuwa hawawezi kutumia tarakilishi kwa sababu ya kutojua kiingereza sasa hawana
kisingizio. Matumizi ya Kiswahili yatapanua na kuimarisha mawasiliano baina ya watu wanaoishi vijijini na
pembe zote za ulimwengu.
Jambo la kutia moyo zaidi ni kuwa sasa vyuo vikuu vinavyotoa masomo kwa kutumia mitandao vimepewa
idhini ya kutumia program hizi. Walimu na wanafunzi wanapata habari moja kwa moja kwa Kiswahili bila
kutafsiri. Kuna uwezekano sasa wa kusambaza mafunzo katika Nyanja na viwango vyote kwa mfumo wa
elimu ya mbali.
Katika ulimwengu wa utandawazi, tukio kama hili lina manufaa makubwa. Wananchi wa vijijini
wanaweza kupata habari na maarifa kutoka pembe zote za dunia na kuhusu masuala tofauti kwa lugha
wanayoielewa barabara.
Kusambaa kwa matumizi ya ngamizi vijijini kutaimarisha biashara inayofungamana na teknolijia ya
mawasiliano. Hali hii itainua maendeleo ya kiteknolojia na kiwango cha maisha vijijini. Bila shaka mwachano
uliopo baina ya sehemu za mijini na vijijini utapungua.
Haya ndiyo maendeleo anayokamia kila mja wa siku hizi. Lililopo ni serikali kupania kupanua na
kusambaza muundo mbinu kama umeme na simu katika sehemu zote za nchi. Pamoja na haya, kuna haja ya
kupunguza bei ya ngamizi na vipuri vyake ili kuwatia motisha watu kununua kompyuta kwa wingi.
Ikumbukwe kuwa lengo la kuanzisha mradi huu lilikuwa kusaidia serikali kupanua na kusambaza matumizi
ya huduma za kompyuta na mtandao katika shule, vituo vya kijamii na maeneo ya makaazi. Huduma hizi ni
msingi wa elimu, biashara na mawasiliano ya kisiasa.

MASWALI
Ufupisho
a) Fupisha aya nne za kwanza kwa maneno kati ya 70 – 80. ( alama 9) (alama1 ya utiririko).
Matayarisho

…………………………………
Jibu

………………………

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 3

b) Eleza faida za mradi wa kutumia program ya kompyuta. Tumia maneno (45 – 55) (alama6 – al.1 ya
utiririsho)

…………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

a)
i) Eleza maana ya kiimbo. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
ii) Kiimbo huwa na majukumu yepi? (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……
b)
i. Silabi funge huwa na maana gani? (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……
ii. Toa mifano miwili ya maneno yenye silabi funge (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……
c) Kwa kutoa mifano onyesha matumizi mawili mawili ya alama zifuatazo za uakifishaji. (Al. 2)

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 4

i) Paradesi……………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
….
ii) Kibainishi…………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
….
d) Tunga sentensi changamano huku ukibainisha vishazi vilivyomo. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
e)
i) Tumia kiambishi – ni katika sentensi kama kiunganishi (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……
ii) Tunga sentensi ukitumia – po- kama kiambishi cha hali ya mazoea. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
……
f) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 3)
Elizabeth alimwambia Yohana kuwa angewakaribisha wageni siku hiyo jioni kasha angeondoka kwenda
kwake siku
iliyofuata……………………………………………………………………………….................
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
g) Ainisha virai vilivyopigwa mstari katika sentensi zifuatazo. (alama 3)
i) Rehema aliyeenda Ulaya kumtembelea mchumba wake. Amerudi:
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
ii) Mtu mwenye lile duka kubwa amefariki.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………..
h) Tofautisha vitate vifuatavyo – kimaana (alama 3)
I. Masaibu……………………………………………………………………………………………
….

II. Mashaibu……………………………………………………………………………………………

III. Masahibu……………………………………………………………………………………………

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 5

i) Andika sentensi hii upya katika hali ya ukubwa wingi. (alama 2)
Kigome cha kiharamia
kimelipuliwa…………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
j) Andika sentensi hii upya ukinyambua kitenzi katika kauli iliyo mabanoni. (alama 2)
a) mgonjwa amelazwa mapema
(tendesheka)……………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………………
….
b) paka alimuua panya juzi asubuhi
(tendeshwa)……………………………………………………………
..................................................................................................................................................................
..
k) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
babangu alitumiwa pesa na kakangu kwa
rununu……………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
l) Kwa kutolea mifano eleza miundo miwili ya nomino katika ngeli ya i – zi (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
……………
m)
i) Tunga sentensi ukitumia kihisishi cha dharau (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
ii) Tambulisha aina za viunganishi katika sentensi hizi. (alama 2)
a) Iwapo utampata, mpashe ujumbe wangu.
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
…………
b) Alifukuzwa shuleni madhali amekuwa mhuni.
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
……….

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 6

n) Eleza maana zinazotokana na vivumishi katika sentensi hizi. (alama 2)
i) Mwanafunzi mwenye bidii amefika.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
ii) Mwanafunzi mwenyewe atajieleza.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………
o) Kanusha sentensi ifuatayo bila kutumia ‘amba’. (alama 2)
Gari ambalo huendeshwa kwa kasi husababisha ajali

………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……

p) Unda nomino mbili kutokana na nomino ifuatayo. (alama 1)

i) Ulaji……………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

q) Eleza maana ya msemo ufuatao kwa kutumia katika sentensi. (alama 2)

Laila maji / mate

………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……

4.
a) Ni nini maana ya isimu jamii (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………
b) Jadili dhima ya lugha ya Kiswahili katika jamii. (alama 5)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
…………..
c) Binadamu anaweza kuwasiliana bila kutumia lugha. Eleza njia zozote tatu zaidi anazoweza kutumia
kuwasiliana (alama 3)

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 7

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

Kiswahili Karatasi Ya 2 Kidato Cha Tatu Page 8

You might also like