You are on page 1of 15

August 2016

TAFAKURI NDOTO NA FIKRA WEZESHI KITAALUMA


KWA WANAFUNZI TANZANIA.

MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP)

TSNP OFFICES AT SINZA DARAJAN-TP GROUND,


P.O.BOX 110024,
KINONDONI, DAR ES SALAAM TANZANIA.
E-mail: tsnp.students@yahoo.com.
Blog: www.wanafunzitz.blogspot.com.
Fb Page: Sauti Ya Wanafunzi Wa Tanzania.

Na: Idara ya Utafiti na Mafunzo@TSNP


TSNP Research and Training Department (R&T)
SIMU: +255762 599 672/+255659 366 125
August 2016

Utangulizi.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania ni azaki isiyo ya kiserikali, ambayo haifungamani na itikadi


ya chama chochote kile cha siasa, iliyoanzishwa na kusajiliwasajiliwa rasmi tarehe 23
Oktoba 2001[SO. NO. 42386], kwa malengo ya utetezi wa haki na wajibu wa Wanafunzi
nchini lakini vile vile kuimarisha mtandao imara wa Wanafunzi toka vyuo vikuu hadi Shule
za Misingi. Kuanzishwa kwa Mtandao huu kulitokana na kukosekana kwa umoja imara wa
kutetea haki na wajibu wa wanafunzi Tanzania.

USULI

Andiko hili la kitafiti, wezeshi kifikra, lililobeba ndoto njema za wanafunzi Tanzania, ni andiko
lililoandikwa na ndugu Abdul Nondo, Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) na Mratibu wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP-Tanzania Students
Networking Programme) Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na wajumbe wa idara ya Utafiti
na Mafunzo taifa (TSNP Research and Training Departmment)

Pamoja na changamoto tulizonazo katika Mfumo wa Elimu Tanzania ambazo kila siku
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania na wadau wa Elimu tumekuwa tukipigania, andiko hili
limetoa majawabu mengi haswa kwa kuzingatia misingi ya haki na wajibu wa Wanafunzi
Tanzania.

Andiko hili wezeshi na amshi kifikra, litawatoa Wanafunzi wengi gizani, litahuisha afya za
wanafunzi kitaaluma, litawapa dira na ndoto murua wanafunzi wa Kitanzania na vile vile
litafanya Wanafunzi wote Tanzania kujikita sana katika wajibu wao na si kusingizia
changamoto tulizonazo katika mfumo wa Elimu Tanzania kama kigezo cha kutofanya vizuri
katika masomo.

Tunashauri wadau wote wa Elimu mathalani, waalimu, wanafunzi, wazazi na Serikali ya


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Elimu. Ipitie andiko hili na kuona
namna ya kuendelea mageuzi ya Elimu Tanzania.
August 2016
MAISHA YA MWANAFUNZI YA KILA SIKU KATIKA SAFARI YAKE YA KITAALUMA

Mwanafunzi kwa kiingereza anaitwa “Student”. Ni neno linalotokana na neno “study’ au


kitendo ambacho maana yake ni “kusoma”(Verb). Hivyo basi student kwa maana ya
kawaida ni msomaji anayejifunza(Mwanafunzi).

Hivyo katika maisha yako yote wewe unayeitwa mwanafunzi, sio kwa bahati mbaya ni kwa
sababu wewe ni msomaji na ni mwanafunzi. Hivyo kama mwanafunzi unajukumu moja tu, ni
jukumu la kusoma ili uitwe “student”. Kama husomi, huna mkakati wowote wa kusoma na
kufanya vizuri wewe utakuwa umesaliti jina lako (Student).

Na hautakuwa na tofauti yoyote na mtu ambaye hasomi yupo mtaani tu au kijiweni hana
kazi yoyote. Katika maisha yako yote mwanafunzi lazima uwe na njia na taratibu zako za
msingi za kukufanya uendelee kuitwa mwanafunzi kwa sababu itafika siku hautaitwa tena
mwanafunzi na lazima uwe umefanya jambo umelivuna kutokana na uwanafunzi wako.

Hivyo basi katika maisha ya mwanafunzi ambaye anapenda kufanikiwa na kufanya vizuri
kuna mambo saba (7) ambayo anatakiwa kuwa nayo katika kutimiza safari yake ya
kitaaluma, kwani mambo hayo ni kama daraja (Bridge) ambalo huunganisha jitihada zake
na mafanikio ya jitihada hizo, kwani unaweza kuwa na jitihada lakini kama hauna mambo
haya saba (7) hauwezi kufanikiwa na kufanya vizuri katika masomo yako au mitihani yako.

1. MWANAFUNZI LAZIMA AJITAMBUE.


(AWE NA KITU KIITWACHO SELF-ESTIMATION/SELF DETERMINATION)

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza kuwa mwanafunzi lazima


ujitathmini na ujitambue kuwa wewe sasa ni mwanafuzi (Student) msomaji ambaye una
jukumu moja kubwa la kusoma na kuwa na mikakati madhubuti. Hivyo lazima ujitofautishe
na wengine ambao sio wanafunzi ili kuepuka kufanya mambo ambayo wewe kama
mwanafunzi hautakiwi kuyafanya.

 Lazima utambue kuwa wewe ni maskini hauna uwezo wowote, na wazazi wako ni
maskini ila wanajibana ili wewe usome na ufanikiwe.
 Lazima utambue kuwa kufeli kwako au kufanya kwako vibaya kwa uzembe wa
kutokusoma ni kumsaliti Mungu na wazazi wako, kwani Mungu kupitia vitabu vyake
anaamrisha tusome. Pia wazazi wanajinyima ili usome ila unafeli kwa uzembe wa
kutokusoma ni dhambi pia.
August 2016
 Lazima utambue kuwa elimu ndio ufunguo katika mafanikio. Wanafunzi wengi huwa
wakidanganyana kuwa weng wamefanikiwa bila kusoma, ni kweli hawa mara nyingi
ni wale ambao familia zao zina mnyororo wa mafanikio ambapo yeye anaweza
kurithi mali. Je, wewe kwenu kuna mali zozote? Mbali na mali zenu bado Elimu ni
muhimu zaidi ya hizo mali. Kitendo cha kuwa na elimu tu ni zaidi ya mafanikio. Mali
huja baada ya Elimu hivyo Elimu bado ni bora.
 Lazima utambue kuwa Elimu yako ni faida kwako, familia yako na taifa lako ambalo
linapambana kukusomesha na hata kukupa mkopo ukifika Elimu ya juu. Hivyo ni
lazima uwe na uchungu wa kupambana ili kufanikiwa kitaaluma.
Self-Estimation (Kujitambua) ni jambo nzuri sana kwani mwanafunzi
akijitambua ni mwanzo mzuri wa kufanya makubwa na kutimiza ndoto zake.

2. MWANAFUNZI LAZIMA AWE NA DIRA/MAONO (VISION)

Lazima mwanafunzi uwe na dira ya kujua wapi unaelekea na ufahamu nini ufanye, uwe
kama nani anayekuvutia, wapi unataka ufike kitaaluma. Je, Chuo Kikuu? Na ukifika chuo
kikuu unapenda usome nini?. Uwe mwanasheria au usome kilimo, au uwe mwalimu? Ukiwa
na haya maono, Dira kujua wapi unaelekea lazima itakufanya uwe na mikakati (Mission) ya
kutekeleza hii adhma yako, kwani dira yako itasimama kama malengo yako (Objectives).
Hivyo hivyo dira yako itakufanya kuwa na mikakati ya kutekeleza yote unayodhamiria, hivyo
dira (Vision) ni jambo la msingi uwe nalo.

3. MATUMAINI (HOPE)

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza kuwa mwanafunzi lazima awe na


matumaini makubwa ya kufanya vizuri, akiwa na matumaini ni njia kubwa sana yeye kuwa
na mipango. Amini kuwa unaweza, Jiambie mwenyewe kuwa “NAWEZA”, “YES I CAN” OR
“I CAN PASS” (Naweza kufaulu).

Hii ni tofauti kabisa na mwanafunzi ambaye anasoma lakini hana matumaini ya kufaulu.
Huyu ni rahisi sana kufeli na kufanya vibaya kwa sababu hatakuwa na mipango yoyote,
wala njia zozote (Strategies) kwa sababu hana matumaini yoyote. Yeye tayari amekata
tama kuwa hawezi kufaulu.

Hii ni kwa sababu ya tamaduni tuliyojijengea kuwa shule yangu wanafunzi huwa wanafaulu
wachache sana na ni wale wanaoongoza darasani. Wanafunzi wengi huangalia matokeo ya
August 2016
nyuma ya shule zao, halafu wanakata tama kuwa hawawezi kufaulu, na sio jambo la
kushangaza kufeli kidato cha nne ni kawaida kwa sababu wengi huwa wanafeli.

Badilika kuanzia leo, kuwa na matumaini, usiangalie mabaya yaliyoko nyuma, yaangalie
kwa njia ya kutorudia mabaya lakini si kwa njia ya kukuvunja moyo.”DON’T GIVE UP!”
Sema “I DON’T GIVE UP AGAIN!”, “I DON’T GIVE UP!” Sema “I CAN PASS”, weka ahadi
na Mungu kuwa utasoma kwa jitihada zote na utafaulu.

4. MWANAFUNZI LAZIMA AWE NA IMANI KATIKA MUNGU(FAITH)

Hii ni kwa sababu lazima tufahamu kuwa mambo yote tunayoyafanya ni lazima tumuombe
Mungu na tumuamini Mungu. Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza
kuwa Lazima mwanafunzi aishi katika imani ya kumuomba Mungu ili yote anayoyafanya
yafanikiwe. kama ni Musilamu lazima umuombe Mungu akujalie kwa yote unayoyafanya na
jitihada zako zote. Kama ni Mkristo lazima umuombe Mungu akusaidie.

Pia kumbuka Mungu tayari yeye mwenyewe anasisitiza umuhimu wa Elimu. Ukisoma
vitabu vyake tukufu vyote anasema, mfano:-

DINI YA KIISLAMU:-

 Anasema Mtume (S.a.w):


“Kutafuta Elimu ni lazima kwa kila Muislamu wa Kiume au wa kike”

Amesema Mtume (S.a.w):


“Tafuteni Elimu hata kama ikiwa China”

“Elimu haipatikani kwa kurithi kwa baba na mama, wala haipatikani ndotoni.
Inapatikana kwa kutafuta usiku na mchana. (Imesemwa na Mwanazuoni).

DINI YA KIKRISTO:-

 Biblia inasema:
Mithali 4:13, “Mkamate sana Elimu usimwache aende zake, mshike maana yeye ni
uzima wako”.
August 2016
Hivyo ni wajibu wako kuamini yote anayoagiza Mungu na kama utayadharau haya utakuwa
umemkosea Mungu, na kama hautafanya jitihada basi utapata dhambi kwa sababu utakuwa
unakaidi aagizayo Mungu hivyo ni njia moja ya kwenda motoni.

Na ukiacha kusoma na kutokuwa na jitihada yoyote Mungu anaweza kukupa adhabu ya


kuwa na maisha magumu kwa sababu umeyadharau maagizo yake, hivyo maisha yako
yatakuwa magumu kwa sababu ya kupuuzia maagizo ya Mungu.

Ondoa imani potofu eti ukifeli Mungu ndio kapanga, sio kweli na haina ukweli. Mungu
ameagiza tusome na kufaulu, tufanikiwe. Mungu hapendi kuona wewe unaangamia, hivyo
kuanzia leo timiza hili agizo la Mungu.

5. MWANAFUNZI LAZIMA AWE NA HESHIMA NA NIDHAMU (RESPECT AND


DISCIPLINE)

Mwanafunzi bora ni Yule ambaye ana heshima na nidhamu, nidhamu hii ianze kwa
wazazi, walimu, na hata wanafunzi wenzako. Nidhamu huambatana na Baraka juu ya
mafanikio yako

Tuzungumzie nidhamu kwa Walimu. Mwalimu siku zote anapenda mwanafunzi


mwenye nidhamu na heshima. Hii inamfanya mwalimu akupe maarifa yake kwa namna
yoyote, na hii itamfanya mwalimu apende kuona unafahulu vizuri.

Pia heshima na nidhamu kwa wanafunzi wenzako. Wanafunzi mkishindwa


kuheshimiana, mtadharauliana na matokeo yake itaathiri umoja wenu na ushirikiano
pamoja na taaluma yenu.

Epuka maneno kama:-

 SIwezi kufundishwa au kuelekezwa na wewe.


 Siwezi kufanya majadiliano ya kimasomo (Discussion) na wewe.
 Simpendi yule mwalimu, anapenda sifa.

Heshima ni nyenzo ya Msingi sana.

6. UPENDO NA USHIRIKIANO (LOVE AND COOPERATION)


August 2016
Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza kuwa mwanafunzi awe na
upendo na ushirikiano na wanafunzi wenzake. Miongoni mwenu mkiwa na upendo na
ushirikiao mtafahulu karibu wote kwa sababu mtakuwa mkifundishana, mkiazimana
vitabu na vifaa vingine vya masomo (Academic materials), na kushirikiana kufanya
majadiliano ya kimasomo kwa pamoja (Group discussion). Yote haya hamuwezi kufanya
kama hamna Upendo na ushirikiano.

Epuka kusema:-

 Simpendi yule Joseph.


 Ananiudhi, anajiona.
 Simpendi yule mwalimu.
 Siwezi kumuazimisha vitabu vyangu.
 Kila Mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

7. MWANAFUNZI LAZIMA AWE NA UVUMILIVU (TOLERANCE, ENDURANCE,2


PERSEVERANCE, PATIENCE).

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza, mwanafunzi bora ni yule


mwenye uvumilivu, kwani katika safari ya kitaaluma kuna changamoto nyingi zinazohitaji
uvumilivu.

Hivyo Mwanafunzi lazima awe mvumilivu (Patient, endurable, tolerant), asiwe mwepesi
kukata tamaa pale anapokumbana na changamoto. Mfano, Wazazi hawana ada
unapata mawazo ya kuacha shule, hapana lazima uwe mvumilivu, usiwe na mawazo ya
kushindwa jambo Fulani kutokana na changamoto.

Huna fedha ya kusoma masomo ya ziada (Tuition) unakata tama, huna fedha ya kula
shule unakata tama, unapata alama kidogo unakata tama, hapana pambana. Shida
unazozipata leo ni furaha na faraja ya kesho ila raha uzipatazo leo ni shida na maumivu
ya kesho.

 Ukiwa hausomi unalala tu, unakaa kijiweni, unakwenda disko, unashinda na boda
boda, unaona faraja kuwa na wasichana wengi, unaona faraja kudhurula tambua
hiyo ni dalili kubwa ya shida na matatizo ya kesho (ELEWA HIVYO). Hivyo vumilia
shida zote leo ili kesho uepukane nazo.
August 2016
Hayo juu ni mambo ambayo Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza
kuwa mwanafunzi awe nayo katika maisha yake yote ya kitaaluma.

Lakini hayo hayatoshi bila mwanafunzi mwenyewe kutimiza wajibu wake kama ambavyo
TSNP inaendelea kueleza.

Pia Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unapendekeza na kuwaomba wanafunzi


wote Tanzania kufuata na kutumia njia hizi katika kutimiza majukumu yao kama
wanafunzi.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unafahamu changamoto zinazoikumba hali ya


Elimu Tanzania. Kwa mfano, uhaba wa walimu, uhaba wa vitabu, lakini Mtandao wa
wanafunzi Tanzania TSNP unapendekeza kuwa mwanafunzi atimize majukumu yake
kwanza mbali na changamoto hizi kwani changamoto hizi zipo katika shule nyingi
Tanzania.

Tumegundua kuwa wanafunzi wengi hukimbia majukumu kwa kisingizio cha


changamoto hizi. Mfano, uhaba wa walimu na vitabu, ila mwanafunzi lazima aoneshe
jitihada zake kwa asilimia zote (100%) na kujivika majukumu kama mwanafunzi.

MAJUKUMU YA MWANAFUNZI

(STUDENT’S RESPONSIBILITY)

NJIA BORA YA MWANAFUNZI YA KUJISOMEA NA KUFAHULU KWA URAHISI

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP unawaomba wanafunzi wote kuzifuata njia hizi,
kuzitii, kuzitekeleza na kuziheshimu.

1. TENGENEZA RATIBA YAKO.


Tengeneza ratiba ambayo itatoa muda na masomo ambayo utasoma kila siku kwa
wiki.
Mara nyingi wanafunzi wengi ratiba zao zinakuwa fixed kwa muda wa kuanza na
kusihia, hii sio nzuri sana. Tengeneza ratiba ambayo itakuwa na muda wa kuanza,
August 2016
kumaliza ni hadi pale utakapochoka. Pale ambapo utajisikia kupumzika, pumzika
kama ni mchana pia usiku uwe na muda wa kuanza hakikisha unasoma kwa muda
unaoweza, lakini hakikisha unapata masaa 7 au 6 ya kulala usiku mfano, Saa 4
usiku hadi Saa 6, au Saa 7 usiku halafu pumzika.
HESHIMU RATIBA YAKO, USIISALITI RATIBA YAKO, IFUATE RATIBA YAKO!

2. MUDA WA KUPUMZIKA
Mwanafunzi lazima atenge muda wa kupumzika mchana ili kufanya ubongo na akili
yake kuwa imara (Active). Mfano, unarudi kutoka shule, unakula, unaoga kisha
unalala angalau Saa moja na nusu, halafu ukiamka unaweza amua ku relax,
kutembea tembea kidogo au kwenda mazoezini, ukirudi jioni unaweza kula usiku
halafu ukaendelea na ratiba yako ya kujisomea usiku muda wowote ambao
umepanga mwenyewe.

3. PATA MUDA WA KU RELAX


Pata muda wa ku relax wa kufanya mambo ambayo ni tofauti na mambo ya
kitaaluma angalau nusu saa au saa moja mfano, kucheza Mpira, kuangalia movie au
kutembea tembea. Usifanye jambo ambalo litafanya akili na muda wako wote
kuegemea huko. Wanafunzi wengi hukosea, wakirudi nyumbani muda wote uliobaki
wanatumia kufanya mambo yao ambayo hayana faida kitaaluma mfano, boda boda
kijiweni, kushinda katika mabanda ya video, kuchati facebook na whatsapp
(Mitandao ya kijamii) hii hautofahulu kwa namna yoyote, lazima ubadilike.

4. KUFANYA MAZOEZI
Pata muda wa kufanya mazoezi hata kwa nusu saa au saa moja, hii itakusaidia
kuwa imara (Active) na kuzidisha kumbukumbu. Hakuna dawa ya akili au ya
kuongeza kumbukumbu bali ni kutekeleza haya kwa moyo wote kama ambavyo
TSNP inavyowashauri.
August 2016

5. PATA MUDA WA KUFANYA DISKASHENI.


Pata muda wa kufanya majadiliano ya kimasomo katika vikundi (Discussion) na
wanafunzi wenzako, hii itakusaidia kufahamu mambo mengi na kujua maswali
ambayo ni magumu. Ni vizuri sana kuwa na kikundi cha kujisomea yaani group
discussion hii itakufanya uwe imara.

6. KUFANYA MITIHANI MINGI ILIYOPITA (PAST PAPERS)


Mtandao wa wanafunzi TSNP unapendekeza wanafunzi katika kusoma kwao wawe
wanajipima mitihani iliyopita kwa sababau maswali huwa yanajirudia, pia itawafanya
wawe na uwezo wa kujua kutegua (Tackle) maswali magumu.
Pia mwnafunzi anatakiwa kujipima maswali au kupeana maswali na kujitengea muda
wa kumaliza. Hii itasaidia spidi ya uandishi. Mfano, unajipa dakika 25 swali la “essay”
au dakika 20.

7. KUSOMA KATIKA SEHEMU TULIVU


Mwanafunzi anapaswa kusoma katika sehemu tulivu, epuka vitu ambavyo vinaweza
kukufanya kutokuwa makini na unachosoma. Mfano, kusoma huku unachati, kusoma
huku unaona TV, kusoma huku unasikia redio, ingawaje wengine hupenda ni vizuri
lakini hakikisha kuwa unakielewa unachokisoma.

8. KUFUNDISHA WENGINE
Pia TSNP unamuomba na kumshauri mwanafunzi apende pia kuwafundisha
wenzake, hii kwanza itamfanya awe na mahusiano mazuri na wenzake, pili
itamfanya aweze kukumbuka kwa urahisi anachokisoma.

9. KUEPUKA MAKUNDI YASIYO NA UTARATIBU KAMA WAKO


August 2016
Epuka makundi ambayo hayana utaratibu kama wako. TSNP inakushauri wanafunzi
kuepuka makundi yote ya marafiki ambao hawana utaratibu kama wako. Mfano,
makundi ambayo hayapendi kusoma au hayapendi mambo yoyote ya kitaaluma,
yaepuke hayo makundi kabisa.

Makundi yanayopenda disco, club, kukaa vijiweni, makundi ambayo yanapenda


sana wasichana na vishawishi vingine, makundi haya yatakufanya usitimize malengo
yako kwani kati yao utajiona upo tofauti nao hivyo ni rahisi wenyewe kukubadilisha
wewe, hivyo ni vizuri kuwa mbali na makundi hayo.
Epuka mahusiano ya kimapenzi ambayo hayana faida. Mapenzi sio kufanya ngono
tu (Sex), mapenzi yana maana kubwa. Kama unampenzi asiyependa kusoma
muepuke kwani atakufanya na wewe ufanye vibaya.

Mpenzi bora ni yule anayeshirikiana na wewe katika maswala yote ya kitaaluma na


mnaishi kwa malengo. Ukiona mapenzi kwako ni maumivu tu kila wakati achana
nayo, jikite katika masomo. Panga mipango yako kwani bado unasafari ndefu,
mapenzi yapo tu, wanaume na wasichana wapo kila sehemu, wewe jikite katika
masomo yako ili ufanye vizuri. Achana na ushawishi usio na maana.

Achana na maneno:-
 Sisomi kwa sababu yako.
 Nafeli kwa sababu yako.
 Unanifanya niwe na mawazo.
Achana na hizi sentensi.

Haya yote ni majukumu ambayo mwanafunzi anapaswa kuyatimiza mbali na walimu. Uhaba
wa walimu na vitabu hizi ni changamoto ambazo zipo tu. Hivyo mwanafunzi katika
kutekeleza haya anapaswa awe “committed” awe amejidhatiti kufanya yote haya. Sasa hivi
kuna notes kila mahali, mitandao ipo, tutumie simu zetu kwa faida. Mfano, “THL” ni progam
ipo playstore unaweza kuidownload halafu unakuta notes za kila somo, na maswali yote
unayoyahitaji.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania TSNP umejidhatiti kwa nguvu kuinua ufahulu wa


wanafunzi Tanzania hasa kidato cha nne kwa njia tofauti tofauti.
August 2016

NJIA BORA YA KUJISOMEA MWENYEWE (INDIVIDUAL STUDY/ READING)

AU (Reading Strategies)

Mtandao wa wanafunzi Tanzania TSNP umefanya uchunguzi na utafiti kupitia idara yake ya
mafunzo na tafiti (Research development and training department) na kuweza kugundua
njia bora za usomaji ili kufahulu mitihani na masomo kwa mwanafunzi.

Mwanafunzi anatakiwa kusoma kwa lengo la kujifunza na kuelewa (Learnig goals) epuka
kukariri. Kariri panapohitajika ila penda kusoma kwa lengo la kuelewa.

Mara nyingi wengi wanapenda kusoma kipindi cha mitihani au kipindi cha jaribio (test) hii
njia inaitwa “performance goal”. Anapenda kusoma kwa ajili tu ajibu mtihani kwa muda ule,
hii ni hatari sana kwani si rahisi mwnafunzi kufanya vizuri kupitia njia hii, kusoma ni kila siku
na sio kipindi cha mitihani tu.

Mwanafalsafa Nolen na Nicholas wanapendekeza tena njia ya kusoma kwa ushirikiano na


wenzako, njia hii inaitwa “social collaboration.”

Kusoma kwa makundi (reading in groups). Hii itasaidia katika kuelewa vitu au mambo
magumu kwa sababu mtakuwa mkichangia mawazo. Anayependa kujifungia chumbai na
kujisomea peke yake kila siku huwa hafanyi vizuri siku zote, ni vizuri pia kusoma na
wenzako. Lakini pia tenga muda wa kusoma peke yako (Individual learning).

KUJISOMEA MWENYEWE

(Individual reading)

Mtandao wa wanafunzi Tanzania unashauri wote kuwa njia bora ya kusoma ni ile inayoitwa
kusoma kwa UMAKINI. Yaani “INTENSIVE READING”. Hii ndiyo njia bora kwani
mwanafunzi lazima asome kwa uangalifu na kwa kuelewa ili aweze kukumbuka.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania(Tanzania Students Networking programme) kupitia idara


yake ya tafiti na mafunzo imetafiti na kugundua kuwa wanafunzi wengi husoma masomo
August 2016
yao kama gazeti, anaperuzi tu. Hii njia ya kuperuzi inaitwa “skimming.” Hii njia haifai hata
kidogo kwa sababu sio maalumu kwa wanafunzi na wala haimfanyi mwanafunzi aelewe na
ndio maana mwanafunzi anaweza kusoma lakini akajikuta hajaelewa choxhote ni kwa
sababu anatumia njia hii ya skimming ya kusoma kama gazeti.

 Njia bora ya kusoma initwa intensive reading. Kusoma kwa umakini, kusoma neno
kwa neno, herufi kwa herufi.

Hii INTENSIVE READING lazima iwe na vitu vifuatavyo.

SQ3R ( SQ TRIPPLE R)

I. Survey
II. Question
III. Read
IV. Recall
V. Review

Ili kutumia INTENSIVE READING, lazima mwanafunzi atumie njia hizo tano za SQ3R.

I. TAFITI (SURVEY)
Hapa mwanafunzi achunguze ajue kidato alichopo masomo yako yana topiki zipi,
mfano yupo kidato cha 3 lazima ujue history kidato cha tatu kuna topiki ngapi,
Kiswahili kina topic ngapi, Physics ina topiki ngapi baada ya kufahamu ni topiki
ngapi unapaswa uzisome. Hii itakuwa ni hatua nzuri kwako, kujua nini kifanyike,
wanafunzi wengi wanasoma bila kufahamu, wala hataki ku-survey kujua kuna
“topiki” ngapi hawajui, mwanafunzi wa namna hii ni vigumu na sio rahisi kufahulu.

II. MASWALI (QUESTIONS)


Baada ya kujua katika masomo yako kuna topiki zipi chukua topiki moja mfano,
Nationalism, jiulize swali what is Nationalism? What is nationalism about?
Can I explain Nationalism to others? Kama ukishindwa kujibu haya maswali
katika topiki Fulani ya somo lako nenda katika hatua ya tatu.

III. KUSOMA(READING)
August 2016
Baaada ya kufahamu kuwa huwezi kujibu maswali yoyote kutoka topic flani kazi
iliyobaki ni kusoma hiyo topiki au kutafuta mtu akuelekeze yote ili uelewe. Ni
vizuri katika kusoma uwe unasummarize pembeni hii inasaidia kukumbuka vizuri
unachokisoma.

IV. KUKUMBUKA (KUKUMBUKA/KUJIKUMBUSHA)


Baada ya kusoma anza kujikumbusha kwa kuandika pembeni kuanzia
ulipoanzia hadi ulipoishia kwa muda huo.
Anza kujiuliza maswali. Mfano, Can I explain Nationalism? Can I define it?
Andika uliyoyasoma na kuyaelewa pembeni kwa maneno yako (Paraphrase)
endelea hivyo hivyo. Soma (Read), jikumbushe (Recall) na andika kwa maneno
yako baada ya kuelewa (Paraphrase).

V. KUPITIA TENA (REVIEW)


Baada ya kumaliza topiki ya colonialism nenda kachukue maswali ya topiki hiyo,
hasa maswali yaliyopita au ya shule za jirani jipime.

TUNAKUTAKIA UTEKELEZAJI MWEMA WA YOTE ULIYOYASOMA NA KUJIFUNZA.

USIKATE TAMAA, AMINI KUWA UNAWEZA!

UFAULU UPO MIKONONI MWAKO

AHSANTE!
August 2016

IMEANDALIWA NA: - ABDUL OMARY NONDO (MRATIBU WA MTANDAO WA


WANAFUNZI TANZANIA(TSNP) MKOA WA KIGOMA KWA USHIRIKIANO WA IDARA YA
UTAFITI NA MAFUNZO (RESEACH &TRAINING DEPARTMENT@TSNP)

You might also like