You are on page 1of 2

WAKISO MUSLIM S.

S TAASIS YA VIONGOZI

Kama wahenga wasemavyo “pole pole ndio mwendo”, Wakiso Muslim ilianza pole pole na sasa
imepanda ngazi. Wakiso muslim ni taasis ya msingi kwa viongozi wa nchi yetu Uganda kwa siku
zijazo. Shuleni hii wanafunzi hupewa Nafasi ya kuomba kuwa viongozi wa wanafunzi wenzao il
kudumisha shule na kuwatayarisha wanafunzi kwa maisha yao ya siku zijazo yawe taratibu. Kwa
niaba ya mkuu wa tume ya shule ya uchaguzi bwana Onyango Patrick na walimu wengine
wanafunzi katika Shule ya Upuli ya Kiislamu Wakiso hupewa mafunzo ya uongozi ili kutayarisha
maisha yao ya kesho.

Viongozi wa wanafunzi huhaguliwa kupitia nadharia ya kidemokrasia. Mwanafunzi akipata


nafasi ya kuongoza wenzake bila shaka huasiliwa vizuri kwauongozi bora. Baada ya muhula wa
uongozi, viongozi hawa huachilia uongozi kwa amani ili kupigana dhidi ya upambaji. Wanafunzi
katika Wakiso Muslim hufunzwa jinsi ya kushirikiana na wengine. Jambi hili huwawezesha
wanafunzi hawa kuwa na maisha bora katika siku zao zijazo.

Wakiso Muslim ni shule la kupendeza sana kwamba kila mwanafunzi shuleni hufunzwa jinsi ya
kudumisha sheria na maadili kuelekea kufikia maono na matarajio ya shule. Jambo hili
linawawezesha wanafunzi kuwa na tabia bora. Mara nyingi hufanya hivi kupitia mihubiri ya dini,
makao ya ushauri na mwongozo, na kwa makao ya ujumla ya shule.

Mwalimu mkuu Hajjat Amina Nakiganda husaidia sana wanafunzi katika shule ya upili Wakiso
Muslim kupitia ushauri na mwongozo wa kila makao ya ujumla ya shule. Jambo hili
limewawezesha wanafunzi kuwa wazuri kitabia. Wanafunzi kwa muda kadhaa hupewa Nafasi
ya kuhotubia wenzao kama njia ya kuwaandaa wanafunzi na ujuzi wa mawasiliano. Jambo hili
pia limeongeza tofali kwenye msingi wa uongozi wa wanafunzi katika shule ya upili ya kiislamu
Wakiso.

Wanafunzi katika shule hili hupewa nafasi ya kujiendeleza kimawasiliano hasa hasa wakati wa
mijadala inayoandaliwa na walimu. Kila Jumamosi wanafunzi huwa mijadaloni mbalimbali.
Jambo ambalo limewafanya kusimama imara wakiwa mbele ya watu shuleni na baada ya
kumaliza shule.

Wakiso muslim ni shule ya kibinafsi kwa msingi na walimu wanafanya iwezekanavyo kuona
kwamba wanafunzi wawe viongozi bora wa kesho. Mara nyingi walimu wa vijidarasa hupewa
kazi ya kuzungumza na wanafunzi wa vijidarasa hivyo kuona kwamba wanafauru kimaisha.

Kama wahenga husema “mwamini Mungu si mtovu” katika shule ya upili Wakiso Muslim kuna
sheikh wanaofundisha wanafunzi dini ili kuwaendeleza wanafunzi kwenye msingi wa dini
uliyobora zaidi. Kila siku wanahakikisha kwamba wanafunzi waislamu hufanya ibada kama vile
kuswali na kufunga ili kuwaweka kwenye njia iliyo sahihi.
Prepared by,

Mwalimu Akandwanaho Fagil

Mkuu wa Idara ya Kiswahili

You might also like