You are on page 1of 1

Sera ya Fursa Sawa

Quwwat-ul-Islam Girls’ School imechukua wajibu wa kuhamasisha ufahamu wa kanuni na


utendaji wa usawa na haki.

Malengo
Lengo letu ni kuwajaza wanafunzi ufahamu wa jamii yetu anauwai na kutambua thamani ya
utofauti. Hayo yatafikiwa kwa kushikamana na kanuni zifuatazo:
• - Ubaguzi juu ya misingi ya rangi, utamaduni. Asili, jinsia au uwezi haukubaliki

• - Lengo kuu la shule ni kuelimisha, kuwakuza na kuwatayarisha wanafunzi wote kwa ajili
ya maisha, pasi na kujali rangi zao, asili au tamaduni

• - Wanafunzi na walimu watalipeleka mbele zaidi lengo hili kwa kuchangia katika
mazingira mazuri na yenye kujali kwa kuheshimiana kila mmoja.

Kusimamia Usawa na Utendaji


Kupokelewa – Shule hairuhusu mbari, rangi au dini kutumika kama sifa ya kupokea wanafunzi.
Usajili – Majina ya wanafunzi yataandikishwa kwa usahihi na kutamkwa vyema. Wanafunzi
watahamasishwa kuyakubali na kuyaheshimu majina ya tamaduni zingine.
Ubaguzi – Ubaguzi wa aina yoyote kutoka kwa mtu yeyote aliye katika majukumu ya shule
utashughulikiwa ipasavyo kwa kuwa mwenendo huo haukubaliki. Alama za kimbari, tepe na
alama katika nguo na vifaa zimekatazwa shuleni. Wafanyakazi wanapaswa watambue
uwezekano wa dhana za kitamaduni na baguzi zilizo katika tabia zao. Katika miadi yote ya
wafanyakazi mtaradhia bora atateuliwa kwa kuzingatia vigezo kamili vya kitaaluma. Wazazi
wanapaswa watambue wajibu wa shule katika fursa sawa.
Lugha – Shule inauangalia uanuwai wa kilugha kwa mtazamo chanya. Wanafuzni na
wafanyakazi lazima wajisikie kuwa lugha zao za asili zinathaminiwa.
Nyenzo – Lengo la shule ni kuwapa wanafunzi wote kulingana na mahitahi yao, bila ya
kuzingatia asili ya kimbari, kabila au dini.
Usawa wa fursa umeenea katika mtalaa wote na utakuwa unafanyiwa mapitio mara kwa mara.

You might also like