Mchungaji wa mtaa, Wazee wa kanisa, Viongozi wa Vijana Makanisani na Kanda.
YAH: REFRESHER COURSE KWA MASTERGUIDE NA SYL.
Nawasalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Union Ya Kusini Mwa Tanzania imeandaa Refresher Course (Mafunzo maalum) kwa ajili ya Masterguide na SYL itakayofanyika Mlali-Dodoma tarehe 8-15/12/2024. Mafunzo haya yatafanyikia nje ya nyumba, hivyo wahusika wajiandae kwa ukambikaji (Mahema na Chakula). Wajumbe/Wahusika wa mafunzo haya ni wachungaji wa mitaa, Chaplain wote (Vyuo na shule),wazee wa makanisa wanaolea idara ya vijana, Wadhamini wa vijana wakubwa, Masterguide wote waliohitimu (wakiwemo wale waliohitimu zamani na huenda walishapoteza vyeti vyao), Masteguide & SYL wote mafunzoni (wanaotazamia kuhitimishwa 2024, walioanza na wanaotarajia kuanza mafunzo), Kupitia refresher course hii, tutatengeneza tanzi data (DATABASE) ya STU kujua idadi ya Masterguide na SYL wote waliohitimu. Hivyo ni muhimu kwa Masterguide na SYL waliohitimu kufika ili kutambulika na kuingizwa kwenye mfumo huo. Pia tutazindua rasmi kozi mpya ya Club Ministries Training (CMT) ambayo ni mpya kabisa kwa Masterguide na SYL, sambamba na uzinduzi wa kadi jipya la Masterguide. Wajumbe watapaswa kulipa shilingi elfu ishirini na tano tu (25,000) kwa ajili ya kiingilio na bima. Mwisho wa kutoa kiingilio na bima ni tarehe 05/10/2025. Kiingilio kilipwe kupitia akaunti ya Konferensi (21210032030 – SDA COLLECTION ACCOUNT – NMB). Eneo la kukambika liko Km 35 toka PANDA MBILI, njia ya kuelekea Mlali kutokea barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Dodoma. Maelekezo mengine tutazidi kuwajulisha kwa kadri inavyowezekana.
Taarifa Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Rukwa Kwa Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu-Tamisemi-Mhe - Aggrey Mwanri (MB) Katika Ziara Yake Mkoani Rukwa Tarehe 07 - 15 January 2013.