Professional Documents
Culture Documents
1.5 Eneo la kipaumbele lipendekezwalo: Kutoa elimu kwa wanavikundi na Kuboresha vitalu
vya kuoteshea miche kwa kununua vitendea kazi.
1
mpaka kufikia hatua ya kupandwa pamoja na mafunzo ya uhifadhi misitu na mazingira kwa
ujumla. Pia kununua baadhi ya vitendea kazi vya bustani.
1.8 Aina ya uwezeshwaji unaoombwa: Gharama za semina kama usafiri kwa wanasemina na
wawezeshaji, chakula na chai, malazi na kununua vitendea kazi vya bustani za miche.
(i) Kutoa elimu na uelewa wa uoteshaji, utunzaji miti na mazingira kwa ujumla kwa jamii
katika maeneo yatakayopandwa miti.
(iii) Kutoa hamasa ya matumizi endelevu ya misitu na mazao yatokanayo na misitu kama
vile kufuga nyuki.
(iv) Kuongeza mazao yatokanayo na misitu kwa ajili ya kunyanyua kipato kwa jamii.
2
1.11 Matokeo yanayotarajiwa kutoka kwenye Mradi
(i) Kurudisha uoto wa asili uliokuwepo siku na miaka ya nyuma na kuboresha upatikaji wa
mazao ya misitu, nishati,mvua na maji.
(ii) Kuongeza kipato kwa wanajamii wa Singida Vijijini kupitia mazao ya misitu, ufugaji
wa nyuki lakini pia shughuli za kilimo na ufugaji zitaboreka zaidi.
(iii) Kuweka mfumo endelevu wa wanajamii wote wa Singida wa kutunza mazingira kupitia
vikundi mbalimbali kama shule, SACCOS, vijana, akina mama n.k.
(iv) Kuimarika kwa afya na kuondoa maradhi ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuimarika
kwa mazingira.
Wanavikundi 2848 watanufaika moja kwa moja kwa kupata elimu ya uoteshaji na
utunzaji wa bustani za miti.
Wanufaikaji wasio wa moja kwa moja, hawa ni wananchi wa Wilaya ambao ndiyo
watakuwa wapandaji wa miti na watanufaika kwa kuimarika kwa misitu na mazingira.
Mradi huu utaongeza upatikanaji wa maisha bora kwa wananchi wote kwa uboreshaji wa
mazingira na misitu ambao utaongeza ubora wa maisha.
Kuongeza vizuizi vya upepo ambavyo kwa namna nyingine vitapunguza mmomonyoko
wa udongo na uharibifu wa mazao.
3
Kuboresha maisha/kipato cha wanajamii kwa kuuza matunda kama machungwa, maembe
pamoja na mazao mengine ya misitu kwa mfano asali.
2. Ridhaa
(a). Mapendekezo ya Mkuu wa Taasisi zinazo/inayoomba
Maoni: Mradi wa upandaji miti kwa Wilaya ya Singida umeanza tangu 2015. Hata hivyo mradi
bado unahitaji uwezashwaji wa ruzuku ili kutawezesha kufanikisha malengo na azma ya
kuboresha mazingira na misitu kwa ufanisi zaidi.
4
Maoni:____________________________________________
Jina : __________________________ Muhuri: _________________
Saini:___________________Tarehe:______________________
5
3.2 Utangulizi
Mradi wa uoteshaji na upandaji miti chini ya asasi ya WAENDELEE ni mradi endelevu ambao
utafanyika kwa muda usiopungua miaka kumi. Mpango wa asasi ni kufikia uwezo wa kuotesha
na kupanda miti 1, 500,000 kila mwaka. Kwa msimu wa kwanza wa mradi (2015/2016) asasi
imefanikiwa kupanda miti 160,000 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya kwa kushirikiana na
vikundi/vitalu 13 vilivyoanzishwa wilayani. Kwa msimu wa pili wa mradi (2016/2017) asasi
imefanikiwa kuongeza vikundi/vitalu hadi kufikia 48 ambavyo vinataratajiwa kuotesha miti 1,
300,000
Mradi wa kuotesha na kupanda miti ulianza Agosti 2015 mara tu baada ya taasisi ya
WAENDELEE kuanzishwa na kusajiliwa. Katika kuongeza ufanisi taasisi ya WAENDELEE
kwa sasa inatilia mkazo suala la kuipatia jamii elimu kwa kupitia vikundi na wadau
mbalimbali kwani suala la elimu ni la muhimu na ndio msingi katika kufanikisha malengo ya
mradi huu.
Mradi wa kuotesha na kupanda miti ni endelevu na lengo kuu ni kuifanya Wilaya ya Singida
kuwa ya kijani
6
3.4 Mbinu za kutekeleza mradi
Zifuatazo ni mbinu za kutekeleza Mradi.
Kuwapatia viongozi wa vikundi Mafunzo juu ya usimamizi wa vikundi
vinavyojishughulisha na upandaji wa miti na namna ya kutekeleza sheria ndogo ndogo
za misitu na mazingira.
Kuwashirikisha viongozi wa Kata zote za wilaya ya Singida pamoja na wataalamu wa
misitu Wilaya juu ya utekelezaji wa mradi ili kuweza kupata michango mbali mbali
kutoka kwao.
Kuimarisha ushiriki wa vikundi vyote vinavyojihusisha na shughuli za upandaji miti.
Kushirikiana na uongozi wa vijiji kwa ajili ya kuandaa mpango wa usimamizi wa
Misitu pamoja na sheria ndogo ndogo za Misitu.
7
3.6 Mpango wa Uperembaji na Tathmini
Asasi ya WAENDELEE itafanya usimamizi na ufutiliaji wa karinbu katika kipindi chote cha
mradi. Ufutiliaji utajumuisha usimamizi sahihi wa fedha ili kufikia lengo la mradi. Tathmini
ya mradi itafanyika kwa parameta halisi na kulinganishwa ili kupata uwiano sahihi wa
mabadiliko yaliyotokana na utekelezaji wa mradi. Mabadiliko hayo yatapimwa kwa
kulinganisha parameta mbalimbali kabla na baada ya mradi kama vile ongezeko la miche
bora, uelewa wa wanavikundi kuhusu elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira n.k.
8
Kielelezo cha bajeti ya ruzuku ya kati
Kipengele/Shughuli Kizio Kiasi Gharama ya Jumla ya gharama
kizio sh. Sh.
Mafunzo ya kuotesha na kukuza miche
kwa siku tatu
Nauli ya kwenda na kurudi mtu 96 14,000 1,344,000
Malazi kwa siku tatu mtu 96 21,000 2,016,000
Chakula kwa siku tatu-chai, chakula cha mtu 96 24,375 2,340,000
mchana na usiku
Gharama ya ukumbi wa mafunzo kwa ukum 1 300,000 300,000
siku tatu bi
Gharama ya wakufuzi wa semina kwa mtu 4 450,000 1,800,000
siku tatu
Gharama ya zana za kufundishia-kalamu kala 100 500 50,000
mu
Gharama ya ya zana za kufundishia- Dafta 100 1,500 150,000
madaftari ri
Jumla ndogo ya 40% ya awamu ya mwanzo ya mradi 8,000,000
Gharama ya vifaa/vitendea kazi kwa
vikundi 48 vinavyotarajia kuotesha
miche zaidi-viriba na mbegu
9
Gharama ya kufuata mbegu mtu 1 54,000 54,000
Dodoma(kwenda na kurudi,chakula na
malazi ya siku moja)
Jumla ndogo ya 30% ya awamu ya pili ya mradi 6,000,000
Gharama ya kufanya ufuatiliaji na
tathmini - kutembelea vikundi 48
wilayani kwa siku 14
Gharama ya usafiri kwa siku 14 mtu 3 420,000 1,260,000
Gharama ya chakula kwa siku 14 mtu 3 84,000 252,000
Gharama ya mawasiliano kwa siku 14 mtu 1 78,000 78,000
Posho kwa wafuatiliaji kwa siku mtu 3 1,120,000 3,360,000
14@80,000
Gharama ya kuandika ripoti ya vikundi mtu 3 150,000 450,000
48
Posho ya waandishi wa ripoti mtu 3 200,000 600,000
Jumla ndogo ya 30% ya awamu ya 6,000,000
mwisho ya mradi
JUMLA KUU 20,000,000
OMBI KUTOKA MFUKO 19,000,000
MICHANGO MINGINE
MCHANGO WA 1,000,000
MWOMBAJI
10
Mpango kazi wa mradi
Malengo SHUGHULI 7 8 9 10 11 12 1 2 3 4
MAHSUSI
Uhabarisho wa
mradi
Mafunzo ya
kuotesha,
kupanda, kutunza
miti pamoja na
kuhifadhi misitu
Kununua vifaa
vya bustani za
miche na
kukabithi kwa
vikundi
Ufutiliaji na
kufanya tathmini
ya mradi
Kuandika ripoti
ya mradi
11