You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI LA NCHI ZA UMOJA WA MASHARIKI


NA KUSINI MWA AFRIKA WA UDHIBITI UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU
(ESAAMLG).

Baraza la Mawaziri kutoka Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa


Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu The Eastern and Southern Afrika Anti
Money Laundering Group ESAAMLG, litakutana Tanzania tarehe 08 Septemba
2017, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Visiwani Zanzibar.

Aidha, mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Maafisa Waandamizi (Makatibu


Wakuu) utakaofanyika kuanzia tarehe 02 - 06 Septemba, 2017 katika ukumbi wa
Hoteli hiyo ya Zanzibar Beach Resort.

Kwa sasa Tanzania ndio Mwenyekiti wa Umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja,
baada ya kupokea Uenyekiti kutoka Jamhuri ya Zimbabwe iliyomaliza muda wake
mwezi Agosti, 2017, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. PHILIP ISDOR
MPANGO (MB), ambae pia ni Mwenyekiti President of the Council ataongoza
Mkutano huo.

1
Katika Mkutano huo, pamoja na masuala mbali mbali yatakayojadiliwa, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itatumia fursa hiyo kuwasilisha Taarifa ya hatua
iliyofikia katika utekelezaji wa Mpango wa Financial Action Task Force (FATF)
ulioasisiwa mwaka 2009.

Mpango huo ulizitaka nchi wanachama kufanya Tathmini ya utekelezaji wa maazimio


yaliyoainishwa kwenye FATF, katika maeneo mbalimbali ya Kisheria, Kisera,
Miongozo ya Kitaasisi zikiwemo Sekta za Fedha na maeneo ya ushirikiano wa
kimataifa. Lengo ni kubaini jinsi nchi wanachama zilivyojipanga katika kudhibiti
suala la Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi (Anti-money Laundering
and Combating the Financing of Terrorism).

Katika mkutano huo, mbinu na mikakati mbali mbali itakayosaidia kudhibiti


Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi itajadiliwa, hatua ambayo italeta
matokeo chanya na kuongeza kasi ya ukuaji wa Uchumi na kufikia maendeleo
tarajiwa katika Nchi yetu na nchi wanachama kwa ujumla.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi waanzilishi wa Umoja huo ulioasisiwa jijini Arusha,
mwaka 1999, Nchi nyingine ni Uganda, Kenya, Mauritius, Namibia, Sychelles
na Swaziland ambazo zilisaini makubaliano (Memorandum of Understanding - MOU).
Hatua ambayo ilisababisha Makao Makuu ya Sekretariati ya Umoja huo wenye nchi
wanachama (18) ambazo ni Angola, Botswana, Ethiopia, Kenya, Lesotho,
Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini,
Swaziland, Sychelles, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe kuwa jijini
Dar es Salaam Tanzania.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO.

You might also like