You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 026 2322761-5 Ofisi ya Bunge


Fax No. +255 026 2324218 S.L.P. 941
E-mail: info@bunge.go.tz DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


__________

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewataka Waheshimiwa Wabunge


kuchukua tahadhari juu ya usalama wao mahali popote wanapokuwa ili
kujiepusha na matukio ya kihalifu yanayotokea hapa Nchini.

Spika Ndugai ametoa tahadhari hiyo jana Bungeni Mjini Dodoma baada ya
Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha
Mkutano wa Nane wa Bunge.

Tuchukue hatua katika maisha yetu, kama mnavyosikia matukio ni mengi


katika Nchi yetu, usalama unanza na wewe kwanza halafu vyombo vya ulinzi
vinavyotulinda vinasaidia tu kidogo, tutazame nyendo zetu, alisema.

Aidha, Mheshimiwa Ndugai amewaomba Waheshimiwa Wabunge na


Watanzania wote kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa
Tundu Lissu pamoja na wale wanaomuuguza wakiwemo waheshimiwa
Wabunge.

Vilevile Meshimiwa Spika amewapangia Kamati Waheshimiwa Wabunge


wapya wanane(8) wa Chama cha Wananchi (CUF) walioapishwa katika
Mkutano huu wa Nane wa Bunge.
Wajumbe hao na Kamati zao ni Mheshimiwa Shamsia Mtamba (Kamati ya
Viwanda, Biashara na mazingira), Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed (Kamati ya
Miundombinu), Zainabu Mndolwa Amir (Kamati ya Katiba na Sheria),
Mheshimiwa Alfredina kahigi (Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa), Rehema
Migila, Sonia Jumaa Magogo na Nuru Bafadhili (Kamati ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii) na Mheshimiwa Kiza Hussen Mayeye (Kamati ya Nishati na
Madini).

Mapema akiahirisa Bunge Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa pamoja


na mambo mengine amezungumzia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa
Mwaka wa Fedha 2017/18 unaridhisha na kwamba Serikali itaongeza jitahada
za kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki.

Amesema katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Agosti mwaka huu, Serikali
imefanikiwa kukusanya Shilingi Tririoni 2.7 ambapo katika ya mapato hayo
Mamlaka ya Mapato (TRA) imekusanya Shilingi Tririoni 2.3.

Bunge limeahirishwa mpaka Novemba 7 mwaka 2017.

Imetolewana:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano


Ofisi ya Bunge
DODOMA

15 Septemba,2017.

You might also like