You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Simu: 026-2322129 Jengo la LAPF,


Nukushi: 026-2322128 Ghorofa ya Nane,
Baruapepe: km@habari.go.tz Makole Uhindini,
Tovuti: www. habari.go.tz S. L. P 25,
DODOMA.
40481.
TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe


ametuma salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa mwandishi wa habari nguli
na Mkuu wa Wilaya za Handeni na Morogoro, Ndugu Muhingo Rweyemamu,
kilichotokea jana tarehe 2 Septemba, 2017.

Waziri Mwakyembe ameeleza kupokea kwa mshituko na masikitiko taarifa za


kifo cha Muhingo ambaye mwezi Juni mwaka huu alikwenda kumjulia hali
hospitali ya AgaKhan alipokuwa amelazwa na kuonyesha dalili za matumaini.

"Kifo chake ni pigo kubwa kwa wanatasnia na wadau wa habari wote na


wananchi aliowahi kuwaongoza katika uhai wake, naiombea familia ya
marehemu, ndugu na marafiki waweze kupita kipindi hiki kigumu na Mungu
awape nguvu na ujasiri", amesema Dkt. Mwakyembe.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na:

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
03/09/2017.

You might also like