You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MKUU WA WILAYA IKUNGI-SINGIDA

Simu: 2502170/2502089/2502249 IKUNGI,


Nukushi: 2502078 S.L.P 94,
Tovuti: www.tanzania.go.tz SINGIDA.

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU KUKAMATWA WAFUASI WA CHADEMA IKUNGI

Septemba 9, 2017:

Kumekuwa na taarifa potofu katika mitandao ya kijamii kuwa wafuasi 11 wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Ikungi walikamatwa kwa kosa la kuendesha
michango kwa ajili ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa
risasi na watu wasiojulikana.

Ukweli ni kwamba taarifa hizi ni potofu na zenye lengo la kuwafitinisha wana Ikungi na
jimbo la Singida Mashariki kwa ujumla. Viongozi waliokamatwa na ambao baadaye
walihojiwa na kuachiwa kwa dhamana hawakuwa wakiratibu michango yoyote bali
walikutwa wakiandika mabango yenye uchochezi dhidi ya viongozi wa Serikali na wakitaka
kuandamana bila kibali.

Wakati Mhe Lissu anaendelea kupatiwa matibabu nje ya nchi na Serikali ikiwa inalifuatilia
jambo hili kwa karibu ili kuwachukulia hatua kali wote waliohusika, natoa rai kwa wana
Ikungi kuwa ni vyema tukaungana badala ya kuingiza siasa na mihemko katika jambo hili
kama Taifa lilivyoungana katika tatizo la Kibiti ambalo sasa limemalizika.

Aidha, kwa kuwa tayari viongozi wa kitaifa wa Chadema wameshatangaza utaratibu wa


kuchangia, nawashauri viongozi wa chama hicho wilaya kutumia mkondo huo. Vile vile, kwa
wadhifa wangu, nimeshamwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri yetu ya Ikungi ili aitishe
kikao cha madiwani wote kuweka utaratibu wa pamoja wa namna gani ya kuchangia
matibabu ya mbunge wetu.

Nichukue fursa hii kumpa pole Mhe. Lissu na wananchi wenzangu wa Ikungi na mahsusi
jimbo la Singida Mashariki kwa tukio hili baya. Serikali ya Wilaya inalaani vikali wote
waliohusika katika tukio hili ambalo linakwenda tofauti na mila na desturi za Kitanzania.

Tunamwombea Mhe Lissu nafuu ya haraka ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya
kuwatumikia wananchi.

Imetolewa na:

Ndugu Miraji J. Mtaturu

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

1
2

You might also like