You are on page 1of 1

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

18 Barabara ya Kivukoni, S.L.P 796, 11992 Dar es Salaam, Simu:+255 22 2122722/4


Nukushi: +255 22 2130852, Barua pepe: dg@nbs.go.tz, Tovuti www.nbs.go.tz

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


1. Hivi karibuni kumekuwa na takwimu zinazotolewa na Kampuni ya GeoPoll yenye Ofisi ya
Kanda ya Afrika Mjini, Nairobi Kenya. Takwimu hizo ambazo hutolewa kwa njia ya
mitandao ya kijamii, zinahusu ukusanyaji wa taarifa za Televisheni na Redio nchini kwa
idadi ya watazamaji na zinatolewa kila baada ya miezi mitatu.
2. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuujulisha umma kuwa takwimu hizo sio
Takwimu Rasmi (Official Statistics) kwa kuwa hukusanywa kwa mfumo ambao
hautambuliwi na NBS kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka
2015.
3. Takwimu Rasmi kama ilivyofafanuliwa katika kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ni
takwimu ambazo zimetolewa kwa kufuata Misingi ya utoaji Takwimu Rasmi (Fundamental
Principles of Official Statistics) na utolewaji wake umeratibiwa na NBS. Hivyo basi,
takwimu zinazotolewa na taasisi au mtu yeyote zitatambuliwa kuwa Takwimu Rasmi
iwapo tu zitakidhi vigezo vinavyotolewa na kusimamiwa na NBS.
4. Kwa mantiki hiyo, takwimu zinazotolewa na mtu au taasisi yoyote bila kufuata au kukidhi
vigezo vinavyotolewa na NBS kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu, hazitambuliwi kuwa ni
Takwimu Rasmi na kwa maana hiyo haziwezi kutumika katika kupanga mipango ya
maendeleo ya nchi.
5. NBS inaitaka Kampuni ya GeoPoll kufuata taratibu zilizoainishwa katika Sheria ya
Takwimu, kwa kuwa takwimu zinazotolewa na kampuni hiyo hazijakidhi vigezo vya
Takwimu Rasmi na zinapotosha umma na kuleta mkanganyiko kwa wadau pamoja na
kuathiri mahusiano ya kiutendaji baina ya vyombo vya habari hapa nchini.
Kuhusu Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya
Takwimu ya Mwaka 2015. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa,
kusimamia na kuratibu upatikanaji wa takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya Serikali na
wadau wa takwimu.
Aidha, kifungu cha 6 cha Sheria hiyo ya takwimu, kinaipa NBS jukumu la kutoa na
kusimamia Miongozo na Viwango vya utoaji wa Takwimu Rasmi.

Imetolewa na: Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dar es Salaam.

07 Agosti, 2017.

You might also like