You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Simu: 026-2322129 Jengo la LAPF,


Nukushi: 026-2322128 Ghorofa ya Nane,
Baruapepe: km@habari.go.tz Makole Uhindini,
Tovuti: www. habari.go.tz S. L. P 25,
DODOMA.

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe


ameunda Kamati ya kuchunguza ubia wa Kampuni ya StarTimes na Shirika la Utangazaji
la Taifa (TBC) kufuatia hoja mbalimbali zilizojitokeza.

Kamati hiyo iliyoundwa na Waziri Mwakyembe itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya


Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi.

Kamati hiyo itakuwa na jumla ya Wajumbe 10 watakaochunguza utendaji wa Kampuni


ya ubia ya StarTimes, ambapo watano (5) ni wa upande wa Tanzania na wengine
watano (5) ni wa kutoka Star Media China.

Wajumbe wanaounda Kamati hiyo kwa upande wa Tanzania ni kama wafuatao;-


1. Dkt. Hassan Abbasi (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo)
2. Kyando Evod (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo)
3. Frederick Ntobi (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA)
4. Eng. James Kisaka (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA)
5. Mbwilo Kitujime (Shirika la Utangazaji la Taifa-TBC)

Aidha, majina ya Wajumbe watano walioteuliwa kutoka Star Media China


yatawasilishwa kutoka China ili kukamilisha idadi kamili ya wajumbe 10 wa kamati
hiyo.

Kamati hiyo imepewa hadidu za rejea takribani nane na inatakiwa kufanya kazi kwa
muda wa siku saba ili kukamilisha kazi hiyo.

Imetolewa na:

Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
15 Julai, 2017.

You might also like