You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 026 2322761-5 Ofisi ya Bunge


Fax No. +255 026 2324218 S.L.P. 941
E-mail: info@bunge.go.tz DODOMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA MKUTANO WA


NANE WA BUNGE
__________

Mkutano wa Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho Jumanne tarehe 5


Septemba, 2017 na kumalizika tarehe 15 Septemba 2017 Mjini Dodoma.
Shughuli zilizopangwa kufanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-

1.0 KIAPO CHA UAMINIFU

Kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Waheshimiwa Wabunge saba wa


Chama cha Wananchi (CUF) walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi
karibuni. Wabunge hao wapya watakaoapishwa ni:-

i) Mhe. Alfredina Apolinary Kahigi


ii) Mhe. Kiaza Hussein Mayeye
iii) Mhe. Nuru Awadhi Bafadhili
iv) Mhe. Rukia Ahmed Kassim
v) Mhe. Shamsia Aziz Mtamba
vi) Mhe. Sonia Jumaa Magogo
vii) Mhe. Zainab Mndolwa Amir

2.0 MISWADA YA SERIKALI

Katika Mkutano huu wa Nane wa Bunge jumla ya Miswada mitatu


inatarajiwa kusomwa kwa hatua zake zote. Miswada hiyo ni :-

1

(i) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa
Mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3)
Bill, 2017)

(ii) Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017 (The Railways Bill, 2017)

(iii) Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam


wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 (The Medical, Dental and Allied
Health Professionals Bill, 2016)

3.0 MAAZIMIO.

Aidha, Katika Mkutano huu wa Bunge Maazimio matano yanatarajiwa


kuridhiwa. Maazimio hayo ni:-

i) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya


Afya ya Mimea, Usalama wa Wanyama na Chakula (The East African
Community Protocol on Sanitary and Phytonisanitary (SPS) Measures).

ii) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya


Afrika Mashariki (East African Community Protocol on Peace and
Security.

iii) Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba ya kuanzisha Kamisheni ya


Pamoja kati ya Tanzania na Malawi kuendeleza Bonde la Mto Songwe
(Convection of Establishment of Joint Songwe River Basin Commission
between Tanzania and Malawi).

iv) Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba (Intergovernmental Agreement


IGA) baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu Mradi wa Ujenzi wa bomba la
kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki. (East Africa Crude Oil
Pipeline EACOP) kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).

2

v) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Nyongeza ya Tisa ya Mwaka 2016
ya Katiba ya Umoja wa Posta Duniani.

4.0 TAARIFA YA KAMATI

Bunge pia linatarajia kupokea Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Sheria


Ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria Ndogo.

5.0 MASWALI

Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa


na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa
Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.

6.0 TAARIFA ZA KAMATI MAALUM

Katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Kumi na Moja Mheshimiwa Spika


aliunda Kamati Maalum mbili (2) kwa ajili ya kuchunguza biashara ya Madini
aina ya Tanzanite na Almasi. Kamati hizo zilizopewa siku 30 zimekamilisha kazi
hiyo na zitawasilisha taarifa zao keshokutwa tarehe 6 Septemba 2017 katika
hafla fupi itakayofanyika katika viwanja vya Bunge na kuhudhuriwa na
viongozi wa Kitaifa. Katika tukio hilo, Mhe. Spika atapokea taarifa hizo na
kuzikabidhi kwa Mhe. Waziri Mkuu. Matangazo ya hafla hiyo yatarushwa
moja kwa moja katika Channel ya Bunge.

Ratiba yote ya Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge inapatikana katika


Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.

Imetolewana:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano


Ofisi ya Bunge
DODOMA

04 Septemba, 2017.
3

You might also like