You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


IDARA YA UHAMIAJI

TAARIFA KWA UMMA


KUZINDULIWA KWA HUDUMA YA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI
MTANDAONI (ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM)

Idara ya Uhamiaji inapenda kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi


huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport
Application Form). Huduma hii inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia
link ifuatayo: https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza
kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017.

Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti


wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing)
na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma


inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale
itakapotangazwa vinginevyo.

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika


mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi
kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ambayo ni
info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao.

Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo


mbalimbali vya habari.
Imetolewa na:

KITENGO CHA UHUSIANO,


MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
04 AGOSTI, 2017.

You might also like