You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Simu ya maandishi: “ZIMAMOTO KUU” JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


Simu Nambari: +255-22-2113537 9 Barabra ya Ohio
Nukushi: + 255-22-2184569 S. L. P. 5821,
Barua Pepe: fire.rescue@frf.go.tz DAR ES SALAAM.
Tovuti : www.frr.go.tz

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia


tukio la moto kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lililotokea mnamo tarehe 09 Aprili, 2018 majira ya saa 1:28 usiku mkoani
Dodoma.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na shoti


iliyotokana na Power bank iliyokuwa inatumiwa kuchaji simu. Shoti hiyo
ilisababisha kuungua kwa simu, Power bank, sehemu ya meza na kapeti
kitendo kilicholeta moshi mkubwa na taharuki miongoni mwa Wabunge.
Ukiachilia mbali taharuki kwa Waheshimiwa Wabunge hakuna madhara kwa
binadamu yaliyotokana na moto huo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa rai kwa


Watanzania wote kuchukua tahadhari kubwa hasa wanapokua wanatumia
vifaa vya kieletroniki ambavyo kwa sasa vipo katika matumizi hadi katika ngazi
ya familia. Moto huzuka tu endapo kitapatikana chakula cha moto, joto la
kutosha na hewa ya oksijeni (fuel, heat and oxygen).

Sambamba na hayo Kamishna Jenerali anahimiza uzingatiaji wa kinga na


tahadhari ya moto katika maeneo yote. Wamiliki wa maeneo ya umma, binafsi
na biashara wanapaswa kufunga vizimia moto kwa kuzingatia ushauri
unaotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lipo imara na litaendelea kuwaelimisha


Watanzania kuzingatia kinga na tahadhari ya moto ili kuhakikisha maisha na
mali vinakuwa salama.

Imetolewa na;

CGF. Thobias Andengenye


Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
10 Aprili, 2018

You might also like