You are on page 1of 8

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA YA KUKAMILIKA KWA KAZI YA TUME YA UCHUNGUZI WA
MALALAMIKO YALIYOTOKANA NA UTEKELEZAJI WA
OPERESHENI TOKOMEZA
___________________________________________
1.0

Utangulizi:
1.1

Tarehe 01/05/2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,


Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliunda Tume ya Uchunguzi
kuhusu malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni
Tokomeza. Aliteua Makamishna watatu ambao ni Mhe. Balozi Jaji
(Mst) Hamisi Amiri Msumi (Mwenyekiti wa Tume), Mhe. Jaji (Mst)
Stephen Ernest Ntashima Ihema (Kamishna), Mhe. Jaji (Mst)
Vincent Kitubio Damian Lyimo (Kamishna) na Ndugu Frederick
Kapela Manyanda (Katibu wa Tume).

1.2

Operesheni Tokomeza ilikuwa Operesheni iliyobuniwa na Wizara


ya Maliasili na Utalii kwa lengo jema na muhimu la kupambana
na ujangili unaotishia urithi wetu wa wanyama pori, hususani
tembo, faru, nyati, twiga, pundamilia n.k.

2.0

Hadidu Rejea kwa Tume


2.1

Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;

2.2.

Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza


walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

3.0

2.3.

Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza


walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa;

2.4.

Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa


utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua
zilizochukuliwa na maafisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya
wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;

2.5.

Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maaafisa


wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na
hadidu rejea za Operesheni Tokomeza; na

2.6.

Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika kupanga


na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii ili kuzuia na
kuepuka malalamiko mengine kama yaliyotokea kwenye
Operesheni Tokomeza.

Kukamilika kwa kazi ya Tume


3.1

Tume imekamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa kwa Rais wa


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, tarehe
10 Aprili, 2015. Kwa maagizo ya Rais
tumeisoma na kuichambua taarifa hiyo vya kutosha. Kwa hakika
Tume imefanya kazi kubwa sana, na nzuri sana ya uchunguzi na
uandishi wa taarifa. Kazi imefanywa kwa weledi na umakini wa
hali ya juu na kwa lengo dhahiri la kutenda haki. Katika siku 265,
Tume ilitembelea wilaya 38 katika mikoa 20 na kuhoji jumla ya
mashahidi 259. Mikoa iliyohusika ni Kigoma, Katavi, Rukwa,
Mbeya, Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara, Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Iringa, Morogoro, Pwani, Tabora, Singida, Manyara,
Arusha na Tanga.

3.2

Tume imejitahidi kuwahoji wote waliokuwa na malalamiko,


kuwahoji mashuhuda, kuwahoji watuhumiwa, na kukusanya
ushahidi wa aina mbalimbali ili ama kuthibitisha makosa pale
yalipofanyika na kupendekeza hatua za kuchukua, au kujiridhisha
kuwa tuhuma na malalamiko hayakuwa ya msingi. Kazi hiyo
imefanywa vizuri na kurahisisha kazi ya Serikali ya kuchukua
hatua zinazostahili.

4.0

Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa


4.1

Tume ilibaini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja cha


utekelezaji wa Operesheni Tokomeza iliyoanza tarehe 4 Oktoba,
2013, mafanikio mengi yalipatikana, ikiwemo:
4.1.1 Watuhumiwa 1,030 wa makosa mbalimbali yanayohusu
ujangili na uvunaji haramu wa misitu walikamatwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria;
4.1.2 Kukamatwa kwa meno ya 211 yenye uzito wa kilo 522,
meno ya ngiri 11, mikia ya wanyama mbalimbali 36, ngozi
za wanyama mbalimbali 21, pembe za swala 46, mitego ya
wanyama 134, ngombe 7,621 waliokuwa wanachungwa
ndani ya hifadhi na misitu, baiskeli 58, pikipiki 8 na magari
9;
4.1.3 Katika kipindi cha Operesheni kulikamatwa jumla ya
bunduki za kijeshi 18, bunduki za kiraia 1,579, risasi 1,964,
mbao vipande 27,913, mkaa magunia 1,242, magogo 858
na misumeno 60.
4.1.4 Operesheni ilifanikiwa kupunguza kasi ya mauaji ya tembo
kutoka tembo wawili kwa siku hadi tembo wawili kwa
mwezi wakati wa Operesheni;

4.2

Operesheni ilisitishwa rasmi tarehe 01/11/2013 ili kupisha


uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza. Baada tu ya kusitishwa
kwa Operesheni wafugaji wengi wamerudisha mifugo yao katika
maeneo ya hifadhi yaani Mapori ya Akiba, Hifadhi za Taifa,
Hifadhi za Misitu na Maeneo Oevu na ujangili ukaanza kurejea.
Aidha watuhumiwa waliokuwa wametoroka kukimbia Operesheni
wameanza kurejea kwenye makazi yao.

5.0 Vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu


Rejea
5.1

Tume imebaini kuwa katika utekelezaji wa Operesheni kulikuwa


na matukio ya ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu
Rejea. Ukiukwaji huu umesababisha madhara kwa wananchi
mbalimbali ikiwemo vifo, madhara ya mwili na kadhalika.

5.2

Tume ilichunguza matukio 15 ya vifo, na kuridhika kuwa vifo tisa


(9) kati ya hivyo vilisababishwa na mateso ambapo watendaji
kwenye Operesheni walitumia nguvu kubwa kupita kiasi dhidi ya
watuhumiwa wakati wa ukamataji au kuhoji. Kabla ya vifo watu
hao walikuwa chini ya ulinzi wa askari wa Operesheni na kuna
ushahidi wa kitabibu (medical reports), ushahidi wa kimazingira
na ushahidi wa kuona, unaohusisha vifo vya marehemu hao na
mateso kutoka kwa askari wa Operesheni. Tume haikupata
ushahidi wa kuhusisha vifo sita (6) vilivyobaki moja kwa moja na
Operesheni Tokomeza.

5.3

Tume ilichunguza madai ya mateso yaliyosababisha madhara


kwenye miili ya wahusika. Walalamikaji walieleza Tume kwamba
waliteswa ili waoneshe silaha au nyara zilipofichwa au wakiri
kujihusisha na ujangili au ujambazi na wataje washirika wao wa
mtandao wa ujangili. Kulikuwa pia na malalamiko ya
udhalilishwaji. Malalamiko hayo yalitoka kwenye wilaya ishirini na
mbili (22) za mikoa mbalimbali. Yapo matukio ambayo
walalamikaji waliweza kuleta mbele ya Tume uthibitisho wa
kuteswa, na walionesha makovu na kutoa vyeti vya matibabu na
PF 3 walizopewa baada ya kuumia.

5.4

Tume imebaini kuwepo matendo mbalimbali ya ukiukwaji wa


sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea uliofanywa na baadhi ya
askari wa Operesheni na maafisa wengine walioshiriki katika
utekelezaji wake, ikiwemo matukio yanayoashiria rushwa na
udanganyifu mbalimbali.

5.5

Tume ilishughulikia pia tuhuma za wizi, upotevu na uporaji wa


mali. Walalamikaji wa kundi hili walieleza Tume kuwa wakati wa
utekelezaji wa Operesheni, waliibiwa au kupoteza fedha na mali
zao wakati na baada ya kukamatwa au kupekuliwa na askari wa
Operesheni. Tume ilichunguza jumla ya matukio ishirini na tatu
(23) ya aina hiyo na kubaini kuwa malalamiko mengi yalitokana
na askari wa Operesheni kutofuata sheria, kanuni na taratibu za
ukamataji, kuhoji na upekuzi maungoni mwa watuhumiwa na
kwenye nyumba zao. Kasoro zilizoonekana ni pamoja na
kutoshirikisha viongozi au watu huru katika upekuzi na kutojazwa
hati za upekuzi mara baada ya upekuzi. Kasoro nyingine ni askari
wengi kuingia kwenye nyumba kwa wakati mmoja. Aidha, Tume

imebaini walalamikaji wengine waliongeza chumvi katika


ushahidi wao kuhusu idadi ya mali na fedha zilizopotea au
kuibiwa na hivyo ushahidi wao kutoaminika au kuthibitika.
5.6

Tume ilichunguza malalamiko ya kubakwa wakati wa utekelezaji


wa Operesheni. Matukio yaliyochunguzwa na Tume yalikuwa
katika Kijiji cha Iputi, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro na
Kijiji cha Mwantimba Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu na
Wilayani Sikonge. Hata hivyo wote waliodai kubakwa
hawakujitokeza mbele ya Tume kutoa ushahidi wao, hivyo Tume
haikuweza kuchunguza malalamiko yao. Alijitokeza mlalamikaji
mmoja Wilayani Ulanga, Morogoro, lakini Tume haikuridhika na
maelezo yake, ambayo hayakutosheleza kubainisha kosa kwenye
utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

5.7

Tume ilibaini kuwa wapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamani


na kutiwa hatiani na wengine kuachiwa. Tume imeona kuwa
hatua hii ilikuwa sahihi kisheria. Lakini Tume ilibaini pia kuwa
baadhi ya watuhumiwa hawakufikishwa mahakamani. Badala
yake maafisa wa Operesheni walijichukulia mamlaka ya kutoa
adhabu kwa watuhumiwa kama vile kukamata na kuzuia mali
zao, kuchoma moto nyumba na mali zilizokuwa kwenye maeneo
ya hifadhi, kuua au kujeruhi mifugo iliyokutwa kwenye maeneo
ya hifadhi au kuuza kwa mnada ngombe waliokamatwa kwenye
maeneo ya hifadhi. Hatua nyingine inayolalamikiwa ni kuchukua
bunduki zinazomilikiwa kisheria.

5.8

Tume imebaini kwamba katika baadhi ya maeneo askari wa


Operesheni walichoma nyumba moto kwa madai ya nyumba hizo
kujengwa kwenye hifadhi. Malalamiko hayo yalitoka katika
Wilaya za Mlele na Mpanda, Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Momba,
Mkoa wa Mbeya; Wilaya za Nkasi na Sumbawanga, Mkoa wa
Rukwa; na Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara. Katika
uchunguzi wa matukio haya Tume imebaini yafuatayo:

Wanakijiji hawakupewa taarifa ya kutosha kuhamisha mali zao


kabla ya kuchoma nyumba zao;

Baadhi ya wanakijiji walipoteza vyakula na mali zao katika


zoezi hilo la uchomaji moto;

Kuna vijiji vilivyosajiliwa lakini sehemu ya vitongoji vyake viko


ndani ya Hifadhi za Taifa;

Kuna maeneo ya hifadhi au ushoroba (buffer zone) ambayo


hayana alama za mipaka kati ya hifadhi au ushoroba na vijiji
husika;

Kuna nyumba ambazo hazikuwa kwenye eneo la hifadhi au


ushoroba na hivyo zilichomwa moto kinyume cha sheria.

Baadhi ya matukio na malalamiko ya kuchomewa moto nyumba


yalitokea kabla ya Operesheni.

5.9

Uchunguzi wa Tume umebaini kuwepo kwa tatizo kubwa la


wafugaji kutoka nje ya nchi na wafugaji wenyeji kuingiza mifugo
yao katika Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Misitu, Maeneo Oevu na
Hifadhi za Taifa. Maeneo yaliyoathirika sana na tatizo hili ni
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Pori la Akiba la Kigosi Moyowosi,
Pori la Akiba la Maswa, Mapori ya Akiba ya Biharamulo Burigi
Kimisi na Pori la Akiba la Kijereshi.
Katika baadhi ya maeneo imethibitika kwamba wapo ngombe
waliouawa kwa kupigwa risasi baada ya kukutwa ndani ya
hifadhi.
Aidha, Tume imeridhika kwamba kuna ngombe wa walalamikaji
waliokamatwa na kuuzwa kwa mnada. Uuzaji wa ngombe katika
tukio hili haukuzingatia utaratibu wa kisheria.

5.10 Tume ilipata ushahidi kwamba katika maeneo mbalimbali askari


wa Operesheni walikamata au kuchukua bunduki, risasi pamoja
na vitabu vyake hata kwa silaha zinazomilikiwa kihalali. Maeneo
ambayo yalikuwa na malalamiko ya watu kuchukuliwa silaha zao
ni mikoa saba (7) ambayo ni Katavi, Mbeya, Lindi, Morogoro,
Tabora, Manyara na Pwani ambapo jumla ya watu sitini na mbili
(62) walijitokeza mbele ya Tume kulalamika tukio hili.

6.0

Hatua Zitakazochukuliwa na Serikali


6.1

Baada ya kupitia kwa kina taarifa ya Tume, pamoja na


mapendekezo ya Tume, Serikali itafanya yafuatayo:
6.1.1 Hatua za kimashtaka zitaendelea kwa shauri la mauaji
ambalo upelelezi wake umekamilika na hatua za
kiuchunguzi zitaendelea kwa mashauri mengine nane (8)
ya mauaji ambayo upelelezi wake haujakamilika;
6.1.2 Hatua za kisheria na kiutawala zitachukuliwa dhidi ya
watuhumiwa waliothibitika kuwatesa watu 15 wakati wa
Operesheni;
6.1.3 Hatua za kiuchunguzi zinazofanywa na TAKUKURU kuhusu
tuhuma za rushwa na udanganyifu zilizothibitika
zitaendelea;
6.1.4 Silaha zinazodaiwa kumilikiwa kihalali zitafanyiwa uhakiki
na ukaguzi wa kina kuhusu umiliki na matumizi yake na
endapo hakutakuwa na sababu nyingine za kisheria za
kuzuia urejeshwaji, wamiliki warejeshewe silaha zao kwa
mujibu wa sheria na taratibu;
6.1.5 Mali ambazo zimethibitika kuchukuliwa wakati wa
Operesheni kwa tuhuma za kuhusishwa na uvunaji haramu
wa mazao ya misitu zirejeshwe endapo hakutakuwa na
sababu za kisheria kuendelea kuzishikilia;
6.1.6 Serikali itafanya uhakiki wa vijiji ambavyo vimesajiliwa na
vimo ndani ya hifadhi ili kutatua migogoro ya ardhi kati ya
hifadhi na vijiji. Aidha, Serikali itahakikisha kunakuwa na
ushirikiano wa karibu kati ya Msajili wa vijiji au mamlaka
husika na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuepuka kusajili
vijiji ndani ya maeneo ya hifadhi;
6.1.7 Wizara ya Maliasili na Utalii itatayarisha kanuni
zitakazoweka utaratibu wa kuwaondoa watu waliovamia na
kujenga makazi katika hifadhi;

6.1.8 Sheria zote zinazolinda maeneo ya hifadhi zitafanyiwa


marekebisho ili kuongeza adhabu kwa kosa la kuingiza
mifugo kwenye Hifadhi bila kujali uraia wa wamiliki wa
mifugo hiyo;
6.2

7.0

Kwa vile Tume imejiridhisha na faida kubwa na mafanikio ya


Operesheni
Tokomeza, Serikali itaendelea na Operesheni kama
hizo kadri
itakavyojitajika ili kuokoa maliasili za Taifa, ikiwemo
wanyama, hifadhi
na misitu. Hata hivyo ushauri wa Tume juu ya
kuboresha upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa Operesheni
hizo itazingatiwa kikamilifu.

Mawaziri Waliojiuzulu
Tume ilijiridhisha kuwa Mawaziri wote waliojiuzulu, yaani Mhe. Dkt.
Emmanuel J. Nchimbi, Mb., Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, Mb., Mhe.
Mathayo D. Mathayo, Mb., na Mhe. Shamsi V. Nahodha, Mb.,
hawakuhusika moja kwa moja na makosa yoyote ya utekelezaji kwenye
Operesheni Tokomeza. Hivyo, waliwajibika kisiasa tu na hakuna hatua
nyingine inayostahili dhidi yao.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
8 Mei, 2015

You might also like