You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI

Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi
na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata
taratibu za ujenzi.
Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na
huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo
kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i.

Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika
kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.

Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:


ii.

Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi
katika maeneo yao.

Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha
zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
a) Bila kibali cha ujenzi
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na
taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni Mbezi, Tegeta,
Bunju, Mwenge na Kinondoni Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe
18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

You might also like