You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU


NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA
AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 18
JANUARI 2016
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wizara yangu iliahidi kuendelea kutoa taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo
wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini kila wiki. Kuanzia Mwezi Agosti 2015
ugonjwa ulipoanza hapa nchini hadi tarehe 17 Januari 2016, jumla ya watu
14,105 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 218 wamepoteza maisha
kwa ugonjwa huu. Karibia mikoa yote ya Tanzania Bara ilikwisha athirika na
ugonjwa huu isipokuwa mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara ambayo
haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu.
Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, kuanzia tarehe 11 hadi 17 Januari 2016,
kulikuwa na wagonjwa wapya 549 na vifo 10 na mikoa ambayo imeripoti kuwa
na ugonjwa imeongezeka kutoka 11 hadi 16 ukilinganisha na wiki iliyopita.
Mikoa hiyo iliyoongezeka kwa kurudia kuripoti wagonjwa wapya baada ya
kudhibiti ugonjwa kwa wiki zilizopita ni Dar es Salaam, Lindi, Rukwa, Kagera
na Kilimanjaro. Mikoa mingine ambayo bado imeendelea kuripoti wagonjwa
ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma,
Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mkoa wa Morogoro
1

umeendelea kuongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa (Manispaa ya


Morogoro 120, Halmashauri ya Morogoro 40), ukifuatiwa na Simiyu (Bariadi
50), Manyara (Simanjiro 41), Mwanza (Ukerewe 24) na

Halmashauri ya

Arusha (19).
Ndugu Waandishi wa Habari,
Napenda kuikumbusha jamii kuwa kipindupindu ni ugonjwa unaoambukizwa
kwa kula chakula au kinywaji chenye vimelea ambavyo hupatikana kwenye
kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu au kwenye kitu chochote
kilichochafuliwa na kinyesi au matapishi ya mgonjwa. Aidha dalili kuu za
ugonjwa huu ni kuanza ghafla kuharisha mfululizo kinyesi cha majimaji meupe
kama maji yaliyooshea mchele na kinaweza kuambatana na kutapika,
kulegea, kusikia kiu, midomo kukauka, na kuishiwa nguvu. Mgonjwa anaweza
kupoteza maisha endapo hatapata huduma yoyote ya tiba katika muda mfupi
na hasa kutokana na kuishiwa maji. Vilevile, jamii ina fursa ya kujifunza zaidi
kuhusu ugonjwa wa kipindupindu kupitia njia ya simu kwa kupiga namba 117
na kusikiliza ujumbe wa sauti au kuandika neno kipindupindu/cholera
kwenda namba 15774 ili kupata habari zaidi. Hakuna malipo kwa mtumiaji wa
huduma hii.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea
kusisitiza kwa jamii kuzingatia yafuatayo:
- kunywa maji yaliyo safi na salama
- kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na
salama
2

- kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka.


- kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji
vya mito, maziwa na mabwawa.
Napenda kurudia kutoa agizo kwa Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja
na watendaji wake kote nchini kuendeleza juhudi za kuzuia kusambaa kwa
mlipuko ambazo ni pamoja na:
Ushirikishwaji

wa

viongozi

ngazi

mbali

mbali,

hasa

ngazi

za

Halmashauri kwa kushirikisha madiwani na viongozi wa kata, vijiji, na


mitaa.
Mamlaka husika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni
pamoja na uwekaji wa dawa ya klorini kwenye maji na kupima usalama
wa maji mara kwa mara.
Upatikanaji wa dawa za kutibu maji (Water Guard, Aqua Tabs) katika
maeneo ya mlipuko.
Juhudi kubwa ziongezwe kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya vyoo
bora kwa kila kaya.
Uelimishwaji wa Baba na Mama Lishe, na wauzaji wengine wa vyakula
kuhusu kanuni za afya.
Kusimamia utekelezwaji wa Sheria ya Afya ya Mazingira na Sheria
ndogo ndogo (By-Laws).
Uhamasishaji wa Wananchi wanaopata ugonjwa kuwahi kutumia maji ya
chumvi chumvi (ORS) na kuripoti mapema katika vituo vya huduma
Ushirikishwaji wa wadau mbali mbali huko Mikoani, Wilayani, na kwenye
Halmashauri, ikiwemo Sekta Binafsi, na Viongozi wa dini, katika jitihada
za kupambana na Kipindupindu.

Hitimisho
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inatoa rai kwa
jamii, wataalamu na viongozi katika ngazi zote kila mmoja kutimiza wajibu
wake katika harakati za kuudhibiti ugonjwa huu. Aidha napenda kusisitiza
umuhimu wa Mikoa kutuma taarifa sahihi zinazohusu mlipuko wa ugonjwa wa
Kipindupindu na kuwachukulia hatua kali watumishi watakao zembea au
kujaribu kuficha taarifa hizo.
Napenda

kumalizia

kwa

kuahidi

kwamba

Wizara

yangu

itaendelea

kushirikiana na sekta zote husika pamoja na wadau mbalimbali katika


kuudhibiti ugonjwa huu. Aidha tunawashukuru wadau wote, yakiwemo
Mashirika ya Kimataifa kwa mchango wao mkubwa katika jitihada zetu za
kupambana na Kipindupindu.
Pamoja tukishirikiana tutaweza kuutokomeza ugonjwa huu.
Nawashukuru kwa kunisikiliza.

You might also like